Yaliyojiri Ligi ya Mabingwa Africa : Nkana FC yaichapa Simba SC kwa magoli 2-1

brave one

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
4,876
7,366
Ligi ya mabingwa Africa round ya Kwanza Leo inatimua vumbi Kati mashetani wekundu kutoka Zambia Nkana Red Devils na wekundu wa msimbazi Simba. Mshindi wa jumla katika michezo 2 watakayocheza atafuzu moja kwa moja hatua ya makundi huku atakaeshinda atupwa kwenye kombe la shilikisho barani Africa.

Wachambuzi wa soka barani Africa waipa wanaipa nafasi kubwa kushinda mshezo huu wa Leo kutokana na kuwa na kikosi Bora huku wakitandaza soka maridadi la kuvutia kiasi kufanishwa na kikosi Cha Manchester city.

Simba Leo itawategemea golikipa namba moja wa taifa stars aishi manula, akilindwa na mchezaji kiongozi Paschal Wawa, katikati mkude kotei na Chama watakuwa wakitawala kwa pasi fupi fupi za uhakika na mbele okwi, kagere na Bocco wakiongoza mashambulizi ya uhakika.

Watabiri wa masuala ya kubet wameipa Simba ushindi mnono.

Mchezaji tishio wa Nkana ni Walter Bwalya Simba wamepewa tahadhari ya kuwa makini nae. Pia mtanzania Hasan kessy atakuwa akiiwakilisha Nkana FC

Usikose mtanage huu hapa hapa JF mida ya saa 10 kamili jioni na saa 9 kwa muda wa Zambia

Inst-image-5.jpeg


UPDATE

Timu ya soka ya Nkana FC imeifunga timu ya Simba kwa magoli 2-1 katika mechi ya kwanza iliyofanyika katika uwanja wa Nkana mjini Kitwe, Zambia

Hadi mapumziko Nkana walikuwa wanaongoza kwa goli moja lililofungwa na Robert Kampamba katika dakika ya 27

Nkana walifanikiwa kujipatia goli la pili katika dakika ya 56 lililofungwa na Kelvin Kampamba

Wawakilishi wa Tanzania Simba walifanikiwa kufunga goli moja katika dakika ya 74 kwa mkwaju wa penalti, iliyofungwa na Kapteni John Boko baada yamshambuliaji wao Kagere kuangushwa katika penalti boksi

Sasa Simba inahitaji ushindi wa goli 1 ili iweze kufuzu katika hatua inayofuata katika mechi yao ya marudiano
 
daah Leo niliota ndoto mbaya and nzuri pia
matokea ikawa kama ifuatavyo
Nkana 1-0simba
Nkana 1-1simba
Nkana 1-3simba
Okwi atakosa goli.la WAZi
kagere na okwi wata score
Simba baada ya kipindi cha kwanza atatafuta sare ya kutaka kufungana

Mpira dk 95 Tusubiri matokeo
 
Kila la kheri Timu yangu ya Simba leo ipate ushindi. Na leo nimebet kwa kuweka mzigo kwa Simba. Hivyo tusiposhinda nitapata maumivu mara mbili.
 
daah Leo niliota ndoto mbaya and nzuri pia
matokea ikawa kama ifuatavyo
Nkana 1-0simba
Nkana 1-1simba
Nkana 1-3simba
Okwi atakosa goli.la WAZi
kagere na okwi wata score
Simba baada ya kipindi cha kwanza atatafuta sare ya kutoka kufungana

Mpira dk 95 Tusubiri matokeo
Jaribu, jackpot kuna 400,000,000/=
 
Back
Top Bottom