Yaliyojiri leo (Oktoba 21, 2021) katika Mkutano wa Kitaifa wa Wadau wa upatikanaji wa Haki Jinai kwa Watoto waathirika wa Ukatili wa Kingono Tanzania

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,795
11,958
Mkutano wa Kitaifa wa Wadau wa upatikanaji wa Haki Jinai kwa Watoto waathirika wa Ukatiki wa Kingono Tanzania umeendelea leo Oktoba 21, 2021 Mkoani Dodoma na Hon. Lady Justice, Mwanabaraka Mnyukwa (Judge of the High Court-Tanzania) ameongea yafuatayo:

▪️ Waraka wa Jaji Mkuu no. 2 (2018), mtoto ambaye ni mwathirika wa ukatili wa kingono hatajwi jina lake, anuani, shule anayosoma kwa upande wa Mahakama. Lakin pia katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, mwathirika hatakiwi kutajwa jina lake na taarifa nyingine.

▪️ Uendeshwaji wa mashauri ya watoto waliopitia ukatili wa kingono aina nyingine za ukatili zinatakiwa kusikilizwa ndani ya miezi 6. Kama muda huo umekoma na kesi haijaisha lazima kuwe na sababu za msingi na Sheria imetoa kipindi cha miezi 3 ya ziada ili mashauri hayo yamalizike.

▪️ Sheria inasisitiza mashauri ya watoto waliokinzana na sheria yanapaswa kusikilizwa katika mazingira rafiki kwa watoto, ili muathirika aone yupo katika mazingira salama (In-Camera). Wahusika katika kesi hizi ni Hakimu, Mwendesha Mashtaka, Afisa Upelelezi, Afisa Ustawi wa Jamii, Mzazi/Mlezi/Ndugu wa mwathirika.

▪️ Kubakwa kwa mujibu wa sheria (Statutory rape): Mtoto aliye chini ya miaka 18 hawezi kuridhia kujamiiana, kwa kufanya hivyo mtoto huyu amebakwa kwa mujibu wa sheria.

▪️ Mahakama ya Rufani kupitia maamuzi yake imetoa muongozo wa kisheria kwa baadhi ya maneno yakitumika kwenye kesi ya Ukatili wa kingono, basi ni kiashiria kitakachoisaidia Mahakama za chini kugundua kwamba ukatili wa kingono ulifanyika huo (ubakaji/ulawiti). Mfano; “Amenifanyia tabia mbaya”, “Aliniwekea dudu yake” n.k
 
Back
Top Bottom