Yaliyojiri kutoka Karimjee Hall: Wakuu wa Wilaya za Dar waapishwa

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,726
32,818
image.jpeg
Hapa mkuu wa Wilaya ya Kigamboni akikabidhiwa Ilani ya CCM na kuapa kwenda kuitekeleza kwa vitendo
image.jpeg
image.jpeg
Leo ndio mkuu wa Mkoa wa Dsm anawaapisha Wakuu wa Wilaya wapya wa Dsm.Tukio hili linafanyika katika ukumbi wa Karimjee.
Wakuu wa Wilaya za Temeke,Ilala,Kinondoni,Ubungo na Kigamboni.Wakuu wa Wilaya wanne ndio wamefika isipokuwa Mkuu wa Wilaya mpya ya Ubungo ndugu Humphrey Polepole ambaye hataapishwa leo,sababu ikiwa ni kufiwa na baba yake.

Shughuli hii inasimamiwa na Clouds Media huku ikionyeshwa moja kwa moja kupitia Clouds Tv na MC wa sherehe hii ni Ephraim Kibonde.Wakuu hao wa Wilaya ni
Felix Jackson
Mgandilwa Hashim
Sophia Mjema
Ally S Happi
Baada ya kuapishwa mkuu wa mkoa atatoa muongozo kwa Wakuu wa Wilaya na baadae waandishi wa Habari watapewa nafasi ya kuwauliza Wakuu wa Wilaya maswali ya moja kwa moja kuhusu Wilaya zao na mipango yao

Mkuu wa Mkoa anasisitiza kuwa Wakuu wa Wilaya wana nafasi ya kuingia katika vikao vya madiwani,na haambiwi cha kufanya na Meya,sababu Meya ni Spika tu wa baraza la madiwani na ndio maana nafasi yake ni kuongoza vikao na huitajika ofisini mara mbili tu kwa week.Shughuli zote zinakuwa chini ya Mkuu wa Wilaya ambaye ndie mwakilishi wa Rais katika Wilaya na si Meya.

Mh Makonda anasema ndio maana Meya analindwa na Mgambo wakati Mkuu wa Wilaya analindwa na Jeshi,Polisi na ana usalama wa Taifa,hivyo Mameya wa Dsm wawaache wakuu wa wilaya kufanya kazi zao sbb wapo kwa mujibu wa Katiba ya Tz.

Mkuu wa Mkoa anawaagiza Wakuu wa Wilaya kupambana na ushoga,na kuwa ana taarifa ya NGO iliyopewa dola milioni 70 katika mkoa wa Dsm ili kuimarisha swala la mashoga,ameipa onyo NGO hiyo na kuahidi kuifutilia mbali sababu inatumika kueneza tabia za kishoga ambazo kwa mujibu wa Katiba ya nchi ni kosa linahitaji hukumu.

Makonda amesisitiza kuwa vita ya shisha ndio imeanza,na kwa mujibu wa TFDA shisha ni madawa ya kulevya na husababisha saratani ya Koo,anasema unaenda Double Tree Hotel unamkuta binti mdogo mzuriii halafu anavuta shisha,anaagiza kuwa shisha ni marufuku na yoyote atakayeuza Segerea inamsubiri.Wavutaji wa sigara wote wanatakiwa kuvuta maeneo ya "private" na kama wanataka kuonyeshwa hizo sehemu za Private basi wavute hadharani ndio wataijuwa hiyo "more private" ipo wapi.

Ombaomba wametangaziwa "kiama",kwamba kwenye mitandao watu wameanza kusema zoezi hilo limeshindwa,lkn anawapa week mbili kuhakikisha wameweka mpango kazi kuondoa hawa ombaomba.Watumie mpango kazi na ilani ya CCM kusaidia watu,na baada ya siku 90 wakuu wote wa mkoa watakuja hadharani mbele za watu pale ukumbi wa Mwalimu Nyerere kusema mambo gani waliyoyafanya na kuyapanga katika wilaya zao
 
Kama Mh Makonda akiweza kusimamia kwa vitendo kila anachoongea basi Dar es Salaam ingekuwa kama Milan au Madrid..Jamaa anamawazo mapana ila tatizo ni vitendo na watendaji wa kutekeleza anachosema. Kwa ushauri wangu ni bora angekuwa anachuja awe anaongea vile anavyoweza kutekeleza tu,,.. Unafikaje kwenye level ya shisha na sigara za kawaida wakati bado Bangi na Gongo zipo na zinapatikana kwa wingi hapa Dar..
 
Kwa hiyo jemedali polepole anakula kiapo cha pili kwa muda usiozidi miezi miwili katika nafasi hiyo hiyo!?
 
Kwa hiyo jemedali polepole anakula kiapo cha pili kwa muda usiozidi miezi miwili katika nafasi hiyo hiyo!?
Ndio maana yake...Na kufikia mwakani anahikikisha Kubenea kapotea kwenye siasa za Ubungo,ndio kazi aliyotumwa
 
Hii ni hasara kubwa kuwa na viongozi wa namna hii..hasara kabisa

kwa hio anawatuma kwenda kupambana na madiwani? au?

and hiyo NGO anaijua amechukua hatua gani zaidi ya porojo...haoni kukitaja sana kitu pia ni kukipa publicity?

Kwa nini asipambane na Clouds media iliyotumika na hao mashoga kujitangaza?

Shisha ipo katika category ya dawa za kulevya? imezuiliwa kisheria?

Inabidi ifike wakati tujue nchi hii inaendeshwa kwa sheria na sio anachowaza tu mtu
 
Ndio maana yake...Na kufikia mwakani anahikikisha Kubenea kapotea kwenye siasa za Ubungo,ndio kazi aliyotumwa
Hakuna mkuu wa mkoa wala wilaya atakayeweza kuwabadilisha wananchi juu ya maamuzi ya kumchagua mbunge wamtakaye.Ingekuwa wakuu wa wilaya na mikoa wana nguvu hiyo basi upinzani ungekufa kabisa uchaguzi uliopita badala yake umeimarika.
 
Kama Mh Makonda akiweza kusimamia kwa vitendo kila anachoongea basi Dar es Salaam ingekuwa kama Milan au Madrid..Jamaa anamawazo mapana ila tatizo ni vitendo na watendaji wa kutekeleza anachosema. Kwa ushauri wangu ni bora angekuwa anachuja awe anaongea vile anavyoweza kutekeleza tu,,.. Unafikaje kwenye level ya shisha na sigara za kawaida wakati bado Bangi na Gongo zipo na zinapatikana kwa wingi hapa Dar..
Ndio maana nguvu itatumika kuwakabili nyie vichwa ngumu. Waungwana tumesikia tutatekeleza. Ukishughulikiwa wewe NUNDA sisi tutaacha moja kwa moja. Lakini ukiachwa tutakufuata. Nafikiri serikali itakuachia pumzi tu katika kukushughulikia wewe mkaidi hata ikibidi kukubaka, kukulawiti, kupiga, kukufunga yaani chochote ambacho kitakufanya ungie kwenye mstari wafanye ili uache nasi tusikufuate.
 
kwani wanatekeleza ilani ya ccm au kwenda kufanya kazi za serekali au wakuu wa mikoa wamekua wabunge sikuizi
 
Makonda mdomo ni Mali yake mi namuona amekuwa mc wa mkoa yeye anachowaza ni mashindano tu kila pakiitwa Leo we fikiria kuwa kila kinacholazimishwa hakifai kwa wananchi mkuu wa wilaya ni mwanasiasa tu hata wakiukataa ukweli nmeshangaa kuona anasema mameya wasiwapangie cha kusema wakuu wa wilaya anajielewa kweli huyu
 
Ndio maana nguvu itatumika kuwakabili nyie vichwa ngumu. Waungwana tumesikia tutatekeleza. Ukishughulikiwa wewe NUNDA sisi tutaacha moja kwa moja. Lakini ukiachwa tutakufuata. Nafikiri serikali itakuachia pumzi tu katika kukushughulikia wewe mkaidi hata ikibidi kukubaka, kukulawiti, kupiga, kukufunga yaani chochote ambacho kitakufanya ungie kwenye mstari wafanye ili uache nasi tusikufuate.
Seriously!
 
Seriously!
Lazima mkaidi wa makusudi atendewe tofauti na mkaidi wa kutokujua mantiki ya anachokipinga. Kiala hatua hata utaalamu wa kumtambua mpingaji wa makusudi itatumika na kujua akifanyiwa nini atashika adabu itatumika pia. Watu tutii sheria bila shuruti
 
Wakati wakiapishwa Ma D.C. wa DSM Yule wa Ubungo sijamsikia kabisa maana wenzetu wa kinondon mkuu wao ameanza na agizo la Nyumba kupakwa rangi. Nikawa najiuliza huyu wa wilaya mpya kaanza na nini?
 
Back
Top Bottom