Yaliyojiri: Kongamano la Katiba: 15 Januari 2011 Nkrumah UDSM

Prof:Shivji anasema uzuri wa katiba hautokani na ibara zake,bali kushirikishwa kwa wananchi wote katika kuandaa katiba.Tunahitaji katiba mpya kwa sababu katiba iliyopa hakuwashirikisha wananchi.Katiba lazima iwe na uhalali wa kisiasa na uhalali wa kisheria.
 
Ni vema baada ya kongamano mkamuhoji akilinganisha na kauli aliyoitoa amejifunza nini katika köngamano hili
 
Issa Shivji, KICHWA, anamwaga vitu si vya kawaida. Huyu Mzee ni kichwa.
 
Prof:Shivji anasema historia ni muhimu sana katika mchakato wa kuandaa katiba mpya.Historia inasema tumekuwa na katiba mpya 5.Katia ya kwanza ni ile ya uhuru ambayo haikutokana na wananchi ilitoka katika bunge la Uingereza.Mwaka 1962 tukawa na katiba ya Jamhuri ambapo bunge la kawaida likajigeuza kuwa bunge maalum likiwa na wabunge pekee wa TANU.Katiba ya tatu ni ile ya mwaka 1964,ilitokana na muafaka kati ya Tanganyika na Zanzibar ambayo pia haikuwashirikisha wananchi.Katiba ya nne ni ile ya mwaka 1965 ambayo ikafuta rasmi mfumo wa vyama vingi,na chama cha TANU NA ASP vikashika hatamu.Katiba ya sasa ni mwaka 1977 ambayo ilitokana na nia ya kunganisha vyama vya TANU na ASP.Rais Nyerere wakati huo akatoa tangazo kwenye gazeti la serikali Na. 30 ya tarehe 25/5/1977 ya kutunga katiba mpya na kuwateuwa wajumbe 20,10 kutoka bara na 10 kutoka visiwani ambayo pia ndio waliohusika kutunga katiba ya CCM.
 
Shivji anaikosoa uundaji wa katiba ya 1977.kiufupi mambo yalipelekwa haraka haraka.wananchi hawakushirikishwa.hivyo haina political legitimacy na pia kuna mashaka ya uhalali wa kisheria
 
Back
Top Bottom