Yaliyojiri kwenye mechi ya Yanga SC vs Ndanda FC

Yanga imechukuwa point 3 muhimu, hizo porojo nyingine kapige na mashoga zako.
Mkuu, mimi sijaangalia mechi hii, ila nilimuona alipocheza Ngao ya Hisani, na alicheza vizuri sana. Sasa kosa langu ni lipi hadi unitukane? Kwani kumuulizia Tshishimbi ni ushoga?
 
Kiukweli yanga lipeni vizuri wachezaji wenu. Timu inacheza kinyonge sana,sema ndanda nayo ilikuwa mdobwedo. Mechi ijayo ya mtibwa kwa udhaifu huo..........niishie hapo maana hamuchelewi kutukana.
 
Kiukweli yanga lipeni vizuri wachezaji wenu. Timu inacheza kinyonge sana,sema ndanda nayo ilikuwa mdobwedo. Mechi ijayo ya mtibwa kwa udhaifu huo..........niishie hapo maana hamuchelewi kutukana.
Cha kushangaza timu inayolipwa vizuri inaambulia droo, maajabu haya yanapatikana Tanzania tu.
 
Inaelekea timu nyingi zinaiogopa sana Simba kiasi kwamba zikitoa sare inakuwa kama vile maajabu fulani. Nimefuatilia sare za Simba, kuanzia ile Yanga ilipofungwa kwa penati ngao ya hisani, kisha Azam na then juzi Mbao. Yaani wanaopata sare wanafurahi kwa kutaja bajeti ya usajili ya Simba! Jamani mjiamini, sio sare tu, hata kushinda mnaweza pia!
Of course, kutoa draw na kikosi cha billion 1.3 nadhan ni ajabu, draw kwa squad ya 1.3billion ni kama umeshinda
 
Nilikua najadiliana na washkaji hapa kitu hicho ulichoongea,huyu lwandamina mbovu sana,speed yetu haionekani tena,mpaka nimejiuliza au huyu mzee ni mshabiki wa mikia nini
Kwa mchezo aliocheza leo Ndanda ilibidi tumpige goli zisizopungua tatu ila ndio hivyo timu imekuwa mbovu na wale wachezaji wetu machachari kama vile Ngoma na Chirwa wanazidi kudidimia kila kukicha.
 
Yanga hamna kitu.

Kocha inabidi tumfukuze anatuharibia timu kila kukicha.
Daaa mdau umeongea la msingi sana,mimi sina taaluma ya ukocha lakini kila nikiangalia hii Yanga inavyocheza mwaka huu tutapata vidonda vya tumbo.Mikoani walisema viwanja vibovu leo hapa taifa napo daa,watu tunaangalia mpira huku mikono iko mashavuni na roho zinadunda mno
 
Yanga ya pluijm kwa mechi kama ya leo tulikuwa tunatoka na goli hata 4.
 
Yanga ya pluijm kwa mechi kama ya leo tulikuwa tunatoka na goli hata 4.
Siyo 4 tu ilikuwa na zaidi kabisa.Ndanda wenyewe walikuwa hawjiwezi na sisi tumeishia kuchechemea tu,yaani inanisikitisha sana.Watu wote wa mpira waliojaa pale Yanga ina maana hawaoni kama timu inazidi kuwa mbovu kila kukicha
 
Huenda ikawa! ila mkuu huenda kuna kitu nyuma ya pazia! Viongozi wakae na wachezaji wajue tatizo! Hivi kweli mechi 4 tumefunga goli 4! Hapana hii sio Yanga tunayoijua!
Hakuna kitu nyuma ya pazia .

Tatizo ni kocha tu na si vinginevyo.

Ukitaka kuamini hilo ,tazama hata mechi za msimu uliopita Yanga zilizocheza chini ya Lwandamina.
 
Yaani pale Yanga wamekosea sana eti kocha msaidizi mnampa Shadrack Nsajigwa kweli wako serious au wanataka kuleta masihara.Kocha mkuu mwenyewe hana mbinu,mgumu kufanya sub,timu haina kasi,forward line ndiyo kabisa hawana jipya kabisa
 
Back
Top Bottom