Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,517
- 217,784
Wakuu natanguliza salamu na baada ya salamu naingia moja kwa moja kwenye mada, kama mnavyojua Kampeni zinaendelea na leo tena Mh Lissu ambaye anapewa asilimia kubwa kutwaa urais wa nchi atakuwa kwenye mikoa ya Kagera na Geita, katika kanda hii kunatarajiwa kupigwa mkutano maalum wa kipekee kwenye jimbo la Chato.
Endelea kubaki hapahapa JF kwa taarifa za uhakika.
========
UPDATES:
Picha mbalimbali za Mkutano wa Kampeni wa Mgombea Urais wa Chadema, Mhe. Tundu Lissu mapema asubuhi leo, Septemba 21 katika eneo la Nyakanazi, Kata ya Lusahunga, Wilaya ya Biharamulo, mkoani Kagera.
Akiwa hapo Mhe. Lissu amewanadi Mgombea Ubunge wa Chadema (mwenye kofia na rungu mkononi), Mbelwa Petro na Mgombea Udiwani Kata ya Lusahunga, Damasi Buyago.
Mhe. Tundu Lissu hapo, amesema;
Wananchi Nyakanazi Ahsante kwakutupokea Vizuri natumelala hapa Nawashukuru sana.
Kwenye Uchaguzi mkuu huu Tunahitaji kufanya Mabadiliko makubwa sana, na moja ni manyanyaso yenu wananchi kuuziwa Vitambulisho vya Wajasiriamali. Kwanini muuziwe vitambulisho, nchi hii Vitambulisho vinatolewa bure lakini serikali ya CCM inauza vitambulisho kwa wananchi wake, na hawatoi hata receipts za EFD. Nasema kuwa tunaliwa na hawa MaCCM. Sasa haya yote mwisho ni tarehe 28 Mwezi wakumi 2020.
Hapa Nyakanazi Wengine niwakulima wanahangaika wenyenyewe kipindi cha kulima na kupalilia Ila ukivuna tu.. Wanaweza mageti kila unapopita.
Sasa Uchaguzi Mkuu Huu twendeni tukachague wagombea wa Chadema Ili tuondoe Huu Udhalimu.
Chagueni Mbunge Wangu Wa Jimbo La Biharamulo "Mbelwa Petro" nanisikia mnamuita asiyempenda kaja, na diwani Bwana Damasi Buyago wachagueni Tufanye Mabadiliko. Nakwenye Kura Ya Urais Uamuzi ni Wenu Kati Ya Tundu Lissu au Jiwe... Sasa watu wa Nyakanazi naombeni kura zenu mnipe dhamana Yakuongoza.
Ahsanteni watu wa Nyakanazi.
NGARA; Picha zikionesha matukio mbalimbali kwenye Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chadema, Mhe. Tundu Lissu katika Uwanja wa Kokoto, Ngara mjini. Tundu Lissu pia alimpatia pole Mgombea Udiwani Kata ya Ngara mjini kwa tiketi ya Chadema, Bi. Herieth Gwaje, aliyefiwa na Baba yake mzazi, Mzee Malingumu, usiku wa kuamkia leo.
Picha; Wananchi wakifuatilia Mkutano wa Kampeni wa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chadema, Mhe. Tundu Lissu, baada ya kumsimamisha katika eneo la Nyakahura, Biharamulo (mizani) akiwa njiani kuelekea Ngara.
Tundu Lissu hapa chini kwenye Video Akisalimiana na Wananchi wa Nyakanazi Biharamlo baada ya Kuamka, alilala Nyakanazi, Video ya Pili ni akiwasili Ngara Kagera