Yaliyojiri Kesi ya Mbowe na Wenzake Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi - 27/09/2021

Leo tena kama kawaida tunakuletea moja kwa moja yanayojiri kwenye Mahakama kuu , divisheni ya Uhujumu Uchumi , ambako kesi ya ugaidi unaogharimu kitita cha tsh laki 6 inaendelea.

---
Jaji ameshaingia

Kesi inatajwa
Kesi namba 16 ya Mwaka 2021, Jamuhuri dhidi ya Halfan Bwire, Adam Hassana Kasekwa (Adamoo), Mohammed Abdalah Ling'wenya na Freeman Aikael Mbowe

Jaji: Wakili wa Serikali

Wakili Kidando anatambulisha Jopo lake....
  1. Robert Kidando
  2. Nassoro Katuga
  3. Ignas Mwanuka
  4. Esther Martin
  5. Tulumanywa Majigo

Wakili Kibatala anatambulisha Jopo lake
  1. Adv Peter Kibatala
  2. Adv Sisty Aloyce
  3. Adv Gaston Garubindi
  4. Adv Idd Msawanga
  5. Adv Alex Massaba
  6. Adv Evaresta Kisanga
  7. Adv Hadija Aron
  8. Adv Michael Mwangasa
  9. Adv Faraji Mangula
  10. Adv Fredrick Kiwhelo
  11. Adv Nashon Nkungu
  12. Adv Jonathan Mndeme
  13. Adv John Mallya
Kwa Mshtakiwa wa Kwanza - Nashon Nkungu
Mshitakiwa wa Pili - John Mallya
Mshitakiwa wa tatu - Fredrick Kiwhelo
Mawakili Wengine wote ni Kwa mshitakiwa wa Nne Freeman Mbowe

Jaji: Siku ya Ijumaa shahidi( Mshtakiwa wa pili) alikuwa hajakamilisha Utetezi wake. Arejee kwenye Kizimba tuweze Kuendelea

Shahidi anaenda

Jaji: Wakili wa Serikali mpo tayari..?

Jaji: Upande wa Utetezi mpo tayari?

Wote wapo tayari

Jaji: Shahidi bado upo chini ya Kiapo kama tulivyokuapisha Siku ya Ijumaa. Mawakili wa Serikali watakuhoji Maswali na Baadae Upande wa Utetezi hususani Wakili wako anaweza kuja kukuongoza tena Kwa Kukuuliza Maswali. Unaweza kuchagua Kukaa au Kusimama

Shahidi: Nitakaa Mheshimiwa Jaji

Jaji: Bila shaka. Wakili wa Serikali Chavula unaendelea. Tafadhali endelea

Wakili wa Serikali: Naam Mheshimiwa

Wakili wa Serikali: Awali siku ya Ijumaa kabla hatujaahirisha, nilikuuuliza kuhusiana na wale waliokuvamia maeneo ya Rau hawakupata kujitambulisha, Kweli au Si Kweli

Shahidi: Kweli

Wakili wa Serikali: Wale watu Mlivyotoka pale kwenda Kituo cha Polisi hawakulueleza Majina yao akina nani.? Kweli au Si Kweli

Shahidi: Kweli

Wakili wa Serikali: Walivyokutoa Moshi kukuleta Dar es salaam hawakukueleza wao Majina yao ni Akina nani. Walipokupeleka Mbweni hawakukueleza Majina yao akina nani?

Shahidi: Kweli hawakunieleza

Wakili wa Serikali: Haukupata Kuwafahamu amajina yao wakati wote?

Shahidi: Niliwafahamu kwa wao alipokuwa wanaitana Majina yao na Nikaja kuthibitisha Majina yao hapa Mahakamani walipojitambulisha

Wakili wa Serikali: Wakati wa Kukusafirisha Moshi Kuja Dar es salaam Watu wale walikufunga Kitambaa Usoni?

Shahidi: ni Sahihi

Wakili wa Serikali: ni Jacket, Si Ndiyo?

Shahidi: ni Jacket ndiyo

Wakili wa Serikali: Hukujua ni akina nani unasafiri nao

Shahidi: Kweli kama nilivyoeleza

Wakili wa Serikali: Na hata Ulipofika Dar es salaam ukafikishwa Kituo cha Kwanza cha Polisi hukujua upo wapi

Wakili wa Serikali: We Jibu swali langu Kweli au si Kweli

Shahidi: Kweli

Wakili wa Serikali: Umedai ulipokuwa unasafirishwa Ulikalishwa Chini kwenye gari,Kweli au si kweli

Shahidi: Ni kweli

Wakili wa Serikali: Uliweza Kujua ni sehemu gani ya gari ..?

Shahidi: Nilipita Upande wa Kulia Kwa Uelewa wangu siyo Kwa Kuona, Nikafahamu nimekaa nyuma ya gari

Wakili wa Serikali: Ulikaa nyuma ya gari

Shahidi: Ndani ya gari,Sehemu ya Nyuma

Shahidi: Siwezi Kujua ni gari gani

Wakili wa Serikali: Unakubaliana na Mimi ukiwa Umefungwa Machoni uwezi Kuona .?

Shahidi: Ndiyo uwezi Kuona, ila ukiwa unatendewa unahisi

Wakili wa Serikali: Ukiwa umefungwa macho uwezi kuona hata kile kifaa wanachokusababishia Maumivu

Shahidi: Ni sahihi

Wakili wa Serikali: Nakurudisha Moshi,umesema walipokuwa wanakutesa Moshi walikuwa wabakuuliza Umekuja Moshi Kufanya nini

Shahidi: ni sahihi

Wakili wa Serikali: Wewe Ukajibu umekuja Moshi Kufanya VIP protection ni Sahihi

Shahidi: ni sahihi

Wakili wa Serikali: Ulisema ulipofika Dar es salaam kituo cha kwanza cha Polisi walikupa Chakula .?

Shahidi: ni sahihi

Wakili wa Serikali: Ni Chakula gani

Shahidi: Ugali na Mboga za Majani

Wakili wa Serikali: na wakati wote ulipokuwa pale hukufanyiwa Mateso

Shahidi: Sahihi

Wakili wa Serikali: na hata ulipokuwa Mbweni hakuna aliyekuja Kukupiga..?

Shahidi: ni sahihi

Wakili wa Serikali: Alipokuja Ramadhani Kingai alipolutaka Uthibitishe Marlezo yako na Kutia Sahihi alikupa Vitisho wala hakukupiga.?

Shahidi: ni sahihi

Wakili wa Serikali: Ni Lipi Mahakama ichukue kati ya haya Mawili,Ulielezq Mahakama kwamba Wakati unatoa Maelezo hapa Mahakamani,kwamba ulitoa Maelezo kwa sababu ulikuwa unateswa,Sasa unasema kwamba Kingai na wenzake hawakukupatia Mateso isipokuwa Walipa Vitisho tuh

Shahidi: Rudia swali lako

Wakili wa Serikali: Wakati wa Kesi Kubwa Umesema Kuwa Kingai wenzake walichukua Maelezo yangu baada ya Mateso,Leo unasema Alikuja Bwana Kingai kunitishia

Shahidi: Umeuliza wakati wa Kuchukuliwa Maelezo, Mimi wakati wote nilikuwa Chini ya Mateso

Wakili wa Serikali: Aahaaaaaa

Wakili Mallya: OBJECTION. Naomba Shahidi akiwa anatoa Maelezo yake apewe nafasi ya Kumaliza Kujibu Maswali

Wakili wa Serikali: Ulipokuwa Dar es Salaam hukuteswa isipokuwa Bwana Kingai alikutishia.?

Shahidi: Aliniuliza kuhusu Kupigwa siyo Kuhusu mateso,kwa sababu, Mimi nilikuwa Chini yao na Nimefungwa pingu, bado hayo kwangu ni Mateso

Jaji: Shahidi nafikiri ungejibu sasa hilo unalotaka wala hakuna tatizo kwamba uliteswa au lah

Jaji: Naweza kukusomea

Shahidi: Ningependa unisomee Mheshimiwa Jaji

Jaji: Kingai "Hakunipiga tulipokuwa Mbweni, alinipiga na Kunitishia" Sasa tuambie nini kilichokuwa kimetokea

Shahidi: Vyote vichukue

Wakili wa Serikali: Kwa hiyo Mahakama ichukue Vyote

Jaji: Sasa niandike vipi Hukutoa Maelezo na Ulitoa Maelezo ..?

Shahidi: Ananiuliza Mambo Mawili tofauti ambayo ajayatenganisha, Mimi nilitoa Maelezo Moshi Chini ya Mateso,nalisaini bila Mateso

Jaji: Nilisaini Maelezo bila Mateso lakini nisaini baada ya Vitisho

Shahidi: ni sahihi Mheshimiwa Jaji

Mahakama Kichekooooooo

Wakili wa Serikali:
Kabla ya Kuletwa Dar es salaam tarehe 07,Kabla ya siku hiyo uliwahi Kufika Dar es salaam.?

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Makazi yako yapo Dar es salaam.?

Shahidi: Hapana

Wakili wa Serikali: unafahamu wapi?

Shahidi: Kambi ya Jeshi Twalipo na Maeneo ya Uwanja wa Taifa

Wakili wa Serikali: Ujawahi Kufika Tazara.?

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Ulishawahi Kufika Mbweni

Shahidi: Hapana

Jaji: Kwa hiyo Kabla ya kesi ujawahi kufika Tazara wala Mbweni

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Hakuna Wakati ,unafikishwa Kituo cha Polisi wakakuacha wazi.?

Shahidi: sijwahi Kutolewa nje ya kituo cha Polisi

Jaji: Mnaeleeana kweli..?

Jaji: Kutoka Tazara kwenda Mbweni ulifungwa Jacket.?

Shahidi: Nilifungwa Jacket Usoni Mheshimiwa

Jaji: Wakili ulimaanisha hivyo.?

Wakili wa Serikali: Ndiyo Mheshimiwa

Jaji: Sasa nitaomba Mnapomtajia Vituo vya Polisi Mtaje na Majina

Wakili wa Serikali: Naanza Upya Ulitolewa akitambaa ama Jacket lako ulipofilishwa ndani ya Kituo cha Tazara

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Mpaka Unaingia Kituo cha Polisi Tazara ulikuwa umefungwa Usoni

Wakili wa Serikali: Moshi Mlikamatwa wangapi

Shahidi: tulikamatwa wawili

Wakili wa Serikali: Na nani.?

Shahidi: Na Mohammed Abdilah Ling'wenya

Wakili wa Serikali: Wakati wote unasafirishwa hukujua yupo wapi

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Kingai na Mwenzake Mahita,walieleza Mahakama kwamba waliwasafirisha wewe na Ling'wenya Kwenye gari moja

Shahidi: Kweli walitoa Ushahidi huo

Wakili wa Serikali: Hakuna Mtu aliyewaambia Mashahidi wale kuwa Si kweli Nyie hamkusafirishwa pamoja.?

Shahidi: sasa

Wakili wa Serikali: Jibu swali langu

Jaji: Je ulisikia au Hukusikia.?

Shahidi: Sikusikia

Wakili wa Serikali: Kama wakati wote unasafirishwa Mpaka unafikishwa Kituo cha Polisi Tazara ulikuwa hufahamu Mohammed Abdilah Ling'wenya yupo wapi, Kweli au si Kweli

Shahidi: Sahihi

Wakili wa Serikali: Ulikuwa peke yako Kwenye mahabusu

Shahidi: Nilikuwa peke yangu kwenye Chumba Changu, ila Mahabusu wengine walikuwa Kwenye Vyumba vyao

Jaji: Kwa hiyo ulikuwa Mwenyewe Kwenye Chumba cha Mahabusu..?

Shahidi: Ndiyo

Jaji: Hapakuwa na Mahabusu wengine..?

Shahidi: Walikwepo kwenye Vyumba vyao

Jaji: Hapa naona tusingeelewana

Wakili Mallya: Shahidi alitupa Picha Kuwa kuna mahabusu Yenye Vyumba Vidogo Vidogo na yeye alikuwa kwenye kichumba Chake ndani ya mahabusu

Jaji: Naomba Kusoma "Nilifunguliwa Jacket nikawa naona Sasa,nikajivuta hadi Mlangoni nikaanza kuona Mahabusu wengime wakiwa kwenye Vyumba Vyao" nafikiri ndicho nilichoandika

Jaji: Sasa tujielekeze Hapo

Wakili wa Serikali: Umesema ulikuwa Peke yako Kwenye Chumba

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Kushoto na Kulia palikuwa na Ukuta

Shahidi: Ni sahihi Kabisa

Wakili wa Serikali: Ulikuwa kwenye tafakari kwanini haya yananiyokea, nimekosa nini.?

washitakiwa 1,2,na 3 walikubali wanafahamianina wa wakiwa wanafanya kazi Ngerengere KJ92

Wahitakiwa 1,2, na 3 Walikuwa wanafahamiana kabla ya Kesi Kuanza


Wakili wa Serikali: Hukubisha kwamba kwamba hukuondolewa Jeshini kwa Maswala ya Kinidhamu, na asasa unasema Uliondolewa Jeshini kwa Maswala ya Afya

Shahidi: Siwezi kulijibia

Wakili wa Serikali: Kwanini uwezi Kulijibia

Shahidi: Documents zote sijawahi kuzitolea Maelezo, zilikuja na kuletwa na watu walioandaa

Wakili wa Serikali: Documents zipi hizi?

Shahidi: Zilioletwa kufungulia Kesi ya Ugaidi

Wakili wa Serikali: Ulisaini hukusoma.?

Shahidi: Nilisaini

Wakili wa Serikali: Na Mahakama ilikusomea.?

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Unasema Ulikuwa kwenye Misheni Congo

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali: Ulikuwa Battalion ya 3, wewe ulikuwa kikosi cha Mizinga

Shahidi: Hapana

Wakili wa Serikali: Wewe ulikuwa unafanya nini

Shahidi: Nilikuwa Special Force

Wakili wa Serikali: Huko Special Force ulikuwa unafanya kazi gani

Shahidi: Kazi zote

Wakili wa Serikali: Zitaje

Shahidi: Zote kuanzia kupika Mpaka Kwenda Vitani

Wakili wa Serikali: Huko Vitani huwa mnajihusisha na Kuteka Watu

Shahidi: Siyo kazi yangu kuzungumzia Maswala ya Vita

Wakili wa Serikali: Lakini Vitani huwa watu wanatekwa

Shahidi: Ukingalia kwenye Muvi wanatekwa ila Mimi ya Vitani siwezi kuyaeleza, Kuna watu wake Maalum wa Kuyaeleza

Wakili wa Serikali: Moja ya kazi ni Kulinda Lindo, mnalinda dhidi ya nani?

Shahidi: Dhidi ya Adui

Wakili wa Serikali: Unapokuwa umemkamata Mtu lindo Moja ya jambo ni Kumfunga pingu ili asitoroke

Shahidi: Kweli

Wakili wa Serikali: Kweli kwa sababu mmeyafanya huko Vitani

Wakili wa Serikali anaongea na Jopo lao

Wakili wa Serikali:
Wewe huwa unatesa watu.?

