Yaliyojiri Mahakama Kuu divisheni ya Makosa ya Uhujumu Uchumi na Rushwa, kesi ya Mbowe na wenzake - 30 Nov 2021

Wakili wa Serikali: Katika Moja wapo ya Vitu Ulivyo tweet Ukasema "kesi Mikazo, Mashahidi wa Michongo" ulikuwa unamaanisha nini

Shahidi: Maana yake ni Mashahidi Wa Kuungaunga!

Wakili wa Serikali: Vipi Kuhusu Mawakili wa Serikali wa Michongo na Majaji wa Michingo

Shahidi: Kwa sababu Mawakili wa Serikali Wanateta Mashahidi Wa Uongo

Wakili wa Serikali: Na Vipi Kuhusu Majaji wa Michongo?

Shahidi: Ndiyo Kuna Hukumu ambazo Wanatoa hazipo Sawasawa

Wakili wa Serikali: Kwa hiyo Una malalamiko Kuhusu Kesi hii

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Kwa hiyo wewe ni Shahidi Mwenye Malalamiko

Shahidi: Ninayo Malalamiko Kwa Sababu Mahakama inadanganywa

Wakili wa Serikali: Kwa hiyo Unatamani Siku Moja Mawakili Wa Serikali unaowataka Wewe?

Shahidi: Nataka Haki itendeke tu

Wakili wa Serikali: Jibu swali Langu

Wakili wa Serikali: Kwa hiyo Unatamani Siku Moja Mawakili Wa Serikali unaowataka Wewe

Shahidi: Ambao Watakuwa Wapo Sahihi, Ndiyo kabisa.
Amejibu vema kabisa , anajua anachokisema, precisely!
 
Mawakili wa mbowe wanachelewesha tu kesi,mara diary mara GPO badala ya kujikita kwenye kupangua kesi.

Yaani kuna siku alikua anapinga maelezo ya askari kwamba wakati wa tukio alikua Arusha kikazi na sasa yupo oysterbay.

Kibatala hajui kwamba askari anaweza kuwa yupo mbinga lakini anafanya upelelezi chake chake?
Sheria ya askari hairuhusu hilo,lazima kuwe na movmne order na task unayofanya mahaki ulipo.in short Nazi ya askari INA mipaka ukiingia kwenye mipaka ya mwingine lazima uwe na movement order,hilo unalosema linawezekana kwa tiss siyo jeshi lingine.Nenda kwenye PGO
 
Mawakili wa mbowe wanachelewesha tu kesi,mara diary mara GPO badala ya kujikita kwenye kupangua kesi.

Yaani kuna siku alikua anapinga maelezo ya askari kwamba wakati wa tukio alikua Arusha kikazi na sasa yupo oysterbay.

Kibatala hajui kwamba askari anaweza kuwa yupo mbinga lakini anafanya upelelezi chake chake?
Wewe ni askari polisi au mwanasheria?
 
Bandu bandu humaliza gogo. Unadhani Mandela alipotiwa ndani watu waliandamana? Unadhani Bashir alifunga wangapi mpaka watu wakaamua kuingia mtaani?
Mbona chama chako nacho kinawatumia ili wapate wabunge na ruzuku. Pamoja na utajiri wote mliokuwa nao sijawahi kusikia mkikataa ruzuku. Ila wengine wakifanya hivyo mnaona nongwa.

Amandla...
Yule Bashir alitesa sana watu kwa miaka, fukuto la hasira za watu likirundikana kwa miaka, hatimaye liliwashwa na msichana mdogo tu Bashir akang'olewa. Haya yanayoendelea hapa, CCM wanafurahia na kukenua meno wakiringia TISS na Polisi, baadaye, hata kama siyo leo, fukuto la hasira litawaka tu na nchi kuingia matatizoni.
 
Bandu bandu humaliza gogo. Unadhani Mandela alipotiwa ndani watu waliandamana? Unadhani Bashir alifunga wangapi mpaka watu wakaamua kuingia mtaani?
Mbona chama chako nacho kinawatumia ili wapate wabunge na ruzuku. Pamoja na utajiri wote mliokuwa nao sijawahi kusikia mkikataa ruzuku. Ila wengine wakifanya hivyo mnaona nongwa.

Amandla...
Yule Bashir alitesa sana watu kwa miaka, fukuto la hasira za watu likirundikana kwa miaka, hatimaye liliwashwa na msichana mdogo tu Bashir akang'olewa. Haya yanayoendelea hapa, CCM wanafurahia na kukenua meno wakiringia TISS na Polisi, baadaye, hata kama siyo leo, fukuto la hasira litawaka tu na nchi kuingia matatizoni.
 
Naomba unisaidie kuona ushahidi wowote au kielelezo chochote kinachoonyesha 'kula njama kutenda vitendo vya kigaidi'. Najaribu kutafuta kila siku sijafanikiwa. Labda ni mimi sielewi.
Hamna vielelezo vyovyote zaidi ya hayo maelezo ya kulazimisha ya akina Adam.. ukiondoa hayo maelezo hamna kesi hapo. Na sijaelewa mantiki ya wao kudai walichukulia maelezo Central, kwanini toka mwanzo wasingetaja Tazara au Mbweni...
 
Kesi inayomkabili Mbowe na wenzake 3 inaendelea mahakamani leo Novemba 30, 2021

=======

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya Kusikilizwa, Naomba tupatiwe Nyaraka ilikuweza Kuzikagua.

Wamekabidhiwa Nyaraka na Kuanza Kukagua Moja baada ya Nyingine.

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Tuna mapingamizi Kuhusiana na Upokelewaji Wa Nyaraka hizo Nne Zinazotaka Kutolewa na Shahidi Wa Pili Mheshimiwa Jaji tumeandaa Mapingamizi ngamizi ifuatavyo.

Vilivyotakiwa katika Vifungu Vya 65, 66, na 67 ya Sheria ya Ushahidi Sura ya Sita.

Mheshimiwa Jaji Kuhusiana na Dispatch, Shahidi aliyepo Mahakamani siyo Competent Witness Kuweza Kuitoa hiyo Dispatch.. Mheshimiwa Jaji sisi tupo tayari Kuendelea na Hizo Hoja zetu za Kisheria kwa maana Kufanya Submission na ataanza Pius Hilla..

Jaji: Kwa hiyo ni Mapingamizi Matatu

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Nyaraka ambazo Wenzetu Wanataka Kutender Kwenye Ushahidi..

Jaji: Hapo unamaanisha Dispatch?

Wakili wa Serikali: KUHUSU RELEVANCE Nyaraka Wanazotaka Kutumbukiza Kwenye Ushahidi Barua, Proceedings, na Charge sheet

Wakili wa Serikali: Nyaraka hazina Indicator Zozote kama D/C Msemwa aliwahi Kufanya Kazi Kituo cha Polisi Oysterbay kipindi cha Mwezi May 2020, Nyaraka hizi pia hazina Bearing yoyote ile za Ukamatwaji Wa Ling'wenya, Uandikaji wa Maelezo Ya Ling'wenya, Mambo ambayo Ndiyo Issue Iliyopo Mbele Yako

Nyaraka hizi pia Mheshimiwa Jaji hazina Bearing yoyote ile Kwamba Lembrus MCHOME (DW2) Kuwa amewahi Kukaa Kituo cha Police Oysterbay.

Mheshimiwa Jaji Jaji Kwa Mujibu wa kifungu cha 7 cha Sheria ya Ushahidi Sura ya 6, Kwamba Ushahidi Mheshimiwa Jaji, Utatolewa na Kupokelewa Mahakamani Kama Upo Relevant, na wala sio vinginevyo.

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Mahakama Yako hii inaongozwa na Sheria, Kwamba Kila Kinachofanyika Mahakamani lazima Kifanyike Kwa Mujibu wa Sheria.. Kila kitakachopokelewa lazima Kiwe na connection (Uhusiano)

Mheshimiwa Jaji Kesi ya DPP VS SHARIF MOHAMMED ATHUMAN AND SIX OTHERS Criminal appeal namba 74 ya Mwaka 2016 katika Ukurasa Wa 6 Aya ya Mwisho Mahakama Ya Rufaa Ilipata Kusema Kwamba, Ushahidi ambao ni Irrelevant ni inadmissible

Mheshimiwa Jaji Page ya 7 ya Hukumu hiyo paragraph Ya Kwanza, Mahakama Ya Rufani Inasema Kwamba fact inakuwa Relevant kama Inakusudia Ku Prove au Ku disaprove Ushahidi, Bila Kuzingatia hayo Mahakama Ingaletewa Mambo Mengi ya siyo Ya Msingi.

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Mahakama Inapaswa Kuletewa Mambo ambayo ni Relevant.

Mheshimiwa Jaji Barua inayo taka Kuletwa Mahakamani inatoka TANAFRICA LAW imesainiwa na Wakili Peter Kibatala Imeelekezwa kwa Hakimu Mkazi Kisutu imenakiliwa kwa Lembrus MCHOME na Kwa Deputy Registar wa pale Oysterbay Police.. Mheshimiwa Jaji Charge Sheet na Proceedings Zinahusiana na Mashtaka, Publication of photographs. Shahidi aliyepo Mahakamani alikamatwa kwa Kupigwa Picha Fulani Kwa Kiongozi Fulani akashtakiwa Kwa Matumizi Mabovu ya Mtandao.

Mheshimiwa Jaji Swali la Kujiuliza ni Je Shauri hili lina Uhusiano gani na Matumizi Mabovu ya Mtandao, Yana Uhusiano gani wa Kupiga Picha Kiongozi Fulani au Taasisi fulani.. Mashtaka haya ya Publication of Photograph Yana Uhusiano gani na D/C Msemwa Kuwepo Oysterbay police?

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Nyaraka zinatakiwa kujiongelea Zenyewe, Ni Wasilisho letu Kwamba Nyaraka hizi haziongelea Chochote Kuhusiana na Ishu iliyopo Mahakamani, Nyaraka zinaongelea Vitu Vingine kabisa, Nyaraka hazina Uhusiano na Ukamataji na Uchukuliwaji wa maelezo ya Ling'wenya

Alitakiwa aieleze Mahakama Yako Tukufu Kwenye Hizo Nyaraka Kuna Moja Mbili Tatu Kuhusiana na D/C Msemwa, Mheshimiwa Jaji Shahidi alijaribu Kueleza Mahakama Yako tukufu Kwamba alikaa na Msemwa Kwa Muda, Hicho siyo Kigezo Cha Kuleta Hizo Nyaraka.

Nyaraka zilitakiwa zijitambulishe Zenyenwe na Shahidi aongee Kuzitambulisha, Kwa Kifupi pasipo Kuichosha Mahakama Yako tukufu Nyaraka hizi ni Irrelevant, Hazina Sifa za Kupokelewa, Kwamba Kitendo Cha Shahidi Kutokuongelea ni Kitu gani kwenye Nyaraka Kinahusiana na D/C Msemwa

Wakili wa Serikali: Inabainisha Kwamba Wala Hana Knowledge Ya Kile Kilichopo Katika hii Nyaraka, Mheshimiwa Jaji nizungumzie Sasa Kuhusiana na Charge Kuwa Nakala, Mheshimiwa Jaji Kinacholetwa Mbele Yako Hakuna Ubishi it's a photo Copy.

Tunasema Hakuna Ubishi Kwa Sababu Shahidi Mwenyewe Alianza Kwa Kusema Hivyo, Rules of Evidence zinademand Kufuatwa Kwa Procedures ili Kuleta Ushahidi, Mheshimiwa Jaji ni Wasilisho Letu kuwa Nyaraka hii Imeletwa kwenye Violation.

Ni Violation ya kifungu cha 63 - 66 ya Sheria ya Ushahidi Sura ya 6, Kwamba Kwakuwa Walifahamu Kwamba Nyaraka ni Photocopy (Secondary) Walitakiwa Mheshimiwa Jaji Wa Comply na Masharti.. Mheshimiwa Jaji Ushahidi Ambao ni Photocopy (Secondary) it's a General Rule Kuwa ni Admissible.

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji baada ya Kusema hayo naomba Wakili Mwenzangu Abdallah Chavula aendelee pale Nilipo Ishia, atakuja kwa suala la Dispatch.

Mheshimiwa Jaji ni Kama alivyotanguliq Kusema Mwenzangu, Nitaanzia Hapa Alipoishia Yeye.

Na Yeye Aliishia Kwamba hii Hati ya Mashtaka Imekiuka Kifungu namba 63 Mpaka 66.. Mheshimiwa Jaji Kifungu cha 63 kimatoa Ruhusa kwa Nyaraka kwa namna mbili.. Kwa primary Evidence na Secondary Evidence.

Na Kifungu ha 64 kimeweka Bayana Kwamba Primary ni Documents, Mheshimiwa Jaji Shahidi akaweka Bayana kwamba alipewa Photocopy. Kwa hiyo siyo Primary Evidence, Kwa Maana hiyo anataka Kuijulisha Mahakama Hii ni secondary Evidence.

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Kifungu cha 65 ya Sheria ya Ushahidi Sura ya 6, kinasema kwamba ANASOMA.. (a), (b) (C), (d), na (e).. Mheshimiwa Jaji Katika Ushahidi Wake hajaeleza Mahakama Kwamba Nyaraka hii Imekuwa Certified na Ukatazama Nyaraka Yenyewe Pia Hazijawa Certified

Shahidi hajaeleza Mahakama Kwamba Nyaraka hii Imetengenezwa Kutoka Kwenye Nyaraka, Hajaileleza Mahakama Mheshimiwa Jaji Kwamba Baada Ya Kufanyiwa Photocopy Wali linganisha Kujiridhisha Kwamba Kilichopo humu ndiyo Kipo kwa Original Charge Sheet

Vilevile Hajaelezea Kwa mdomo Kwamba hii ni sehemu ya Ile Original Document. Mheshimiwa Jaji Ni Hoja yetu Kwamba Shahidi huyu wakati wa Kuomba Kutoa Nyaraka Hajakidhi Matakwa ya Kifungu cha 65.

Wakili wa Serikali: Twende Mbele zaidi, Fungu la 67 liinaweka Masharti Kwamba Secondary Evidence Inapaswa Kutolewa Mahakamani. Ni Maoni yetu Siye kwa Madai Ya Kwamba Eti Kule Mahakamani Kisutu Kwamba walielezwa Nyaraka Ya Mashtaka ipo Moja tu, Kwa Bahati Mbayo siyo Sababu Iliyo Tajwa Kisheria

Kuleta Nyaraka hiyo.. Ni Maoni yetu Vigezo Vilivyomo Katika Kifungu cha 65 vinakosekana kwa Ushahidi na Shahidi Mwenyewe. Na hii ya Kupewa Photocopy Haikamiilishi Kifungu. Kifungu Cha 68 Kinachotaka Wao Ku Introduce hiyo Document na Wao hawakufanya.

Na Kwa Sababu HawaKutumia hiyo nafasi, Basi Maombi yao yanakuwa Batili Mbele ya Mahakama hii. Mheshimiwa Jaji naomba tuelekee Kwenye Pingamizi La Dispatch.

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji ni Msimamo Wa Sheria na Katika Nyakati tofauti Tofauti Tumekuwa tulielekeza Mahakama Yako Kwenye Shauri la JAMHURI Vs CHARLES GAZILABO NA WENZAKE Katika Ukurasa Wa 12, Na Pia Kesi ya DPP VS MIZIRAHI

Mheshimiwa Jaji hapa Kuna suala la Knowledge, Ilikuwa ni Lazima Kuonyesha Mahakama Kwamba alishawahi Kumiliki Kielelezo hiki. Sisi ni Maoni yetu Kwamba Kuna Eneo Muhimu Sana ambalo tunaona ni lazima Mahakama itambue.

