Yaliyojiri kikao cha Rais Magufuli na Mawaziri, Makatibu Wakuu, MaRCs, MaRAS na TRA

Mkuu acha kutumika kisiasa maana kauli zilizotolewa leo ni za kisiasa maana kama angekua anataka suluhisho suluhisho husika lingewekwa kisheria
 
ja ajabu hakuna aliyeuliza kila kitambulisho kimegharimu sh.ngapi na hizo pesa za kutengeneza hivyo vitambulisho zimetoka kwenye fugu gani,hapo ndipo ingejulikana ni hasara au ni faida.hivi hawa viongozi wetu hawalioni hilo?au kuuliza swali kama hilo ni uhaini?mimi na elimu yangu ndogo nimliona hilo ndilo lilikuwa la msingi sana kujua,hivi hao na usomi wao wameshindwa kuelewa kweli?
 
Kwanza kabisa Namshukuru Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema kwa Neema Zake Tumeweza kuufikilia Mwisho wa Mwaka 2018 na natumai Kwa Neema Zake tutavimalizia visiku vichache vilivyosalia kabla ya kuingia mwaka 2019.

Sasa nijikite kwenye Pongezi zangu pamoja na ushauri wangu
Ndg Rais nachukua Fursa Hii kukupongeza sana kwa jitiada zako zakuwapigania ndugu zako watanzania na wanyonge wanchi hii. niukweli usio nachembe ya unafiki kwamba ni juhudi zako madhubuti kabisa za kuwapigania wafanyabiashara wadogo wadogo wataifaili, Ambao kwa muda mrefu wamekua wakipata changamoto na manyanyaso mengi kutoka kwa manspaa za miji pamoja na TRA.

Niukweli usiopingika kwamba kutokana na mifumo ya kodi pamoja na makadirio ya biashara zao yallikua yamewafanya wawe kama digi digi katikati ya kundi la simba wakali.

unakuta mimi nina biashara ya duka dogo la reja reja. nanapenda kuchangia kodi kwa ujenzi wataifa langu, naamua kwenda TRA kwa lengo lakupata TN namba yautambulisho wa mlipa kodi. natoa ushirikiano mzuri kwa mkadiriaji, namwambia mtaji wangu ni Milion 1 mpaka 2 ananiuliza kwa siku unauza kiasigani namwambia kwa siku nauza elf 20 mpaka 30 cha ajabu anakukadiria kodi kwenye iyo iyo ela ya mauzo ya siku, hajui kwamba iyo ela ukipiga mahesabu wewe unaweza katika iyo ela ukiikokotoa unajikuta wewe unapata elf 3 kwa siku kutoa ela ya manunuzi katika vitu ulivyo uza kwa siku iyo katika iyo elf 20 mpaka 30

tuje kwa machinga na mama lishe waliowengi katika nchi hii, hawa wamekua wahanga wakubwa kwa askari mgambo wa manspaa za miji. unakuta mtu anatoka asubui kwenda kutafuta rizki yake halali lakini anakumbana na migambo, na watu wa ushuru wanawatoza ushuru ambao ukipiga mahesabu unakuta jioni amegawana kile kidogo na watu waushuru nakujikuta hanakitu.

lakini kwa utaratibu huu sasa kila mjasiria mali mwenye mtaji mdogo usiozidi milion 4 atapata kitambulisho hiki, nakumwezesha kujijenga kibiashara pamoja na kukuza mtajiwake, ili mwisho wa siku baada yakukuza mtaji wake awezekuchangia zaidi kodi kwaajili ya ujenzi wataifa hili.

MWISHO
Wito wangu kwa wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya.
siokwenda kuvifungia vitambulisho hivi maofisini kwao. waitishe mikutano ya hadhara nakupita na magari yamatangazo kuwatangazia wananchi wajitokeze hasa wale wenye sifa za kupata vitambulisho hivi kuweza kuhakikiwa na kupewa vitambulisho hivi.
Asante.
Hongera ndg kwa hoja yako najua utapata likes chache na pengne kurasa zinaweza kupungua si kwa sababu ulichokiandika. La hasha bali ni kwa mwenye kubeba theme ya ulichokiandika!!!! Yaani kwa sabab ya pongezi kwa Rais Magufuli!!!

Nakuomba usishangae binadamu tuko hvyo na mie nmpe moyo tu Rais wangu kwamba siku zote ni ngumu kila mwandamu umridhishe kwa kile unachokifanya ila pongezi hizi ni haki yake kbsa na paspo unafiki ni halali yake!!

Waache waseme ila naww umesema ukweli wako. Magufuli ndye kiongozi mwenye kujali makundi ya hawa watu... Mungu azidi kumlinda najua ana mengi anayotaka kulifanyia taifa hili.... Asivunjike moyo mungu atampigani!!

Asante sana ndg kwa ukweli wako na ubarikiwe sana!!!!
 
Mtindo wa ufanyaji biashara ni wa ovyo sijawahi kuona kuchekeana tu. Eti mtu unaweza kuwa unafanya biashara na kulipa kodi mtu mwingine anakuja mbele ya duka lako anafanya biasha hiyo hiyo halipi kodi eti biashara yake ni ndogo. Anaweza kushusha bei mkashindana naye na TRA wanamchekea na wakija kama ujafanikiwa kulipa kodi wanakusambaratisha yeyea anabaki. Hiyo ndo system ya biashara Tanzania.
 
Rais Magufuli ana lengo zuri na nchi hii. Aungwe mkono na kila mtanzania kwa kulipa kodi na kudai risiti.
 
Naona ni hotuba nzuri,ila katika kuwatambua walipa kodi
si ajabu tunaolipa kodi hatufiki hiyo 2.2 milioni.
sababu yangu ni hii hapa,unakuta mtu ni mfanyakazi
analipa kodi kila mwezi lakini hiyo kodi haiingii
kwenye TIN yake,badala yake kiduka chenye mtaji
wa milioni moja ndo ameandikiwa kama mlipakodi'
hapa najiuliza,kama kweli kodi yangu kama
mfanyakazi inatambulika na nahesabiwa na serikali
kama mlipa kodi,si ninapolipia kodi kiduka changu
si ninahesabika mara mbili?
Ni kwanini kodi zetu zisiingie kwenye TIN moja
kwa kila kodi ninayolipa ili kuepuka
kuhesabu mlipakodi huyo huyo mara mbili au tatu?
 
Asante mzee Membe, tishio lako linaweza kutoa mtu roho nchi ikabaki na faraja.
 
Safi Sana ifike kipindi watanzania wajifunze uzalendo kwa nchi yao Kama ambavyo Kenya wanafanya.
 
Mtindo wa ufanyaji biashara ni wa ovyo sijawahi kuona kuchekeana tu. Eti mtu unaweza kuwa unafanya biashara na kulipa kodi mtu mwingine anakuja mbele ya duka lako anafanya biasha hiyo hiyo halipi kodi eti biashara yake ni ndogo. Anaweza kushusha bei mkashindana naye na TRA wanamchekea na wakija kama ujafanikiwa kulipa kodi wanakusambaratisha yeyea anabaki. Hiyo ndo system ya biashara Tanzania.

Mkuu inakera sana sana ,hili suala
 
Back
Top Bottom