Shahidi: Sijawahi

Wakili wa Serikali: Ukiwa umekamata Adui ukamfunga Pingu utakuwa umemtesa

Shahidi: Utakuwa hujamtesa, Ndiyo maana umemuita Adui

Wakili wa Serikali: Naomba kuwaachia wenzangu

Jaji: Nawakumbusha tuna dakika 20 kabla hatuja-break

Wakili wa Serikali 2: Mheshimiwa mimi ninayo Machache kati ya mengi yaliyoulizwa na Mwenzangu

Jaj: Labda nimuulize Shahidi Mwenyewe, Una nguvu au tunaweza kuendelea na Maswali?

Shahidi: Tuendelee Mheshimiwa Jaji

Wakili wa Serikali 02: Wakati umeanza kuulizwa na Wakili wa Serikali umeongea Ukweli, Tunaomba uendelee kusema Ukweli

Wakili wa Serikali 02: Wakati unakamatwa, Ling'wenya je yeye alikuwa umbali gani?

Shahidi: Alikuwa karibu yangu, Sababu nilikuwa Pembeni naongea na Simu

Wakili wa Serikali 02: Umesema Ling'wenya alishuhudia wakati Unawekewa Madawa ya Kulevya?

Shahidi: Siyo yeye tuh watu wote waliona kwa Sababu Jambo hilo lilifanyika hadharani mbele za watu

Wakili wa Serikali 02: Kati yako wewe na Ling'wenya nani Mtaalamu wa Madawa ya Kulevya

Shahidi: Hakuna, Suala la Madawa walisema wao Wenyewe kuwa "Tumemkuta na Madawa ya kulevya"

Wakili wa Serikali 2: Kwenye ushahidi wako wako ulisema kuwa kuhusiana na Suala la kusaini hati yakukabidhi vitu vyako

Shahidi: Sikusema

Wakili wa Serikali 02: Ulimuonyesha Jaji Kuhusu makovu, Je unamakovu Mangapi?

Shahidi: Mengine yapo kichwani

Wakili wa Serikali 02: Uliiambia Mahakama kuwa makovu haya mengine yatofautishwe na Miguuni

Shahidi: Mahakama haikuuliza,Kuwa hayo Mengine yametokana na nini

Wakili wa Serikali 02: Mahakama itatofautishaje sasa?

Shahidi: Hiyo ni kazi ya Mahakama siwezi kuifundisha

Wakili wa Serikali 02: Ulipokuwa Mbweni Kuna Askari alikwambia Upo Mbweni Baada ya Kuwaonea Huruma

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali 02: Huyo wa Pili aliyekuwa anasema huyo Askari ni nani.?

Shahidi: Mohammed Abdilah Ling'wenya

Wakili wa Serikali 02: Kumbe mlikuwa naye na Mkaonana Mbweni

Shahidi: Kujua tupo naye nilijua nimesema, Sikuwahi kumuona kwa macho

Wakili wa Serikali 02: Umeiambia Mahakama aliyekupiga Rungu Moshi ni nani

Shahidi: Sikuwa namfahamu

Wakili wa Serikali 02: Maelezo aliyokuletea Bwana Kingai ukayasaini na Kuyathibitisha,Ukiyqona utayakumbuka.?

Shahidi: Siwezi Kuyakumbuka, Kwa sababu sikuyasoma, Labda sehemu za sahihi yangu na nilipoandika

Wakili wa Serikali 02: Wakati unateswa Moshi uliwajibu Kuwa umeenda kwa VIP PROTECTION ,ukawajibu upo kwenye mazungumzo

Shahidi: Ni Kweli

Wakili wa Serikali 02: Wakati Wakili Kibatala anakuuliza wakati wa Maelezo ulisema Ungeweza Kumuita Mwajiri wako

Shahidi: Muajiri Mtarajiwa

Wakili wa Serikali 02: Kwa hiyo Mahakama iandike hujawahi kuajiriwa na Mshitakiwa wa nne

Shahidi: Ni sahihi

Wakili wa Serikali 02: Kwa hiyo ni sahihi nikisema katika hayo Mazungumzo yenu mliwahi Kufanyia Aishi Hotel

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali 02: Wakati mnafanya hayo Mazungumzo mlikuwa na Mshitakiwa wa 3.?

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali 02: Wakati Upo Tazara unasema uligudua kwa Vitu Viwili Kwa Honi ya Treni na Kuambiwa hiki ni kituo cha Kuhifadhia Watuhumiwa wa Ugaidi

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali 02: Ulishaiambia Mahakama Kwamba Unatuhumiwa kwa Ugaidi.?

Shahidi: Hapana

Jaji: Subiri Kidogo

Wakili wa Serikali 02: Nina swali moja la Mwisho

Jaji: Sawa endelea

Wakili wa Serikali 02: Wakati unachomwa na Bisibisi ushawahi kuiambia Mahakama walikuwa wanataka nini, kama vile Moshi walikuwa wanakuuliza Umefuata nini..?

Shahidi: Hapana

Jaji: Sawa tunapumzika kwa Muda tutarejea Baada ya Dakika 20

Jaji ananyanyuka


Mahakama imerejea


Jaji ameingia Leo Mapema sana kuliko watu wengi na Watuhumiwa. Imebidi Jaji asubiri watuhumiwa waletwe

Kesi imetajwaa

Jaji: Nataka kuanza Utamaduni wa Kuanza Kuzingatia muda. Nikisema naanza Saa 3 Mtanikuta humu. Nikisema tunaanza saa 3 itakuwa Saa 3 Kamili. Na Nikisema Saa 4 itakuwa Saa 4 Kamili. Itapendeza kama Tutazingatia Muda. Na huo ndiyo Ustaarabu,Ikitokea Mtu anadharula nijulishwe. Haipendezi kesi Ikianza milango inafunguliwa kila Saa

Jaji: Upande wa Jamuhuri wapo tayari Kuendelea?

Utetezi.?

Shahidi.?

Wote wapo Tayari

Wakili wa Serikali 03: Wakati tukiendelea na hii Kesi tangu Mwanzoni na kingai,Mawakili wako na Ushahidi wako ulihojiwa Mantle Status ya akili yako,Ni kweli Jambo hili limejitokeza.?

Shahidi: Ni kweli limejitokeza.?

Wakili wa Serikali 03: Kwa usahihi ukaita Battle Confusion.?

Shahidi: ni sahihi

Wakili wa Serikali 03: Kama Kweli hali hiyo imejitokeza Moja ya Jambo ambalo litakukumba ni Kupoteza kuona mambo kwa usahihi.?

Shahidi: Sijui

Wakili wa Serikali 03: Hujui kwa sababu hukumbuki wakati ukiwa na tatizo hilo nini kilikuwa kinakutokea.?

Shahidi: Ndiyo

Wakili wa Serikali 03: Umewahi Kupoteza Uwezo wa watu unaowatambua au maeneo unayoyafahamu.?

Shahidi: Sijawahi

Wakili wa Serikali: Vipi Kuhusiana kutambua Muda na Tarehe.? umewahi Kuwa na tatizo la kuchanganya hivi vitu.?

Shahidi: Hapana sijawahi

Wakili wa Serikali 03: Vipi kwenye Kuchukua Maamuzi Sahihi, Kwamba Umempiga Mtu bila Sababu halafu baadae ukaja Kukumbuka

Shahidi: Hapana sijawahi Kufanya Maamuzi ya namna hiyo

Wakili wa Serikali 03: Kwa sababu ya Jambo la Battle Confusion ujaeleza Kwanini lilikukuta

Shahidi: Nilieleza Mahakama kuwa tatizo hilo nililipata baada ya Kutoka Vitani

Wakili wa Serikali 03: Sababu ya Battle Confusion zipo Nyingi,utakubaliana na mimi

Shahidi: Mimi siyo Mtaalamu

Wakili wa Serikali 03: Moja ya Sababu ya Kupata Battle Confusion ni Matumizi ya madawa ya kulevya yaliyokithiri, Ni sawa.?

Shahidi: Sababu zenu hizo siwezi Kuwabishia

Wakili wa Serikali 03: Katika Kipindi cha hili tatizo ulipangiwa kazi..?

