Yaliyojiri Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Uhujumu Uchumi na Rushwa, kesi ya Mbowe na wenzake 3 - Kesi imeahirishwa hadi Nov. 29 2021

Nacheka vile judj anahangaika kutafuta gaps na kuingilia sn kwenye kila hoja za upande wa utetezi. Yaani hatumii tu neno Objectuon lakini, kinachofanyika ni kama vile refa tutoa penat halafu unataka kufukuA na goli kipa kabisa asikae golini. Sioni akihangaika sn na maelezo ya washtaki.

Pia sijamuelewa anaposema nyie mpo huko, ila mimi nipo huku...'hamjui'.. Sijajua anateseka na kitu gani pale alipokaa. Ni kama ananena kwa lugha.

Sent from my TECNO CC7 using JamiiForums mobile app
 
Kesi inayomkabili Mbowe na wenzake 3 inaendelea mahakani ambapo upande wa washtakiwa wanatoa ushahidi, abdalah Mohamed Ling'wenya anaendelea leo.

Kujua kesi ilipoishia, soma: Yaliyojiri Mahakamani kesi ya Mbowe na wenzake: Upande wa Utetezi waanza kutoa ushahidi. Kesi yaahirishwa mpaka 26 Novemba, 2021

========
UPDATES:


Jaji ameingia

Kesi namba 16/2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa

WS Robert Kidando: Mh Jaji Ikupendeze naomba Kumtambulisha

Pius Hilla
Abdallah Chavula
Jenitreza Kitali
Nassoro Katuga
Esther Martin
Tulimanywa Majige
Esther Martin

Wakili Peter Kibatala anatambulisha Jopo la Mawakili wa Utetezi

Jeremiah Mtobesya
John Mallya
Fredrick Kihwelo
Dickson Matata
Michael Mwangasa
Khadija Aron
Evaresta Kisanga
Maria Mushi

Jaji: anaita washtakiwa Wote wanne wanaitikia

WS Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya Mapingamizi ya Kisheria, na ataendelea Mr Chavula

Jaji: Sijawauliza Upande wa Utetezi kama Mpo tayari

Kibatala: Tupo tayari Mheshimiwa Jaji

WS Abdallah Chavula: Mheshimiwa Jaji kwenye Hoja ya Chain of Custody ni Hoja yetu Kwamba Shahidi ameshindwa Kuitengeneza kwa Ruhusa yako Mheshimiwa Jaji Naomba nipatiwe Kielelezo Mheshimiwa Jaji Hoja hii ipo katika Maeneo Mawili

Eneo la Kwanza Shahidi Katika Ushahidi Wake ameeeleza Mahakama Kuonyeshwa Barua hiyo, La Pili Shahidi ameeleza za Mahakama Kwamba Alimpa Maelezo Wakili wake Fredrick Kihwelo aandike Barua hii, Barua hii inaonekana Imeandikwa na Wakili Peter Kibatala

Mahakama haijaelezwa Barua hii Imetoka Vipi kwa Wakili Peter Kibatala na Kumfikia Shahidi Siku ya Jana.. Katika Mazingira ama Msingi uliowekwa na Shahidi, labda Vinginevyo Wakili Peter Kibatala aende pale (Kizimbani) akatoe Ushahidi Wake wa Namna ya Barua hii ilovyotembea

Mpaka Kufika Kwa Kamanda wa Polisi Wa Mkoa wa Kipolisi Ilala na Kurejeshwa hapa Mahakamani Kwa ajili ya Kutolewa Kama Kielelezo.. Walau hapo tunaweza Kusema Chain Imekuwa Established.. Lakini kwa Hali Ilivyo hata yeye Mwenyewe awezi Kwenda Kutoa Ushahidi, Kwa hiyo Mnyororo Wa Uhifadhi wa Nyaraka hii, Kuanzia ilipopokelewa Kuanzia Kwa Kamanda Wa Mkoa wa Kipolisi Ilala Mpaka Kumfikia Shahidi Jana.. Mwenzetu Matata Ameshindwa Kumuongoza Shahidi Wak

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji kama tulivyo kwisha Zungumza Jana, Tuna rejea tena tuliyikwisha yasema Jana, Kielelezo Hicho Sicho ambacho Shahidi anataka Kukitoa. Shahidi anataka Kutoa Barua aliyompelekea Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ilala.`

Barua anayotaka Kutoa Ina muhuri wa Mahakama Kuu, Divisheni, Barua anayotaka Kutoa ina Muhuri Wa High Court Of Tanzania, Corruption and Economic Crimes Division, Kwa hiyo ni Barua tofauti.. Jaji: Sijaelewa hebu rudia.....

WS Abdallah Chavula: alichokisema Kwamba Barua aliyokuwa anataka Kutoa Ina Muhuri Wa Mahakama Kuu Division, Lakini Barua anayotaka Kuitoa ina Muhuri Wa High Court Of Tanzania, Corruption and Economic Crimes Division.. Hivi ni Vitu Viwili tofauti..

Na siye tunasema Ama ni Hoja yetu, Ule Mnyororo Wa Uhifadhi Kwa hali hii Umekatika, Pasipo Kuwa na Maelezo ama Ushahidi Hapa Mnyororo umekatika Wa Uhifadhi.. Na kukatika Kwa Mnyororo wa Uhifadhi Unaenda Kuathiri Authentic ya Kielelezo..

Wakili wa Serikali: Na Kwa Nyaraka inayojileza ni, Nyaraka iliyopelekwa kwa Naibu Msajili, Haijaelezwa wala Kutolewa Ushahidi Mbele ya Mahakama Yako.. Ni nani haswa aliyekabidhiwa Nyaraka hii na Msajili Baada ya Ku Acknowledge Kupokea.. Na huyo aliyekabidhiwa Nyaraka hii Kwa Mheshimiwa Naibu Msajili alifikisha Kwa Namna gani Kwa Shahidi.. Mheshimiwa Jaji katika Hatua hii Mahakama yako Ilipaswa ipatiwe Ushahidi ana Shahidi Hapa, Yenye Kuonyesha Kielelezo hicho baada ya Kutoka Kwa Msajili Kilikuwa Katika Miliki ya nani na Yeye kilimfikiaje

Kwa hiyo hata Kama hiki Kielelezo Ndicho Kilichopelekwa Kwa Kamanda Wa Polisi Wa Mkoa wa Kipolisi Ilala, Bado Mnyororo wake wa Uhifadhi Una mapungufu

Mheshimiwa Jaji Kwa Hoja Hizo tunaiomba Mahakama Yako isipokee Kielelezo hiki kwa Sababu Misingi Ya Uhifadhi ya Kielelezo hiki kuanzia Ilipotoka Kwa Mheshimiwa Naibu Msajili Mpaka Kumfikia Shahidi hapa Mahakamani Siku ya Jana

Na vivyohivyo Misingi ya Uhifadhi Ya Kielelezo Hiki kutoka kwa Kamanda wa Polisi Wa Mkoa wa Kipolisi Ilala Mpaka Kumfikia Shahidi Siku ya Jana, Haijaelezwa kwa Bayana

Haijawekwa Wazi, Tunatambua ni Kanuni ya Sheria, Chain of Custody haiwezi Kuwa Established, na Mahakama Ita Determine hilo Mwisho wa Shauri Lakini Kanuni hiyo haina Maana kwamba wakati wa Shahidi anatoa Ushahidi Wake as ieleze namna Kielelezo hicho Kilivyo Mfikia Mikononi Mwake

Wakili wa Serikali: Tunaielekeza Mahakama Katika Shauri la DPP Vs SHARIF MOHAMMED ATHUMAN AND SIX OTHER.. Ambalo Jana tulielekeza Mahakama Kuanzia Ukurasa wa 8 Mpaka Ukurasa wa 10, Hivyo basi Kwa Hoja Hizo tunaiomba Mahakama isipokee Kielelezo Hicho

Mheshimiwa Jaji Naomba Nielekee Kwenye eneo la RELEVANCE Moja ya Vigezo Vya Upokelewaji Wa Kielelezo Ni RELEVANCE kwamba Kielelezo Lazima Kiwe Relevant..

Na hii imebainishwa akatika Shauri la DPP Vs SHARIF MOHAMMED ATHUMAN AND SIX OTHER Kwenye Ukurasa wa Saba, Aya ya Tatu Mpaka Ukurasa wa Nane Aya ya kwanza

Na katika Shauri hilohilo Katika Ukurasa wa Saba, Aya ya Pili Mahakama ilisema Kwamba Kigezo hiki pamoja na Vingine Nilivyo taja Vinatumika hata Kwenye Ushahidi huu ulipo Hapa Mahakamani Shauri hili Dogo Lililopo Mbele Yako ni linamuhusu Mohammed Abdilah Ling'wenya

Dhidi Yetu sisi Jamhuri..Na Dhidi ya Mshitakiwa wa kwanza, Wa pili na Wanne.. Barua hii Kwa namna Ilivyo na Kwa namna Ilivyoandikwa inamuhusu Freeman Aikael Mbowe Na hata aliyeandika amebainisha anamwakilisha Freeman Aikael Mbowe..

John Mallya: OBJECTION Mheshimiwa Jaji Sisi Maafisa Wa Mahakama Kuu, Tunawajibu wa kuisaidia Mahakama Kuu, Napinga anachokifanya Kaka Yangu dhidi ya Amri yako ya Jana na Nina hakika Mahakama italinda hadhi yake.

