Uchaguzi 2020 Yaliyojiri kwenye kampeni za Mgombea Urais wa CHADEMA Mhe Tundu Lissu Mkoani Mwanza

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
77,371
2,000

Wakuu natanguliza salamu , kama mjuavyo kampeni za uchaguzi mkuu bado zinaendelea , sasa basi leo tena yule mgombea urais anayeongoza kura za maoni atakuwa Mkoa wa Mwanza kunadi sera za chama chake na kuomba kura za ndio.

Endelea kufuatilia hapahapa JF kwa taarifa za uhakika

Leo Ijumaa Sept 25_ Mgombea Urais wetu atafanya mikutano ya hadhara;  _black_small_square_︎ Mi...jpg

========

Mkutano Mheshimiwaa Tundu Lissu Kwenye Viwanja vya Polisi - Misungwi, Mwanza.

Akiongea na watu Misungwi Amezungumzia yafuatayo.

1. Kuenguliwa kwa wagombea
2. Kuvunja Tume ya Uchaguzi
3. Mamlaka kwa wananchi
4. Kujitokeza Kupiga Kura kwa wingi.
5. Uchaguzi Wa huru na haki.

Halmashauri nzima haina mgombea yeyote wa Chadema.
]
IMG-20200925-WA0025.jpg
IMG-20200925-WA0024.jpg
IMG-20200925-WA0023.jpg
IMG-20200925-WA0022.jpg
IMG-20200925-WA0021.jpg
IMG-20200925-WA0034.jpg
IMG-20200925-WA0033.jpg
IMG-20200925-WA0032.jpg
IMG-20200925-WA0031.jpg
IMG-20200925-WA0029.jpg
IMG-20200925-WA0028.jpgMkutano Mhe. Tundu Lissu Kwenye Viwanja vya Sokoni G'hungumalwa- Kwimba, Mwanza.

Akiongea na watu Hungumalwa Amezungumzia yafuatayo.

1. Kuenguliwa kwa wagombea ( Mgombea Ubunge nawagombea wa Tano wa udiwani.)
2. Kurudisha mamlaka kwa wananchi
3. Mjitokeze Kupiga Kura na Kulinda kura.
4. Kilimo cha Pamba na mazao mengine.
5. Utozwaji ushuru na msururu wa kodi kwa wafanyabiashara.
6. Uchaguzi Wa huru na haki.
7. Nyongeza za mishahara na upandishwaji wa Madaraja kwa watumishi wa umma.

Ahsanteni sana watu wa G'hungumalwa.
IMG-20200925-WA0051.jpg
IMG-20200925-WA0049.jpg
IMG-20200925-WA0048.jpg

Mkutano Mhe. Tundu Lissu Kwenye Viwanja vya Nyambiti Sumve - Mwanza.

Akiongea na watu Sumve amezungumzia haya.

1. Gharama Za Chapa ya Ng'ombe
2. Msururu wa ushuru wa mazao.
3. Malipo kwa wakulima wa Pamba.
4. Barabara ya Nyambiti
5. Uboreshwaji wa huduma za afya na maji.
6. Uchaguzi Wa huru na haki.

Mgombea ubunge wa Jimbo la Sumve Bwana *Sangarali Shija Masanja.* Nadiwani Ni *Bi. Eunice Tabuse.*

Ahsanteni watu wa Sumve.
IMG-20200925-WA0068.jpg
IMG-20200925-WA0065.jpg
IMG-20200925-WA0066.jpg
IMG-20200925-WA0069.jpgMwanza , Nyamagana

Maelfu ya wananchi wa Mwanza kwenye Mkutano wa Kampeni wa Mhe. Tundu Lissu uliofanyika Uwanja wa Shule ya Msingi Mabatini, Nyamagana.

Ameongea na Wananchi wa Nyamagana...

"Ahsanteni Mwanza ahsante Nyamagana.. Imekuwa wiki yakuvunja record, leo record iko Nyamagana.

Leo Naomba mniruhusu nizungumze mambo mawili tu.

Jambo la kwanza nikuhusu wanajeshi wa Tanzania, ninapozungumza Wanajeshi wanajeshi ni Ma jeshi yaliyotajwa kwenye katiba yetu yaani Jeshi la wananchi, jeshi la polisi, jeshi la Magereza, jeshi la akiba (Mgambo) na hawa Usalama wa Taifa ambao hawajatajwa.
Rai yangu kwenu kwa wanajeshi wa Tanzania, nmeona umati huu umati huu, nmeona wananchi wanataka nini, sasa msije mkataka kutumika kuharibu uchaguzi huu. Msije mkageuza silaha kwa wananchi wanaojua wanataka nini. Ukombozi huu wa Tanzania unawahusu na nyinyi askari wetu, Chadema Ikiingia Madarakani itawalipa na kuwaongeza mishahara.

Lapili watu wa Nyamagana nawaomba tarehe 28 tukapige kura ya mafuriko kama haya ya Leo. Tukipiga kura ya mafuriko hawataweza kuiba, tukapige kura tukawatoe hawa wanaotutia umasikini wakudumu. Tukapige kura ili kira mtu nchi hii atendewe haki, sote tupate haki. Tukapige kura ili tusitishe unyanyasaji uliodumu muda mrefu. Kura za mafuriko kama haya zitaamua hatima ya maisha yetu.

