Yaliyojiri kwenye Mkutano wa Mkuu wa Polisi IGP Simon Sirro na Wanahabari, ajali zapungua. Wanaoficha Magari yanayodaiwa kukiona..

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
837
1,000
Salaam Wakuu,

Leo 04/01/2021 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, anazungumza na waandishi wa habari baada ya kikao kazi na askari wa Kikosi cha usalama barabarani wa mikoa ya Kanda Maalum DSM, Rufiji na Pwani.

Atakuwa Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay (Police Officers Mess) Dar es salaam.

Tuwaletea kila kinachojiri kutokea hapa Oysterbay.

Stay tuned

=====

UPDATES1440HRS


IMG_20210104_142811_383.jpg

Simon Sirro anasema;

=> Leo tulikuwa na kikao cha tathimini ya trafiki katika utendaji kwazi kwa Mwaka 2020

=> Katika 2020 tumejitahidi kupunguza ajali kulinganisha na miaka mingine kwani ajali zimepungua kwa 34% Tumepanga Mwaka huu 2021, tupunguze ajali kwa 50%


=> Makosa ya jinai yamepungua kwa 20% tumejitahidi laki Makosa ya barabarani 2020 tunaenda vizuri zaidi.

=> Upande wa maadili tuna changamoto bado kuna lugha mbaya zinayolewa na Watendaji wetu, Swala la customer care ni la kuzingatiwa sana hivyo tutazidi kutoa elimu kwa Watendaji wetu wawe na lugha nzuri kwa wateja wetu. Lakini piaKuna wateja ukishampiga faini atasema chochote sababu anakuwa na hasira, hivyo watendaji wetu wanatakiwa kuwa na ivumilivu pia.

=> Nimeambiwa tuna upungufu wa vipima ulevi, tutajitahidi kuvipata haraka iwezekanavyo.

=> Tunawashukuru Wadau wetu wa Usalama barabarani. Wadau wetu wa Usalama barabarani wamekuwa msaada mkubwa sana kwetu.

=> Kuna Askari wetu unakuta wanamshikilia mtu muda mrefu kwa makosa madogo tunasema hapana. Labda kama mtu kasababisha ajali ya kuua.

=> Tumefanya makubwa kuhakikisha ajali zinapungua.

= Kuna hili swala linazungumziwa na Wananchi la Malengo ya pesa kwa Trafiki, Kwamba Trafiki wanaagizwa walete kiasi fulani cha pesa. Hili swala halipo ni Uongo, makosa yenu ndo yanafanywa mpigwe faini.

=> Kuna Watu wana madeni wanadaiwa, wanachofanya wanaficha magari ndani. Naomba niwambie mkono wa Serikali ni mrefu. Wengine wanabadilisha plate namba.. Mfano mtu ana malori 40, anabadilisha plate namba. Nmetoa maagizo wafuatiliwe na Sheria ichukue mkondo wake.

=> Tumebaini kuna vijana wetu wanaingiza gari za IT kwenye System wakati kuna utaratibu wake wa kishughulika na Magari ya IT. Taratibu zifuatwe.

=> Kwa ajali east Afrika hakuna nchi ya kujilinganisha na sisi katika kupunguza ajali.
IMG_20210104_141756_938.jpg

MASWALI

IGP Sirro kaulizwa Maswali kuhusu hali ya Usalama Mtwara, Mwanaharakati aliyekamatwa na Polisi waliokamatwa na Rushwa Arusha.

Majibu:

=> Mtwara tunakwenda vizuri, nawashukuru wananchi wa Mtwara. Wazazi wawaeleze watoto wao wasiingie kwemye makundi ya Ugaidi sababu tutapambana nao kama Gaidi.

=> Kuhusu Mwanaharakati, watu wa uhamiaji ndo watatolea majibu. Kwasababu mambo yake yamahusiana na Uhamiaji.

=> Askari Waliokamatwa kwa Rushwa Arusha wameshapelekwa Mahakamani. Askari akishakuwa Mharifu si askari tena, Padri akiwa mharifu si Padri tena, Shekh akiwa Mharifu sio Shekh tena, tunamshughulikia kama Mharifu.

Asanteni sana.
 

All - Rounder

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
2,671
2,000
Binafsi nimpongeze tu IGP na Polisi nzima Kuunda Kikosi Maalum chao ambacho kwakweli nimekishuhudia kikileta Utulivu mahala pagumu DSM.
 

Twilumba

JF-Expert Member
Dec 5, 2010
8,039
2,000
Jeshi la polisi lina kazi ya kulinda raia na mali zake hvy badi itafaa IGP Siro akija na jibu la aliko raia Azirony Gwanda na Ben Sanane na wengine.
 

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
98,052
2,000
Kama akifanya vibaya anasdhibiwa basi akifanta vizuri Kupongeza ni ustaarabu. Hata mwanao akifaulu mpongeze na zawadi mpe.
Kufaulu ni wajibu wake maana hukumpeleka shule akacheze mtunje.

Hata hao polisi ni wajibu wao kuhakikisha nchi yote inakuwa salama.
 

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
9,021
2,000
Hili jeshi limechoka Sana. Huwa intelijensia yake iko kwenye mikutano na maandamano ya chadema tu. Nie ya hapo hawana tofauti na mgambo wa mtaani kwangu.

Polisi sasa hiivi ni idara ndani ya ccm.

Tunataka press yake azungumzie Azory Gwanda yuko wapi? Ben Sa8 yuko wapi? Nani alimpiga risasi Tundu Lisu?
 

Idimulwa

JF-Expert Member
May 27, 2011
4,293
2,000
Polisi wapo Kweli?Bila Chadema kuwaruhusu kufanya mikutano ya kujenga chama,wataanza kuendesha Bodaboda muda siyo mrefu...wamekoswa Kazi.
 

ighaghe

JF-Expert Member
Mar 25, 2013
2,171
2,000
Kufauru ni wajibu wake maana hukumpeleka shule akacheze mtunje.

Hata hao polisi ni wajibu wao kuhakikisha nchi yote inakuwa salama.
Ww wajibu wako kama mwananchi ni kulipa kodi na kutii sheria bila shuruti. Ukilipa kodi vizuri unapongezwa usipolipa unaadhibiwa. Kupongezana ni jambo la kistaarabu
 

elvischirwa

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
8,671
2,000
Jeshi la polisi lina kazi ya kulinda raia na mali zake hvy badi itafaa IGP Siro akija na jibu la aliko raia Azirony Gwanda na Ben Sanane na wengine.
Huenda ndiyo sababu kushirikisha pwani na usalama barabarani kwani alichukuliwa na gari.
 

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
107,148
2,000
Kufanya vizuri kwa lipi? Wakati kuna mauaji yamefanyika miaka inakatika hakuna uchunguzi huko ni kufanya vizuri? Changa la macho hilo baada ya kuona reputation na credibility ya polisiccm imeanguka hadi SIFURI.
Kama akifanya vibaya anasdhibiwa basi akifanta vizuri Kupongeza ni ustaarabu. Hata mwanao akifaulu mpongeze na zawadi mpe.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom