Uchaguzi 2020 Yaliyojiri kwenye Kampeni za Mgombea Urais wa CHADEMA, Tundu Lissu mikoa ya Kigoma na Kagera

Kama watu wasioitaka ccm ni wengi kwanini huwa inashinda miaka yote ?
Mkuu watu wanabadilika, CCM kabla ya 2015 ni tofauti Sana na CCM baada ya 2015, hilo litambue wazi kabisa.

Vyama vikongwe na vilivyojiwekeza kama CCM daima vinaangushwa si na wapinzani nje ya chama bali kwa ushirikiano wa wanachama wao kwa vyama pinzani.

Mungu aliona mbali kuficha moyo wa mtu mbali na macho ya watu kwani moyo ndilo hekalu la siri zote.
 
Yale mambo ya kusema eti CCM inabebwa na taasisi za serikali pamoja na majeshi yake inabidi yakome mwaka huu. Hivyo vyombo vinakuwa na nguvu vinapokabiliana na mtu mmoja mmoja aliyehitilafiana na haki. Lakini kama ni umma unaodai haki, hapatatosha! Na mwaka huu hakuna kumwachia Mungu hata tone la uonevu.
Mara hii wajitafakari wapenda haki wako macho.
 
Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chadema Tundu Lissu Jana ameingia Kigoma kwa kishindo kikuu.

Alilakiwa na Maelfu Elfu ya watu waliojipanga majiani huku wakitandika mikeka chini shujaa huyo wa karne hii apite juu yake.

Akihutubia umati mkubwa unaokadiriwa kuwa na watu zaidi ya Elfu 30 katika viwanja vya Community Centre Lissu alisema alichokishuhudia Kigoma ni kwamba wananchi wameamua kuondoa utawala wa kidhalimu na kuweka utawala utakaojali #UTUHAKINAMAENDELEOYAWATU#

Tundu Lissu alisema Chadema kinatambua mchango mkubwa unaotolewa na Zitto Kabwe ambaye ni mzaliwa wa Mkoa huo.Lissu aliuambia umati huo Chadema na ACT ni kitu kimoja katika uchaguzi huu na kwamba wananchi wamchague mgombea anayeweza kuitoa CCM madarakani ambaye ana ushawishi Hoja na anayeungwa mkono na watu.

Huku wakimjibu kwa kelele za Shangwe wananchi hao walipaaza sauti na kusema ni Zitto Kabwe watakayemchagua kuwa mbunge wao na kura zote za Urais wataelekeza kwa Tundu Lissu

Awali Lissu aliwaambia wananchi hao kwamba wakati anaumwa alipata Salaam kutoka kwa watu wa Kigoma walizomtuma kijana wao Zitto Kabwe.

Mara baada ya kuhutubia Shujaa huyo akisindikizwa Kifalme na umati mkubwa uliokuwa ukiimba Rais Rais Rais mpaka Hotelini kwake.

Siku moja kabla ya Tundu Lissu Kuwasili Kigoma Kiongozi wa ACT Zitto Kabwe alitoa tangazo rasmi la kunikaribisha mkoani humo na kuwataka wananchi kumpokea kwa Shangwe
Wapenda haki wanapokuja pamoja Mungu huwabariki .
 
I swear before God and Man! Kuna usiku niliota kitu cha namna hii.

Usiku wa majuzi wiki iliyopita niliota Lissu kambwaga Magufuli kwenye uchaguzi huu wa 2020.
Kazi iliyobaki kwa Lissu ni kulinda ushindi wake na ndilo jukumu la watanzania.
Ushindi wa Lissu utalindwa kwa Damu na maji, atakayejaribu kuiba kura za Lissu atakuwa halali yetu
 
Ushindi wa Lissu utalindwa kwa Damu na maji, atakayejaribu kuiba kura za Lissu atakuwa halali yetu
Na hiki ndicho kinachotatanisha zaidi. Watanzania walizoea kutanguliza amani mbele ya haki ili kuepuka umwagaji damu lkn wamegundua ukosefu wa haki unaweza kumwaga damu ama kupoteza maisha. Too late but better than never.
 
Mkuu watu wanabadilika, CCM kabla ya 2015 ni tofauti Sana na CCM baada ya 2015, hilo litambue wazi kabisa.

Vyama vikongwe na vilivyojiwekeza kama CCM daima vinaangushwa si na wapinzani nje ya chama bali kwa ushirikiano wa wanachama wao kwa vyama pinzani.

Mungu aliona mbali kuficha moyo wa mtu mbali na macho ya watu kwani moyo ndilo hekalu la siri zote.
ccm ilipoteza ushawishi kipndi cha jk lkn hii awamu ya JPM imerudisha nguvu ya CCM sababu vitu ambavyo upinzani ulitumia kama fimbo vimetatuliwa tayari

now day wanalia na uhuru tu swali wanataka uhuru gan ?
 
Hamasisha watu wakapige kura 28/10 (waliojiandikisha).
Kuishabikia cdm bila kuwajibika kwenye sanduku la kura nao ni uzwazwa.
Kumbe unajua. This was done already.... Unaomgelea kilichotekelezwa tayari tangu 2015......

Ni uzwazwa kushabikia ccm
 
Ni muhimu kudili na mawakala, wawe recruited effectively. Wawe equipped na tech, wapewe body camera pamoja na vinasa sauti.

Kwenye kampeni wananchi wapewe somo la uraia, wajue umuhimu, thamani pamoja na matokeo ya kura zao.
Swali fikirishi je wewe unajua anaye zinatangaza kura za Urais na sababu zake
 
ccm ilipoteza ushawishi kipndi cha jk lkn hii awamu ya JPM imerudisha nguvu ya CCM sababu vitu ambavyo upinzani ulitumia kama fimbo vimetatuliwa tayari

now day wanalia na uhuru tu swali wanataka uhuru gan ?
fimbo ya wapinzani haikuwa utekaji na matusi kwa raia
 
Back
Top Bottom