Yaliyojiri kuagwa kwa mwili wa Samuel Sitta, Viwanja vya Karimjee

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397


Fuatilia shughuli ya kuaga mwili wa aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pia Spika wa Bunge Maalum la Katiba(BMK), Marehemu Samwel Sitta.

Rais Magufuli ataongoza waombolezaji kuuaga mwili wa Marehemu Sitta katika Viwanja vya Karimjee.

======

Baada ya Ibada fupi iliyoongozwa na Askofu wa KKKT-DMP (Dayosisi ya Mashariki na Pwani) Dk Alex Malasusa sasa unasomwa wasifu wa Marehemu, Mzee Samuel Sitta.

Waziri wa Ofisi ya Rais Utumishi, Angela Kairuki anasoma salamu za rambi rambi kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda anatoa historia ya namna alivyofahamiana na Mzee Samuel Sitta.

Msemaji wa Chama cha Mapinduzi(CCM) Christopher Ole Sendeka anasoma salamu kutoka chama hicho.

Neno kutoka kwa msemaji wa familia ambaye ni Binti wa Mzee Samuel Sitta, Caroline Sitta.
 
Leo kuna shughuli ya kuaga mwili wa aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pia Spika wa Bunge Maalum la Katiba(BMK), Marehemu Samwel Sitta.

- Rais Magufuli ataongoza waombolezaji kuuaga mwili wa Marehemu Sittakatika Viwanja vya Karimjee.
 
Nilichoshuhudia wiki nzima hii, na kitakachoendelea mpaka mazishi yake ni kiwango kikubwa cha unafiki usiomithilika utakaoonyeshwa na kila mtu atakayepata nafasi ya kuongea mbele ya camera
Marehemu atapambwa kwa lugha tamu na maneno yote mazuri utadhani alikuwa malaika na hajawahi kukosea katika maisha yote! Na hii tabia iko kwa Marehemu wote hasa viongozi wa kisiasa
Mzee Sita keshafariki apumzike kwa amani ila tupunguze unafiki wa kusifia kunakopitiliza
 
Back
Top Bottom