Wakati anaeleza Kuhusu Barua, alieleza Barua ile Ina Reference namba, Mheshimiwa Jaji Shahidi a Kwenda Mbele na Kutuambia hizo Reference Nmab ni zipi.. Ni Maoni yetu Kwamba Shahidi ameshindwa Kunukuu Reference namba za Barua ambazo yeye Anadai Kwamba hazikamiliki.

Wakili wa Serikali: Ni Maoni yetu Kwamba Shahidi hana Knowledge ya Kielelezo ambacho anataka Kukitoa. Na Vilevile Kwamba Kielelezo hicho Hakina Uhusiano na Kesi iliyopo Mahakamani.

Nashon Nkungu: OBJECTION Mheshimiwa Jaji tungejikita na P. O zile tatu naona hii ni P. O Mpya Na Yalifanyika Tarehe 23 November Mwaka huu, na Yeye alikuja Tarehe 24 November 2021, Hakuna Sehemu alitaka Kwamba FAITH Alimkabidhi Dispatch, Lakini hajaileleza Mahakama Kwa Namna alivyo Kihifadhi Kielelezo Hicho Haja eleza Mahakama Kwamba Mpaka anafika hapa Kielelezo hicho Kilivyo kuwa wapi na Kilikuwa kinatunza kwa namna gani, Naomba Niezekee Mahakama Yako Kwenye Kesi Ya DPP Vs SHARIF MOHAMMED ATHUMAN na Wenzake

Wakili JOHN MALLYA: OBJECTION naona Wakili analeta Jambo Jipya, Sababu Hapa P.O ilikuwa ni Kuhusu Competence ya Shahidi Juu ya Kielelezo..

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji nafikiri Wakili angetulia kwanza anisikilize na Mahakama Yako iniachie nafasi Nionyeshe Natokea wapi..

Kufungua Bonet ilioneshe Ushahidi Wake.. Na Wakati Wa Ushahidi Wale alisema Anatokea Himo wakati Gari Ipo Moshi Ndiyo zikatokea Hizo Issue.. Kwa hiyo Mheshimiwa Jaji Shahidi Ilikuonyesha Kwamba Alilipata wapi Kielelezo na alikaa nacho ilikuweza kukileta Kielelezo hilo hakufanya na wala Hakuileza Mahakama Hiki Kielelezo alikabidhiwa na nani, Ni Hoja yetu Kwamba Kukosekana Kwa Ushahidi huo, Kwa hayo tuliyoyaeleza ni Maoni yetu Kwamba Kielelezo Hiki (Dispatch) haiwezi Kupokelewa, Mheshimiwa Jaji naomba Kumalizia Kwa Kurejea kwenye Hati ya Mashtaka

Wakili wa Serikali: Hati ya Mashtaka ina walakini na Ushahidi Wa shahidi, Pale anaposema alikamatwa na Kufunguliwa Mashtaka kwa Makosa aliyofanya Wilaya ya Mwanga, Hati anayotaka Kuleta Yeye inaongelea Makosa Yaliyofanyika Dar es Salaam.

Hakuna Sehemu aliyoweza Kulinganisha Kosa alilofanya Wilaya ya Mwanga na Makosa aliyoshtakiwa Dar es Salaam, Haya yote Kwa Ujumla hayana Sifa Ya Kupokelewa na Mahakama hii, Ni Maoni yetu Kwamba Katika Mazingira haya Tunaomba Mahakama Isipokee Vielelezo hivyo.

Jaji: Mmemaliza..?

Wakili wa Serikali: Ndiyo

Jaji: Nakukumbusha Wakili Nashon Nkungu Kwenye Sababu Zako Za Kuunga Mkono Usijibu Hoja ambazo zimetolewa na Upande Wa Mashtaka.

Nashon Nkungu: Sawa Mheshimiwa Jaji, Ingawa napata Ugumu, Naomba Mahakama inivumilie naona Hoja Nyingi Zinakuwa against na Hoja zao

JAJI: Ndiyo Changamoto tunazopata eneo hili

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Naomba Kuwakumbusha Kwamba Siyo Haki yao Kujibu, Huyu siyo Mtu aliyeleta Motion.

Jaji: Nakukumbusha Mr. Hila Kwamba Hilo siyo Jambo Jipya, nimemkumbusha Kwa sababu Hakuwepo Mahakamani

Nashon Nkungu: Mhe Jaji Naunga Mkono Upokelewaji wa Vidhibiti hivi Kwa Pamoja kwa sababu Nimeona vimekidhi Matakwa Makubwa 3 ambayo ni RELEVANCE, MATERIALITY na COMPETENCE

Nashon Nkungu: Kabla Sijaenda Kwa Haraka Haraka kwenye Proceedings Za Mahakama hii, Lakini niliona ina Case Namba, Ina jina la Mshtakiwa,

Jaji: Hiyo ni Nyaraka gani

Nashon Nkungu: Court Proceedings

Nashon Nkungu: Pia Nikihamia Kwenye Charge sheet, Sitoenda Kwenye Content nitajikita Hasa Maeneo alisema ni Copy, Nimeona kweli ni Copy Nimeona namba ya Kesi namba 77/2020 na Relevance InaKuja Kwa sababu akishatueleza Kwamba alipelekewa Oysterbay na Kwa kutumia Charg Sheet hii alipelekewa Mahakama ya Kisutu. Kwa Suala la Relevance Kwa Mujibu Wa Kifungu cha...

Wakili wa Serikali: OBJECTION Mheshimiwa Jaji anachokifanya Wakili anajibu....

Jaji: Mr. Hila anachokisema Unaenda Ndani Sana

Nashon Nkungu: Sawa Mheshimiwa Jaji, Kingine Kinachonifanya niunge Mkono ni Kesi ya DPP VS MIZIRAHI Ukurasa wa 8,

Jaji: Wewe Unayo hiyo Nakala ya MIZIRAHI Kwa Maana Nakumbuka Inachukuliwa na kutoka. Kwenye kesi ya ABEL GAZILABO.

Nashon Nkungu: Mimi ninayo tutawapatia pia, Nimeona Kwenye kesi hii Inasisitiza Knowledge Wala Siyo Sufficient Knowledge. Kwa hayo Machache, Naomba Sababu za Kuunga Mkono Zichukuliwe.

Wakili John Mallya: Mheshimiwa Jaji Nitaongea kwa Kifupi Sana na Kwa Bahati Nzuri sikuwa nawasikiliza Upande wa Mashtaka. Suala la Kwanza la Barua Naona Lazima Barua Isomwe na Charge Sheet na Proceedings kwa hiyo Barua ni Relevant.

Mallya: Zaidi Mheshimiwa Jaji Kifungu cha 8 cha Sheria Ya Ushahidi, Kwamba Matters ambazo zipo Connected at anytime zinaweza kuibuliwa, Shahidi alieleza Ni Muda gani Kila Nyaraka aliiimiliki, kwa Madhumuni gani na alishughulikia Vipi, kwa Hiyo naona ni Shahidi Competent!

Mallya: Kwa sababu hiyo tunaomba Nyaraka za Shahidi Zipokelewe Bila Wasiwasi wowote.

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Kwa niaba ya Mshtakiwa Wa Nne tunaunga Mkono, Kupokea Kwa Set Ya Nyaraka zote Nne, Kwa Maana Nyaraka zote zimekidhi Vigezo Vya Msingi. Na Yeye Mwenyewe ameweza Kutengeneza Misingi ya hizo Nyaraka!

Kibatala: Ameeleza Kwa namna alivyokaa na Vielelezo Vyote kuanzia alipokabidhiwa, Na sisi Washtakiwa wanne tunasubiria Kuja na kuzijaribu Velacity yake Mbele ya Safari wakati wa Cross Examination.

