Yaliyojiri kesi ya Mbowe na Wenzake Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Uhujumu Uchumi - Sept 17, 2021

Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
18,740
2,000
Man mbona unaonekana kama una matatizo ya afya ya akili? Chukua hatua mkuu usidharau jaribu kwenda hospitali uonane na psychologist
Wenye akili hawana muda wa kwenda mahakamani kutwa kucha halafu wanarudi kula kwa baba na mama
 

The Palm Tree

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
7,776
2,000
Hali ya ndani ya mahakama kuu Divisheni ya makosa ya uhujumu uchumi na Rushwa ni shwari

Leo tumepita getini bila bugudha na hakuna polisi wa nje zaidi ya hawa maalum wa mahakama

Hakika Jambo la jana kupigania haki ya mahakama na kutaka isimame kama mhimili huru ni nzuri sana

Jopo la mawakili wetu wa utetezi (mawakili wa Freeman Mbowe na wenzake) kama kawaida yao, limefika on-time, Mapema sana ikiwa sifa yake kuu nidhamu, Ushirikiano, upendo na kwenda na muda, pia kusikiliza na kujali hisia na sauti za ndugu, jamaa, marafiki wa wateja wao (watuhumiwa)

Ndugu zangu mnaouliza kuhusu shahidi wa leo ni nani, hakika wasikilizaji hatuwezi kufahamu. Hiyo ni kazi ya Jamhuri kuwasilisha jina la shahidi wao mbele ya mahakama kati ya wale mashahidi 24 waliotajwa kwenye preliminary hearing...

Hivi sasa ni saa 4 asubuhi na dakika zake 19 kwa saa za Afrika ya mashariki, bado mheshimiwa Jaji na mawakili wa upande wa Jamhuri (serikali) hawajaingia ndani ya chumba cha mahakama kuu Divisheni ya makosa ya uhujumu uchumi na Rushwa. Mahakama sasa imejaa TOP!

Pia, tunawashukuru jeshi la polisi kutoka moyoni kabisa, mmepungua ndani ya chumba cha mahakama, mbarikiwe.. Eeh! Mmeona watu wameingia wenyewe mahakamani, wamejipanga wenyewe na sasa wanasubiri mahakama ianze. SISI ni wastaarabu na tunahubiri ustaarabu kila siku #MboweSioGaidi

Hivi sasa ni saa 4 na dakika 25 saa za Afrika ya mashariki bado mawakili wa serikali na mheshimiwa Jaji hawajaingia ndani ya chumba cha mahakama kuu Divisheni ya makosa ya uhujumu uchumi na Rushwa..

Pamoja na kwamba polisi leo sio wengi kama siku zote, lakini kuna mzozo umeibuka hapa Mahakamani. Wananchi wanasema wamekosa nafasi za kuketi, hivyo wanaomba askari polisi wapungue mahakamani, wakaimarishe ulinzi wa raia na mali zao, ili nafasi zipatikane nyingi. Bado wapo!

Askari mmoja hapa anahamaki na kusema polisi na usalama nao wanayo haki ya kusikiliza mwenendo wa kesi maana ni open court na wanahoji kwamba tunapata wapi haki ya kuipangia mahakama nani wa kuingia na kukaa ndani? Swali hilo ukiwauliza wao kwanini walituzia jana, hawana jibu?

Raia bado wanasisitiza askari wasimame na kupungua mahakamani ndani, walinde watu na mali zao, ili wananchi wapate nafasi ya kuketi. Wananchi wanawakazia macho na kuwatambua. Lakini tunawaeleza wananchi watulie, waache askari hao wafuatilie kesi. Wasipate sababu kwamba VURUGU..

Hivi sasa ni saa 4 na dakika 53 kwa saa za Afrika ya mashariki, bado kesi inayowahusu Freeman Mbowe na wenzake watatu haijaanza, tunamsubiria mheshimiwa Jaji na mawakili wa serikali waingie ndani ya chumba cha mahakama.
Hivi sasa ni saa 5 na dakika zake 6 saa za Afrika ya mashariki.

Hali ya eneo la mahakama ni shwari kabisa, ni kata ya Sinza, wilaya ya Ubungo, Mkoani Dar es Salaam

Hali ya hewa ni mawingu kiasi na nyuzi Joto 27.7 inayoruhusu kabisa shahidi kuendelea na kesi, bila visingizio!

Pamoja na mheshimiwa Jaji kusisitiza Jana kuwa kesi ianze leo saa 4 kamili Kufuatia ombi la mawakili wa serikali, Lakini mpaka sasa, ni 5 na dakika 15 kesi bado haijaanza, lakini hatuelewi, labda sababu zilizo nje ya uwezo wao. Tuendelee kuwa na subira, maana yavuta kheri..

Mstari wa pili kutoka mwisho, wameketi waandishi wa habari (leo tupo nao live), Wameingia Kwa wingi sana kuliko Siku zote (inspiration), Leo na wao wamenufaika na msimamo wa Jana. Wabarikiwe.

Mstari wa mwisho (Backbench) wameketi watu mchanganyanyiko wakiwepo Polisi na TISS.

Sema kwa sauti mbowe sio gaidi

Unpopular opinion: wewe unadhani kwa kuchelewa huku mawakili wa serikali kuingia ndani ya chumba cha mahakama kuu Divisheni ya makosa ya uhujumu uchumi na Rushwa, Je, wanamshauri DPP aachane na hii kesi dhidi ya Freeman Mbowe na wenzake maana wanajua #MboweSioGaidi, namna gani?

Jopo la mawakili wa utetezi

1.Peter Kibatala
2.Jeremiah Mtobesya
3.Jonathan Mndeme
4.John Malya
5.Evaresta Kisanga
6.Hadija Aron
7.Maria Mushi
8.Gaston Garubindi
9.Seleman Matauka
10.Ferdinand Makore
11.Dickson Matata
12.Rita Ntagazwa
13.Alex Masaba
14.Michael Mwangasa

Habari njema sana, ule mtiti mdogo wa wananchi umesaidia benchi lilikuwa reserved kwa makarao, wameanza kukaa familia na ndugu wa watuhumiwa..

Ubishi na makavu yanasaidia sana.. Tusiache kuongea na kupiga kelele kuhusu haki zetu wakati wote ndugu zangu. Msiache kuongea.


Jopo la mawakili wa utetezi (wanaitwa mawakili wasomi, utake usitake), yaani mawakili wa Freeman Mbowe na wenzake wakijadiliana jambo la kitaalam.. Unaweza kuwapa jina, hebu pendekeza jina, hii timu yao inapaswa kupewa jina gani?

Pamoja na kwamba watuhumiwa wamefikishwa mapema (tangu saa 3 asubuhi) na mawakili wa utetezi kufika mapema ndani ya chumba cha mahakama kuu Divisheni ya makosa ya uhujumu uchumi, bado mawakili wa serikali hawajafika. Hivi sasa ni saa 5 na dakika 29 saa za Afrika ya mashariki

Shukrani za pekee leo zimuendee Wakili Gabriel Fikirini ambaye kafika mahakamani kwa mara ya kwanza akisafiri kutokea Jijini Mwanza kwa ajili ya kuongeza nguvu kwenye kesi ya Freeman Mbowe na na wenzake..

Wakili Deogratius Mahinyila (@AdvMahinyila) aliyetoka Jijini Dodoma hadi Dar es Salaam kuongeza nguvu tangu wiki iliyopita.. Niliwapa simulizi yake kwa ufupi, niwape tena? Umri wake ni mdogo mara 3 ya umri wa Humphrey Polepole na mara 5 ya umri wa Mzee Kabudi.

Wakili Deogratius Mahinyila (@AdvMahinyila) atakumbukwa akiwa mgombea wa udiwani kupitia Chadema Dodoma, kata ya Berega, alishitakiwa kwa makosa uhujumu uchumi, akiwa gerezani, Isanga (gereza katili) akafanya mitihani ya uwakili na kufaulu kuwa wakili wa mahakama kuu.
Duuh, hebu fikiri kwa sauti kubwa kidogo, kwamba;

1. Mawakili upande wa mashitaka waliomba kesi ianze mapema saa 4abh, Jaji/mahakama na mawakili wa utetezi wakasema, SAWA NA IWE HIVYO...

2. Leo ni siku ya kesi. Watuhumiwa wameletwa tangu saa 3abh...

3. Jaji Mustapha Siyani na mawakili wa upande wa mashitaka [yaani watengeneza kesi] mpaka karibu saa 6 mchana sasa hawajaingia mahakamani...!!

MASWALI;

å Unadhani katika mazingira kama haya mtu yeyote mwenye akili timamu anaweza kufikiri na kuja na conclusion gani eti...?

å Je, haudhani kuwa hii ni dalili ya mwisho za kushindwa kwa project hii ya Kingai na Simon Sirro IGP...?

NOTE: Ukiona taulo limetupwa ulingoni, usishangae..

Maana nasema hivi..

SHETANI/IBILISI HAJAWAHI NA HATAKUJA KUMSHINDA MUNGU YEHOVA..!!
 

kelphin kepph

JF-Expert Member
Dec 24, 2019
4,377
2,000
Man mbona unaonekana kama una matatizo ya afya ya akili? Chukua hatua mkuu usidharau jaribu kwenda hospitali uonane na psychologist

Kaka dawa ndio zinafanya kazi mkuu
Tuvumilie
Doctor alisema kwenye kipindi hiki mgonjwa anaweza asiwe anaelewa kitu
 

Stan Mashamba

JF-Expert Member
Apr 22, 2020
2,888
2,000
Duuh, hebu fikiri kwa sauti kubwa kidogo, kwamba;

1. Mawakili upande wa mashitaka waliomba kesi ianze mapema saa 4abh, Jaji/mahakama na mawakili wa utetezi wakasema, SAWA NA IWE HIVYO...

2. Leo ni siku ya kesi. Watuhumiwa wameletwa tangu saa 3abh...

3. Jaji Mustapha Siyani na mawakili wa upande wa mashitaka [yaani watengeneza kesi] mpaka karibu saa 6 mchana sasa hawajaingia mahakamani...!!

MASWALI;

å Unadhani katika mazingira kama haya mtu yeyote mwenye akili timamu anaweza kufikiri na kuja na conclusion gani eti...?

å Je, haudhani kuwa hii ni dalili ya mwisho za kushindwa kwa project hii ya Kingai na Simon Sirro IGP...?

NOTE: Ukiona taulo limetupwa ulingoni, usishangae..

Maana nasema hivi..

SHETANI/IBILISI HAJAWAHI NA HATAKUJA KUMSHINDA MUNGU YEHOVA..!!
Usichukulie poa. Ni mbinu ya kuwachosha wasikilizaji ili wakate tamaa kufatilia kesi hii. Ni mbinu ya kurejesha giza.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom