Elections 2010 Yaliyojiri kwenye kikao cha kamati kuu CCM - jumapili iliyopita

kaburunye

JF-Expert Member
May 12, 2010
672
74
Kikao cha kamati kuu ya CCM kilifanyika siku ya jumapili hapo ikulu. Wana JF naomba mwenye fununu ya agenda zilizojadiliwa na yaliyojiri kwenye kikao hiki atujulishe.
 
Kilizungumzia jinsi maji yalivyofika shingoni na kuweka mikakati mipya ya kampeni katika kipindi kilichosalia. Nadhani hivi punde tutawaona majukwaani Wazee wa CCM waliokuwa wamekaa kimya wakilazimika kujitosa kuokoa jahazi linaloelekea kuzama. Nasikia JK na timu yake wamewaangukia wazee na kuwaomba wamsaidie!
 
Kikao cha kamati kuu ya CCM kilifanyika siku ya jumapili hapo ikulu. Wana JF naomba mwenye fununu ya agenda zilizojadiliwa na yaliyojiri kwenye kikao hiki atujulishe.

Badala ya ku worry about yaliyojadiliwa kwenye CC jumapili, kwanini msijiangalie ninyi kwanza hayo ya CCM waachiwe CCM.
 
hahaaa watakaa sana mwaka huu na hivo vikao vyao vya kamati kuu...mwaka huu ngoma nzito walidhani watauza mgombea kwa sura..wanalo mwaka huu
 
Pia walijadili mbinu mpya za kuiba kura ikiwemo kutucheleweshea masanduku ya kura na muda wa kufungua vituo hasa maeneo yenye upinzani mkubwa...

Pia wakasema matokeo yatatangazwa maramoja baada ya kuhesabu kura ila watasema jakaya kashinda kwa 80%...

Pia wakasema wasimamizi wa kimataifa wapelekwe maeneo ambayo ccm wanauhakika wa kushinda kama jimboni kwa mwakyembe, pinda na ole sendeka...na huko masanduku yanawaishwa saa 11 usiku na vituo vinafunguliwa saa 12 asubuhi....nyeti zaidi in details nitawapa baadae leo jioni nitakutana na mzee mizengo p....

Ohhh...nilisahau...wamepanga pia kufanya mazoezi ya kijeshi kurusha ndege chakavu za kichina tulizonunua maeneo ya vijijini ili kuwatisha wapiga kura kuwa vita inaweza kutokea ukichagua wapinzani
 
CCM ina kiburi sana, kama ilikuwa inapenda kutawala milele kwa nini isifanye mambo ambayo yangewafurahisha wale wenye uwezo wa kuwapa kipindi kingine cha ajira? (wapiga kura). Ona sasa inawabidi kutumia mbinu chafu, nguvu ya ziada na vitisho kuhakikisha wanaendelea kuwepo ilihali watoa ajira hawataki. Wakae pembeni na kujipanga upya.
 
Agenda:

1. Kupokea taarifa za Kampeni
2. Kupitisha malipo (final invoice) kwa REDET na SYNOVATE
3. Kufuta likizo zote za watendaji wa CCM
4. Kupokea taarifa ya mama Salma
5. Taarifa ya kutumia SMS kumchafua Dr. Slaa
6. AOB
 
Hapo sina Comment yoyote kwakweli mkuu kwa hilo uliloli nena hapo juu bali naongezea kidogo hapa chini mengineyo,

Tatizo la hawa CCM wanapenda Fire fight na sio ku solve matatizo ya wajiri wao(Wapiga kura) chaguzi zikiisha basi wanawasahau wapiga kura wao kabisaaaa na kuigeuza katiba ya nchi chini juu na sheria zote zilizotungwa kama mwongozo wa kuiongoza serikali na nchi kwa ujumla na zitapindishwa mpaka 2015 tena wakirudi na sera nyingi za ahadi.

Agenda:
........
4. Kupokea taarifa ya mama Salma

Ile aliyosema kuwa Vijana wengi hawaipendi CCM na wahamia upinzani????

Au ni Ipi maana hii ndio nzito zaidi kama mke wa kiongozi mkuu wa nchi amekiri kuwa Vijana wengi ambao ndio wapiga kura 70% ya nchi wanasupport upinzani iweje REDET na SYNOVATE waseme JK atashinda kwa 80% takwimi gani au kigezo gani walitumia kutupa tathimini hiyo??
 
Hapo kweney red haswa, watafanyanini kuwashawishi hawa vijana, maana wameona kwa macho yao jinsi baba na mama zao walivyoambiwa hahitaji kura za wafanyakazi, wameona jinsi waalimu wao walivyo kuwa wakinyanyaswa, kaka zao jinsi wanavyo hangaika na mikopo ya vyuo; hawa hawadanganyiki!!!!!!!!!!!!!1
 
Agenda:

1. Kupokea taarifa za Kampeni
2. Kupitisha malipo (final invoice) kwa REDET na SYNOVATE
3. Kufuta likizo zote za watendaji wa CCM
4. Kupokea taarifa ya mama Salma
5. Taarifa ya kutumia SMS kumchafua Dr. Slaa
6. AOB

Doubtful esp on 4
 
Wazee wa CCM itakuwa vigumu kumbeba JK kwani wote wamestuka wanaona nchi inaendeshwa kifalme ni JK na familia yake. Jasho litamtoka mwaka huu. Alipashwa amwambie mkewe na mwanae wakae chini waache longalonga..JK utavuna ulichopanda hahahhaha ukipanda mahindi utavuna mahindi na si maharagwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii.
 