Wakili Fredrick Kihwelo: Mheshimiwa Jaji Kwa niaba ya Mshtakiwa Wa tatu ataanza Wakili Matata Na Baadae nitafuata Mimi.

Wakili Dickson Matata: ASANTE Mheshimiwa Jaji, Upande wa Jamhuri waliweka Mapingamizi Matatu, Moja ikiwa kwa Nyaraka ambazo Shahidi anaomba Kuingiza Mahakamani kwa Maana Barua, Charge sheet, Proceedings na Dispatch hazina Relevant.

La Pili Ni kwamba Hati Ya Mashtaka ni Photocopy na Kwamba haijakidhi Kifungu Cha 66 cha Sheria ya Ushahidi Sura ya 6, Na Pingamizi la Tatu Kwamba Dispatch, Shahidi Siyo Competent Kuweza Kutender Dispatch.

Mheshimiwa Jaji nitajibu Kwa Ujumla na Wakili Mwenzangu atakuja Kujibu pale Nitakapo Ishia, Mheshimiwa Jaji nianze na Swala la Relevance

Matata: Mheshimiwa Jaji ipo katika Kumbukumbu Za Mahakama hii Kupitia Shahidi Kwamba Jana alieleza Mahakama Kwamba alipata Taarifa za Shahidi D/C Msemwa ambaye alikuwa Shahidi Wa Jamhuri Katika Shauri Dogo.

Shahidi anasema hiyo tarehe Hakuwa Kweli Kwa sababu yeye Mwaka Jana, Tarehe 14 May 2020 baada ya Kukamatwa Mwanga na Kuletwa Dar es Salaam alipokelewa na D/C Msemwa

Sitaki Kuzungumza Sana Kuhusu D/C Msemwa Pale Oysterbay, Itoshe Kusema Kwamba baada ya Kuongea Sababu hiyo na Kwamba Kwa Sababu anajua D/C Msemwa alikuwa Oysterbay aliamua Kuja Kujitolea Kutoa Ushahidi Ili Kuja Ku Disaprove alichokisema D/C Msemwa

Matata: Shahidi akasema ili Kuthibitisha Hayo, aliwasiliana na Wakili wake (Peter Kibatala) Kwamba Ni Wakili aliyehusika Kumtetea Mwaka Jana Katika Kesi namba 77 ya Mwaka 2020 ambayo ni Jamhuri Vs Lembrus MCHOME ambayo ilikuwa Mahakama Hakimu Mkazi Kisutu

Matata: Aliwasilina na Wakili wake ili aweze Kupata Charge sheet na Proceedings Za Kesi hiyo na Alisema Kwamba Sababu ya Kuomba Nyaraka hizo, Ilikuwa ni Kuthibitisha Kwamba aliwahi Kufika Kituo cha Polisi Oysterbay Na Baada ya Hapo Ndiyo alipelekewa Kwa Hakimu Mkazi Kisutu!

Matata: Na Kwamba alipokuwa Kituo cha Polisi Oysterbay Ndipo alipokutana na D/C Msemwa, Kwa hiyo Mheshimiwa Jaji Ni Wasilisho letu Kwamba Nyaraka hizi ni Relevant na Kwa sababu Malengo ya Nyaraka hizo ni Kutaka Ku' Disprove Kile alichokisema D/C Msemwa

Matata: Kwa hiyo Mheshimiwa Jaji Pingamizi walilileta Upande wa Serikali Kwamba Nyaraka hizi siyo Relevant, Tunaona ni Pingamizi ambalo halina Mashiko. Kwa Sababu Hakuna Namna D/C Msemwa angeweza kuwa Oysterbay na wakati huo huo akawa Polisi Central DSM Wakati ni Vituo tofauti

Matata: Na Mheshimiwa Jaji Bila hata Kuingia Kwenye Barua yenyewe, ilikuwa ni Barua ya Kuomba Nyaraka Kuja kutumika Kwenye Kesi hii.

Matata: Mheshimiwa Jaji nije kwenye suala la Photocopy, ni Pingamizi la JAMHURI Kwamba Hati ya Mashtaka ni Photocopy na Kwamba Imekiuka Kifungu cha 66 cha Sheria ya Ushahidi Sura ya 6 Kama Ilivyofanyiwa marekebisho Mwaka 2019... Wamesema Kwamba Imekiuka Kifungu Cha 65,66,67 na 68

Mheshimiwa Jaji Nianze Kwa Kusema Kwamba Shahidi Alianza Kwa Ku' lay Foundation Vizuri kwa kuieleza Mahakama ni Kwanini amekuja na Photocopy.. Ni Maelezo ya Shahidi Kwamba Yeye Mwenyewe akiwa na Dada anayeitwa FAITH

Baada ya Kukabidhiwa Barua Kama Nyaraka Walizooomba Mahakama Ya Kisutu, Kwamba alienda Kisutu akiwa na FAITH na Alipofika Alikutana na mama Kwenye Chumba ambacho alikitaja.

Matata: Na Kwamba Baada ya Kufika alimkabidhi Barua aliyopewa na Peter Kibatala ya Kuomba Nyaraka hizo, na Kwamba Yule Mama baada ya Kujiridhisha inafananq na Barua iliyopo Pale Mahakamani, Alimpitia Lembrus MCHOME Court Proceedings na akampa Photocopy ya Charge sheet.

Matata: Shahidi akauliza mbona nimeomba Certified Copy, Mama akajibu Kwamba hii Ndiyo tuliyonayo. Mheshimiwa Jaji ni Wasilisho letu Kwamba Fault ya Kupewa Photocopy haijatokana na Mteja wetu ni Fault Ya Mahakama. Sisi tunaona Pingamizi Halina Mashiko.

Matata: Kwa sababu Kifungu cha 67 ya Sheria ya Ushahidi Sura ya 6 Kama Ilivyofanyiwa Marekebisho Mwaka 2019 Inaruhusu Kutumiwa Kwa Photocopy pale ambapo Kuna Mazingira kama Yaliyotokea Kwenye kesi hii.

Matata: Mheshimiwa Jaji ni Wasilisho la Upande wa Jamhuri Kwamba tulitakiwa Kuomba Notice to Produce Chinese ni ya kifungu cha 68, Mheshimiwa Jaji ni Wasilisho Letu Kwamba Kifungu Hiki hawajakitazama kwa usahihi, Katika Mazingira ya kesi yetu Ili kifungu cha 68 ya Sheria ya Shahidi Kiweze Kutumika ni pale ambapo Masharti Yaliyowekwa Katika Kifungu (a), Mheshimiwa Jaji naomba kukisoma.

Matata: Mhe Jaji Kwa Kifupi Kifungu cha 68 kinasema Kwamba huwezi Kutumia Evidence ambayo ni Secondary Kama Inaangukia Kwenye Kifungu 67(a), Kwa hiyo ni Wasilisho letu Kwamba Kielelezo Kinacho Ombwa Kuingia Mahakamani Kipo sahihi na hakija Kosa Sifa yoyote ya Sheria Ya Ushahidi

Matata: Mheshimiwa Jaji Kwa namna Nyingine Kwamba, Tufanye Kweli Tulitakiwa Kutoa Notice to Produce Kitu ambacho nakipinga Kwa Nguvu zote, Lakini Bado Mahakama Inayo Uwezo Wa Kupokea Secondary Evidence Kwa Kutumia Kifungu hicho hicho cha 68(g).

Matata: Mheshimiwa Jaji Kwa kuzingatia Kwamba Photocopy hii alipewa na Mahakama na Kwa Kuzingatia tupo Kwenye kesi Ndogo inayohitaji Uharaka, Na Kwa kuzingatia Kipengele (g) Mahakama Inayo Mamlaka ya Kukipokea, Ni Wasilisho letu Pingamizi hilo halina Mashiko na litupiliwe Mbali

Matata: Mheshimiwa Jaji nije kwenye suala la Competence. Na specifically nitazungumzia Kuhusu Dispatch. Mheshimiwa Jaji Ni Submission ya Shahidi Kwamba alipofika Dar es Salaam alienda Kuonana na Wakili wake Peter Kibatala. Na Baada Kuonana na Wakili wake, Wakili wake alimkabidhi Barua na Dispatch akiwa yeye Shahidi Na Mtu anaitwa FAITH, Na Kwamba Baada ya Kukabidhiwa yeye na FAITH waliongozana Kwenda Mahakama Ya Kisutu Wakiwa na hiyo Barua na Dispatch.

Matata: Na ni Ushahidi Wake Kwamba kwanza Alipopewa Dispatch na Barua alijiridhisha Kama Dispatch na Barua Zinahusiana na Kesi namba 77 ya 2020. Na Kwamba waliofika Mahakamani Walienda Kuonana na mama Katika Chumba ambacho alikitaja yeye Shahidi akiwa na Barua na Dispatch

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji tumevumilia Sana Lakini Sasa Wakili asitoe Ushahidi, Hakuna Sehemu Shahidi alisema alienda akiwa na Dispatch alisema alienda na Barua..

Matata: Naomba Mahakama itukumbushe, Mimi Nilisikia Kwamba Walienda na Barua pamoja na Dispatch

Jaji anapekua faili lake

Jaji anasoma ila Hakuna Sehemu Kaandika Kuhusu Dispatch kabisa

Jaji: Mimi niliandika kwamba alikabidhiwa barua sioni sehemu ya Dispatch Wakili

Peter Kibatala: Kuna mahala tunalinganisha hapa KWAMBA, panaonyesha majibu ya wakili na shahidi Kibatala ANASOMA

Jaji: Unalinganisha wapi.. Kwenye LIVE?

Kibatala: Sawa, lakini Kama Mahakama Haikuandika hatuwezi Kufanya lolote.. Kwamba Hakusema suala la Dispatch?

Jaji: Mbeleni Mpaka Wanafika Mahakamani hapa Walikuwa na Dispatch Ila sijaona sehemu Kwamba FAITH Alimkabidhi Barua na Dispatch, Ila Baadae alikuwa na Dispatch!

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Kwa Hiyo Dispatch ipo au Haipo? Jaji: Dispatch ipo kwa Sababu Mbeleni huku naona Kuna sehemu alisema Kwamba walipo fika hapa walikuwa na Dispatch

Wakili wa Serikali: Lakini haionyeshi Dispatch alipata wapi na Ilikuwa Kwenye Custody yake tangu saa ngapi.

Matata: Mheshimiwa Jaji Shahidi aliweza Kusema Kwamba alikabidhiwa Barua na Dispatch na Aliweza Kutaja Kuwa Ilikuwa na Rangi ya Pinki, Juu Imeandikwa Classic Dispatch Book Ina maneno yameandikwa COURT 2, Ndani yake ina anuani ya Mahakama.

Matata: Kwa Maoni yetu shahidi aliweza Kusema Kwamba alipata wapi na alikaa nayo, Ni Ushahidi Wetu Kwamba Shahidi ni Competent. Kwa sababu Pingamizi lao Lilikuwa linahusiana na Competence na siyo suala la Chain of Custody.

Matata: Tunaiomba Mahakama Inapokuwa inatoa Maamuzi Juu ya Competence, Ijielekeze kwenye Kile Kilicho amriwa Katika Kesi Ya DPP VS MIZIRAHI na wenzake Watatu Mahakama ya Rufaa Dar es Salaam, Criminal appeal namba 293 ya Mwaka 2016, Ukurasa wa Saba na Nane aya ya kwanza.

Matata: Iliposema posseser anaweza Ku tender Document, Inasema(ANASOMA) Shahidi alionyesha ana hiyo Knowledge na ali' posess Nyaraka hiyo tunaomba Mahakama Imuone ni Competent na Tunaomba Mahakama Itupile mbali Pingamizi hilo.

Mhe Jaji naomba Wakili Mwenzangu amalizie

Wakili Fredrick Kihwelo: Mheshimiwa Jaji Mimi nitakuwa na Jambo Moja Mheshimiwa Jaji Wakili Wa Serikali Wakati anazungumzia suala la Dispatch, alisema Kutajwa kwa Reference namba kwenye Dispatch, Kwa Maoni yangu Mhe Jaji alikuwa anazungumzia Authentication ya Dispatch hiyo

Kihwelo: Mheshimiwa Jaji Wakati Shahidi anatoa Ushahidi Wake, Alizumgumzia Kidogo Kuhusu Dispatch hiyo kwa Kutaja unique Features Mbalimbali kama Rangi, Jina Lililopo Juu Kwa Maana Classic Dispatch Book na COURT 2

Kihwelo: Na Shahidi alikwenda Mbali Kwamba Ndani palikuwa na Tarehe, Anuani ya Barua na Sahihi ya Mpokeaji, Kwa Maoni yangu Kwamba aliweza Ku authenticate, Mheshimiwa Jaji Pia naomba nizungumzie Kuhusu suala la Hati ya Mashtaka.

Kwamba Shahidi Ameleta Nakala, Na Shahidi alieleza kwamba Kwanini alileta Nakala, Kwa kuwa Shahidi amesema Kwanini Shahidi Ameleta Nakala, Ni Submission Yetu Kwamba Ushahidi Wa Shahidi Unapaswa Kuchukuliwa akwa Uzito unaostahili.

Kihwelo: Na hilo pia lipo Katika Sheria Kesi Ya GOODLUCK KYANDO Vs REPUBLIC Criminal appeal 118, ya 2003 ipo kwenye Tanzania Law Report Kwenye Ukurasa wa 363 na Specifically 367.

Mheshimiwa Jaji Kwa hili na yake ambayo yemezungumzwa na Wakili Mwenzangu Dickson Matata Naomba, Itupilie Mbali Mapingamizi na Ikubali Vielelezo Vilivyoletwa Mbele Yako Ni hayo tuh Mheshimiwa Jaji

Jaji: Jamhuri?

Wakili wa Serikali: Mhe Jaji Kwa Ufupi sana Naanza na Hoja ya Wakili Msomi Dickson Matata Alianza Kujibu Hoja ya Relevance, Wakati anazungumzia Hoja ya Relevance, Ni kweli Shahidi alieleza hayo, lakini Hoja yetu ya Msingi ni Hayo aliyosema alipaswa aoanishe kwenye Hizo Nyaraka

Wakili Peter Kibatala: OBJECTION Wakili anaruhusiwa Kwenda Ndani tena ya Proceedings????

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Eneo Lingine Mwenzetu aligusia Swala la Secondary Evidence. Mwenzetu alielekeza Mahakama Kifungu cha 67 1(c) na aakaisomea Mahakama Kwa Ufasaha, Katika Hiki Kifungu, Wenzetu hawawezi Kupata Hifadhi hapa.

Walitakiwa Kuieleza Mahakama Kati haya Matatu, Nyaraka Halisi either Imepokea, ama Nyaraka halisi imeharibika, ama kwa Sababu ambazo hazitokani na wao Wameshindwa Kuleta Nyaraka hiyo Ndani ya wakati. Sasa Kusema Pekee Kwamba aliyetuhudumia akituambia Kwamba hii Ndiyo Nyaraka pekee, haitoshi kwa Kusema.. Badala yake Walipaswa Waonyeshe Jitihada Walifanya Nini Baada ya Kuambiwa Hivyo.

Wakili wa Serikali: Badala yake wanaitupia Mahakama Lawama Badala ya Kusema Walifanya nini, Kwa Maoni yetu siyo Sahihi. Vilevile Mheshimiwa Jaji Mwenzetu anaomba Mahakama Ipokee Nyaraka hiyo kwa kutumia Kifungu Cha 68(g).

Huu siyo Wakati wake Kitendo Cha Kuto Jibu Maana yake Wenzetu wamekubali na hawana Kipingamizi nalo, Vilevile Wenzetu Wamezungumzia Kuhusiana Na Suala la Competence Ya Dispatch, Wamezungumzia Competence Ya Shahidi Yenye Connection Na Dispatch Mheshimiwa Jaji hapa tunaona Wenzetu walichanganya Mambo mawili Kwa Wakati Mmoja, Wenzetu Wanasema Kwamba Kwa Sababu Shahidi ameweza Ku Identity Unique Features basi ana Knowledge

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Utambuzi wa Nyaraka na Kilichopo ndani ya Nyaraka Ni Vitu Viwili tofauti, Kutambua Nyaraka Pekee yake Haitoshi, Kwa Maoni yetu Kutambua Nyaraka Na Kujua Kilichopo ndani ya Nyaraka Ni Tofauti. Wenzetu Walitakiwa Wajibu Hoja yetu Katika Misingi huu, Kitu ambacho hawajafanya, Mwisho Wenzetu Wameielekeza Mahakama Katika Kesi Ya GOODLUCK KYANDO, Kitu ambacho sisi tunasema Principle hii haiwezi Kutumika hapa, Kwenye kesi hii Wanaongelea Kielelezo ambacho Kipo Kwenye Kumbukumbu za Mahakama, Sisi tunasema Hoja za Wenzetu hazijajibu Hoja zetu, Sisi tunaomba Mahakama Isizingatie Hoja zao Kwa Sababu Hazina Nguvu Kisheria.


Jaji: Nimewasikia pande zote mbili kwa hoja zote mbili nahitaji ku' digest Nahitaji muda wa dakika 45 kama naweza kuwaita mapema nitawaiteni

Tutarudi saa nane na dakika 25

Jaji anatoka
====

9:00 Mchana jaji bado hajarudi

Jaji: Muda Mfupi Uliopita kabla Mahakama Kupumzika, Niilisikiliza Hoja za Pande zote mbili, Sasa Uamuzi ni Kama Ufutavyo

Shahidi Wakati anatoa Ushahidi Wake ambapo ni Barua Kutoka Kwa Wakili Wake Peter Kibatala Kwenda Mahakama Ya Hakimu Mkazi, Dispatch na Mwenendo Wa Kesi pamoja na Hati ya Mashitaka Kutaka Kuingia Kama Kielelezo.

Jambo ambalo lilipingwa na Mawakili wa Serikali Kwamba Moja Nyaraka hizo hazina Uhusiano na Kesi (Relevance), Na Pia Kwamba Hati Ya Mashitaka Ilikuwa ni Nakala na siyo Nakala Halisi. Tatu ilikuwa Kwamba Shahidi ajaonyesha Kwamba anaifahamu Dispatch, Mahakama Kwa kuzingatia Hoja zote za pande Mbili, Na Mahakama Ikazingatia Kwamba Nyaraka hizi Zinazoombwa Kuingia zitaishia Kwenye kesi hii Ndogo.

Jaji: Pia Kwamba Shahidi ana tatizo la kina Ki Afya, Na Kwamba Ni Kweli Kwamba Nyaraka zinatumika Kuuliza Maswali lakini Mahakama Inayo Muda wa Kuzichunguza, Kwa Sababu hiyo Mahakama Imeona izipokee Nyaraka kuzingatia Uamuzi Wake utaokuja Kutoa Mbele

Jaji: Mahakama Inapokea Barua Kwenda Kwa Hakimu Mkazi Kisutu kama Kielelezo Namba 1.. Mahakama Inapokea Dispatch Kama Kielelezo Namba 2.. Mahakama Inapokea Nakala ya Hati Ya Mashtaka ambayo ilikuwa imefunguliwa Mahakama ya Kisutu Jamhuri Vs Lembrus MCHOME, Mahakama Inapokea Pia Mwenendo Wa Kesi hiyo namba 77 ya Mwaka 2020, Kama nilivyosema Kwamba Mahakama Itatoa Uamuzi Juu ya Nyaraka hizi wakati Maamuzi wa Kesi Ndogo.

Wakili wa Serikali: Naomba Kwa Record Juu ya Namba, Kuna Kielelezo Cha Goodluck.

Jaji: Basi naomba Kubadilisha Namba,
Barua itakuwa D2
Dispatch Itakuwa D3
Hati ya Mashitaka ni D4
Na Mwenendo ni D5

Jaji: Naomba Sasa Shahidi akabidhiwe aweze Kusoma

Jaji: Shahidi nakukumbusha kwamba uliapa, na utaendelea kuwa chini ya kiapo Wakili Fredrick: Isome barua

Shahidi: ANASOMA BARUA Kutoka TANAFRICA LAW kwenda kwa Hakimu Mkazi Kisutu Shahidi anasoma kwa kiingereza kile cha ndani ndani kabisa (yaani kutoka Buckingham Palace)

====

Mahakama imetupilia mbali mapingamizi yote ya Jamhuri dhidi ya vielelezo vya shahidi wa pili wa utetezi, lakini Jaji amesema vielelezo hivyo vitazingatiwa zaidi katika maamuzi ya mwisho wa shauri katika kesi ndogo hii. Hivyo shahidi ameingiza vielelezo.

Jaji: Soma na dispatch book

Shahidi: anasoma dispatch Book.

Wakili Fredrick: Nakukabidhi hati ya mashtaka shahidi Shahidi: shahidi anasoma Hati ya Mashtaka pia Kwa Kiingereza kizuri

Wakili Fredrick: Nitakukabidhi Mwenendo Wa Kesi na Usome Page ya Kwanza na Ya Mwisho

Wakili Fredrick: Kihwelo Shahidi Ulisema Kwamba Oysterbay Ulikaa Siku 14 Je Ulimaanisha nini

Shahidi: Nikipofikishwa Oysterbay Mara ya Kwanza Nilikaa Siku Tano Kuanzia Tarehe 14 May Mpaka Tarehe 15 May 2020, Nilipopelekwa Kisutu

Wakili Fredrick: Baada ya Hapo, Nilisomewa Kesi Na Kunyimwa Dhamana Nakutakia kwenda Magereza nikarudishwa Oysterbay Siku 14,

Fredrick: Ilikuwaje Ukarudishwa Oysterbay

Shahidi: Baada ya Kukosa Dhamana, Hakimu alisema Nipelekwe Keko, Wakati Ule Palikuwa na Corona Sikupelekwa Magereza Badala Yake nikapekwa Oysterbay tena

Wakili Fredrick: Kwanini Sasa Hawakukupeleka Magereza Kama Hakimu alivyosema Shahidi: Kwa Uelewa Wangu Sababu ya Corona

Wakili Fredrick: Ulipimwa lini Corona

Shahidi: Siku ya Tarehe 19 May 2020

Wakili Fredrick: lini tena Ulipima Corona

Shahidi: Hakuna zaidi Ya Kusubiri Majibu ya Corona

Wakili Fredrick: lini Ulirudishwa tena Mahakamani

Shahidi: Siku ya Tarehe 19 ambapo Hakimu alikataa Kunipokea Kwa Sababu Nilikuwa Nimtokea Polisi na siyo Magereza kama alivyoagiza

Wakili Fredrick: Siku ya Tarehe 03 nini Kilitokea

Shahidi: Siku niliyopelekwa Magereza

Wakili Fredrick: Na Siku ya Tarehe 05 June nini Kilitokea

Shahidi: Nilisomewa Mashtaka Kwa Njia Ya Mtandao na Hakimu akasema Kwamba Naweza Kupata Dhamana

Wakili Fredrick: Na Tarehe 08 June, Nini Kilitokea

Shahidi: Siku ambayo nilipata Dhamana Maana Siku ya Tarehe 05 June sikukamilisha Masharti ya Dhamana

Wakili Fredrick: Umetaja Tarehe Nyingi Nyingi Je zote zipo Kwenye Mwenendo Wa Kesi

