Yaliyojiri Kibandamaiti: Mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CUF Jumatano Septemba 09, 2015

Usipende kutumia uwingi hali ya kua uko peke yako et ccm tumewang'amua sema ccm nimewang'amua mapenzi yakizidi ni hasara majuzi amejitambulisha kua yeye ni mrutheli mnasema ni mbinu ya ccm wakati amesema kwa mdomo wake angalia maisha ya watoto wako na familia iliyo kuzunguka huyu mtu hanifai hata kidogo hapa kazi tu
 
Umofia kwenu,

Nimekuwa nafwatilia kwa karibu sana sera na mikakati ya wagombea wa urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania kama ACT wazalemdo, Chadema(a.k.a Ukawa) kiukweli kila mtu anajaribu kumiliki jukwaa miithili ya msanii anayetafuta tuzo.

Katika hali ilonishtua kidogo katika uzinduzi wa kampeni huko Zanzibar, nakupata kigugumizi juu ya nguli wa siasa Edward Lowassa ni kauli aloisema kuwa akipata uraisi

' ntakamilisha kazi ya Maalimu Seif alifanya kazi kubwa sana tutakamilisha serikali 3'- edward lowassa.

' hatima ya kila binadamu kaumbiwa kufa tutahalikisha tunafanikisha mambo yetu na si kuamuliwa' MANSOOR, wa cuf alokuwa anammadi lowassa nakuongeza tukishinda tutahakikisha katiba ya wanachi ndiyo inapita,

Zanzibar kuwa na mamlaka kamili & Tanganyika kuwa na mamlaka kamili halafu serikali ndogo ya Jamhuri ya muungano.

Najiuliza je lowassa anahitaji kweli awe raisi wa Jamhuri ya muungano ambayo itakuwa na mamlaka ndogo zaidi ya hizi serikali 2 yaani ya tanganyika & zanzibar ama ndo kupata tu kura za wazanzibar? maana anajua wanapenda wajitegemee??

Kwa hiyo tujiandae kuwa watanganyika?? maana kutwlekeza hilo jambo si kitu kidogo kama kuahidi ntajenga shule, zahanati, ntaleta maji n.k.
Mfano lowassa akaahinda maaana katika wagombea kuahinda yoyote sio ajabu ni jinsi tu atawashawishi watanzania.

anawajua wazanzibar vizur?? ahadi hii asipoweza itekeleza what will happwn?? wacha tuone mwisho wa movie

kwako kurudisha katiba ya wananchi ni kuvunja muungano!!
 
mnaochamgia kuwa ccm mnakuja kwa namna tofauti hamjasoma uzi vizuri, kuweni na utashi wakuchambua mambo.
ni wapi nimeonyesha chama changu hapo?? ni lini hasa mtaacha siasa ya chuki na isiyopenda mabadiliko?? mimi sina chama kwa ufupi huwa nachagua mgombea yoyote anayefaa sishabikii kundi fulani
 
Mleta mada hebu tueleze inakuaje uwepo wa serikali 3 iwe ni kuvunja muungano?

Baada ya hapo hebu nipe jibu, muungano wa sasa ni baina ya serikali(mamlaka) zipi?
 
Lowasa anafaa kuwa Rais wa kundi la mafisadi na wezi wenzake.
 
Wakuu salama!...

Jana mgombea wa Ukawa Ndugu Maalim Seif alikuna sana wananchi wa Zanzibar hasa baada ya kuonyesha mikakati mbalimbali ya kuwaokoa kiuchumi wakazi na kisiwa hicho...

Mgombea huyo kasema Ukawa wakipewa ridhaa ndani ya muda mfupi nchi hiyo itakuwa na uchumi kama wa Singapore. Kumbuka kijografia nchi hizo mbili zinafanana sana...

Ukirudi katika miaka ya 1960s, Tanzania ilikuwa na uchumi mkubwa sana kuliko Singapore na nchi zote za kusini mashariki mwa Asia, zikiwemo "Four Tigers". Na kwa kipindi hicho Tanzania ilikuwa inatoa msaada wa kiuchumi katika nchi hizo husika..

Ila leo hii baada ya miaka 50 nchi hizo za kusini mashariki mwa Asia zimeingia kwenye uchumi wa kati huku Tanzania baada ya miaka 50 kiwango cha umasiki ndio umeongezeka maradufu....

Mytake: CCM Must Gooooooo
 

Attachments

  • 1441865617424.jpg
    1441865617424.jpg
    26.3 KB · Views: 387
  • 1441865652899.jpg
    1441865652899.jpg
    28 KB · Views: 315
Habari wakuu,
Leo Jumatano Septemba 09, 2015 kuna mkutano wa kampeni CUF kwenye viwanja vya Kibanda Maiti Zanzibar, tuwe sote pamoja kujuzana yanayojiri kutoka mji wa karafuu.
======
=



10:16 Jioni: Mkutano umeshaanza na kinachoendelea sasa ni burudani kutoka kwa vijana wa mguu mbele, mkuu nyuma kutoka Zanzibar.

10:25 Jioni: Mkutano unaendelea na sasa ni zamu ya Super star Abdallah Issa kutoa burudani.

10:41 Jioni: Kipindi cha burudani kimeisha na sasa ni dua ya kufungulia mkutano

10:51 Jioni: Ismail Jussa anatoa muda wa dakika moja kama kumbukumbu ya ajali ya meli ya Mv. Spice Islanders

Salum Mwalimu: Narudia tena na najiamini, Kikwajuni biashara tumemaliza, sasa hivi natafuta tu za wengine. Hata wewe Maalim ni ceremonial tu. Tusijifanye tumesahau madhila tuliyosababishiwa na chama cha mapinduzi, mwaka huu kukuche kusikuche, Maalim Seif kitaeleweka tu.

Mzee Nassor Moyo: Salam zangu ni kidogo tu, nawaombeni wazanzibar wote wanaopenda amani na utulivu wa Zanzibar kura zao kwa maalim Seif.

Babu Duni: Leo si zamu yangu kuzungumza, kesho nina kibarua cha Kwenda Tanganyika juu kuwaletea ukombozi, leo ni zamu ya Maalim Seif.

Edward Lowassa: Nimeambiwa nikija Zanzibar ntapata mahaba, Shariff alikuwa anatuficha, alikuwa hataki tuje hivyo napendekeza tukishinda October tuje hapa. Pili nitoe malalamiko yangu, wenzetu watupa mabango yetu, nawaomba waache kutuingilia, uwezo wa kulinda kura zetu tunao. Mwisho wangapi watanipa kura, nahitaji kura nyingi sana, tukatae dhana kwamba wanaweza kutuibia! Wangapi watanipa kura tena!

Mansour Himid: Namshukuru mwanyezi Mungu, nataka niaze na kauli iliyo thabiti, niwaombe wazanzibari wenzangu mumridhie na mumpe kura zenu mheshimiwa Seif Sharif Hamad. Hakuna jambo lilokuwa na mwanzo lisiwe na mwisho na mwisho wa CCM umeshafika.

Mimi niliwekewa pingamizi na kwa uwezo wa mwenyezi Mungu nimeshinda, tumejiandaa kwa kupambana na mwaka huu watakipata pata na nitashinda jimbo la Chukuwani, yaliyokuwa ya msingi kuelekea 25 ya mwezi ujao.

Miongoni ya ya msingi ni mamlaka kamili ya nchi yetu, bila mamlaka kamili wazanzibar tutakuwa tunauziana maneno, serikali isiyokuwa na meno haiwezi kuwaletea wananchi maendeleo ya maana. Kwa mfumo huu wa muungano, wazanzibar hatuwezi kuendelea, CUF hatuna tatizo na muungano, tunaamini muungano ni majaaliwa ya mwenyezi Mungu, ni wajibu wetu kuusimamisha nakini si kwa mfumo huu wa CCM, tunataka kieleweke, tunataka mamlaka kamili.

Mwaka huu 2015 wazanzibar tubadilike, tuzinduke, hatma ya mwanadamu kufa, hatuwezi kukubali vikosi tulioundiwa, Maalim Seif hana miujiza, inabidi tujitume ndio maana tunahitaji nguvu ya pamoja ya wazanizbari, tumuombe mwenyezi Mungu uhai, tujitokeze kwa wengi dunia ione na tuache uoge na tufanye maamuzi.

Maalim Seif: Niaze kwa kumshukuru mwenyezi Mungu, naamini tutaumaliza mkutano huu chini ya ulinzi wake InshaAllah, niwashukuru viongozi na wanachama walioandaa mkutano huu, asante sana. Pia niwashukuru waliotupa burudani, vijana wa mguu mbele mguu nyuma na mzee Issa.

Muda tulionao ni mdogo sana, siwezi kuyaeleza mambo yaliyo kwenye ilani ya CUF kwa ukamilifu wake lakini mikutano hii itaendelea, kila mmoja na walioko nyumbani tunataka mamlaka kamili ya nchi yetu. Zimechukuliwa juhudi za kuleta tume ya jaji Warioba, mlitaka muungano wa mkataba, kwa busara ya tume wakaweka muungano wa serikali tatu. Nani kasaliti katiba iliyoletwa na chama cha mapinduzi, hata tuliowaamini walivyofika Dodoma waliufyata, wakakubali Zanzibar iendelee kudhalilishwa.

Nawaahidini wanannchi wa Zanzibar, mkinichagua nitashirikiana na Rais Lowassa kupata muungano wa serikali tatu. Hilo nawaahidi, hatuwezi kukubali kabisa kabisa. Tutaomba tume ya jaji Warioba ifanye kazi chini ya muongozo wa Rais Lowassa.

Ile ndoto yangu ya kuifanya Zanzibar kuwa Singapore ya Afrika mashariki iko pale pale, tutahakikisha tunajenga bandari ya kisasa kwa vitendo, nataka kuona uwanja ule unakuwa na cargo terminal, watu wachukue mizigo yao hapa badala ya Dubai.

Serikali nitayoongoza tutafungua benki ya uwekezaji kwa wazanzibar ili kutoa mikopo kwa vijana yetu, watatoa mikopo nafuu, masharti nafuu, kila mmoja atamudu. Tutafanya jitahada ya kuleta wawekezaji, vijana mpate ajira. Tukichukua serikali vijana mpate ajira pia ni dhamira yangu kuona suala la mafuta na gesi isiwe hadithi ya lele mama, nitaunda wizara ya mafuta na gesi ili tushughulie suala la mafuta na gesi.

Mengi niliyokusudia kuyasema muda umemaliza na sisi hatutaki kuvunja sheria, nawaombeni wazanzibari mnipe kura zote pia namuombea mumpe kura mheshimiwa Edward Lowassa.


I m so sorry Lowassa can't win presidential race.
#hapakazitu
. Imejipost
 
Last edited by a moderator:
Na huyo Maalim wako alikuwa part katika hiyo miaka hamsini naona alishindwa kuifanya au ata kuthubutu na sasa ivi pia yumo kwenye serikali ata mifano hajaonesha zaidi ya kununuliwa na white hair aseme na njaa zake kwanza.
 
Kweli wajinga ndio waliwao. Maalim kaiongoza Zanzibar kwa miaka yote hii ,kashika nafasi mbalimbali za uongozi kashindwa kuifanya zanziba kufanana hata na arusha.leo hii anawaambia wananchi kuwa ataifanya kuwa Singapore.nadhani wazanzibari hawaijuwi Singapore
 
Lowassa ni janga la kimataifa

Fafanua Mkuu nikuone wa maana.

Nijuavyo mimi Chenge kila dili chafu yumo, tuhuma ya RADAR ilisababisha Bunge la UK lijadili na kuiamuru Kampuni ile iludishe pesa yote ambayo nayo haijawekwa wazi iko wapi labda Membe atatwambia siku moja.

Lowassa hajawahi kujadiliwa kimataifa na mitambo ya RICHMOND mpaka leo ipo inalipwa na serikali kama SYMBION, je unaweza kutuambia pesa inayolipwa inaingia kwa mfukoni mwa Eddo au inakwenda wapi?
 
Kweli wajinga ndio waliwao. Maalim kaiongoza Zanzibar kwa miaka yote hii ,kashika nafasi mbalimbali za uongozi kashindwa kuifanya zanziba kufanana hata na arusha.leo hii anawaambia wananchi kuwa ataifanya kuwa Singapore.nadhani wazanzibari hawaijuwi Singapore

Unajua maana ya neno "KUONGOZA" au unalopoka bila kujua maana yake. Kuongoza ni kuwa mbele ya wote, huwezi kuwa wa pili, wa tatu au wa kumi ukasema unaongoza! Akili ndogo sana hii ya kupambanua mambo, mnatujazia server bure kwa ----- wenu.

Mbona tuliahidiwa mwaka 2005, Kigoma itakuwa sawa na Dubai, Mwanza sawa na Califonia na Tanga utakuwa mji wa Viwanda lakini leo wanakuja kutwambia yaleyale. Bora tuwape UKAWA nao wafanye yao maana CCM imetudanganya mno mpaka tumeshiba uongo!
 
Unajua maana ya neno "KUONGOZA" au unalopoka bila kujua maana yake. Kuongoza ni kuwa mbele ya wote, huwezi kuwa wa pili, wa tatu au wa kumi ukasema unaongoza! Akili ndogo sana hii ya kupambanua mambo, mnatujazia server bure kwa ----- wenu.

Mbona tuliahidiwa mwaka 2005, Kigoma itakuwa sawa na Dubai, Mwanza sawa na Califonia na Tanga utakuwa mji wa Viwanda lakini leo wanakuja kutwambia yaleyale. Bora tuwape UKAWA nao wafanye yao maana CCM imetudanganya mno mpaka tumeshiba uongo!

Sawa mkuu tumchaguwe maalim seif Zanzibar itakuwa kama Singapore.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom