Uchaguzi 2020 Yaliyojiri Kutoka Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma: Kampeni za Dkt. Magufuli kusaka urais 2020-2025

Sep 8, 2020
67
133
Mgombea Urais wa JMT, Dkt. John Magufuli yupo Kigoma leo Septemba 18, 2020.

Updates zote zitawekwa hapa:

Video: Ngoma ya kinamama wa kabila la Wabembe wa kata ya Kitongani Kigoma mjini wakitumbuiza katika Uwanja wa Lake Tanganyika mkoani humo katika kunogesha mkutano wa kampeni wa JPM leo Ijumaa Septemba 18, 2029.

----
Nataka niwaeleze ndugu zangu, nilipoteuliwa kuwa Rais nilikaa chini nikasema siwezi nikauacha Mkoa wa Kigoma ukaendelea kubaki nyuma.

Mtu akiona taa Barabarani hapa Kigoma asije kusimama akatafuta sifa, sisi ndio tumeweka, hata Chato tumeweka, Mtwara Mikindani na Arusha pia na hatukubagua, Arusha Mbunge CHADEMA tulipeleka, Mtwara Mbunge wa CUF tulipeleka, hapa Kigoma tulileta

Tutapanua pia uwanja wa Kigoma ili hadi Air Bus ziwe zinatua hapa, Ndege zina faida nimefurahi nimeoneshwa Watu wamebeba picha ikimuonesha Zitto anashuka kwenye Bombadier, nyinyi Wajanja kweli Watu wa hapa, mlipanga kunionesha Mimi, si mngemuonesha mwenyewe

Tunataka miaka inayokuja Mtu anatoka hapa Kigoma na Treni ya kisasa inayokimbia KM 150 kwa saa anapasua mpaka DSM, kaeni mkao wa biashara, dagaa zako zitakwenda kuliwa Afrika Kusini, Migebuka itagebukia Uganda, connection ya Barabara tuliyoijenga itatusaidia

Tunajenga Barabara hapa sio ya mchezo ni ya Kimataifa inatuunganisha na Nchi za wenzetu, Mtu atatoka Sudani Kusini ataingia Uganda,Mtukula,Bukoba,Muleba Nyakanazi, Kakonko, Kasulu hadi Afrika Kusini, ukiwa na Barabara ya connection uchumi unapanuka

Kule Mwanza MV Victoria na nyingine zinafanya kazi, sitoi ahadi hewa, tumepanga kununua Meli mbili kubwa zifanye kazi Ziwa Tanganyika, moja itabeba Watu 600 na Tani 400 na Meli ya pili itabeba mizigo tu Tani 4000, tutakarabati pia Meli mbili kwa Bilioni 16

Mpango hili la kununua Meli 2 kubwa Ziwa Tanganyika ukaliweke kwenye mipango yako, ila Watu wa Jimbo lako wakikunyima basi, maana wakati mwingine Watu wa Kigoma wanagomagoma, ila naamini safari hii hamtogoma,nataka niifungue Kigoma, siku moja mtanikumbuka

Mkoa wa Kigoma ulisahaulika, niliwahi kuja hapa nikiwa form Two, Baba yangu mdogo alikuwa anakaa Mwanga,usafiri ulikuwa wa treni tu, ukiwa unatoka Mwanza unaenda kuisubiri Tabora, nilipokuwa Rais nilikaa chini nikasema siwezi kuiacha Kigoma iwe nyuma

Tunajenga barabara ya Nyakanazi kwenda Kibondo Km. 50, Kidawe-Kasulu Km.67, Kasulu-Manyovu Km.68.25, Kanya-Kadyama Mvuge Km. 70.5, Mvunge-Njiapanda ya Nduta Km. 59.35.

Tangu kuanza kwa mwaka huu dunia ilikuwa kwenye taharuki ya ugonjwa wa corona, na sisi tuliepushwa kwa kuwa tulimtanguliza Mungu mbele, wakati sisi tunamtanguliza Mungu wengine walitubeza.

Wakati tunamtanguliza Mungu katika janga la Corona wengine walitubeza na kusema ni ugonjwa wa kisayansi hivyo kumtemgea Mungu ni makosa na tujiandae watu milioni 4 kufarik, Mungu alitusikia Corona imeondoka, nina imani waliosema hivyo sasa wamejua ukubwa wa Mungu.

Napenda watu wachache na wale wa duniani ambao hawamwamini Mungu, waje Tanzania wajifunze namna Mungu alivyotusaidia hata kuindosha Corona na kutufanya sasa tunaendelea na shughuli zetu kama kawaida na kwa amani.

Naomba radhi kwa wanachi ambao walinisubiria njiani na walipenda niongee nao, lakini sikuweza kutokana na sheria za uchaguzi, maana mimi ninaheshimu sheria za uchaguzi.

Ndege ina faida kubwa katika maendeleo, nimefurahi hapa nilikuwa naoneshwa picha, nyie ni wajanja watu wa hapa, ikimuonesha Zitto anateremka kwenye ndege ya Bombadier, nyinyi wajanja kweli watu wa Kigoma hii mlipanga kunionyesha mimi?,si mngemuonesha mwenyewe.

Tatizo la Kigoma liko ndani ya Chama Cha Mapinduzi. Kwa sababu mchana mnakuwa CCM, usiku mnakuwa chama kingine. Naomba mpeni kura Shaban Kirumbe (Mgombea Ubunge Kigoma Mjini). Naipenda Kigoma, nawapenda sana, msiniangushe wana Kigoma




 
MGOMBEA Urais kwa tiketi ya CCM, Dkt John Pombe Magufuli, leo Septemba 18 2020 ameendelea kupiga kampeni, ambapo atakua Kigoma, viwanja vya Lake Tanganyika.
 
wewe ndio zito mwenyewe hahaha

Sent from my MI NOTE Pro using JamiiForums mobile app
Unajua ukweli bora tuseme tuu hakuna mbunge mwenye kazi nyepesi kurudi bungeni kama Zitto. Ila pia naamini kwa Kigoma mjini Lissu atapata kura nyingi kuliko mgombea yeyote ule wa urais!
Yani Lissu atapata kura nyingi ila mgombea wa Chadema wa ubunge hatapita!
 
Back
Top Bottom