Uchaguzi 2020 Yaliyojiri kwenye kampeni za Mgombea Urais wa CHADEMA Mhe Tundu Lissu Mkoani Mwanza

View attachment 1580765
Wakuu natanguliza salamu , kama mjuavyo kampeni za uchaguzi mkuu bado zinaendelea , sasa basi leo tena yule mgombea urais anayeongoza kura za maoni atakuwa Mkoa wa Mwanza kunadi sera za chama chake na kuomba kura za ndio.

Endelea kufuatilia hapahapa JF kwa taarifa za uhakika

View attachment 1580142

========

Mkutano Mheshimiwaa Tundu Lissu Kwenye Viwanja vya Polisi - Misungwi, Mwanza.

Akiongea na watu Misungwi Amezungumzia yafuatayo.

1. Kuenguliwa kwa wagombea
2. Kuvunja Tume ya Uchaguzi
3. Mamlaka kwa wananchi
4. Kujitokeza Kupiga Kura kwa wingi.
5. Uchaguzi Wa huru na haki.

Halmashauri nzima haina mgombea yeyote wa Chadema.
]View attachment 1580503View attachment 1580504View attachment 1580505View attachment 1580506View attachment 1580507View attachment 1580508View attachment 1580509View attachment 1580510View attachment 1580511View attachment 1580513View attachment 1580514
View attachment 1580500

Mkutano Mhe. Tundu Lissu Kwenye Viwanja vya Sokoni G'hungumalwa- Kwimba, Mwanza.

Akiongea na watu Hungumalwa Amezungumzia yafuatayo.

1. Kuenguliwa kwa wagombea ( Mgombea Ubunge nawagombea wa Tano wa udiwani.)
2. Kurudisha mamlaka kwa wananchi
3. Mjitokeze Kupiga Kura na Kulinda kura.
4. Kilimo cha Pamba na mazao mengine.
5. Utozwaji ushuru na msururu wa kodi kwa wafanyabiashara.
6. Uchaguzi Wa huru na haki.
7. Nyongeza za mishahara na upandishwaji wa Madaraja kwa watumishi wa umma.

Ahsanteni sana watu wa G'hungumalwa.
View attachment 1580592View attachment 1580591View attachment 1580590
Mkutano Mhe. Tundu Lissu Kwenye Viwanja vya Nyambiti Sumve - Mwanza.

Akiongea na watu Sumve amezungumzia haya.

1. Gharama Za Chapa ya Ng'ombe
2. Msururu wa ushuru wa mazao.
3. Malipo kwa wakulima wa Pamba.
4. Barabara ya Nyambiti
5. Uboreshwaji wa huduma za afya na maji.
6. Uchaguzi Wa huru na haki.

Mgombea ubunge wa Jimbo la Sumve Bwana *Sangarali Shija Masanja.* Nadiwani Ni *Bi. Eunice Tabuse.*

Ahsanteni watu wa Sumve.
View attachment 1580696View attachment 1580695View attachment 1580694View attachment 1580693


Mwanza , Nyamagana
View attachment 1580764
Maelfu ya wananchi wa Mwanza kwenye Mkutano wa Kampeni wa Mhe. Tundu Lissu uliofanyika Uwanja wa Shule ya Msingi Mabatini, Nyamagana.

Ameongea na Wananchi wa Nyamagana...

"Ahsanteni Mwanza ahsante Nyamagana.. Imekuwa wiki yakuvunja record, leo record iko Nyamagana.

Leo Naomba mniruhusu nizungumze mambo mawili tu.

Jambo la kwanza nikuhusu wanajeshi wa Tanzania, ninapozungumza Wanajeshi wanajeshi ni Ma jeshi yaliyotajwa kwenye katiba yetu yaani Jeshi la wananchi, jeshi la polisi, jeshi la Magereza, jeshi la akiba (Mgambo) na hawa Usalama wa Taifa ambao hawajatajwa.
Rai yangu kwenu kwa wanajeshi wa Tanzania, nmeona umati huu umati huu, nmeona wananchi wanataka nini, sasa msije mkataka kutumika kuharibu uchaguzi huu. Msije mkageuza silaha kwa wananchi wanaojua wanataka nini. Ukombozi huu wa Tanzania unawahusu na nyinyi askari wetu, Chadema Ikiingia Madarakani itawalipa na kuwaongeza mishahara.

Lapili watu wa Nyamagana nawaomba tarehe 28 tukapige kura ya mafuriko kama haya ya Leo. Tukipiga kura ya mafuriko hawataweza kuiba, tukapige kura tukawatoe hawa wanaotutia umasikini wakudumu. Tukapige kura ili kira mtu nchi hii atendewe haki, sote tupate haki. Tukapige kura ili tusitishe unyanyasaji uliodumu muda mrefu. Kura za mafuriko kama haya zitaamua hatima ya maisha yetu.

Chombezoo.. Anamwambia OCD "Najua afande namalizia kuongea ila haya pia yanahusu ukombozi wenu.."

Ahsanteni sana Nyamagana na Mungu awabariki Sana Nyamagana.
View attachment 1580791View attachment 1580790View attachment 1580789View attachment 1580788View attachment 1580783
View attachment 1580781View attachment 1580588
Hii mikutano ya mwaka 1961 baada ya uhuru wa tanganyika. Pale uhuru park
 
Huyo mnywa gongo,hawezi kubadili uwepo wa Magufuli madarakani after 28th October.Hizo ndo Kura zitakazo haribika🤣🤣
Achakujifariji mwenzako kaboost kutoa woga pamoja na elimu yako yote hio unamuamini polepole kwa tafiti alizo ambiwa na mkewe huku jibu analijuwa!!🤔🤔🤔
 

Attachments

  • 2529704_Apandacho_mtu_ndicho_atakachovuna__268_X_480_.mp4
    370.1 KB
Picha mjitahidi kuwaambia kitengo cha uchakuchuaji picha cha Chadema wawahishe kidogo walau saa kumi na moja hivi jioni

Tumechoka kila siku wao wanasubiri kuanzia saa moja usiku Giza limeingia na hatuoni vizuri shauri ya giza wao ndio wanarusha za Lowasa za 2015 na kuziita za leo maeneo mbalimbali aliyopita Lisu
kubwa jinga.....kwenye TV nayo?
 
Back
Top Bottom