Shahidi: Ndiyo zote zipo

Fredrick: Tarehe 03 Mwezi Wa Sita Utaipata Ukurasa wa Ngapi

Shahidi: Ukurasa wa Tano

Wakili Fredrick: Tarehe 08 June 2020 Utaipata Ukurasa Upi

Shahidi: Kwenye Ukurasa Wa Sita

Wakili Fredrick: Nini Kilitokea Mwezi wa 10 August 2020

Shahidi: Hakimu aliniachia Kwa kifungu 225 baada Ya Upelelezi Kutokamilika

Wakili Fredrick: Nini Kilitokea tena

Shahidi: Nilikamatwa na kurudishwa tena Oysterbay

Wakili Fredrick: Uliwakuta Askari Gani

Shahidi: Mkuu wa zamu alikuwa Afande Msemwa, khadija na Sam

Wakili Fredrick: Umekuwa Ulimtaja Afande Msemwa wa Oysterbay

Shahidi: Mwonekano wake ni Mweusi Kidogo kwangu, Ana mwili kunizidi Kidogo

Shahidi: Kitu Kingine ni Namba Yake

Wakili Fredrick: Namba gani

Shahidi: Namba Yake Ya ajira

Wakili Fredrick: ambayo ni namba Ngapi

Shahidi: H4323

Fredrick: Wakati Unajitambulisha Umesema Wewe Ni Mkulima, Ukiachana na Kilimo unafanya Shughuli Gani Nyingine

Shahidi: Najihusisha na siasa

Wakili Fredrick: Kule Mwanga Ulihojiwa Kwa Kosa gani

Shahidi: Makosa ya Kupiga Picha Gari ya Kiongozi Fulani wa Taasisi Fulani Tanzania

Wakili Fredrick: Ukashtakiwa kwa Makosa gani

Shahidi: Kwa Makosa ya Kimtandao, Kitu ambacho Kilinishangaza

Wakili Fredrick: Unasema Ulitambua Afande Msemwa Kwa Namba Yake, Je Ilikuwa sehemu gani

Shahidi: Upande wa Kulia Kifuani

Wakili Fredrick: Wakati Unahojiwa hapa ulisema Kwamba Mwanga hukuandika Jina Popote na Ulipokuwa Moshi pia Huku andikwa Popote

Shahidi: Watu wengi wana fikishwa Vituo Vya Polisi bila Kuandikwa Mahali Popote

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji hayo ni Maoni yake

Wakili Fredrick Kihwelo: Naondoa Mheshimiwa Jaji, Na huo utakuwa Mwisho Wangu

Wakili Nashon: Nkungu Shahidi Ulisema Kwamba Askari walikuja Nyumbani Kwako Kukukamata, Je Walikuja nyesha Arrest Warrant.?

Shahidi: Hapana

Nashon Nkungu: Nilisikia Pia Unasema Waliruka Geti

Shahidi: Ndiyo

Nashon Nkungu: Je Walikuja na Kiongozi yoyote Wa Mtaani Kwako

Shahidi: Hapana

Nashon Nkungu: Nilisikia Unasema Ulishtakiwa Kwa Matumizi Mabaya Ya Mtandao

Shahidi: Ndiyo

Nashon Nkungu: Nilisikia Ulikamatwa Kwa a Kupiga Picha Kiongozi Fulani Mkuu wa Taasisi Fulani hapa Nchini

Shahidi: Ndiyo

Nashon Nkungu: Nilisikia Unasema Kuhusu Askari Msemwa hapa Mahakamani, Je Mna ugomvi

Shahidi: Hatujawahi Kuwa na Ugomvi

Nashon Nkungu: Nilisikia Pia Kwamba Uliletewa Dar es Salaam Tarehe 14 May 2020

Shahidi: Ni sahihi

Nashon Nkungu: Ulimuona Afande Msemwa Siku hiyo

Shahidi: Ndiyo

Nashon Nkungu: Alikuwa Wapi

Shahidi: Mapokezi Oysterbay

Nashon Nkungu: Ulikuwa Unapata Huduma Za Kibinadamu

Shahidi: Ndiyo

Nashon Nkungu: Kama Nini

Shahidi: Kama Chakula na Maji

Nashon Nkungu: Nani alikuwa anakuhudumia Chakula

Shahidi: Mimi nilikuwa Simfahamu Kwa sababu Nilinyimwa Kuonana Na Ndugu zangu

Nashon Nkungu: Askari gani alikuwa anakuhudumia Kule Mahabusu

Shahidi: Askari wengi akiwemo Msemwa

Nashon: Ahsante Mheshimiwa Jaji

Mallya: Sasa Umesema Wewe Mwanasiasa Je Wa Chama Gani

Shahidi: Wa Chadema

Mallya: Je Nikisema Wewe Mwanachama Umekuja Kusema Uongo Mahakamani Kumuokoa Mwenyekiti Wako Mahakamani, Nitakuwa nasema Uongo.?

Shahidi: Uongo Mkubwa

Mallya: kwanini

Shahidi: Kwa sababu hata Ingekuwa Mtu wa CCM anatoa Ushahidi Wa Uongo ningekuja Kuisaidia Mahakama..

Mallya: Je Namba ya Msemwa Iko Kwenye Nini

Shahidi: Beji Kama Chuma Kifuani

Wakili Peter Kibatala: Shahidi Oysterbay ipo sehemu gani au kuna kitu gani Kimepakana Nacho?

Shahidi: Ubalozi Wa Marekani

Kibatala: Asante Mheshimiwa Jaji sina Swali lingine

Wakili wa Serikali: Shahidi Hebu tutajie Majina yako

Shahidi: Lembrus Kapuya Mchome

Wakili wa Serikali: Ulisikia Mtu anaitwa Mchome Je ni Ndugu yako

Shahidi: Hapana, Utakuwa ni Ukoo labda

Wakili wa Serikali: Kinachotofautisha MCHOME wewe na Wengine ni nini

Shahidi: Maboma ya Kifamilia

Wakili wa Serikali: Unamaanisha Nini

Shahidi: Ukoo Mkubwa au Kuna wachome Wengine Wala Hatufahamiani

Wakili wa Serikali: Sasa Umetuambia Kwamba Ulikuwa Unafuatilia Mwenendo wa kesi Hii kwa Mtandao na Magazeti

Shahidi: Sahihi

Wakili wa Serikali: Ulimaanisha Mtandao ni Mitandao ya Kijamii

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Katika Social media unatumia mtandao upi!?

Shahidi: T W I T T E R

Wakili wa Serikali: Unatumia majina gani

Shahidi: Lembrus Mchome

Wakili wa Serikali: Umesema pia wewe ni mwanasiasa

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Katika Sasa unanafasi gani

Shahidi: Ni Katibu Wa Chadema Wilaya ya Mwanga na Pia Katibu Wa Bavicha Mkoa wa Kilimanjaro

Wakili wa Serikali: na utakuwa Mwanachama Hai wa Chadema Kwa Muda gani

Shahidi: Kwa Muda wa Miaka 11 Sasa hivi

Wakili wa Serikali: Katika Muda wote wa Kuwa Mwanachama Mwenyekiti Wako ni nani

Shahidi: Ni Freeman Aikael Mbowe

Wakili wa Serikali: Nitakuwa Sawa Nikisema Kwamba Kwenye Nyanja za Kisiasa Mnafahamiana Sana

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Na Unapendezwa na Uongozi wake

Shahidi: Sana

Wakili wa Serikali: Kwenye Kesi hii, Ya Uhujumu Uchumi namba 16 ya 2021, Unafahamu alishitakiwa lini

Shahidi: Hapana Sikumbuki

Wakili wa Serikali: Ya Mwaka huu au Mwaka Jana

Shahidi: Mwaka huu

Wakili wa Serikali: Wakati unashtakiwa Hati yako inasema Kwamba Unashtakiwa Kwa Publication of Ponograph

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Unasema Kwamba Kesi hiyo ili maliza Tarehe 10 Mwezi 08 2021

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Wakati Huo Freeman Mbowe ameshashrakiwa tayari

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Baada Ya Kuwa Umeshaaachiwa Je Ulifunguliwa Kesi Nyingine tena

Shahidi: Hapana

Wakili wa Serikali: utakubaliana na Mimi Kwamba Kwa Kipindi hicho kabla ya Kufahamu.. Kwanza Nikuulize Swali, Je Ni kweli Ulifahamu Msemwa alitoa Ushahidi Kupitia Mitandao

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Ni kweli Kwamba, Kabla ya Kuona Taarifa hizo na Ulichukulia Kwamba Shitaka lako limefutwa, Kabla ya Hapo Ulikuwa hujawahi Kuomba Kupatiwa Mwenendo na Hati ya Mashtaka!?

Shahidi: Hapana

Wakili wa Serikali: Katika Mitandao ya Kijamii Haswa Twitter Ambapo Unajulikana Kama Lembrus MCHOME, Namna ya Kutuma Ujumbe Unautengeneza Mwenyewe yaani (User generator)

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Na Ukitaka Kuchukua Ujumbe wa Mtu Mwingine yani Retweet Unafahamu

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Kwenye Mtandao Wa Twitter, Kama Naelewa Utanifahamisha, Ni Information Ambazo Mtu anaweza Kuona zile ambazo umetweet na Kuziona

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Sasa na Mara Nyingine Umekuwa ukiandika Ujumbe Unaohusiana na Kesi hii Kule Twitter

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Katika Moja wapo ya Vitu Ulivyo tweet Ukasema "kesi Mikazo, Mashahidi wa Michongo" ulikuwa unamaanisha nini

Shahidi: Maana yake ni Mashahidi Wa Kuungaunga!

Wakili wa Serikali: Vipi Kuhusu Mawakili wa Serikali wa Michongo na Majaji wa Michingo

Shahidi: Kwa sababu Mawakili wa Serikali Wanateta Mashahidi Wa Uongo

Wakili wa Serikali: Na Vipi Kuhusu Majaji wa Michongo?

Shahidi: Ndiyo Kuna Hukumu ambazo Wanatoa hazipo Sawasawa

Wakili wa Serikali: Kwa hiyo Una malalamiko Kuhusu Kesi hii

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Kwa hiyo wewe ni Shahidi Mwenye Malalamiko

Shahidi: Ninayo Malalamiko Kwa Sababu Mahakama inadanganywa

Wakili wa Serikali: Kwa hiyo Unatamani Siku Moja Mawakili Wa Serikali unaowataka Wewe?

Shahidi: Nataka Haki itendeke tu

Wakili wa Serikali: Jibu swali Langu

Wakili wa Serikali: Kwa hiyo Unatamani Siku Moja Mawakili Wa Serikali unaowataka Wewe

Shahidi: Ambao Watakuwa Wapo Sahihi, Ndiyo kabisa.

Wakili wa Serikali: Ni kweli Watu walikuwa wa nakupa Pole Kwenye Mitandao yako Baada ya Kupata Ajali

Shahidi: Ndiyo
Mwendelezo upetoka kweli?
 
Nimekuwa nikifuatilua hii kesi ya mbowe, mwenendo ya kesi yenyewe na namna ushahidi unavyotolewa mahakamani na jamhuri.

Jamhuri inaonyesha wamejipanga muda mrefu sana kwasababu za kiupelelezi nakadhalika.

Na kwanamna wanavyotoa ushahidi wao hakika umenyooka sana kuliko hata ule ushahidi wa Sabaya wa kuunga unga na gundi.

Siamini kama jamhuri inaweza kupoteza pesa nyingi kutengeneza kesi kubwa namna hii.

Kumbuka mashahidi wanaotoa ushahidi katika kesi hii ukiconnect doti kama unapata jibu chanya.

Jamhuri wametumia kodi ya wananchi katika upelelezi wa kesi hii na mchakato mzima unaohusu hii kesi.

Sasa kama mbowe atakuja kushinda kesi,ni heri jamhuri hata kama mtu amefanya uhaini wowote watumie njia nyingine kumkabili kuliko kumpeleka mahakamani.

Na sasa hivi wanachofanya mawakili wa mbowe ni kuweka mapingamizi mengi ili yakitupwa na mahakama waweze kutengezea picture ya kuwaminisha wananchi yakwamba uwanja wanaochezea haupo fair; jambo ambalo ni utoto kabisa.

Hoja ya kwamba jamhuri inabebwa, wapinzani wamefanya kichaka cha kujifichia

Tunaomba judge asisikilize pressure kutoka kwa wanasiasa au wanaharakati fulani fulani na vyomba vya habari wenye mrengo ule wa kisiasa, kwasababu atainajinsi mahakama. Hata Dunia ipige kelele mhalifu ni muhalifu tu
Maoni yako yanaonyesha umetumwa ila nakukumbusha tu kuwa iwe oungo ama ukweli mungu anajua kila kitu unaweza kimfunga mtu kwa makosa ambayo hajayatenda kwa kuwa tu wewe umejiandaa namna ya kumshitaki mtu husika ila ki uhalisia yeye sio mkosaji kuna mekosa ya kibinadamu ila kuna dhambi kwa mungu mizani ya haki ipo kwa Allah
 
Mawakili wa mbowe wanachelewesha tu kesi,mara diary mara GPO badala ya kujikita kwenye kupangua kesi.

Yaani kuna siku alikua anapinga maelezo ya askari kwamba wakati wa tukio alikua Arusha kikazi na sasa yupo oysterbay.

Kibatala hajui kwamba askari anaweza kuwa yupo mbinga lakini anafanya upelelezi chake chake?
Lakini lazima awe amejaza form maalum kwenda kufanya kazi nje ya kituo chake Cha kazi hiyo ndiyo kibatala alitaka kuona ili ajiridhishe kuwa alifanya kazi kwa mujibu wa sheria ya kazi yake
 
Sheria ya askari hairuhusu hilo,lazima kuwe na movmne order na task unayofanya mahaki ulipo.in short Nazi ya askari INA mipaka ukiingia kwenye mipaka ya mwingine lazima uwe na movement order,hilo unalosema linawezekana kwa tiss siyo jeshi lingine.Nenda kwenye PGO
Hahaaa kwa maslahi ya taifa polisi anaweza kutumika popote
Yaani polisi wa musoma kakutana na jambazi sugu msibani mkuranga,asilishughulikie kisa ni PGO?
 
..kingai,na mahita, walieleza kwamba wao sio askari wa kilimanjaro, bali walikwenda huko kwa kazi maalum...
Hoja dhaifu sana hizo,haziwezi kumuokoa mbowe.

Polisi anaweza kufanya kazi popote.

Mahakama inapochakata ushahidi,inajiegemeza katika kuangalia unamuhusishaje mshitakiwa. Katika kupeleleza polisi wanaweza kumtoa askari nachingwea,kwa sababu ana utaalam na ugaidi ili aende maswa kuna tukio.

Kibatala anatakiwa ajipange kupangua ushadi,sio kupinga mashahidi sijui huyu anatoka kyela kafikaje Arusha,mteja wake atazama
 
Upi huo? Mbona sioni? Nafuatilia kila siku kwamba labda nitapata, lakini hadi leo sijaona mfano - mawasiliano, vilipuzi na mikakati au matayarisho ya 'kula njama kutendo vitendo vya kigaidi'. Naomba mnisaidie, labda ni mimi tu nashindwa kuelewa vizuri ushahidi unavyojieleza.
Upo sahihi kabisa mwenyewe natafuta uhalisia wa makosa ya kula njama kutenda ugaidi sijaona zaidi naona tu matayarisho ya serikali na mawakili wake kuwapa watu makosa wasio yajua hawa wanaokuja na vi post vyao wametumwa kupima upepo wa wananchi katika hili kujua support yao mtandaoni ila wao wenyewe wanajua ni uongo wanaandika
 
Back
Top Bottom