Chombezoo.. Anamwambia OCD "Najua afande namalizia kuongea ila haya pia yanahusu ukombozi wenu.."

Ahsanteni sana Nyamagana na Mungu awabariki Sana Nyamagana.
IMG-20200925-WA0093.jpg
IMG-20200925-WA0108.jpg
IMG-20200925-WA0104.jpg
IMG-20200925-WA0103.jpg
IMG-20200925-WA0104.jpg

IMG-20200925-WA0103.jpg
IMG-20200925-WA0045.jpg
 
YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
25,686
2,000
Picha mjitahidi kuwaambia kitengo cha uchakuchuaji picha cha Chadema wawahishe kidogo walau saa kumi na moja hivi jioni

Tumechoka kila siku wao wanasubiri kuanzia saa moja usiku Giza limeingia na hatuoni vizuri shauri ya giza wao ndio wanarusha za Lowasa za 2015 na kuziita za leo maeneo mbalimbali aliyopita Lisu
 
Msukuma Original

JF-Expert Member
Oct 2, 2018
597
1,000
Picha mjitahidi kuwaambia kitengo cha uchakuchuaji picha wawahishe kidogo walau SAA kumi na moja hivi jioni kila siku wao wanasubiri kuanzia SAA moja Giza limeingia ndio wanarusha za Lowasa za 2015 na kuziita za leo
Halafu kubwa jinga mbona unahangaika sana kuhusu nyomi ya Lissu? Kama huamini si uachane nazo? Toka umeanza kujifariji picha fake umepata nini? Achana na mambo ya CHADEMA utakufa kwa pressure.
 
Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
77,371
2,000
Picha mjitahidi kuwaambia kitengo cha uchakuchuaji picha cha Chadema wawahishe kidogo walau saa kumi na moja hivi jioni

Tumechoka kila siku wao wanasubiri kuanzia saa moja usiku Giza limeingia na hatuoni vizuri shauri ya giza wao ndio wanarusha za Lowasa za 2015 na kuziita za leo maeneo mbalimbali aliyopita Lisu
Pole kwa maumivu
 
mzamifu

JF-Expert Member
Mar 10, 2010
4,992
2,000
Picha mjitahidi kuwaambia kitengo cha uchakuchuaji picha cha Chadema wawahishe kidogo walau saa kumi na moja hivi jioni

Tumechoka kila siku wao wanasubiri kuanzia saa moja usiku Giza limeingia na hatuoni vizuri shauri ya giza wao ndio wanarusha za Lowasa za 2015 na kuziita za leo maeneo mbalimbali aliyopita Lisu
Mkuu, kitu gani kinakufanya useme hivo na kama picha ni kweli ungesemaje? Au unahofu kama ni kweli ni madhara kwa upande mwingine?

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
santesandy

JF-Expert Member
Apr 23, 2012
993
1,000
Picha mjitahidi kuwaambia kitengo cha uchakuchuaji picha cha Chadema wawahishe kidogo walau saa kumi na moja hivi jioni

Tumechoka kila siku wao wanasubiri kuanzia saa moja usiku Giza limeingia na hatuoni vizuri shauri ya giza wao ndio wanarusha za Lowasa za 2015 na kuziita za leo maeneo mbalimbali aliyopita Lisu
Leo tunatoa za mwaka 1980 za Mh. Sokoine
, najua umechoka za 2015 za Lowasa! Alafu usihangaike sana kama Kuku anapotaka kuleta tunda, tulia! Leo picha tunaedit taratibu, tutaweka saa 5 usiku!😂
 
Kiwarhoapandenga

JF-Expert Member
Aug 10, 2019
2,027
2,000
Picha mjitahidi kuwaambia kitengo cha uchakuchuaji picha cha Chadema wawahishe kidogo walau saa kumi na moja hivi jioni

Tumechoka kila siku wao wanasubiri kuanzia saa moja usiku Giza limeingia na hatuoni vizuri shauri ya giza wao ndio wanarusha za Lowasa za 2015 na kuziita za leo maeneo mbalimbali aliyopita Lisu
Sio lazima uchangie anzisha page ya mbogamboga mpo mbona mtazila ziishe

Sent from my BLL-L22 using JamiiForums mobile app
 
Mmassy JM

JF-Expert Member
Jul 30, 2020
888
1,000
Picha mjitahidi kuwaambia kitengo cha uchakuchuaji picha cha Chadema wawahishe kidogo walau saa kumi na moja hivi jioni

Tumechoka kila siku wao wanasubiri kuanzia saa moja usiku Giza limeingia na hatuoni vizuri shauri ya giza wao ndio wanarusha za Lowasa za 2015 na kuziita za leo maeneo mbalimbali aliyopita Lisu

Ndugu na wewe hata Kama ni kada kindakindaki, ila utoto umekuzidi.

Yaani unaonyesha wazi kwamba una hofu kiasi kwamba kila wakati unadai picha zimetengenezwa.

Jaribu kutafuta hoja ili uweze kukitetea Chama Cha Mapinduzi na siyo kuwa muoga Kama fisi
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom