Yaliyojiri Kutoka Ikulu: Mahojiano ya Rais John Magufuli na Wahariri wa Vyombo vya Habari

Atueleze kwa nini watoto wetu wamekosa mkopo wa elimu ya juu ili hali aliahidi kuwa hakuna mwanafunzi atakaekosa mkopo?
Lipa kodi kwanza mwambie mwenyekiti wa kule alipe kodi anazodaiwa na NHC hizo ndio husomeshea watoto wetu kama wanakwepa kulipa kodi na kukimbilia mahakamani unadhani serikali itatoa wapi pesa ya kusomeshe watoto wetu,nadhani hata wewe hulipa kodi ndio maana unaloloma tu hapa ,fanya kazi na ulipe kodi watoto watapata mikopo,mikopo haitelemushi kama mana jangwani
 
Jamani tuache unafiki...sasa hivi usiku nimeangalia hotuba ya mh Rais..mbona kasema vizuri au kwa kuwa wengi ni wapinzani wake na kwa kuwa hawataki mafanikio yake.

Ila kaeleza ukweli kuwa kunawanaccm wa ovyo kweli na wapiga dill kuliko hata wapinzani. Kasema vizuri kabisa watu kutoka ccm wengi wau ndo wamefilisi mabenki.

Sasa kwa maelezo haya ya ukweli, ubaya wake ni upi mpaka watu wakawa wakutukana tu na kuponda kuwa hakuwa critical. Sielewi tulitaka maelezo gani au kwa kuwa kawataja baadhi ya wanaccm kufirisi benki na kula hera za kiwanda lindi au kwa kuwa baadhi ya wapinzani wamepiga za NSSF na NHC na hawataki kulipa.

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni... Mie nampongeza mh rais kwa ufafanuzi wake.
 
I... Suala la Lugumi i.e ikumbukwe kua mh. Rais amekua akitolea ufafanuzi masuala kadhaa lakini hili hajawi ligusa, wangemuuliza
II...Kila mara anasisitiza watu wanao lalamika pesa hakuna mtaani ni wale wapiga dili waliozoea kupata hela ktk njia zisizo sahihi, kwahyo ukifanya kazi hela utapata tu, Huyu Mh. Rais alikuja hadharan na Akasema "HELA HAKUNA MTAANI KUNA WATU WAMEFICHA HELA MAJUMBANI KWENYE MAGODORO, SO ANAUWEZO WA KUCHAPISHA HELA MPYA MDA WOWOTE ILI AWAKOMOE WALIOFICHA, Swali kwake mbona anakataa anasema hela ipo mda mwingne anasema hakuna TUSHIKE LIPI TUACHE LIPI !!?
III..Kwenye hotuba yake ya kwanza Bungeni toka awe Rais alisema kua ktk safu yake ya uongozi atakao wachagua kiongozi atakae pata na kashfa au shutuma chafu, ITATOSHA KUMUONDOA KTK WADHIFA WAKE, SWALI KUNA VIONGOZI WENYE DHAMANA YA JUU TU HUSUSSANI MAWAZIRI WAMEKUMBWA NA KASHFA KUBWA TU TOKA AMEWASHAGUA LAKINI HAKUNA HATUA ZILICHUKULIWA JUU YAO.... TUKIMTOA Mh. C.Kitwanga !?

MASWALI MENGINE ONGEZEA MDAU.... ILA USIMUULIZE MH. RAIS ETI NI NINI HOBI YAKO !? YAKO TUTAPATA CHAKULA KWELI !?
 
Jamani tuache unafiki...sasa hivi usiku nimeangalia hotuba ya mh Rais..mbona kasema vizuri au kwa kuwa wengi ni wapinzani wake na kwa kuwa hawataki mafanikio yake.

Ila kaeleza ukweli kuwa kunawanaccm wa ovyo kweli na wapiga dill kuliko hata wapinzani. Kasema vizuri kabisa watu kutoka ccm wengi wau ndo wamefilisi mabenki.

Sasa kwa maelezo haya ya ukweli, ubaya wake ni upi mpaka watu wakawa wakutukana tu na kuponda kuwa hakuwa critical. Sielewi tulitaka maelezo gani au kwa kuwa kawataja baadhi ya wanaccm kufirisi benki na kula hera za kiwanda lindi au kwa kuwa baadhi ya wapinzani wamepiga za NSSF na NHC na hawataki kulipa.

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni... Mie nampongeza mh rais kwa ufafanuzi wake.
Maneno kuntu
 
Sina hakika Kama wamequote vizuri but Kama ni nchi ya Kenya tu ndo inayotegemea kujenga viwanda Tanzania basi twaweza kuwa na wakati mgumu!

Swali(Rioba): Unasisitiza uchumi wa viwanda, Tanzania imeshawahi kuwa na viwanda vikafa, kuna watu wanaona hili swala waachiwe watu binafsi, wewe unaoneje?


Jibu: Ilani inasema tunataka kujenga nchi ya viwanda, huwezi kutegemea serikali katika kujenga viwanda ndio maana nikasema kuna makampuni kutoka Kenya na sio makampuni ya watu binafsi.
 
haa haa majibu ya mtukufu yanayochanganya ni mengi. hata lile la ajira kuanza serikalini limeacha masuali mengi mtaani mkuu....
 
Mimi naomba ku uliza. Kitu gani au kuna siri gani ambayo wafanya kazi au baadhi za taasisi za serikali wanakuwa. Mashabiki wa moja kwa moja na chama tawala wanaogopa nn ?? Au wanatishwa nn ??
 
Hebu tuondoe itikadi za kisiasa na tumpe muda Raisi wetu....halafu baada ya miaka mitano ndo tuone ametupeleka wapi
 
Habari wana jamii forum!

Ni matumaini yangu mnaendelea vizuri na majukumu hasa baada ya jana kujua kwamba tuna wahariri wa habari wa aina gani. sipendi nijikite huko na kuzisemea taaluma za watu la hasha! napenda kusemea kile nilicho jaribu kukisoma toka kwa mh. JPM kwa ocasion ya jana katika ile press conference

1. Kuna mambo mengi anayajua, anatamani ama anayafanya ila kwangu mimi nimeona kana kwamba hayapo organized kiasi kwamba yapo ki- one man show ambayo in his absence inaweza ikawa hatari kwa mstakabari wa nchi. na sidhani kama yanawekwa kwenye plan kiasi hata mwengine anaweza ya follow in succession. Kifupi rais inaonekana ana plan nyingi kichwani na huenda anajua yeye tu na akihisi sasa anataka afanye bas ndo ana- disclose plan yake.
2. Hakuna swala la katiba kwani haipoo kabisa katika plan yake, hivyo tuendelee na hii iliopo..kwake katiba si kitu kwani yale ni maandishi tu hata yawe yamepambwa kiasi gani hayasaidii kitu....haya aliyatanabaisha mwenyewe jana..kwa hiyo tumwache ainyooshe nchi. kwa hili mh. rais halijakaa sawa kwani hata kama atakuwa na mawazo mazuri kiasi gani, au arudishe maadili kiasi gani kama hayaja wekwa katika maandishi yani katiba,, kimsingi ndo sheria mama basi ajue kwamba atainyosha nchi hii kwa kipindi yeye yupo na kama ataachia madaraka bas rais ajaye atafanya atakalo kwakuwa hakuna kifungu kinacho mbana kuyafuata yale mema yalioachwa na mtangulizi wake kwa mdomo na vitendo pekee. kwa maoni yangu, katiba ni jambo mhimu sana katika kuinyoosha tanzania ya leo na ya kesho. Hata kama haikuwa katika agenda yake basi namwomba angelihuisha swala hili ili matamanio ya tz anayoitka iweze kuwekwa katika katiba ili hata yeye Rais akitoka madarakani tuweze kumbana mrithi wake kikatiba.
3. swala la mswaada wa sheria ya habari na waandishi wa habari. nilimsikia akisema kwa kinywa chake kwamba " kwa hili nisiwe mnafiki kwamba mswada ule ukifika kwangu nausaini siku hiyo hiyo". lo jambo hili limenifanya nimuelewe kivingine mh. rais, yani mswada ukija lazima ausaini, kwamba bilabkujali kilichomo humo kizuri au kibaya yeye ni kuusaini tu kwa sababu tumechelewa sana. sijajua tunakimbilia wapi,. nilitegemea aseme nitaupitia na kama nikiona unafaa nitasaini ikiwa haufai bas utarudishwa bungeni kujadiliwa upya . sasa kusema ukiletwa tu lazima nisaini siku hiyohyo inatia waswas kuna nn ndani ya hili.

mimi nimejaribu kuyaelewa hayo. ila kumuelewa mtu ni something relative na si rahis wote tukamwelewa sawa...na jinsi vile nilivyomwelewa ndicho nimeainisha wasi wasi iliyoko wangu.huenda mwingine atakuwa amemuelewa tofauti bas si dhambi kushare understang.
 
Wazo la leo.....................

Mihimili ya nchi ni mitatu, Bunge, Mahakama na Serikali - ILA mhimili mmoja kati ya hiyo mitatu umechimbiwa chini zaidi...
JPM.

Magufuli: "Nilikuwa nabeep, simu ikajipiga"
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom