Uchaguzi 2020 Yaliyojiri kwenye Kampeni za Mgombea Urais wa CHADEMA, Tundu Lissu mikoa ya Singida, Tabora na Shinyanga

Subpost 6 - Igunga mkoani Tabora wamesema tarehe 28 Oktoba, 2020 kura zote za Mh ( 360 X 640 ).jpg
Subpost 4 - Igunga mkoani Tabora wamesema tarehe 28 Oktoba, 2020 kura zote za Mh ( 360 X 640 ).jpg
Subpost 2 - Igunga mkoani Tabora wamesema tarehe 28 Oktoba, 2020 kura zote za Mh ( 360 X 640 ).jpg
 
Wakuu bado tunaendelea kuwaletea taarifa za Mh Tundu Lissu kutoka popote anapopita kuomba kura

Endelea kubaki hapa hapa JF kwa taarifa za Uhakika

View attachment 1597566

=========

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Tundu Lissu, akiambatana na mkewe, Bi. Alicia Magabe, akimjulia hali Ndugu Wilfred Enock anayejulikana pia kwa jina la Chaijaba ambaye ni maarufu mjini Singida kutokana na kutembea na toroli la kubebea mizigo likiwa na bendera ya Chadema kila aendako. Ndugu Chaijaba alivamiwa, kushambuliwa na kujeruhiwa vibaya maeneo mbalimbali mwilini na watu ambao hadi sasa hawajakamatwa, waliokuwa wakimhoji sababu za mapenzi yake kwa Chadema.
View attachment 1597674View attachment 1597675View attachment 1597676View attachment 1597677View attachment 1597678
"Msafara wa Mheshimiwaa Tundu Lissu umesimamishwa na mamia ya wananchi wa Kijiji cha Tumuli, wilayani Mkalama Mkoani Singida.

Mheshimiwa Tundu Lissu akiongea na wananchi wa Tumuli amewakumbusha kuhusu umuhimu uchaguzi mkuu, miaka mitano ya Magufuli imekuwa ya shida na vurugu. Watu watekwa, wameuliwa, wamenyanyaswa, wamekosa mishahara na kudhulumiwa kila mahali. Mfano halisi mmeona kwangu nimepigwa risasi 16. Nchi imekuwa ikiogopeka nakila mtu sasahivi ni rahisi kumtaja Mungu kuliko kumtaja Magufuli. Ndomaana nasema uchaguzi mkuu huu ni muhimu, tukishindwa tumekwisha.

Na katika kuhakikisha yote haya yanakuwa sawa ndo maana Chadema ilani yetu inazungumza kuhusu Uhuru, Haki na maendeleo ya watu. Najua wote tunataka Uhuru, Haki na maendeleo. Kukiwa na haki hata Taifa huinuka. Basi mchague viongozi wa Chadema wasimamie nakutekeleza ilani ambayo kila mmoja itamgusa.

Ili yote haya tuyakomeshe tarehe 28 nawaomba wananchi wa Tumuli mjitokeze kwa wingi kuchagua viongozi wa Chadema.

Mgombea udiwani wenu hapa Tumuli ni Haruna Khamis

Namgombea Mbunge Oscar Alex Kapalale
View attachment 1597688View attachment 1597687View attachment 1597686
Mungu akuongoze vyema mpakwa mafuta wa Bwana.
 
Back
Top Bottom