Kilizungumzia jinsi maji yalivyofika shingoni na kuweka mikakati mipya ya kampeni katika kipindi kilichosalia. Nadhani hivi punde tutawaona majukwaani Wazee wa CCM waliokuwa wamekaa kimya wakilazimika kujitosa kuokoa jahazi linaloelekea kuzama. Nasikia JK na timu yake wamewaangukia wazee na kuwaomba wamsaidie!
una uhakika mkuu?
 
Agenda:

1. Kupokea taarifa za Kampeni
2. Kupitisha malipo (final invoice) kwa REDET na SYNOVATE
3. Kufuta likizo zote za watendaji wa CCM
4. Kupokea taarifa ya mama Salma
5. Taarifa ya kutumia SMS kumchafua Dr. Slaa
6. AOB

Acha dhihaka katika masuala ya msingi
 
Hakuna chama kisichofanya mikutano kipindi hikii na hasa inayofanya tathmini ya kampeni kuelekea kupata ushindi.
 
Wazee wa CCM itakuwa vigumu kumbeba JK kwani wote wamestuka wanaona nchi inaendeshwa kifalme ni JK na familia yake. Jasho litamtoka mwaka huu. Alipashwa amwambie mkewe na mwanae wakae chini waache longalonga..JK utavuna ulichopanda hahahhaha ukipanda mahindi utavuna mahindi na si maharagwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii.

CCM haijazidiwa na chadema kiasi cha kuhitaji msaada wa wazee. Inakuwaje wanaolia msaada huo ni chadema kuliko wao CCM. Hebu tuambieni mtatufanyia nini watanzania na kisha tuwapime kabla ya kuamua yupi wa kumpigia kura. Siku zimebaki chache sana kuzungumzia ya CCM badala ya yale ya kutufanyia wananchi.
 
Ile aliyosema kuwa Vijana wengi hawaipendi CCM na wahamia upinzani????

Au ni Ipi maana hii ndio nzito zaidi kama mke wa kiongozi mkuu wa nchi amekiri kuwa Vijana wengi ambao ndio wapiga kura 70% ya nchi wanasupport upinzani iweje REDET na SYNOVATE waseme JK atashinda kwa 80% takwimi gani au kigezo gani walitumia kutupa tathimini hiyo??

Vijana wanachukia CCM-Mama Salma

Na Patrick Mabula, Kahama

MKE wa Rais, Mama Salma Kikwete amewataka wanawake kuwakalisha chini vijana wao na kuwataka wakipende Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuwa katika kipindi hiki wengi wao wameonesha kuwa upande wa upinzani.

Akizungumza na wanawake juzi katika ofisi ya CCM ya Wilaya ya Kahama, Mama Kikwete aliwaagiza wanawake katika familia zao kuwakalisha chini vijana na kuwaasa waachane na vyama vya upinzani.

Mama Kikwete ambaye yuko katika kampeni za kumpigia kampeni mume wake, alisema vijana wa sasa hivi kuanzia miaka 18 na kuendelea wameonesha kuwa hawakitaki Chama Cha Mapinduzi kwa vile hawajui mazuri iliyoyafanya na itakayoendelea kuyafanya.

“Vijana wa sasa hivi kuanzia miaka 18 na kuendelea sijui wameigiliwa na nini vichwani mwao, huko wanakokwenda hakueleweki, kwa kuwa akinamama tumewazaa naomba huko katika familia zetu tuwakalishe chini tuwaase wabaki CCM,” alisema Mama Kikwete.

Mama Kikwete aliwataka wanawake kuacha makundi na kununiana ovyo kwa ajili ya kura za maoni, kwa kuwa zimepita na tumepata wagombea kwa tiketi ya CCM tuache hali hiyo na tuwe kitu kimoja ili kukiletea ushindi chama chetu.

Akiwapigia kampeni wagombea ubunge na udiwani wa majimbo ya Kahama na Msalala, Mama Kikwete aliwataka wanawake kuhakikisha CCM inapata ushindi kuanzia kwenye urais, wabunge hadi madiwani.

Alisema mgombea Ubunge wa Jimbo la Msalala anayetetea nafasi hiyo, Bw. Ezekiel Maige ni kijana makini sana, mwenye busara na katika kipindi alichomaliza ameonekana kufanya kazi zake vizuri hivyo lazima wamuenzi kwa kumpa kura ili aendelee kuwatumikia.

Alisema CCM imefanya mambo mengi mazuri kwa upande wa elimu, afya, miundombinu ya barabara chini ya Rais Kikwete na itaendelea kutekeleza ilani yake, hivyo ni lazima tuhakikishe ushindi wa kishindo kwa wagombea wake kwa kuchagua mafiga matatu-rais, bbunge na diwani kutoka CCM. Source: Majira
 
Back
Top Bottom