Yaliyojiri: Kongamano la Katiba: 15 Januari 2011 Nkrumah UDSM

Wanajamvi lile kongamano la KATIBA ni sasa live ITV, mtaniwia radhi kuwataarifu kuptia jukwaa hili. Lengo langu ni kutaka wengi mlijue mapema maana jukwaa hili linatazamwa na wengi muda huu. Mods mwaweza peleka kunakohusika. Kwa kifupi Pr.Shivji kaanza kwa kupewa Dkk45 na atafuatiwa na Jenerali Uliwengu dkk 45 vilevile. Ngoja nivute soseji na kawaha ili niwape zaidi....Katika wageni nimemwona Renatus Mkinga!
 
Dhana ya katiba kuwa mkataba kati ya wananchi na watawala imepitwa na wakati.
Dhana ya kisasa ;katiba ni muafaka wa kitaifa hivyo ni muhimu kushirikisha wananchi.
 
Mh. John Mnyika ameingia hapa punde wakati huohuo Prof. Shivji ameanza kukotoa ungwe yake na kusema chimbuko la katiba ni people's sovereignty, na kuwa katiba kwa mujibu wake ni mwafaka wa kitaifa.
 
Prof:Shivji inasema katiba ni muafaka wa kijamii au kitaifa na sio mkataba wa watawaliwa na watawala,kwa hiyo katiba lazima katiba itokane na watu ambayo ndio msingi wa dola au mamlaka.
 
Mapungufu ya katiba sio hoja ya kubadilisha katiba.
Katiba zote zina mapungufu na zina viraka.
Umri wa katiba si hoja.
 
Back
Top Bottom