Yaliyojiri kumbukizi ya miaka 34 ya kifo cha waziri mkuu Sokoine huko Monduli

Freed Freed

JF-Expert Member
Jun 27, 2017
6,218
6,455
Habari wanajukwaa wa JF siasa.

Siku ya alhamisi kama Leo 12/04/1984, jemedari wa majemedari, mzalendo wa kweli na mwenye udhubutu wa thati na kiongozi mojawapo mzuri kushuhudiwa nchi hii, Waziri mkuu wa Tanzania Edward Moringe Sokoine alifariki ktk ajali ya gari eneo la Dumila Morogoro.

Leo anatimiza miaka 34 tangu atoweke akiwa na umri mdogo wa miaka 46 huku taifa bado likimhitaji.

Waliopo eneo la tukio muuendeleze uzi huu juu yanayojiri huko nyumbani kwao Monduli. Nimeleta Uzi huu tukio hili lisipite humu bila kujulikana kwani sisi Watanzani tu wepesi wa kusahau matukio muhimu ya Jamhuri yetu. Nasikia kuna misa kubwa huko Monduli- Arusha.

UPDATES: Niseme tu Wana JF na Watanzania wengine ambao wangewrmeza kuripoti tukio hili jukwaani, Jana hamjaitendea haki siku hii. Mada imeachwa ukiwa huku mkiripoti matukio mengi amayo hata wakati mwingine huwapa mods wakati mgumu.
 
Attachments

  • sokoine.jpg
    sokoine.jpg
    55.3 KB · Views: 85
sijawahi kumpata mdadavuzi wa mambo hasa akanipa kinagaubaga juu ya jemedar huyu kuna knowledge gape kubwa sana kwenye akili yangu juh ya sokoine
 
*HUYU NDIO EDWARD MORINGE SOKOINE*

Tarehe kama ya Leo 12/04/1984 Taifa lilimpoteza kiongozi wake shupavu, aliyekuwa Waziri Mkuu Hayati Edward Moringe Sokoine, kufuatia ajali ya gari eneo la WAMI-DAKAWA Kilomita 35 nje kidogo ya mji wa Morogoro. Waziri Mkuu huyu alikuwa akitokea Dodoma kuelekea Dar es Salaam baada ya kufunga Kikao cha Bunge mjini Dodoma.

Baada ya kuagwa kiserikali Jijini Dar, marehemu Sokoine alisafirishwa kwenda Monduli Juu Arusha kwa mazishi.

Atakumbukwa kama kiongozi shupavu na ambaye alikuwa hacheleweshi utekelezaji wa jambo pale linapoonekana linatakiwa utekelezaji wa haraka na madhubuti.

Alipigana kupunguza rushwa na ufujaji wa mali, pia ulimimbikizaji wa mali mikononi mwa wachache (Ufisadi).

*WASIFU WA EDWARD SOKOINE*

Edward Moringe Sokoine alizaliwa tarehe 1 Agosti 1938 alikuwa Waziri
Mkuu wa Tanzania tarehe 13 Februari 1977 hadi tarehe 7 Novemba
1980 tena akawa Waziri mkuu toka tarehe 24 February hadi tarehe
12 Aprili 1984.

Alikuwa ni mtu aliyependa usawa kwa kila mtu aliamini
kila mtu anaweza kuwa na maendeleo kama akijituma katika kilimo
na sehemu alipo pamoja na kujitegemea akiwa ni wakala wa
mabadiliko katika nchi, mtu asielaumu na mwaminifu.

Alizaliwa Monduli Mkoani Arusha Tanzania, alipata elimu
ya msingi na sekondari katika miji ya Monduli na Umbwe toka mwaka
1948 hadi 1958.

Mwaka 1961 alijiunga na chama cha TANU
baada ya kuchukua masomo katika Uongozi nchini Ujerumani 1962
hadi mwaka 1963. Aliporudi kutoka Ujerumani alikuwa Afisa Mtendaji
wa Wilaya ya Masai, tena akachaguliwa kuwa mwakilishi wa jimbo
la Masai.

Mwaka 1967 alikuwa naibu waziri wa mawasiliano, usafiri
na kazi. Hatua nyingine katika maisha yake alijitangaza
mpaka kuwa Waziri Mkuu 1970.

Mwaka 1972 alihamia kwenye Waziri wa usalama. Mwaka 1975
alichaguliwa kwenye Bunge tena wakati huu kupitia Monduli.
Miaka miwili baadae akawa Mjumbe wa Kamati kuu ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM), 1977 alianza muhula wa kwanza ofisini akiwa
Waziri Mkuu wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania.

Muhula huu
ulidumu hadi 1981, baada ya kutulia kwa kipindi cha mwaka alikuwa
tena Waziri Mkuu tena mwaka 1983, alikaa mwaka mmoja ofisini
mpaka alipofariki Aprili 1984 kwa ajali ya gari.

Kutokana na heshima na mchango wake kwa Taifa, kuna Chuo Morogoro
Tanzania kilianzishwa kinaitwa jina lake (Sokoine University Of Agriculture (SUA)
kilianza mwaka 1984 kama chuo cha kilimo kinachotoa diploma
katika kilimo. Chuo hicho kikaongezwa hadi kutoa mchepuo wa
kilimo mwaka 1969 chini ya Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam.

Sokoine alikuwa kiongozi wa mfano aliyekataa kujilimbikizia Mali bali alikubali kupunguza Mali zake ili aweze kuwatumikia vyema Watanzania.

Utaendelea kukumbukwa daima na Watanzania kutokana na uzalendo, ushujaa na nia ya dhati ya ujenzi wa Taifa la Tanzania. Ni viongozi wachache sana nchini wenye roho na kariba kama yako.

Sokoine alikuwa kiongozi wa mfano ambaye daima alisimama upande wa umma.

Hakika, Edward Sokoine alikuwa kiongozi wa mfano wa kuigwa kwani aliishi kama ambavyo alikuwa akiyahubiri.
IMG-20180412-WA0004.jpg
 
Naomba wasifu wake wa kitaaluma uliokamilika badala ya kutuwekea "hints" tu hapa.
 
Nilikuwa Primary school du longi. Nyerere alitutangazia na yeye alishindwa kuvumilia machozi yalimtoka
 
nyerere_and_sokoine.jpg

Hayati Edward Moringe Sokoine akiwa na Hayati Mwalimu Julius Nyerere wakijadili jambo.

Nakumbuka mimi pia nilipanga mstari barabara ya Morogoro kuuaga mwili wa Hayati Edward Moringe Sokoine.

1. Hakukuwa na uchunguzi rasmi juu ya kifo cha hayati Sokoine yaani serikali ya Mwalimu Nyerere haikuwa tayari kuamuru uchunguzi wa kina ufanyike na hata kukataa msaada ya Scotland Yard ya Uingereza.

2. Hayati Sokoine ndiye alietarajiwa kuja kuwa raisi wa Tanzania baaada ya hayati Mwalimu kuacha uraisi.

3. Kulikuwa kumejengeka hofu kwamba endapo Hayati Edward Sokoine angekuwa raisi wa Tanzania, basi Mafisadi wengi wangetupwa magerezani.

4. Hayati Sokoine hakuwa na doa la Ufisadi na alichukia Ufisadi na wahujumu uchumi.

Kipindi cha 1979-1984 hali ya uchumi Tanzania ilikuwa ngumu sana na kwa wale vijana wenzangu wa wakti ule mtakumbuka kupewa madaftari kwenda kupanga foleni za kuchukua chakula cha mgao kutoka NMC.

Nchi ilikuwa ndiyo imetoka kupigana vita vya Uganda hivyo kukosa fedha katika akiba ya fedha za kigeni na pia kukosa hata fedha za kulipa mishahara wafanyakazi kwa wakati.

Hayati Sokoine aliamua liwalo na liwe na akaanzisha kampeni nchi nzima kuhakikisha watanzania wanazalisha mali na kuwa na akiba ya chakula ya kutosha.

Moja ya hotuba zake alizotoa wakti ule ni hii ifuatayo ambayo aliitoa mwezi wa October mwaka 1983-

"Wajibu wa kila Mtanzania, kila familia na kila anayekula ni kujilisha mwenyewe. Si wajibu wa Taifa kumlisha mtu. Unaweza ukasaidiwa unapopatikana na janga. Lakini kama hakuna janga ni wajibu wa kila mtu aweze kujitosheleza kwa chakula na atoe ziada kwa Taifa" - Edward Moringe Sokoine.

Tunakukumbuka daima mzee wa Monduli.
 
Ninakumbuka msure alikuwa analeta mchele wa kitumbo. Alituambia tuupime kabla ya kupika maana kuupata ilibidi aache kazi kutwa nzima alishinda NMC. Umenikumbusha mbali sana
 
Habari zenu wana JF siasa.

Jana nilikuja na Mada " Yanayojiri kumbukizi ya miaka 34 ya kifo cha waziri Mkuu Sokoine ". Niliwaomba Watanzania na wana JF waliopo eneo la tukio watupe mrejesho kila muda nini kinajiri ktk kumbukizi hiyo huko Monduli.

Hakuna kilichofanyika zaidi ya blaablaa humu jukwaani. Narudia tena tuyape umuhimu matukio muhimu ya Taifa letu. Jana waziri Mkuu Kassim Majaliwa alikuwepo ktk kumbukizi hiyo lakini hakuna mtiririko wa matukio yaliyojiri huko yaliyoletwa humu jukwaani.

Kumekuwa na mada za ajabu humu hadi kuwapa Mods wakati mgumu. Matukio muhimu yakipuuzwa.
 
Eti watu wengine wanamfananisha sokoine na mtu ambaye hajawahi kuwa hata balozi wa ccm wa nyumba kumi kumi
 
Back
Top Bottom