WS Abdallah Chavula: Mheshimiwa Jaji Hapa tunatizama suala la RELEVANCE na Nilichofanya hapa Nikuzungumza Ushahidi, Na Mheshimiwa Jaji Kuna Kifungu cha 7 cha Sheria Ya Ushahidi

Jaji: Soma Inasemaje

Wakili wa Serikali Abdallah Chavula ANASOMA

Wakili wa Serikali: Sasa Mheshimiwa Jaji Unawezaje Kutaka Kutengenisha na Kilichotokea

Kibatala: Mheshimiwa Jaji Mahakama Ilishatoa Order, Pili anapotosha Mahakama, Anasoma Kifungu Cha 7 Kuhusu Ushahidi ambao Umeshatolewa.. Hapa anachofanya ni Jambo tofauti.

Mtobesya: Mheshimiwa Jaji Hicho Kifungu Kinaongelea Ushahidi Na hapa tunaongelea Kuingiza Ushahidi.. That Piece of paper tunaomba Kuingiza Mahakamani.

Jaji: Umeelewa Mr. CHAVULA Hoja zao?

Wakili wa Serikali: Mh Jaji Hawa Hoja, Hili siyo Jalala Kwamba Wanataka Hapa Mahakamani yaletwe yote Mtu anasema Kwamba hapa Hatuongelei Ushahidi, Sasa tunaongelea Nini? Kifungu kimesema Vizuri kwamba Ili Kielelezo kitolewe lazima Kiwe Relevance na Hapa Mahakamani hatuwezi Kuingiza MATAKATAKA

John Malya: kwanza Mimi Niliongelea Kwamba hairuhusiwi kuiongelea CONTENT...

Jaji: naomba nitoe Maamuzi Sasa, Kutoka Upande wa Utetezi Mmeamka Mawakili 3, Mallya umezungumzia Kuhusu Kutoingia Ndani ya Barua (content), Mr. Kibatala akasema Kwamba Kifungu Kikichonukuliwa siyo sahihi, Mr. Mtobesya amezungumzia Kuhusu hatujaingiza Ushahidi bado..

Sasa Basi Mahakama inasema Kwamba Hakuna Namna utaelezea Relevance halafu usiingie Kwenye Content na Huo Ndiyo Msimamo wa Mahakama.. Kwa namna unavyofanya Mr. Chavula, Unapinga Kuingiza hiyo Barua, lakini unataka Kuingiza Ushahidi huo Kwa namna Nyingine..

WS Abdallah Chavula: Nashukuru Mheshimiwa Jaji...... anaendelea Sasa

Mheshimiwa Jaji Ukiangalia Kwa namna ambayo Shahidi ameshasema Kwamba alitaka Kupeleka Barua kwa Kamanda wa Polisi Wa Mkoa wa Kipolisi Ilala..

Jaji: NAONA KAMA UNA RUDIA TENA

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji ni Maoni yetu Kwamba Kielelezo Hiki ni tofauti Na Shahidi anachotaka Kuzungumza.. Kilichopo Mbele Yako ni Shahidi, Mshtakiwa Wa Tatu Kutoa Maelezo ya Barua kwenda kwa Kamanda Wa Polisi Wa Mkoa wa Kipolisi Ilala

Kwa Mujibu wa Kifungu Cha 7 Cha Sheria ya Ushahidi Sura ya 6 Kama Ilivyofanyiwa Marekebisho Mwaka 2019.. Tulitegemea uletwe Ushahidi Wa Hicho alichotaka Kusema, lakini Kinacho letwa kina kinzana na hicho na Ndiyo Maana tunasema Kielelezo hiki Siyo Relevant

Kwenye Hili tunaielekeza Mahakama Kwenye Mashauri yote Mawili tuliyokuwa tunaielekeza Mahakama Kuanzia Siku ya Jana Mpaka leo.. Mheshimiwa Jaji Naomba tuelekee kwenye Hoja yetu ya FOUNDATION Mheshimiwa Jaji ili Kielelezo kiweze Kupokelewa,

Ni lazima Msingi ama Foundation ya Ushahidi huo Ijengwe.. Tulirejea Ushahidi Uliotolewa na Shahidi Siku ya Jana, Kwa Kumpa Maelekezo Wakili Fredrick Kihwelo na Kuonyeshwa Barua hiyo Jana.. Ni Maoni yetu Kwamba Wenzetu Wameshindwa Kutengeneza Foundation

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Kama Tulivyo kuwa atunaielezea Mahakama hapo awali, Chanzo Cha Nyaraka hii si yeye (anamnyoshea Kidole Shahidi) Wala Siyo wakili wale Fredrick Kihwelo.. Bali Chanzo cha Nyaraka hii ni Adverse party Kwenye hii Kesi

Ambaye Mwisho wa Siku Kama Kielelezo hicho Lita pokelewa atafanya Cross Examination..

Kibatala: OBJECTION. Sijui Kwanini Chavula anafanya Hili analo fanya, Anajivika Joho Jipya, suala la Conflict of Interest.. Kwanini sasa asiombe Ruhusa ya Hoja Mpya ili Ijadiliwe pia.

WS Abdallah Chavula: Mheshimiwa Jaji hata tusipoongelea lakini lipo wazi

Jaji: Haya Jibu Hoja Sasa

WS Abdallah Chavula: Mheshimiwa Jaji sisi tunasema Tupo sahihi lakini Kwa Kukupunguzia wewe Mzigo basi Naondoa hilo

JAJI: Nashukuru Kwa Kunipunguzia Mzigo

Wakili wa Serikali: Mhe Jaji Tunapo zungumzia hili tunarudi Kulekule tulipoku a tunazungumzia Hoja za Competence Na tunaielekeza Mahakama kwenye shauri la DPP Vs SHARIF MOHAMMED ATHUMAN AND SIX OTHER Kwenye Ukurasa Saba, Aya ya Kwanza Kuanzia Mstari wa nne Mpaka Mstari Wa Mstari Wa Saba

Ambapo Mahakama alisema Ilikuweza kumeet Test ya Liability, Ni lazima Foundation ya Ushahidi Iwe imejengwa, Na ukashindwa Kutengeneza Foundation, Athari yake inaenda Kuathiri Competence Ya Kielelezo, Hivyo Mheshimiwa Jaji, Hata Foundation ameshindwa Kutengeneza Shahidi

Kwa hiyo Kwa kigezo Cha Kushindwa Kutengeneza Foundation, Tunaomba Mahakama Isipokee Barua hii, Kwa Sababu Barua hii ni Incompetent, Mheshimiwa Jaji naomba niishie Hapa, Nimuachie Mwenzangu Pius Hilla..

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Nianze Kusema Kwamba nayaunga Mkono Mawasilisho yote ambayo Mr Chavula amefanya. Mheshimiwa Jaji Nita Argue Generally Kwenye Mapingamizi yetu. Mheshimiwa Jaji Shahidi aliyepo Kizimbani, alishindwa Ku authenticate Barua Au Kielelezo

Kwamba Authentication Ilipaswa ilifanyike kabla ya Kuomba Kuingiza Kielelezo, Kwa Mujibu Wa Kesi ya SHARIF MOHAMMED authentication ni Suala la Msingi, na Shahidi hajafanya hivyo.

Mheshimiwa Jaji Vigezo alivyo eleza Kwamba Barua Nitaitambuaje, Na alipoonyeshwa Barua alisema ametambua Signature ya Kibatala, lakini Hakuwa amesema Kwamba na Utaalamu gani, aliona Lini na wapi

Lakini alishindwa Kueleza Features za Barua, Hakuweza Kusema Reference namba za Barua hiyo, Kitu Pekee alichokitaja Kwamba angeweza Kutambua Kwamba Barua hiyo Ina jina lake.

Mheshimiwa Jaji Ni Submission Yangu Kwamba Kwa Mazingira tulinayo Jina lake Pekee haitoshi Ku authenticate Nyaraka hiyo, Halitoshi Kwa Sababu Yeye siyo Mwandishi Wa Barua hiyo wala kumuelekeza Kibatala Kufanya hivyo, alichofanya ni Kumuelekeza wakili wake Fredrick Kihwelo

Hakuna alipo Sema ni Wapi alikaa na hiyo Nyaraka, Kwa Maneno Mengine Hana Knowledge na Kilichopo ndani. Yeye siyo Mmiliki Wala Siyo Mwandishi. Hakuna Mahala ameeleza Mahakama kwamba amejiridhisha. Hakuna Ushahidi Wa Namna hiyo Mheshimiwa Jaji, Jina Pekee Haitoshi.

Wakili wa Serikali: Kwa sababu haja eleza Barua hii Imemfikaje, Kwamba Hakulay hiyo Chain Of Custody wala Foundation, Kwa hiyo Mheshimiwa Jaji Kwa namna hiyo Shahidi Ni Incompetent na Kielelezo ni Incompetent, Mheshimiwa Jaji Wakili Chavula ameeleza Vizuri Suala la Chain of Custody

Ni Maoni yangu Kwamba Mbali na Document lakini hata Maombi ya Mdomo haya apply hapa, Mheshimiwa Jaji Kwenye Oral Chain, Kwamba Kile Kinachozaniwa Kuwa Chenyewe yani ASSURANCE Mheshimiwa Jaji Kwenye Mazingira ya barua hii ASSURANCE haipo

Shahidi Amesema Kwamba Barua ambayo yeye alitolea maelekezo iandikwe ni Kwenda Kwa RPC Ilala, Maana yake Ilipaswa Kuonekana Nakala Barua hiyo kwenda Kwa RPC Ilala

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Samahani, Nilisikia Kwamba Kabla ya Mr. PIUS HILLA Kuongea Kuna Maelekezo fulani uliyatoa, Je ilikuwa ni OFF RECORD au AMRI fulani ya Mahakama?

Jaji: ilikuwa ni OFF RECORD lakini Bado Malekezo yapo palepale..

WS Pius Hilla: Mheshimiwa Jaji Mwenzangu alizumgumzia Kuhusu Mengine Mimi nazungumzia Kuhusu Assurance..

Jaji: Sawa lakini Usirudie aliyozungumza Mwezako

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Kwa hiyo nilikuwa na zungumzia Kuwa assurance Ilitakiwa Kuwa Oral kutoka kwa Shahidi.

Mheshimiwa Jaji Hilo halikufanyika, Na Kwenye hilo tunarejea Shauri la YUSUF MASALU AND THREE OTHERS Vs REPUBLIC kesi Namba 163 ya Mwaka 2071 katika Ukurasa wa 1 Mheshimiwa Jaji Kwa a Mujibu wa Prison Standing Orders, order namba 685 Naomba nisome!

WS Pius Hilla anasoma, Mheshimiwa Jaji hizi ni Standing Order za Mwaka 2003

Jaji: Sasa nini Kilichopo kwenye hiyo order Kwamba Mawasiliano yoyote yaliyofanyika, Yalipaswa Kufanywa kupitia Kwa Maafisa wa magereza (prison Incharge)

Kwamba Katika Mahakama Hakuna Ushahidi Kwamba Nyaraka Hili ilipita kwa officer Incharge ambapo Shahidi anahifadhiwa.. Hakuna Pointa kwa Muda wowote ule Kwamba Nyaraka hii Inafahamy kwa Maafisa wa Magereza.

Wakili wa Serikali: Maana yake Reliability ya hii Nyaraka Mheshimiwa Jaji Inakosekana, Kwa kuwa Nyaraka hii haiko authentic Basi inastahili Kutupiliwa mbali. Kwa Namna Nyingine hii Mahakama inapaswa Kupokea Ushahidi Unaofuata Utaratibu, Mahakama haiwezi Kupokea Nyaraka inayokuja kinyemela

Mheshimiwa Jaji sisi tunasema Kwakuwa huyu Shahidi Yupo Chini ya Magereza, Basi Ushahidi Wake umepatikana Kinyemela, Mheshimiwa Jaji Kwa hayo Machache naomba Kuishia Hapo, Nisiichoshe Mahakama..

Na Wenzangu wameniambia kwamba hawana Cha Kuongeza, Kwa hivyo tunaomba Mahakama Yako Ikubaline na Mapingamizi tulivyo weka, Kwambia Shahidi Siyo Competent, Chain of Custody Haipo, Kielelezo siyo Relevant na Hakuna Foundation iliyojengwa, Naomba kuwasilisha.

WS Pius Hilla Anakaa Chini.

Mtobesya: Mheshimiwa Jaji Kama tulivyo Sema Jana, Tuna Unga Mkono Shahidi aliyepo Kwenye Kizimba cha Ushahidi Kwamba Kielelezo alichotoa Kipokelewe, Mheshimiwa Jaji naomba Ile Barua...

Mtobesya: Kwenye Mahakama Ya Rufani na Kwenye Mahakama hii pia, Ilisha Sema Kwamba Ili Kielelezo Kiingie Mahakamani tunapaswa tuangalie Competence ya Shahidi na Kielelezo.. Iangalie pia Relevance Katika Level hi ya Adminsibility, Na Materiality Ya Level hii ya Adminsibility

WS Abdallah Chavula: Kwamba, Jana Waliomba Kutoa Sababu, Mahakama haikusema Wafanye Submission, Kwa namna hiyo sasa anaanza Kufanya Submission, Naamini Jana Uliposema Jana Watoe Sababu, Siyo Kwa Submission

Mtobesya: namimi sasa Mheshimiwa Jaji nitaomba Unielekeze, Kwamba Nawezaje Kutoa Sababu bila Kufanya Submission au Niondoe Neno "I submit" niweke "I reason"

Jaji: Bwana Robert Kidando, Tuliongea hili, wewe unaonaje!?

WS Robert Kidando: Nadhani Watoe Sababu tu lakini siyo Kwa Kufanya Submission

Jaji: nafikiri tunakubaliana Kwamba Unatoa Sababu

Mtobesya: Sahihi Kabisa

Jaji: Najaribu Kumtizama Line Yako kwa namna unavyo Submit, Nadhani Ungejikita kwenye Barua Yenyewe. Nafikiri Ungefanya hivyo bila Kujibu Hoja zao, Najua Mnapata nafasi ya Kuzungumza kwa sababu huenda Barua hiyo inagusa Washtakiwa Wengine.. Kwa namna hiyo naomba Usijibu Hoja zao.

Mtobesya: nilicho kuwa nasema Mheshimiwa Jaji, unless Nitakuwa nafikiria zaidi ya Mipaka yangu, Nitakapo kuwa nataja Sababu lazima niweke Rejea,

Jaji: Sijasema usiweke Rejea, ila jitahidi Usijibu Hoja zao tafadhali

Mtobesya: Nianze Kwa kusema Shahidi Ni Competent Kwa sababu kwa Ushahidi Wake amesema alionyeshwa...

Wakili wa Serikali: OBJECTION Mheshimiwa Jaji sisi tunapinga hilo

Kibatala: Nisamehe Mheshimiwa Jaji ulipomuinua Mr. Kidando nilifikiri na Mimi ungeniinua.

Kibatala: Na tatizo Kubwa kwamba huyu Mr. Chavula huwa hafiki kwenye Briefing, ambapo tumekubaliana na Mr. Kidando na Yeye Nimeona kaja hapa Kayakana ambayo tumekubaliana..

Jaji: ni Maoni yako lakini, Hajayakana

Kibatala: Sasa Kwa sababu Hakuwepo Hajui tulichozungumza Kwa sababu Kule alitoa Mpaka Mfano ya Kesi Ofisini kwako kwenye Briefing, Tukakubaliana kwamba Hauwezi Kuwazuia watu Kuongea...

Jaji: napata wakati Mgumu kwa sababu Sisi sote tunapigania Haki za Watu wetu, Na Kwamba tumesema Kwamba Mawakili Wote Wataongea na Wakili Wa Mshtakiwa Wa Tatu atakuja Kujibu Hoja, Kwa sababu Wewe na Upande wa Utetezi mpo Upande Mmoja..

Mtobesya: Kwamba Sisi hapa Kwa namna Moja au Nyingine Hatupo Kwenye Joint Defense, Haki yangu niliyo nayo sio kusimama Upande Mmoja na Serikali, NA Mshtakiwa Wa Pili, watatu na Wanne, Kwa sababu nikinyamaza inaweza Kuathiri Mteja wangu.....

Jaji: Hapa issue ni Extent Kwa sababu Lazima tufike Wakati Hoja ya Mr. Kihwelo ndiyo itakuwa Hoja yake Kujibu..

Mtobesya: Kwa wakati gani nitasema Kwamba Shahidi Yupo Competent, labda kana Kwamba ninachokifanya ni an Academic Exercise??

Jaji: na Mimi Sasa Nakuelekeza kwamba Unachokifanya kisivuke Mipaka

Mtobesya: Mheshimiwa Jaji Vipi Kama Ningepinga, pia ningezuiwa Kujibu?

Jaji: Ungewasilisha

Mtobesya: Kwanini sasa Ninapounga Mkono Nizuiwe Kujibu?

Jaji: Wangejibu kwa nafasi yao

Mtobesya: Vipi Kama nitavuka Mipaka yangu ya majibu watafanya nini?

Jaji: Ndiyo kazi yangu Sasa, Kuzuia na Kukurudisha Kwenye Mstari, Mimi napata Wakati Mgumu Kwa Sababu Nipo hapa Mbele, Nyie Mko huko hamjui

Mtobesya: Mhe Jaji, Je naruhusiwa Kuongelea Ushahidi wa shahidi?

WS Abdallah Chavula: hawaruhusiwi

Jaji: Kwanini hawaruhusiwi? Nafikiri Wanaruhusiwa

WS Abdallah Chavula: Mheshimiwa Jaji Ngoja tuwaache tu lakini Hawaruhusiwi

Kibatala: Mheshimiwa Jaji....

Jaji: Mr. Kibatala Naomba Ukae, Mtobesya Endelea tafadhali...

Mtobesya: Mheshimiwa Jaji Shahidi Ni Competent Kwa sababu Shahidi Kuna Mambo ameyasema akiwa Kizimbani Kwamba Kwenye Kielelezo hicho Kuna namba ya kesi

Alisema Kwamba Kwenye Barua Kuna Majina, Tuna Assume Majina yake, Alisema Kuna Sahihi Wa Wakili aliyemtaja.. Alisema kwamba Kuna Muhuri.. Kabla ya kwenda Mbali, Vitu hivyo Vinne vipo, Kuna namba ya Kesi, kuna Majina yake na Muhuri wa Mahakama Kuu

Ni Wasilisho letu Kwamba Vitu alivyotaja Vinaonyesha Kwamba yeye Ame authenticate na Inaweza Kuingia Kwenye Ushahidi Angalau Kwa wakati huu wa Admission..

Mtobesya: Niende Kwenye Relevance, Bila Kwenda Kwenye Content, Ukiangalia Ushahidi Wa shahidi, Nyaraka hii ni Relevant Ku approve the fact kama Shahidi Wa Pili Upande Wa Mashtaka alifanya alichokisema Mahakamani.. Hiyo ni Kwa Relevance

Suala la Materiality Nyaraka Inaweza Kusaidia Kufanya Maamuzi Kama Shahidi Wa Pili Upande wa Mashtaka, Kama alifanya alichokisema hapa Mahakamani, Naomba nirejee kesi ya DPP VS MIZIRAHI Rufaa ya Jinai namba 493 ya Mwaka 2016 iliyokuwa inasikilizwa Dar es Salaam

Aya ya Kwanza Ya Ukurasa wa Kwanza.. Kwenye Paragraph hii Mahakama ya Rufani ilisema Kwamba hata Kwa Kuona Kielelezo Shahidi anaweza Ku' Acquire Knowledge Ipo Kwenye Ukurasa wa Kwanza.. Pia Kuna Maamuzi yaliyotumika kwenye Mahakama hii ya DPP VS SHARIF MOHAMMED ATHUMAN AND SIX OTHERS kesi namba 74 ya Mwaka 2016.. Mwisho kabisa Mheshimiwa Jaji hii siyo Mara ya Kwanza Mahakama Inaitwa kutoa, Maamuzi, Kuna Barua ya namna hii Ililetwa na Mapingamizi yaliletwa ambapo Mahakama Iliamua Barua ile iingie kama Kielelezo

Mtobesya: Tunaomba Kwa namna ileile Vigezo vilivyotumika Kupima Adminsibility ya Kielelezo Kile ndiyo itumie Kupima Adminsibility ya Kielelezo Hiki Kuingia Mahakamani, Ni hayo Mheshimiwa jaji!

John Mallya: Mimi pia Kwa niaba ya Mshtakiwa wa Pili Naunga Mkono Mahakama Ipokee Nyaraka hiyo Kama Exhibit. Na Bahati Mbaya nimeongea Baada ya Mtobesya Kuongea, Na hivyo naomba Ku' Adopt Sababu za Mtobesya

Kwamba Mahakama hii Ilikutana na Mazingira haya haya pale ilipopokea Kielelezo Namba 1 cha Kesi Ndogo, Kwa Maana hiyo naomba Mahakama itumie Vigezo vilevile Kukubali Kielelezo Kuingia Mahakamani, Kwa Ufupi Mheshimiwa Jaji ni hayo tuh

Wakili Peter Kibatala: kwa niaba ya Mshtakiwa Wa Nne tunaunga Mkono Barua Ipokelewe, Sisi Mshtakiwa Wa Nne Tumesikia shahidi Akisema Alieleza kwamba Alielekeza Barua iende kwa RPC ilala, Alitambua Kwa Kiwango Chake Kuna Muhuri Wa Mahakama kuu Divisheni

Nilisikia Pia kisema alitoaa Instruction Kwa wakili Fredrick Kihwelo Akiwepo Kiongozi wa Jopo la Mawakili wa Utetezi, Nimlisikia pia shahidi alisema alionyeshwa Barua hiyo na Wakili wake Fredrick Kihwelo na akiwepo Kiongozi wa Jopo la Mawakili wa Utetezi

Nilisikia Pia akisema Kwamba alikuwa na Uwezo wa Kuilewa ile Barua, Nilisikia Alikisema aliomba STATIONERY DIARY ambapo alifafanua Kwa Context yake kijeshi, Nilisikia Pia akisema Kwamba aliomba OB, Nilisikia Pia AKISEMA Kwamba anaitambua Kwa Sahihi na Mihuri.

Kibatala: sisi Washtakiwa wa Nne Tunategemea Kuona Kwamba Mazingira yale yale Kwamba "Pale Barua inapokuwa purported kwamba imekuwa copied kwa Mtu fulani, There is assumption Kwamba Imepokelelewa" Kwasababu hizo nilizo toa ndiyo Maana Naunga Mkono Sababu za Kupokelewa Barua yetu

Wakili Fredrick Kihwelo: Mheshimiwa Jaji ataanza Wakili Dickson Matata halafu baadae nitafuata Mimi..

Matata: Mheshimiwa Jaji Nita Submit In general halafu Wakili Mwanzangu atamalizia.. Mheshimiwa Jaji Jana wakati Wakili wa Serikali Abdallah Chavula Anawasilisha Alianza kwa Kuzungumzia suala la Mshtakiwa Katika Kesi hii Ndogo kwamba hayuko huru.. Na Kwamba yupo Chini ya Magereza.. Na Kwamba Kwa Mujibu wa General Prison orders, Kwamba Chochote anachokifanya Ikiwemo Kuandikwa Barua lazima Bwana Jela ahusishwe..

Ikiwepo Kuwepo Kwa Muhuri Wa Bwana Jela Kuthibitisha, Na akasema Kwa Mujibu wa Barua hii ambayo tunataka iingie Kama Kielelezo Hakuna Uthibitisho huo. Mheshimiwa Jaji ni Wasilisho letu Kwamba Wakili wa Serikali Abdallah Chavula Alishindwa Kutaja Order inayosema hivyo

Matata: Kutokana na Kutokutaja, Ambapo Kimsingi Sisi tunasema Haipo.. Sisi tunaona Kwamba Hoja hii haina Msingi na haina Nguvu ya Kisheria kuweza Kusimama, Mheshimiwa Jaji ni Wasilisho letu Kwamba Uhusiano Baina ya Wakili na Mteja wake ni Privileged one

Jaji: unasema ni wa..

Matata: Privileged One, na Unalindwa na Katiba yetu ya Jamuhuri ya Muungano Chini ya Ibara ya 13 (6b) ya Mwaka 1977 kama ambavyo imekuwa ikifanyiwa Marejeo Mara kwa mara Kwa Kuzingatia Haki hii, Sisi Mawakili Tumekuwa na Haki, Siyo tu tunapo kuwa Mahakamani, lakini pia tunapoenda Magerezani tunaruhusiwa Kuonana na Wateja wetu Siku yoyote..

Matata: Mheshimiwa Jaji Ukisoma Prisons General Orders ambazo Kimsingi Mheshimiwa Jaji, Orders hizo zimelenga Ku Control Uhusiano Baina ya Askari Magereza Wenyewe kwa namna wanavyo fanya Shughuli zao, lakini pia Baina ya Askari Magereza na Watuhumiwa ama Wafungwa

Mheshimiwa Jaji ni Wasilisho letu Kwamba, Hakuna sehemu Zinazuia au zinakataza privilege iliyowekwa Kisheria na Kikatiba Baina ya Wakili na Mteja wake. Sisi tunaoenda Kila Siku au Mara kwa mara Magerezani, Utaratibu unaohusishwa na Bwana Jela Kugonga Muhuri ni wa Namna 2

Moja ni pale Mtuhumiwa au Mahabusu anapotaka Kuandika Barua akiwa Ndani ya jela kwenda Kwa Ndugu,Mahakamani au Kwa wakili wake, Ndipo itahitaji igongwe Muhuri na Ipitie kwa Bwana Jela

Namna ya pili, Mtu anapotoka Nje Na ana Nyaraka ya Kutaka Kumpelekea Mtuhumiwa Kwenda Ndani Kuisaini Hapo Ndipo Bwana Jela atahusika na Watakachofanya Watachukua Ile Nyaraka na Wata type Wao Wa kisha type Kwa Content Zile ile Wataipeleka, kwa Mtuhumiwa ataisaini na Kisha ataigonga Muhuri Kisha wakili utakabidhiwa na Utaondoka nayo...

Matata: Mheshimiwa Jaji Ukienda na Nyaraka Nyingine ambayo haihitaji Saini ya Mteja wako, hawaigongi Muhuri, Wanacho fanya ni Kukagua na Kujiridhisha kwamba ipo Kisheria.. Hapo namaanisha Mheshimiwa Jaji Kwamba haina Content ambazo Zina Illegality (ambazo zinavunja Sheria)

Sasa Mheshimiwa Jaji ni Ushahidi Wa shahidi aliyepo Kizimbani, amesema Kwamba yeye alionyeshwa Barua, na Wanasheria wake, Naomba Kuweka Sawa hapo, Na Wakili wake, akiwepo Wakili Kiongozi wa Jopo la Utetezi, Jana hapa Mahakamani

Na Hakupewa Kukaa nayo Kwa Maana awe nayo Muda wote, Alionyeshwa tu. Mheshimiwa Jaji Kwa Kusema alionyeshwa Hapa Mahakamani, Hoja ya Kuwa Barua ile Ilitakiwa iwe na Muhuri Wa Magereza na Kupitia Kwa Bwana Jela Inakosa Mashiko

Matata: Mhe Jaji ni Wasilisho Letu pia Kwamba, Mteja anapokuwa Kwenye eneo la Mahakama, anakuwa na Haki ya Kuonana na Mawakili wake na Kuwasiliana na Mawakili wake, Kinachotakiwa ni kuwaomba Askari Magereza Kupitia Kwa Kiongozi wao wa Siku hiyo, Kuweza Kuwasiliana na Mteja wako

Wasilisho letu haihitaji Mpaka Twende kwa Bwana Jela, Ndiyo Maana Mhe Jaji Wakiwa hapa Mahakamani, Sisi Mawakili Tumekuwa na Haki ya Kuwasiliana kwa Vimemo, na Hatupiti Kwa Bwana Jela.. Na Ndiyo Maana wakati wa Break ya Mahakama sisi Mawakili Tumekuwa na Haki ya kuwasiliana nao

Matata: Mheshimiwa Jaji Nikukumbushe Kwamba Jana, Asubuhi Tulikuwa tunajua Upande Wa Jamhuri wanakuja Kuendelea na Ushahidi, Lakini Wakaja na kufunga Ushahidi wao, Tunajiuliza Je tungewezaje Kukaa na Shahidi na Kumuandaa Shahidi Kuja Kutoa Ushahidi Kama tusingepata nafasi?

Matata: Kama hiyo ilifanyika Chini ya Uangalizi Wa Askari Magereza, Ambapo Kimsingi Inaruhusiwa, Je kuna Kosa gani Shahidi Kuonyeshwa Barua ambayo yeye alitoa Instructions za Barua hiyo Kuandikwa kupitia Wakili wake akiwa pamoja na Wakili Kiongozi wa Jopo la Mawakili wa Utetezi?

Matata: Mheshimiwa Jaji ni Hoja yetu Kwamba Pingamizi hili halina Mashiko kwa Sababu haliangukii kwenye Test ya Adminsibility. Ambazo Test hizo zinataka anayetaka Kuomba (tender Documents) Kuingia Kwa Nyaraka awe Competent, Relevance na Materiality

Mheshimiwa Jaji tukija kwenye Suala la Competence, Ni Wasilisho letu Kwamba Shahidi na Barua aliyokwisha Kui tender ni Competent.. Hii Inatokana na Ukweli Kwamba Shahidi yeye Ndiye akiyeanzisha au aliyetoa Instructions kwa wakili Fredrick Kihwelo pamoja na Wakili Kiongozi wa

Jopo la Mawakili wa Utetezi mara baada ya Shahidi Wa Serikali PW2 Askari Msemwa Kutoa Ushahidi Wake na Kusema Kwamba Mshtakiwa Namba 3 pamoja na Mwenzake Adam Kasekwa Walipelekwa Central Police Dar es Salaam Tarehe 07 August 2020 Na Kwamba Yeye Msemwa Ndiye aliye wa pokea na Kuwajaza Kwenye Detention Register, Kitu ambacho yeye (Mohammed Ling'wenya) anapingana nacho, Akatoa instructions za Barua Kuandikwa kwenda kwa RPC wa Ilala, akasema Lengo la Barua ile ilikuwa ni Kutaka Kupata Vitu 3 ambavyo alivitaja.

Matata: Kwamba apate Movement Order ya huyo Askari Msemwa, Inayoonyesha alivyotoka Central Police Dar es Salaam Kwenye Kituo cha Oysterbay, Pia alitaka apate OB ya Matukio ya Siku hiyo, Tatu alitaka apewe Station Diary ambapo yeye alilita Stationery Diary ambayo alifafanua Kifaa cha namna hiyo hiyo Jeshini Kwao Wanaita Roaster.. Na akasema Roaster ni Nini, Kwamba Ni kifaaa Kinachoonyesha Askari kaingia Saa ngapi, Amepewa silaha au Kurudisha silaha na amepangwa wapi..

Na Akaendelea Kusema Kwamba Jana akiwa hapa hapa Mahakamani Alionyeshwa Barua hiyo ambayo yeye aliomba iandikwe na Wakili Fredrick Kihwelo Akiwepo na Wakili Kiongozi wa Jopo la Mawakili wa Utetezi. Mheshimiwa Jaji Nikiwa namuongoza aliweza kutaja Unique Features za Barua hiyo

Na akasema kwenye hizo Unique features alisema Kwamba Kuna Kesi ya namba 16 ya Mwaka 2021, Hakuishia Hapo akasema Pia kuna Jina La Wakili Kiongozi wa Jopo la Mawakili wa Utetezi, Bw. Peter Kibatala, Akasema Kuna Jina La MSEMWA ambaye ni PW2 Kwenye kesi ya Trial Within Trial

Akasema Apia Kuna Muhuri Wa Mahakama, Japo alikuwa anasema Mahakama Kuu ya Division, hatutegemei Kwa Nature ya Shahidi..

WS Pius Hilla: OBJECTION Mheshimiwa Jaji Tunaomba Wakili ajizuie Kusema Vitu ambavyo Shahidi hajasema, Shahidi Hakusema Kwamba Kwa "Nature ya Shahidi"

Jaji: hiyo unapoweka Maoni yako

Matata: nimefuta..

Jaji: Kuhusu kwamba Msemwa Serikali Mnasemaje???

Wakili wa Serikali: Pius Hilla Hakutaja

Matata: alitaja Mheshimiwa Jaji

Jaji: Sawa Mahakama Ita angalia Kwenye Record zake

Matata: lakini Pia shahidi aliweza kutambua Subject matter ambapo alizumgumzia suala la Movement Order, Alizumgumzia suala la OB, na Pia alizumgumzia suala la Station Diary ambayo yeye alikuwa anaita STATIONERY DIARY..

Jaji: Kwa hiyo alisema Stationery Diary au Station Diary?

Matata: alisema Stationery Diary Lakini tunafahamu hakumaanisha Kwamba Diary Iliyo Simama, Ndiyo Maana alifafanua Kwamba Kwa Jeshini Wanaita Roaster. Lakini pia Nilimuuliza suala la Saini ya Wakili Peter Kibatala ameitambuaje..

Akajibu Kwamba Peter Kibatala amekuwa Wakili wao Tangu Mahakama ya Kisutu Kwenye Commital, Na wakiwa huko Walikuwa wanaandika Barua Mara kwa Mara kwa hiyo anaifahamu. Lakini pia tulipokuja hapa kabla ya Mawakili Kujigawa Peter Kibatala alikuwa ni Wakili wake.

Na kaendelea Kusema kwamba Licha ya kujigawa aliendelea Kuwa Wakili Kiongozi wa Jopo la Mawakili

Jaji: alisema hayo Neno Licha?

WS Pius Hilla: Ajizuie Mheshimiwa Jaji yeye Siyo shahidi anukuu bila Kuongeza Maneno

Matata: Mheshimiwa Jaji Sawa nimesikia

Matata: Mheshimiwa Jaji pia alitambua Jina lake na Kwamba Barua ile Ikiwa Copied Kwake, Kwa hiyo ni Wasilisho Letu Kwamba Shahidi ni Competent Kwa Sababu ameonyesha Kwamba ana FULL KNOWLEDGE ya Barua hiyo..

Kwa hiyo Kwa kutumia Kesi ya DPP VS MIZIRAHI ambayo emimeahakuwa a Inatumika Mahakamani hapa, ana vigezo Vya Ku tender (Kuomba) Kielelezo Kikapokelewa Mahakamani Hapa..

Mheshimiwa Jaji Wakati Mahakama Inatoa Uamuzi, Niikumbushe Maamuzi Iliyo yatoa Tarehe 16 November 2021.. Ambapo Ulisema Wakati wa kuipokea Barua, ailiyiletwa na Shahidi Wa Pili Wa Jamhuri Katika Shauri Dogo La Trial Within Trial na Askari Msemwa

Matata: Ambayo Barua ile ilikuwa Inatoka Kwa Naibu Msajili Wa Mahakama hii kwenda National Prosecuton Service, Dodoma ambayo ilikuwa Copied kwa D/C Msemwa Kama ambavyo imekuwa copied Kwa Shahidi Kizimbani

Mahakama ilitoa Uamuzi Kwamba Mtu akiwa copied Kuna a kuwa na Presumption kwamba ameipokea, Mheshimiwa Jaji Kuna Hoja kwamba Barua imeandikwa na Wakili Peter Kibatala

Ni Wasilisho letu Kwamba Shahidi ameweza kulielezea hilo kwa Kusema yeye Mwenyewe alitoa Maagizo kwa wakili wake Fredrick Kihwelo akiwa na Wakili Kiongozi wa Jopo la Mawakili wa Utetezi Bw. PETER KIBATALA,

Na kwamba Fredrick Kihwelo aliliridhia

Jaji: neno hilo alisema?

WS: Abdallah Chavula Mheshimiwa Jaji hakusema.

Matata: Sawa naondoa Hapo,

Matata: Mheshimiwa Jaji Ni Submission Yetu Kwamba tunaona sisi tunaona Sahihi Kwa % Peter Kibatala Kuandika hiyo Barua.. Mheshimiwa Jaji ni Wasilisho letu Kwamba Barua hii ni Relevant kwa Sababu zifuatazo

Moja, Shahidi ameeleza ni Kwanini aliomba Barua hii iandikwe, na akasema Katika Ushahidi Wake Aliomba Barua hii iandikwe ili aweze Kupewa Nyaraka Kutoka kwa RPC Ilala Ili Kuthibitisha au kutokuthibitisha kama Kweli Askari Msemwa ambaye alikuwa ni Shahidi namba 02 katika hii

Kesi Ndogo kama Kweli alikuwa Polisi Central Dar es Salaam na Kama Kweli aliwapokea Mohammed Ling'wenya na Mwenzake kama Kweli aliwapokea Siku hiyo.. Mheshimiwa Jaji sisi tunaona hitaji hili ni Relevant kwenye kesi hii, Sababu itaisaidia Mahakama Kupima kwenye Kesi hii..

Shahidi Hakuishia Hapo, ametaja kesi namba Kitu ambacho Upande wa Mashtaka hawajapinga, Na wala katika Ushahidi wao hawajapinga kwamba Katika Mahakama hii Kuna Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 katika Mahakama hii..

Matata: Mheshimiwa Jaji Shahidi pia alitaja Mshtakiwa Freeman Mbowe, ambaye kimsingi..... Mheshimiwa Jaji naomba kuondoa hicho!

Jaji: nini?

Matata: kuhusu Freeman Mbowe

Matata: lakini Pia Mheshimiwa Jaji Shahidi aliweza ku' Testify kwamba yeye ndiye aliyewaleza wakili Fredrick Kihwelo na Wakili Kiongozi wa Jopo la Mawakili wa Utetezi kuandika Barua kwenda kwa RPC Ilala, Dar es Salaam ili kuwa Kupata Taarifa zinazohusiana na PW2 Kwenye trial within Trial D/C MSEMWA ilikupata information.. Ili kuweza kujiridhisha Na akiwa Kizimbani alithibitisha Kwamba Kweli alionyeshwa Barua hiyo Jana, Ni Wasilisho letu Kwamba Barua hiyo ina Meet kigezo Cha Relevance..

Matata: Mh Jaji Pius Hilla aliwasilisha Juu ya AUTHENTICATION na katika kuanza Hoja yake alisema, Shahidi alitaja Jina la Peter Kibatala.. Ni wasilisho letu Kwamba si kweli Kwamba alitaja Jina la Kibatala Peke yake kwenye Barua na Kwamba Hakuna Features zingine Kwenye Barua

Ni Wasilisho letu Shahidi alitaja Features zingine zaidi ya Jina la Peter Kibatala Kwenye Barua. Alitaja Kesi namba na...

Jaji: Unataka Kurudia kutaja tena

Matata: Ndiyo nataka Kujibu Hoja za Pius Hilla Aliposema Shahidi Hakutaja Features zingine zaidi ya Jina la Peter Kibatala

Matata: Si Kweli Kwa Sababu Shahidi alitaja Kesi namba, Alitaja Majina ya Peter Kibatala, Saini ya Peter Kibatala, Majina yake.. Na Kwamba na rejea pia kumjulisha Wakili wa Serikali Kwamba Mahakama hii Ilishatoa Uamuzi Kwamba Reference namba na Tarehe Siyo Unique Feature Pekee

Niende Kwenye Hoja ya Kama Barua hii Ilipokelewa na RPC Ilala., Mheshimiwa Jaji Hoja hii ni Premature. Kwa sababu hatuwezi Kuzungumzia Kama Ilipokelewa au Haikupokelewa kabla ya Kuzungumzia Barua..

Ni Wasilisho Letu Kwamba ilikuwa lazima tuzungumzie Barua Kisha ndiyo turejee kwamba Barua Imepokelewa au Haijapokelewa.. Hauwezi Kuzungumzia suala la Kupokelewa kabla hatujazungumzia Suala la Barua..

Tungeanza Kuzungumzia Jinsi Barua Ilivyo pokelewa alafu Barua ikaja Kukataliwa Mahakamani. Hiyo Nyaraka ambayo tuseme NI Dispatch itakuwa na (Value) thamani gani.. Na lazima wa take note kwamba Nilikuwa sijamaliza Kumuongoza Shahidi.. Wamejuaje kama tusingeleta?

Matata: Kwa hiyo Mheshimiwa Jaji ni Wasilisho letu Kwamba Hoja hiyo imeletwa Ikiwa PREMATURE. Mheshimiwa Jaji zinapopelekwa Barua sehemu zigongwe Muhuri. Zipo Njia Nyingi za Ku Acknowledge Kwamba Barua Imefika na Kupokelewa

Kwa hiyo Hoja ya kwamba, Barua haina Muhuri siyo ya lazima, na sifahamu Sheria Yoyote Inayosema Kwamba Barua lazima Igongwe Muhuri Kwamba Imepokelelewa,

Kwa hiyo Maombi yetu Kwamba Mapingamizi Ya Serikali yatupiliwe Mbali Kwakuwa Haya Misingi ya Kisheria na Mahakama Ipokee Kielelezo Ch shahidi Wangu Ni hayo tu Mheshimiwa Jaji

Wakili (Fredrick Kihwelo) anasimama..

Jaji: ni Maoni yangu Tu' break kidogo Tukutane baada ya muda gani

Wakili wa Serikali Robert Kidando: baada ya dakika 45, turudi saa 8 na dakika 15

Jaji: Basi tupumzike turudi saa nane na dakika 45

--------

Jaji amerejea Mahakamani

Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa tena

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Kwa Upande wetu Quorum ipo palepale, na Tupo tayari Kuendelea

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Kwa hisani ya Mahakama naomba Kumtambulisha Wakili Nashon Nkungu Mbaye wamebadili Nafasi na Jeremiah Mtobesya Ukiondoa hilo tupo tayari Kuendelea.

Jaji anaandika Kidogo

Wakili Fredrick Kihwelo: Mheshimiwa Jaji awali ya yote naomba Kuunga Mkono yale yote yaliyowasilishwa na Wakili Msomi Dickson Matata.. Na mimi nitakuwa Nayakuongezea Mheshimiwa Jaji Hoja za Mawakili wa Serikali Kwamba Tulikuwa hatujafuata Sheria za Magereza, Ni Wasilisho Letu Kwamba Nyaraka ambayo ipo hapa Mahakamani haikuwahi Kuingia wala Kutoka Gerezani.. Na haya ni Kwa Mujibu wa Shahidi Mwenyewe.

Mheshimiwa Jaji suala la Pili, Wakati Wakili Abdallah Chavula anazungumzia Suala La Competence Ali Site Public Standing Order GN 493 ya Mwaka 2009 na alikuwa Ammended Public Service Standing Order ya Mwaka 2018 GN namba 288

Mheshimiwa Jaji Baada ya hapo naomba niende Kwenye Chain Of Custody, The intent and Purpose of Chain of Custody Principle is to make sure the item is one and the Same..

Kihwelo: Na alieleza namna ya Maelekezo Hayo alivyo Yasimamia na Kuhakikisha Yanatekelezwa.. Lakini pia alionyeshwa Kile alichokiagiza Kwa Maana Barua.. Mheshimiwa Jaji Ni Maamuzi ya Mahakama hii Kwenye Trial within Trial ya PW2 kwamba ilimradi Shahidi ameeleza akwa mdomo namna gani amepata Ushahidi Basi shahidi huyo anaweza Kuaminika.. Lengo la Kupewa Nakala ya Nyaraka ni Mtu ajue na kuwa na Haki ya Kuitumia Nyaraka hiyo.. ni Mawasilisho yetu Kuwa Kwa namna Shahidi alivyosukumwa Kutoa Malekezo kwa Wakili wake na Wakili wa Jopo la Mawakili wa Kwa Namna

Maelekezo hayo yalivyotekelezwa na Namna aliyoonyeshwa Nyaraka hiyo na Namna Ilivyo fika Mahakamani Hapa, Chain of Custody Has been Established.. Mheshimiwa Jaji Wakili Chavula anavyozumgumzia Suala La Relevance, Kwamba Barua hii inakosa na Relevance alizumgumzia Kwamba Shauri hili Dogo no tofauti na Shauri Kubwa.. Ni Wasilisho letu Kwamba Shauri hili Dogo ni sehemu ya Shauri Kubwa..

WS Abdallah Chavula: Mheshimiwa Jaji Sijasema Hivyo Kwamba Shauri hili Dogo ni Tofauti na Shauri Kubwa.

Jaji: namimi nilipata wakati Mgumu, Maana sikusikia akisema hivyo

Wakili Fredrick Kihwelo: Basi Naliondoa hilo Kama Halipo na ni naomba Moja kwa Moja niende Kwenye Foundation na Kwamba Wakili wa Serikali anasema Kwamba Shahidi Hakuweka Foundation.

Kihwelo: Mhe Jaji Shahidi Wakati anatoa Ushahidi Wake alisema Hapa Kwamba akisikia PW2 D/C Msemwa Aliwapokea yeye na Wenzake Central Police DSM. Baada ya Kusikia hayo aliwaelekeza Mawakili wake Kwamba Waweze Ku' establish Kuona Kama Kweli Waliwahi Kufikisha Central Polisi DSM

Mheshimiwa Jaji alisema hapa Kwamba alifuatilia Kujua Kama Mawakili wake Walitekeleza Maagizo Yake, Na Akasema hapa alionyeshwa Barua, Na Mheshimiwa Jaji aliweza Ku Identity, Sahihi, Namba ya Kesi, Muhuri wa Mahakama..

Ni Wasilisho letu Kwamba Shahidi anatoa Ushahidi ambao ana uhakika nao lakini pia Ushahidi anaoufahamu, Mheshimiwa Jaji palikuwa na Hoja pia Kwamba Wao wataaminijie Kwamba Barua Imefika Kwa RPC Ilala..?

Kihwelo: Mheshimiwa Jaji Ni Hoja yetu Kwamba whether or not Barua Ilifika siyo Issue ya Adminsibility. Hoja ya Mwisho Mheshimiwa Jaji Wakili Chavula Alielekeza Mahakama Yako Kwenye Kesi Ya DDP Vs SHARIF MOHAMMED ATHUMAN AND SIX OTHER Kwenye Ukurasa wa 9 na Wa 10

Mheshimiwa Jaji yale yanayozungumzwa kwenye Ukurasa wa 9 na Wa 10 nibTofauti kabisa na hichi Kilichopo Mahakamani.. Mheshimiwa Jaji Kwenye kesi hiyo Shahidi alishindwa Ku Identity Unique Features kwenye Kielelezo..

Wakati Mheshimiwa Jaji Shahidi aliyepo Mahakamani hapa ameweza Ku Identity Unique Features kama Muhuri wa Mahakama, Namba ya Kesi, Jina na Sahihi.. Mheshimiwa Jaji naomba Kuzungumzia suala la Mwisho Juu ya standing Orders ambazo zilikuwa cited na Wakili wa Jamhuri

Jaji: zipi za Public service au?

Kihwelo: Hapana Za Prison, Specifically Walikuwa wametaja Order namba 685 hii inazungumzia Nyaraka zinazo ingia na Kutoka Gerezani Wakati Barua hii haiko Subjected Kuwa hivyo.. Na ilikuwa ni Maagizo ya Shahidi Kwenda Kwa wakili wake na Wakili Kiongozi wa Jopo la Mawakili wa Utetezi, Kwamba Kwa kuwa yeye Yupo Ndani,

Jaji: alisema hivyo?

Wakili Fredrick Kihwelo: alisema, Naomba Utukumbushe

Jaji: Alisema baada ya Kuwa ameona Shahidi Namba Mbili akijinasibu kuwa amewapokea na Kuwaingiza Kwenye Kitabu, na Kwa Sababu alikuwa anafahamu hajawahi Kwenda alimuelekeza Wakili wake.. Ndicho alichosema

Kihwelo: Mheshimiwa Jaji baada ya Mawasilisho Hayo,

Jaji: Pale ambapo ulikuwa unasema Mwanzo Umeacha..

Kihwelo: Ndiyo nilikuwa nasema Kwakuwa haikuwahi Kuingia wala +kutoka Gerezani Haibanwi na Standing Orders hizo

Na Lakini pia Shahidi Hakusema Kwamba Nyaraka hiyo (Barua) iliingia Gerezani, Kwa Maana hiyo Mheshimiwa Jaji naomba Mapingamizi hayo yatupiliwe Mbali na Barua hiyo Ipokelewe Kama Kielelezo, Naomba Kuwasilisha...

WS Abdallah Chavula: Mheshimiwa Jaji tumezisikia Hoja kinzani Z Wenzetu za Bwana Matata Na Bwana Kiwhelo na Kimsingi ni Hoja yetu Kwamba Hoja hizi zote walizozitoa hazijagusa Misingi ya Hoja zetu..

Isipokuwa Hoja hizi Zimekuja Kutia Nguvu Misingi Ya Hoja zetu, Kinachotaka Kutolewa Mbele Ya Mahakama Yako ni Barua ilivyoandikwa Kwenda kwa Kamanda Wa Polisi Wa Mkoa wa Kipolisi Ilala

Ambapo Kwa Maelekezo ya Shahidi Kwenda Kwa Wakili wake Fredrick Kihwelo, Mbele ya Wakili BWAN kibatala, Hoja yetu Siye, Barua ilitolewa Mbele Yako na Shahidi, ambayo yeye anasema ndiyo aliyeelekeza Iende Kwa Kamanda wa Polisi Ilala, Inaenda Kwa Watu 2 Nakala Kwa watu 2

Kwanza Kwake yeye Mohamed Abdilah Ling'wenya na Pili ni Registar wa High Court Of Tanzania, Corruption and Economic Crimes Division, Barua hii Imewekwa Mihuri ya The High Court of Tanzania..

Tukaimbia Mahakama Kwamba Nakala Mliyoleta ni Nakala Ya Neputy Registar Kupokea Barua Hii, Mheshimiwa Jaji tunasema hicho Kilichopo Kwenye Barua hiyo Kinafafana na Barua iliyopelekwa Kwa RPC Mkoa wa Ilala.?

Wakili wa Serikali: Na Mheshimiwa Jaji tukawa tunasema Shahidi Huyu nasema hiyo Barua ameonyeshwa na Miongoni Mwa Vitu aliyoonyeshwa no Muhuri Wa Mahakama Kuu Division,

Lakini tukaimbia Mahakama % Hata Kama alionyeshwa, Haku eleza Mahakama Kitu Kilicho andikwa Ndani ya Barua ni Kitu gani.? Nikile Ambacho yeye alitolea Maelekezo..Ili sasa tuweze Kupima Alichokitolea Maelezo na Hii Barua ya Msajili Matata: OBJECTION Hiyo Barua siyo ya Msajili

WS Abdallah Chavula: Hoja yetu kutoka Mwanzo ni kwamba hii ni Nakala aliyopelekewa Msajili Jaji: Ndiyo Barua aliyopelekewa Msajili Siyo Barua Ya Msajili..

WS Abdallah Chavula: Hiyo ndiyo Hoja yetu ya Kwanza Na Hoja yetu ya Pili Kwamba Shahidi hajawahi Kumiliki hiyo Barua Kwa Maana Kufanyia kazi au Kumiliki hiyo Barua.. Mheshimiwa Jaji na Hayo ndiyo yaliyopelekea tuielekeze Mahakama Kwenye kesi ya CHARLES ABEL GAZILABO

Sisi Hoja yetu hapa Mheshimiwa Jaji, Kesi Ya MIZIRAHI ambayo wao wameisaiti hapa, Hakuna Sehemu inasema Kwamba hata Ukimuinyesha Barua Shahidi Basi Shahidi Huyo atakuwa Competent

Na Kwakuwa Wenzetu Wanakubali walimuonyesha, Basi sisi tunaona wanaithibitishia Mahakama Kwamba Shahidi hana Knowledge.. Walitakiwa kwenda Mbali kuonyesha Kwamba Shahidi anajua Vilivyomo Ndani, Hilo hawajalifanya

Mimi Kwa Kusisitiza, Naielekeza Mahakama Ambapo Kilichopo Kwenye kesi ya MIZIRAHI Mbapo Kimechukuliwa Kwemye kesi ya CHARLES ABEL GAZILABO Ukurasa wa 12 ni Kwamba, Test Ya Shahidi Kutoa Kielelezo, ni Je shahidi huyo ana Knowledge na Je Shahidi Huyo anamiliki hicho Kielelezo

Matata: OBJECTION Matata Mheshimiwa Jaji Suala la Knowledge nimeliongea mimi, Wakili Kihwelo ameongea.....

Jaji: Si Nilikuwa naandika, Kama Watakuwa Wameniingiza Chaka Nitaona

WS Abdallah Chavula: Kwa hiyo Hata Hii Misingi ya Kesi Wameshindwa Ku Introduce.. Kwa hiyo Mheshimiwa Jaji ni Maoni yetu Kwamba, Hoja yao Kupitia Kesi ya DPP VS MIZIRAHI Kwamba Wameweza Ku Establish Competence ya Shahidi haina Mashiko

Mheshimiwa Jaji Wakati Matata anatoa Hoja zake Alianza Kutoa Utaratibu Wa Namna ya Mtu akiwa Chini ya Magereza, akaenda Mbali Kwamba Wao Ndiyo wanajua sababu Wanaenda mara kwa mara..

Nataka nimwambie Kwamba Wao Wana fika Nje tu, Siye tunaingia Mpaka Ndani Kukagua Mahabusu/Magereza... Ndiyo Moja Ya Majukumu yetu..

Jaji: RUDI KWENYE HOJA

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji ni kwamba akafika mbali Kwamba Sijataja ni Kifungu gani Cha Sheria, Na kwambalwa Sababu Sijataja basi ninachosema Hakipo, Mheshimiwa Jaji Wakati anaongea Pius Hilla alisema hapa Kuhusu Standing Order na akaenda moja kwa Moja Kwenye order namba 685

Na Ambapo sitotaka Kurudia Hoja hii, lakini Order imeeleza Namna gani ya Kutoa au Kuingiza Nyaraka Chini ya mtu ambaye tupo Chini ya Magereza, Na wenzetu Wanaongelea Kuhusu Order hii ni Mpaka Mtu anapokuwa Magereza, Sisi tunasema Hapana, Sisi tunasema Hapana Kaleta Vibaya Sheria

Wakili wa Serikali: wenzetu Wanaongelea Kuhusu Order ni Mpaka Mtu anapokuwa Magereza, Sisi tunasema Hapana Kale Vibaya Sheria.. Sheria inasema "To every Prisoner".. standing Orders 3 imeeleza Prisoner ni Kitu gani

Matata: OBJECTION

Jaji: Mwenzio anasimama Kwa Sababu anaona Unaleta Hoja Mpya.

Wakili wa Serikali: Hilo naliacha Kama linawa Offend, Lakini Neno Prisoner ni Pamoja na Kokote Watakapoenda Ina wabana, Hawawezi Kwenda Moja Kwa Moja Lazima Wapite Kwa Incharge..

Yeye Mwenzetu Kwenye Hili Anasema Ana Privilege, na anatuelekeza Kwenye Ibara ya 13 Ibara Ndogo ya 6, Sisi Mheshimiwa Jaji tunakubali Kinacho patikana, Kwamba watu wote ni Innocent Mpaka itakapo Thibitishwa na Mahakama

Lakini Hapa Haijaongelea suala la Privilege, Imeongelewa Kwenye Sheria ya Ushahidi, Na Kwamba pale Unapotaka Jambo liingie Mahakamani Kanuni za Adminsibility lazima zifuatwe..

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Kwa hiyo Ukiamiua Kuleta Taarifa hizo Mahakamani unabanwa na Kanuni, na sisi tunasema Walipaswa Kuifafanukia Mahakama, Kwamba Kielelezo hicho Kilimfikia Mkononi

Na Kwamba Hakuna Namna Utazungumza hayo bila Order ya 685, Mheshimiwa Jaji Wenzetu Kama tumewapata Vizuri, Kwamba Hapakuwa na Muda wa Kujiandaa, Tupo tayari Kurekebishwa,

Jaji: walichosema Kwamba Walipata Taarifa Kwamba Mashtaka wamefunga Ushahidi Wao walipata nafasi ya Kukaa na shahidi ili Kumuandaa..

WS Abdallah Chavula: Sawa Mheshimiwa Kama Wanakiri Walipata nafasi Ya Kumauandaa Shahidi Tunashukuru Mheshimiwa Jaji Kuhusu Mahusiano, ilikuwa ni suala la Relevance Kati ya Shahidi na Ushahidi, Mheshimiwa Jaji sisi tunasema waliyoyaongea Yalipaswa Kuongewa na Shahidi

Jambo ambalo Siyo Sahihi, Ni kweli pia hatukupinga siala la Namba Ya Kesi, ila tunapinga Parties, Hapakuletwa Barua ambayo Imeunganisha...

Wakili wa Serikali: Lakini tunakubaliana na wao Kwamba Shahidi Alitoa Maelezo Kwa Wakili Wake Fredrick Kihwelo Aandike Barua kwa RPC Ilala, Sisi hatuna tatizo Ushahidi huo ila Shida Ipo pale ambapo Ushahidi haujaoanishwa na Barua..

Ndiyo pale tunasema Kwamba tinakosa Relevance, Na Mheshimiwa Jaji no Hoja yetu Kwamba Ukiangalia ile Barua, haina Uhusiano na Shahidi Ina Uhusiano na Watu wengine, Ndiyo Hoja ya Relevance InaKuja hapo. Walichopaswa Kukifanya Nikuonyesha Relevance Ya Barua na Shahidi

Mheshimiwa Jaji ni Wasilisho letu Kwamba Barua waliyo Muonyeshe Shahidi, Ina muhuri Mahakama Kuu Division, Wakati Barua inayo taka Kutolewa Mbele Yako ina Muhuri Wa The high

Wakili wa Serikali: Wenzetu walichopaswa Kukifanya ni Kutoa Ushahidi Unaoonyesha Mahusiano kati ya Mahakama Kuu Division na The high Court of Tanzania Corruption and Economic Crimes Division, Tunabaki Kujiluza Shahidi anakifahamu

Mahakama imebakia kuwa na sintofahamu

Kibatala: OBJECTION. Mh Jaji ni kweli kwamba mahakama imebakia na sintofahamu???

Jaji: ameacha kuwa wakili wa mashtaka anataka kuwa wakili wa mahakama

WS Chavula: Mheshimiwa Jaji watake wasitake ukishakuwa wakili wa Jamhuri ni pamoja na mahakama

Mahakama: Hahaaaaaaaa

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji sisi tunarejea Submission Zetu, Na wenzetu hawajajibu, Wamekwepa Submission Zetu, Sisi tunasema anachokionyesha siyo chake kile anachokionyesha kilipaswa Kupelekwa Kwa amtu Mwingine, na Ndiyo Msingi wa Hoja yetu

Na Kama alitoa Maelekezo ya namna gani iepelekwe huko iliyopelekwa alitakiwa atuambie yeye Kabla, Lakini Hakuyasema hayo, Sasa Inakuwaje Nakala ya Mtu Mwingine Imfikie shahidi, Tulitegemea atoe Nakala yake..

Mheshimiwa Jaji Kwa hoja zao wameshindwa Kujibu Hoja zetu za Competence, Na Kwa kuwa Wameshindwa Kudondosha Kwa Hoja yetu, Tunaiomba Mahakama Ipuuze Hoja yao isiizingatie Hoja zetu..

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Kwa Mara kadhaa Mawakili wa Utetezi Wamekuwa wakisitiza Mahakama ilichoamua Siku ya tarehe 16 November 2021 Mheshimiwa Jaji kilichojiri tarehe 16 November 2021 na Kilichojiri Leo ni Vitu Viwili tofauti kabisa Havishabihani kwa namna yoyote ile

Kilichojitokeza Tarehe 16 November Mwaka huu, Shahidi Wa Pili Katika Kesi yetu siye alikuwa ameleta Barua Mahakamani, Barua iliyokuwa inatoka Kwa Naibu Msajili Wa Mahakama Hii Kwenda Kwa National Prosecuton Service

Na Barua hiyo waliokuwa Copied ni Shahidi Mwenyewe (PW2) NA Ndani yake Ilikuwa Imebainishwa Kwamba Subject Matter ya Kile Kielelezo apewe PW2

Mheshimiwa Jaji na Yeye Akasema Kwamba Nimeenda Kwa Naibu Msajili Na Naibu Msajili akanisainisha na Kunipa Kielelezo Kile, Huo ndiyo ulikuwa Ushahidi wa Shahidi...

Wakili wa Serikali: Kilichopo hapa Shahidi anasema nilitoa Maelezo kwa wakili wangu Fredrick kuandika Barua kwenda Kwa RPC ILALA, Sisi Hoja yetu hapa Nakala Yake huyu Ipo wapi..? Hakuna Namna Mahakama Yako Inafungwa na Maamuzi ya tarehe 16, November Mwaka huu

Angalau Ingekuwa Barua ya Msajili Tungesema Vinashahabiana, Lakini ni Vitu Viwili tofauti na wenzetu hawawezi Kupata hifadhi katika Mahakama Yako Kupitia Uamuzi ule.. Kwa Hiyo Mheshimiwa Jaji Tunaomba Mahakama Yako Ijialike Upya..

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Wenzetu Vile Vile walieleza Mahakama kwa Uthibitisho wa kama Barua Ipokelewe siyo lazima Igongwe muhuri.. Msingi wa Hoja zetu ulikuwa ni lazima Ifanyike Acknowledgement...

Wenzetu Wanasema Kwamba tunajuaje kama tusingetoa Dispatch, kuna Msemo Unasema Ingawa Ni MKali lazima Niuseme tu Leo Kwamba MAHAKAMA SIYO MAMA YAKO.. Mahakama lazima uiambie, Mama yako tu ndiyo anaweza Kujua Kesho utafanya nini..

Wakili wa Serikali: Kama Kuna suala la Dispatch Book Walipaswa kusema lakini Hakusema.. Mwisho wa Siku Wanakuja Kuiambia Mahakama Kwamba "hii Hoja ni Premature" Kwamba Hoja yetu Kwenye Hili Eneo ni Pre Mature, Kwamba Eti Kupokelewa Kwa Barua Kwa RPC ni Premature..

Yeye Mwenyewe ndiyo ameyaleta hapa Mahakamani, Barua inayosema Kwamba imepokelewa na RPC badala yake kaleta Barua Iliyopelekwa Kwa na Naibu Msajili.. Mheshimiwa Jaji kiujumla Wenzetu wameshindwa Kujibu Hoja zetu, Kimsingi Hoja zote ni dhaifu usizitilie maanani Hoja zao, tunaomba izingatie Hoja zetu kwa Sababu tulizobainisha.. Ni hayo tu Mheshimiwa Jaji

Jaji: Vipi Mnaendelea?

Wakili wa Serikali: Tumemaliza Mheshimiwa jaji

Jaji: ni kwamba Hoja ni Nyingi kwa Muda Uliobaki siwezi Kufanya Uamuzi, Naomba Niwapangie Jumatatu, Ni sawa..?

Mawakili wa pande zote mbili wanakubaliana,

Jaji: Jumatatu ni tarehe ngapi?

Kibatala: 29/11

Jaji: tunahairisha shauri hili Mpaka 29/11, Shahidi Utaendelea Kutoa Ushahidi wako Siku hiyo, Washtakiwa Wataendelea Kuwa rumande chini ya magereza
Update za jana vipi!!!!??????? au,,,,,,,........
 
Mkuu Mawakili wa Pande zote mbili huwa wanakutana kabla ya kuingia Mahakamani kwajili ya briefing na baada kwa debriefing. Lakini ukweli ni kwamba wale wa Upande wa Jamhuri hujiona kuwa wao ni Bora na wa kupewa kipaumbele kuliko wengine.

Kwa kifupi msingi wa hii kesi tayari ulishaonyesha mapungufu ya kesheria siku ile Kingai alipokuwa akifanyiwa cross examination. Na Jaji kuonyesha upendeleo (Jaji Siyani). Pale ndipo tungeona nguvu na umuhimu wa Jaji Mkuu.

Nawe nikuulize, unataka kuniambia kuwa hakuna wabobezi wa sheria wanaofuatilia hili shauri na kisha kuweza kumtonya Jaji hata nje ya Mahakama kabla ya kufanya maamuzi??

Mfano Shahidi kakamatwa live akiwa na note book/diary pamoja na kalamu bila kusahau simu. Lakini chakushangaza Jaji alikuja kupeta bila aibu. Jaji Mkuu hakuliona hilo??
Jaji Mkuu ni mteuliwa wa Rais anatakiwa aishi kwa kiapo alichoapa mbele ya Rais.
 
Back
Top Bottom