Shahidi: Nilipangiwa kwenda Hospitali

Wakili wa Serikali: Ilikuchukua Takribani Miezi 02 baada ya Kurudi Jeshini, kabla ya Kufukuzwa kazi kwa Sababu wewe uliendelea kutumia madawa ya kulevya

Shahidi: Sijawahi Kutumia Madawa ya Kulevya

Wakili wa Serikali 03: Post Dramatic Disorder ni Kitu gani.?

Shahidi: Sifahamu

Wakili wa Serikali 03: Kama ufahamu kuhusiana na Ugonjwa wa Post Dramatic Disorder limefikaje hapa Mahakamani, Umewahi Kumwambia nani

Shahidi: Sijawahi Kumwambia Mtu

Wakili wa Serikali 03: Utaribu baada ya Kurudi kazini ulikuwaje?

Shahidi: Nilitakiwa kuendelea kuriport Hospitali

Wakili wa Serikali 03: Kwa hiyo Ugonjwa huu ,umeathiri utimamu wa akili.?

Shahidi: Hapana

Wakili wa Serikali: Unasema ulienda Moshi Kufanya kazi ya VIP PROTECTION, Kile Kitabu chenye Orodha ya Mashahidi na Ushahidi wote we ulikipata.?

Shahidi: Ndiyo ninacho

Wakili wa Serikali 03: Kuna Chochote Mshitakiwa wa nne amesema alikuita wewe na wenzako kwa ajili ya VIP PROTECTION.?

Shahidi: Sijakiona

Wakili wa Serikali 03: Kwa hiyo hili suala lako la VIP PROTECTION hajalisema, hata alipopewa nafasi ya kusema hakuwahi Kulisema popote

Shahidi: Sijui yeye sasa, Miye niliulizwa ndiyo Maana nikajibu

Wakili wa Serikali 03: Ulipokuwa unahojiwa na Mawakili wa Serikali ulikuwa unachukua Muda Sana Kujibu, hata Wakati Mwingine Mheshimiwa Jaji alikuwa akitoa Mwongozo, Nikisema una uwezo Mdogo au Umeathirika kiakili

Shahidi: Kama wewe ni Daktari siwezi Kukubishia Uchunguzi wako, ila Miye nikiwa nashindwa kujibu kwa haraka kwa sababu Maswali yanazunguuuuuka hayajanyooka

Wakili wa Serikali 03: Nipo sahihi nikisema hali ya Akili yako ipo sawa sawa.?

Shahidi: Upo sahihi

Wakili wa Serikali 03: Ujatueleza Umuhimu wa Kutueleza Utimamu wa kwanini Umeieleza Mahakama Ya tatizo la Akili kwa wakati Fulani

Shahidi: Nimeeleza Umuhimu, kwa Kufuatia Swali nililoulizwa Mahakamani

Wakili wa Serikali 03: Ina uhusiano gani suala la Ugonjwa wako na Makosa ya Njama za Kutenda Ugaidi

Shahidi: Kwangu naona Vina uhusiano kwa Sababu nimeulizwa na Mahakama, Isingekuwa na Umuhimu nisingeulizwa

Wakili wa Serikali 03: Je, unajua umuhimu wa kwamba umewahi kupata Battle Confusion ..?

Shahidi: Umuhimu unajua Mahakama yenyewe iliyouliza hilo swali

Wakili wa Serikali 03: Mheshimiwa Jaji naomba tukomee Hapa hakuna Swali Lingine

Jaji: Wakili Mallya kama Una maswali ya marejeo

Mallya: Mheshimiwa Jaji ninayo Machache

Mallya: Swali langu la Kwanza kwamba wewe Ni Komandoo umefundishwa kukaa na Njaa na Kuhimili Mateso, JE uelewa Wako ni nini katika Swali hili

Wakili wa Serikali 03: OBJECTION hilo swali haliruhusiwi katika Re-Examination, Yeye ange recall tu katika yale aliyojibu katika Examination

Jaji: Mallya Unakubaliana na alichosema Wakili wa Serikali

Mallya: Sababu ya Muda naomba ni Rudie Swali tu

Jaji: Hapana, Je umekubaliana naye?

Mallya: Sikubaliani naye lakini sababu ya Muda Nirudie swali tu.

Jaji: Sasa hapo tulimalize kwanza kabla Ujaenda Mbali, Kuliko kwenda na Mambo ambayo Mtu hajaridhika nayo

Mallya: Sijaja na Swali Jipya napitia Maswali yale yale na majibu yaleyale

Jaji: Sawa unaweza ukaanza na Swali Mwanzoni

Mallya: Swali langu la Kwanza kwamba wewe Ni Komandoo umefundishwa kukaa na Njaa na Kuhimili Mateso, JE uelewa Wako ni nini katika Swali hili

Shahidi: Katika Upande wa Mafunzo una kanuni zake na taratibu zake na kwa Upande wa ukamataji wa watuhumiwa kuna Kanuni zake na Taratibu zake

Wakili wa Serikali: OBJECTION

Jaji: Subiri kwanza Shahidi ajibu kwanza tuone kama linahusika na mnachotaka kufanya Objection

Wakili wa Serikali: Hakuna sehemu tuliyomuuliza kuhusiana na kuvumilia njaa

Jaji: Mliuliza nini siku hiyo.?

Wakili wa Serikali Chavula: Katika Mafunzo yenu Mnafundishwa Kuvumilia Njaa.?

Jaji: Kwanini uliuliza hilo swali,Ulilenga Ku-Establish kitu gani?

Wakili wa Serikali: Nililenga Kuwa ni Mtu ambaye ni Trained na yale ya Kukaa na Njaa si Kitu kigeni kwake

Jaji: Sawa kaeni Chini nafikiri hakuna Kitu Kigeni kati ya mlichouliza, kilichoulizwa na Kinachojibiwa

Jaji: Namruhusu wakili Mallya Kuendelea

Mallya: Kwa uelewa wako kwanini uliulizwa swali hilo

Shahidi: Nimeelewa Kuwa kukaa na Njaa ni Haki kwangu, Kupitia Mateso ni Haki yangu na Kwamba Kukamatwa Bila kuzingatia Sheria ni Haki yangu kwa sababu tu ni Vitu nilivyowahi Kupitia

Mallya: Kuna sehemu umesema Ulipigwa na kuna sehemu Uliteswa mgawanyiko wa hili Jambo likoje?

Shahidi: Kupigwa ni sehemu ya mateso, Kutishiwa ni Sehemu ya mateso, Ndiyo maana nilisema anilipofika Dar es salaam nilikuwa bado nipo Ndani ya Mateso. Kitendo Cha Kutolewa Kwenye Chumba na kuambiwa Kitakurudia kilichokutokea Moshi ni sehemu ya mateso wakati huo Comfortability yangu imeshapotewa kwa sababu nilikuwa nasimamiwa na Bastola. Na Vilevile Kitendo Cha Kushinda na Njaa ni Mateso pia

Kitendo Cha Kutolewa kituo Kimoja kimoja cha Polisi na Kupelekwa Kingime na Kubadirishiwa jina unalotambulika na Ulimwengu,Kwangu iliniathiri na Nikaona bado Nipo Chini ya mateso

Mallya: Umeulizwa kumjua au Kumuona Mahabusu ya Tazara na Mbweni, ulipokuwa unasema Ulijua yupo ila sikumuona?

Shahidi: Nilikuwa nikimaanisha alipokuwa Mahabusu Nyingine tuliweza kusalimiana hata kwa sauti ya Juu, Lakini siyo Kuonana Kwa face to face

Mallya: Nia ya kuonesha Makovu ilikuwa ni nini.?

Shahidi: Kwa sababu kuonesha Kuwa baada Matendo yale yaliacha Alama za kuumia, ndiyo maana nikaonesha Makovu

Mallya: Umeulizwa Pia Kuhusiana na Kupigwa ukiwa moshi na Kuwaona waliokutesa moshi kama uliwatambua au hukuwatambua

Shahidi: Kwenye kile chumba nilichokuwa nateswa palikuwa na watu wengi, Wengine nilikuja kuwatambua mbele ya Mahakama na Mtu Mwingine sikuweza Kumfahamu

Mallya: Uliulizwa kuhusiana Kutobolewa na Bisibisi Kwenye Makalio...

Wakili wa Serikali: OBJECTION. Aulize Yaliyojitokeza kwenye Examination, Hii kwamba elezea hiyo, Ni Maswali ambayo hayaruhusiwi

Jaji: Wakili Mallya?

Mallya: Re examination wajibu wake ni Kufanya Explanation

Jaji: Nafikiri Wakili wa Serikali yupo sahihi, unachouliza Unaacha uwanja Mpana wa Shahidi Kueleza Jambo Jipya badala Kuziba Mwanya wa Kilichoulizwa

Mallya: Wale waliokuwa wanakuchoma Bisibisi, Walikuwa wanataka nini?

Shahidi: Ilikuwa ni sehemu ya Mateso. Walikuwa wanasema Nyinyi si mmejifanya kutusaliti, sasa mtaona

Jaji: Nafikiri sasa tunafungu Box kwa kile nilichokuwa naeleza

Mallya: Mawakili wa Serikali alikuuliza Swali kwamba waliokuwa wanakuchoma bisibisi walitaka Kujua nini.?

Jaji: Naona Mawakili wa serikali wanataka mshauriane hapo, Inaruhusiwa

Mallya: Nitarudi baadae kwenye swali hilo. Je hapa Kwa ufahamu wako kinachoendelea Mahakamani ni Jambo gani?

Shahidi: Ni Shauri dogo katika Shauri Kubwa

Jaji: Lile swali lako umeuliza kweli?

Mallya: Nimeliweka akiba nitalirejea

Mallya anaenda Kushauriana na Jopo lake

Mallya
: Wakati wanakuchoma walikuwa wanataka nini?

Shahidi: Muendelezo wa Mateso

Mallya: Nafikiri nimemaliza

Shahidi (Mshitakiwa wa pili) Anatoka Kizimbani

Jaji
: Wakili Mallya endelea Uwanja ni Wako...

Mallya: Tunae shahidi mwingine Mohammed Abdilah Ling'wenya

Jaji: Jitambulishe

Shahidi: Mohammed Abdilah Ling'wenya.

Shahidi: Dini Muislamu

Jaji: Thibitisha Wallah Billah taalah Natihibitisha mbele ya Mahakama hii Ushahidi nitakaotoa utakuwa ni Kweli tupu,Eeh Mwenyezi Mungu Nisaidie

Jaji: Tutapisha Hadhana halafu tutaendelea

Hadhana Inaendeleeeee

Jaji
: Wakili Kibatala Ulitaka Kuzungumza

Kibatala: Naomba nimtambulishe Wakili Dickson Matata kwa ajili ya Mshitakiwa watatu

Jaji: Sawa nakushukuru. Hapa Kuna Maelezo

Jaji: Kuna Shida Kumuita Mshitakiwa watatu kuwa Shahidi, Serikali.?

Jaji: Kiwhelo Kuna tatizo kwa Mshitakiwa wako kuwa Shahidi?

Wakili Kiwhelo: Hapana

Mallya: Makazi yako kwa sasa hivi Kimara King'ong'o?

Jaji: Makazi yako kwa sasa hivi?

Shahidi: Natokea Gereza la Ukonga

Mallya: Kabla ya Kukamatwa ulikuwa wapi

Shahidi: Mtwara kampuni DOT kampuni ya kusaga Kokoto

Mallya: Kabla ya hapo..?

Shahidi: Nilikuwa Ngorongoro

Mallya: Unamfahamu Mshitakiwa wa 2

Shahidi: Ndiyo

Mallya: Umemfahamu wapi.?

Shahidi: Jeshini KJ 92 JWTZ Ngerengere

Mallya: Umeanza Lini?

Shahidi: Mwaka 2008 Mpaka 2017

Mallya: Kazi gani ulikuwa unafanya .?

Shahidi: Komandoo,Special Force

Mallya: Unamfahamu Vipi Mshtakiwa wa Pili

Shahidi: Nilikuwa nipo Mtwara nikapigiwa Simu na Askari Mwenzangu ambaye nilikuwa nipo naye Jeshini anaitwa Dennis Urio kwamba Kuna kazi ya kwenda kumlinda Mtu bila kunitajia huyo Mtu ni nani. Nikamwambia asubiri nikifika Nyumbani aongee na Baba akikubali sawa. Nilipofika Nyumbani akapiga simu nikampa akaongea na Baba. Baba akauliza si unamfahamu, nikasema Ndiyo akaniambia nakuombea Dua nenda

Mallya: Siku ya tarehe 05 Mwezi 08 2021 Maeneo ya Rau Madukani kulitokea kitu gani?

Shahidi: Nilikuwa kwa Dada yangu Mmoja anaitwa Asma, akiwa Dukani kwake mimi na Adamoo tukawa tunasubiria Chakula

Mallya: Kilichokupeleka Rau Moshi ni kitu gani?

Shahidi: Tulikuwa tunaenda kukutana na Mwajiri wetu ili tuje kukubaliana naye

Mallya: Mshitakiwa wa pili alikuwa anafanya kitu gani?

Shahidi: Wakati nipo Dukani, Kwenye Upenyo Coridor nikasikia Kelele sana, Nikataka niende kuona. Nikakuta Adamoo ameshanyanyuliwa na Kukabwa. Nikauliza Tatizo ni nini.? Nikashikwa Mkono wakaniuliza wewe Unamfahamu huyu?

Mallya: Ulipata Kujua ni akina nani.?

Shahidi: Niliwaona kwa mara ya kwanza. Wakaniuliza unamfahamu huyu.? Akatoka mwingine akasema ana pistol ana pistol ana pistol

Alinyofoa Kutoka amwilini Kwa Adamoo Upande wa Kulia akasema ana pistol ana pistol akasema na madawa ya kulevya anayo

Mallya: Eleza sasa Pistol anatoa wapi.?

Wakili wa Serikali: OBJECTION anamfeed Majibu

Mallya: Baada ya kumkuta Adamoo amenyanyuliwa Juu kitu gani kiliendelea? Ukisema alimtolea bastola unataka Mahakama ipate apicha gani

Shahidi: Baada ya Kuona Wanamfanyia Adamoo yale na Adamoo namfahamu na nilikuwa naye muda mrefu, Nikauvuta Mkono wangu kwa aliyekuwa amenishika. Nikawaambia Kuwa adamoo hakuwa na hivyo Vitu, nikatoa Simu na wallet nikaweza Kibarazani

Jaji: Ulitoa simu na nini

Shahidi: Simu na wallet

Mallya: Kusema walimuwekea unamanisha nini.?

Shahidi: Kwa Sababu nilianza Safari ya kwenda Moshi na Adamoo kuanzia Chalinze, Nafahamu hakuwa na Vitu hivyo. Nikasema huyu Mtu kwakuwa mmemuwekea na Mimi ngoja nitoe Vitu vyangu.

Mallya: Wakati huo Adamoo Yupo wapi?

Shahidi: Wamemshusha Chini ila wanampiga pale pale chini

Mallya: Uliweka vitu vyako wapi?

Shahidi: Waliochukua walikuwa ni Polisi?

Mallya: Kwenye wallet kulikuwa na nini.?

Shahidi: Palikuwa na Pesa.?

Mallya: Kiasi gani.?

Shahidi; Laki tatu

Mallya: Zipo wapi?

Shahidi: Hapana sielewi

Mallya: Watu waliomvamia Adamoo Unaweza Kujua walikuwa ni watu wangapi.?

Shahidi: Walikuwa Zaidi ya watano

Mallya: Baada ya Kupanda gari Mmlielekea Wapi.?

Shahidi: Central Moshi

Mallya: Kichofuata nini.?

Shahidi: Waliotuleta wakatoka, baada ya kutuacha. Walitutenganisha. Nakumbuka Mmoja alikuwa Askari Bonge nilimueleza kuwa mimi nilikuwa mwanajeshi. Wakauliza Kama nawajua Komba na Mselem

Jaji: Komba ni Mtu Mwingine na Msellemu Mtu Mwingine

Mallya: Nini ulishuhudia Kinachomuhusu Adamoo?

Shahidi: Nilishihudia akiwa yeye ni wa Kwanza kuinginzwa selo yake na Mimi nikawekwa selo Nyingine

Mally: Walipomtoa selo Ulionaje.?

Shahidi: Selo ya Kwanza Ya Kwangu na Yapili,Wakati wanamuingiza Cello yake sikumuona ila wakati wanamtoa alikuja Mtu kwenye Cello yangu akaita Ling'wenya Nyuma yake wakampitisha amtu wamemuinamisha

Mallya: Ulimtambuaje..?

Shahidi: Alikuwa na Jinzi Nyeusi na Shati la maua Maua

Mallya: nini Kilifuata?

Shahidi: Nilisikia kilio huko alipopelekwa Kwa Sababu haikuwa mbali na selo yangu, Nilisikia kilio akilia na nilimtambua kwa Sauti sababu namuitaga sauti ya zege

Mallya: Ulitambua sauti ni ya nani.?

Shahidi: Nilitambua ni Sauti ya Adamoo

Mallya: Ilikuwa ni Sauti ya namna gani.?

Shahidi: Ya amtu anayepigwa, alikuwa analia Eeeehiii Ehiiiiiii Ehiiiiiiiiiiiiiiii ya mtu anayeteswa

Mallya: Ilidumu kwa Muda gani

Shahidi: Sina uhakika ila ni Kama Nusu saa

Mallya: Umesikia Sauti ya zege analia kwa Nusu saa,Nini Kilifuata

Shahidi: Baada ya muda amfupi Kupita akapitishwa Mtu yule yuke aliyevaa Jinzi Nyeusi na shati la maua akiwa hawezi kutembea alishikwa huku kushoto na kulia na kwamba wakamburuza hadi Cello inayofuata baada ya kwangu

Mallya: Nini Kilifuata

Shahidi: Nikajua anayefuata ni mimi

Mallya: Baada ya kujia Unayefuata ni wewe, kilifuata nini

Shahidi: Walinichukua Mimi wakanipeleka huko, Nikaenda nikakuta watu wamekaa na wana simu zao wananirekodi

Wakasema taja majina Matatu

Nikawatajia

Wakaniuliza Unafanya kazi gani

Nikawatajia nimetoka Mtwara

Wakanipiga Buti wakasema wanajua mimi nimefuata nini Moshi

Mallya: Mahita yupi unayemzungumzia.?

Shahidi: Mara ya Mwisho nilimuona hapa mahakamani akitoa Ushahidi

Mallya: Hapo Mlikuwa sehemu gani?

Shahidi: Ni ndani ya Central Police palepale, nilitolewa Cello nikapalekwa kwenye Kijumba Kidogo. Palikuwa na Bomba refu, nikiwa nimefungwa Mikono na miguu, Mimi kwa ufahamu wangu inaitwa killing zone

Mallya: Killing zone ni Kitu gani?

Shahidi: Unakuwa Unaning'inizwa Miguu Juu Kichwa chini

Mallya: Kilifuata kitu gani..?

Shahidi: Nilipigwa sana kwenye Unyayo kwa sababu zilikuwa zimekaa Juu

Mallya: Wakati wanakupiga wanasemaje?

Shahidi: Aliyenipiga ni Mahita tu

Mallya: Walikuwa wanahitaji kitu gani?

Shahidi: Niliwaambia nimekuja kwa kazi ya VIP PROTECTION Kwa Kumlinda Mwenyekiti wa Chadema. Wakasema Utasema tu?

Mallya: Ilichukua Muda gani

Shahidi: Kama Nusu saa

Mallya: Ikawaje

Shahidi: Alikuja Mtu Mtu aliyevaa kiraia akatoa Amri "Mwacheni sasa msimpige

Wakawa wameniweka nimekaa Chini nikiwa na Pingu na Mguuni nimefungwa kamba

Jaji: Miguuni Ulifungwa nini?

Shahidi: Miguuni nilifungwa kamba

Mallya: Baada ya hapo Ulipelekwa wapi?

Akaniambia huku Hoi na yeye akaniambia Mimi Mwenyewe Huku Hoi

Jaji: Ukisema Mimi Huku hoi unamaanisha nini.?

Shahidi: Yaani nimeumia sana na kuchoka sana

Mallya: Mahita alikuwa anakupiga na Kitu gani?

Shahidi: Sijakishika vizuri lakini kama Shaba Nzito

Mallya: nini Kilifuata?

Shahidi: Ni kwamba kwa wao walivyonipiga walifikiri sitoweza Kutembea, Lakini Mimi walipomaliza Kunipiga niliweza Kutembea na palepale Walipomaliza Kunipiga nikiwa nimekaa chini niliwaomba waniruhusu nirukeruke kutuliza Maumivu. Wakati wanajitoa Nje Afande Jumanne akaropoka " Mwenzako amepigwa Sana, Bahati yako Ulipata Mtetezi"

Wakati mimi nikiwa tayari ndani ya gari tayari nilimuona Adamoo anatolewa kwa kukokotwa, Wakaniwahi Mahita akampa Goodluck shuka wakanifunga Kichwani

Nikawa nimetulia, Nikaona Mlango wa gari umefunguliwa, na Mtu akaingia na kuanza Safari.

Mallya: Baada ya kumuona Adamoo wakakuzuia na kukufunika usoni, Je ulimuona akiwa na Hali gani?

Shahidi: Nilimuona akiwa anakokotwa hawezi hata kutembea

Mallya: Baada ya kuinamishwa kichwa na kufungwa Shuka usoni kitu gani Kilifuata?

Shahidi: Nilikuwa kimya wakati huo gari ikawa wakati wote inatembea

Mallya: Wakati huo nini Kilifuata

Shahidi: Mimi nilikuwa katikatika nimekalishwa Kushoto yupo Goodluck na Kulia yupo Jumanne. Na Hali hiyo niliishuhudia kabla sijapigwa Shuka usoni

Mallya: Wakati huo nini Kiliendelea?

Shahidi: Ilikuwa wakati wote kimya hata nikiiinua shingo Kujinyoosha wananirudisha tena chini

Mallya: Unakadiria ilikuwa ni safari ya namna gani?

Shahidi: Ilikuwa ni safari ndefu kama ya mkoa kwa mkoa. Baada ya kufika na gari Kusimama nilishushwa kwa kushikwa nyuma kwa kuinamisha na kitambaa changu Vilevile Mpaka wakafungua Geti, nilipoingia wakanitoa Kitambaa

Mallya: Wakati huo wote mlisimama Kula Chakula.?

Shahidi: Hatukusimama Popote kula chakula. Waliponitoa tu Kitambaa alijitokeza Jamaa Mmoja wa kirangi, Mweupe akaniuliza nini shida.?

Kwa mwonekano wake walikuwa na Ndevu ndefu na Juu alikuwa amevaa Combat lakini siyo ya kitanzania

Nikamwambia Mimi nimekamatwa na tumeletwa hapa sijui ni Wapi

Akaniambia "Hapa ni Tazara Kituo cha Polisi"

Wakati naongea na Yule mrangi kuna mwingine akajitokeza kijana Mweusi, nikawambia nimeletwa hapa lakini Mimi nilikuwa ni Askari

Yule akijana Mweusi akasema Vipi MIC? MIC ni neno la Kijeshi

Nikamwambia Mbona wewe upo hapa.?

Akaniambia Mimi ni Askari nilikuwa naswali kwa Azizi Ally kambi yangu ni Twalipo

Alipokuwa amepaki Pikipiki nje akiwa anaswali ndani, wakamsubiri atoke wakampini wakamleta Tazara na akasema yupo Tazara kwa Miezi nane.

Nikamuuliza shida nini.?

Akasema wanaoletwa hapa ni Kesi za Kigaidi.

Mallya: Alikuwa anasema hapa, anamaanisha hapa Wapi?

Shahidi: Hapa Tazara

Nikamuomba aangalie Cello inayofuata kama kuna Mwenzangu kwa sababu wao Cello yao ilikuwa haijafungwa na walikuwa wakifanya Mpaka Usafi mle ndani

Wao Cello yao walikuwa wanaona Kila kitu, wakaniambia Kuna Wenzako Mmoja yupo Cello ya Mbele

Nikaanza Kuita Adamoo Adamoo Adamooo

Kuna Askari Mmoja akasema tuache Kelele yeye hajatuleta

Shahidi: Nikawa naendelea kupiga Story na Yule Mwanajeshi niliyemkuta pale

Wenzake wakamsii asiongee na Mimi na Mimi wakanipa ishara kwamba watu wenu wanakuja

Mallya: Kitu gani kilifuata?

Shahidi: Nikawa nachungulia Kwenye Cello yangu, hawakufika kwenye Cello yangu

Mallya: Wakati gani tena ulimuona mshitakiwa wa Pili?

Shahidi: Siku inayofuata nikiwa kwenye Cello siku inayofuata nikasikia Kilio, nikachungulia Kule Nyuma nikaona watu niliiokuwa nao Depo JKT , TPDF na 92KJ Komandoo (Wadepo wangu)

Mapumziko


Jaji anaingia.

Shauri Limetajwa Tayari.

Jaji: Lin'gwenya aendelee

Jaji: Leo saa Kumi tunafunga hadi kesho.

Jaji Kamkumbusha Lin'gwenya Tulipoishia

Shahidi: Nilishuhudia Chuma Chugulu na Alex akiwa na Kijitabu na wenzie wakiwa Wanadepo Wenzangu Kupitia Matundu ya Dirisha walikuwa wanamtesa Mtu. Ambapo baade nilimfahamu yule Mtu Kwa Majina anatolewa Kwenye Magari Mabovu alipokuwa anateswa kwa kushikwa na Mtu Mmoja na Mmoja yupo nyuma yake nilimfahamu aliyekuwa anateswa Kuwa ni Dennis Urio ambaye ni Luteni wa Jeshi ambaye alinitafutia hii Kazi ya VIP PROTECTION kwa Mwenyekiti wa Chadema

Mallya: Awali ulisikia Kilio baadae ukaona Mtu Mwenye kitabu na Rungu na baadae Urio anatolewa Kule kwenye Magari Mabovu, kwa aufahamu wako nani alikuwa anateswa Kule?

Shahidi: Kwa nilivyoona Mimi Leteni Dennis Urio ndiye alikuwa anateswa. Siwezi Kuwa na Ukahika nao ila Kama Dakika 15 Mpaka 20

Mallya: Kipi ulitangulia Kuona Kwanza Kati ya Wanadepo Wenzio na baade Askari Polisi na Urio?

Shahidi: Nilishuhudia Alex ndiye wa kwanza Kutoka baadae katoka Chuma Chungulu na Mapolisi wakiwa na Urio

Mallya: Kilifuata nini..?

Shahidi: Ilipofika Usiku nilitolewa nikafungwa Kitambaa

Mallya: Ulifungwa Kitambaa Ukiwa wapi.?

Shahidi: Ndani ya Gari

Mallya: Kabla ya Kufungwa Kitambaa Uliwatambua waliokuwa ndani ya Gari.?

Shahidi: Nilimtambua Goodluck na Mahita

Mallya: Ni Kabla ya Gari Kuondoka ndiyo Ulifungwa Kitambaa.?

Shahidi: Ndiyo

Mallya: Unaweza kutambua Gari ilitumia Muda gani.?

Shahidi: Ni Muda Mrefu sana,Ila siyo Kama Ule wa Kwenda Mkoani

Mallya: Kitu gani Kiliendelea..?

Shahidi: Maaskari wakasema Mwenzenu Moses Lijenje tumeshamtupa, Ameshatangulia huku wakinigusa Kichwani na Kitu nilichokuwa nahisi kuwa ni Bastola, Ukileta Ujanja Ujanja na wewe tunakutupa

Mallya: Maneno haya ulikuwa unaambiwa wakati gani wakati wa Safari au baada ya Kufika

Shahidi: Wakati wa Safari. Tulipofika nilikuwa nimebakia kwenye gari, Nilihisi watu wakifungua milango na Kushuka

Ikatoka Amri nishushwe, nikashushwa wakaniinamisha chini nikiwa bado na Kitambaa Usoni Pale Mapokezi nilipahisi hivyo kwa sababu tulisimama na Kuulizwa naitwa nani.? Mmoja akajibu Johnson John Wakaniinamisha Kichwa Wakanipeleka Mpaka Cello kule nilipoingia ndiyo wakanitoa Kitambaa

Mallya: Ulijuaje pale ni Cello

Shahidi: Nilipofikishwa tuh ile sehemu nikatolewa Kitambaa nikaanza Kuona Mazingira kama ya Tazara, Kama Milango ya Chuma na Vingine

Mallya: Huyu Johnson John waliyemtambulisha ulipata Kumjua??

Shahidi: Sikupata Kumjua, Walinipa Jina la Bandia

Kesho yake wakati wanakagua Mahabusu Johnson John halikuitwa hilo Jina, Wakapita Mpaka Kwenye Cello yangu wakaniuliza we unaitwa nani. Nikawajibu naitwa Johnson John

Mallya: Unasema Uliambiwa Usema Jina lako Unaitwa Johnson John, Nani alikwambia utaitwa Johnson John

Shahidi: Na Jumanne. Alinipa na Kikaratasi Kuwa Kuanzia Leo Mtu yoyote akija Utasema wewe ni Johnson John

Mallya: Alipopita Mtu akakuuliza baada ya Kutoitwa Jina lako.?

Shahidi: Nikamwambia naitwa Johnson John, Akawaita Askari wengine,Nahisi yule Mwanamama alikuwa ni Mkuubwa Kituo na alipotoka

Akaja Askari Mwingine akaniambia sasa tuambie Jina lako la Ukweli

Mallya: Ukajibu Vipi

Shahidi: Nikawapa Jina langu la Ukweli, wakaniuliza na Hili la Johnson John.?

Nikawajibu Kuwa hili nimepewa hapahapa

Wakaniuliza Una kesi gani?

Nikawajibu nimekamatwa Moshi baada ya kwenda kumlinda Mwenyekiti wa CHADEMA, Sijajua nimeshikiliwa kwa Kesi zaidi

Mallya: Ulifanya jitihada gani Kujua pale ulipo ni wapi?

Shahidi: Baada ya Ile zamu alikuja Koplo Mweupe nikaanza Kuongea naye

Nikamwambia mimi ni Mzaliwa wa Mwanza, akaniambia na yeye alishawahi kuishi Mwanza

Nikamwambia nilishawahi Kuwa Mwanajeshi wa KJ 92

Akaniambia kuwa kama Ulikuwa Mwanajeshi wa 92 KJ basi mmeshafika hapa watatu sasa

Mallya: Unaweza Kutueleza Mahakamani Ulijuaje ni Koplo.?

Shahidi: Kwa Uniform zake na Jinsi Renki zilivyokaa

Mallya: Kuna wakati gani ulimwambia hapa ni wapi?

Shahidi: Baada ya Kuniambia tumeshafika watatu na hapa ni Mbweni

Mallya: Ulipata kujua au Kumuona Mshitakiwa wa Pili Adamoo?

Shahidi: Alinimbia Mmoja yupo ila hakai sana Mlangoni anajificha ficha sana Kwenye Kona ktk Cello yake

Jaji: Umesema Mmoja..?

Shahidi: Kwenye Cello yake hakai Mlangoni anajibu akiwa apembeni Ila Mmoja nimeongea naye kajitambulisha ni Luteni wa Jeshi anatoka KJ 92. Anaitwa Dennis Urio

Mallya: Unaposema anatoka 92 KJ Unamaanisha nini..?

Shahidi: Anatokea Kikosi cha Komandoo

Jaji: Subiri Kidogo

Ulimtumia?.?

Shahidi: Nikimtumia Yuleyule Askari kuwa yule aliyejificha anaitwa Adamoo Mwambie Ling'wenya anakuuliza Vipi hali?

Mallya: Ulijuaje aliyejificha ni Adamoo

Shahidi: Ni kwa Ufahamu wangu baada ya Kuambiwa tupo watatu na na Adamoo na Urio nimewaona Tazara nikajua ndiyo hao hao

Mallya: Kitu gani kilifuata baada ya hapo?

Shahidi: Aliniambia anaendeela Vizuri, Tukawa tumezoeana hata alipokuwa anaingia kazini alikuwa lazima aaanze Kuita " Sauti ya zegeeeeee" hata akija kiraia

Mallya: Unaweza kukumbuka pale Mbweni ulikaa kwa Muda gani.?

Shahidi: Nilikaa kuanzia Tarehe 09 Mpaka tarehe 19 Nilipofikishwa Mahakamani

Jaji: Tarehe 19 ya Mwezi gani .?

Shahidi: 09 ya Mwezi wa 08 Mpaka Tarehe 19 ya Mezi 08 Mwaka 2020

Mallya: Nakurudisha Moshi, Ulipopigwa Kwa marungu ukaomba Kurukaruka nini Maana yake.?

Shahidi: Niliomba Kurukaruka ili nichezeshe Visigino,Maumivu yasikae sana

Wakili wa Serikali: OBJECTION wakati Shahidi anatoa Ushahidi wake Asubuhi hakusema kuwa Mahita ndiye aliyempiga

Jaji: What is your Concern katika hilo

Wakili wa Serikali: Mwanzo halikutajwa Jina la Mahita ndiye aliyempiga

Jaji: Lilisemwa au halikusema

Jaji: Sasa itabidi nirejee nilichokiandika Asubuhi

Jaji anasoma

" Wakati anatoa ushahidi wake Mshtakiwa alisema alipigwa na Mahita peke yake" Wengine walikuwa wanauliza Kwanini nilikuwa Moshi

Jaji: Bila shaka Mahita ndiye aliyetajwa Kufanya kazi hiyo, Tunaweza Kuendelea

Mallya: Kile Kitendo cha Kuomba Kurukaruka maana yake ni nini?

Shahidi: Yale Maumivu ya Kupigwa kwenye Nyayo kama ningekaa yangezidi,Kwangu niliona Bora Kurukaruka kuyapunguza, Sikutaka Kukaa kabisa

Mallya: Wakati Unasafirishwa Kutoka Kilimanjaro Kuja Dar es salaam Mikono yako ilikuwaje

Shahidi: Ilikuwa imefungwa Pingu

Mallya: Na Uliposhuka pale Tazara Mikono yako ilikuwa katika hali gani

Shahidi: Ilikuwa na Pingu

Mallya: Na Ulipokuwa Mbweni Mikono yako ilikuwaje

Shahidi: Nilikuwa na Pingu

Jaji: Kwa hiyo ukiwa Cello Tazara na Mbweni Mikono yako wakati wote ilikuwa na Pingu

Shahidi: Ndiyo Mheshimiwa Jaji

Mallya: Wakati wote huo unafungwa pingu unaweza Kuielezea Mahakama Ulikuwa unajisikiaje

Shahidi: Sikuwa najisikia Vizuri,Ukizungatia Goodluck lazima azibane Sana zile Pingu hata Nikimwambia Mahita,Yeye anasema muache hivyo hivyo

Mallya: Wakati wote huo Ukiwa Mbweni Adamoo ulimsikia tena

Shahidi: nilimsikia kwa sababu kila Siku Asubuhi lazima Nimuita Vipi hukooooooo,Yeye anajibu Mdogo Mdogo

Mallya: Katika Kesi hii Ndogo elezea uhusika na Ushiriki wake

Shahidi: Pale Rau yeye Ndoye alikuwa anatoa Amri zote Kama Kutupiga pingu, Kutuchukua Kutuweka kwenye gari

Mahita wakati ananishughulikia katika Kijumba nilipopatia Mateso yeye ndiye alikuwa akinihoji

Mallya: kwa hiyo ASP Kingai akikwepo wakati Unafanyiwa mateso

Shahidi: Alikwepo

Mallya: Na uwepo wake alikuwa anafanya kitu gani

Shahidi: Yeye ndiye aliyekuwa anatoa Amri, pale Tazara Kingai alikwepo na Goodluck akaniambia kiukweli Mwenzako anatumia madawa ya kulevya, Nikajibu si kweli akasema Ngoja tuone mbeleni

Mallya: Unasema Ulimuona Kingai pale Mbweni

Shahidi: Alikwepo

Mallya: Ulimuona kiwa anafanya nini.?

Jaji: Subirni Hadhana inalia

Mahakama Kimyaaaaaaaaaa

Jaji: Tunaweza Kuendelea

Jaji: Unasema ulimuona Kingai Mbweni ulipotolewa Nje ,ulitolewa nje na nani.?

Mallya: Ulimuona Wakati gani

Shahidi: Wakati Goodluck na Mahita Wananitoa nilipishana naye nikapelekwa kwenye Kile Chumba

Mallya: Mheshimiwa Jaji Sina swali la ziada

Jaji: Sijui kama Muda Uliobakia Unatosha kwa Maswali au Tu break Mpaka Kesho

Kibatala ananyanyuka na kwenda kwa Mawakili wa Serikali kwa Mashauriano

Jaji: Wakili Kibatala...

Kibatala: Busara inatuongoza tupumzike Mpaka Kesho

Jaji: nashukuru sana Tunaahirisha Mpaka kesho Saa 3 Kamili Asubuhi ambapo Shahidi wa Pili wa Utetezi ataendelea Kutoa Ushahidi wake
Aibu kubwa Polisiccm wamewaonea sana hao walinzi wa mbowe, endapo watashinda kesi wafungue kesi ya kudai fidia kwa hao Polisiccm akina mahita walioshiriki vitendo vya kishetani kuwapiga kuwatesa kwa kiwango cha Kinyama
 
Kwann serikali haitaki wananchi tupate mfululizo wa hii kesi wanaogopa nn?
Sasa siri imevuja kuwa walipigwa sana kulazimishwa wakili uongo wamsingizie mbowe huku wakiwabambikia dawa za kulevya ni Aibu kubwa kupata kutokea
 
Bado najiuliza serikali wanafaidika vipi na hii kesi?
Wanatafuta kuficha Aibu ya madudu kwenye idara ya upelelezi lakini wamechelewa kwani tayari siri nyingi zimevuja mitaani mpigie sele 0715132277 au 0787132277 atakupa picha yote
 
wengi pamoja na wewe hamkuelewa nini maana ya mateso na kipigo. Je muda wa kusaini maelezo aliteswa?..jibu ni hapana. utashikaje pen wakati una pingu? utakaaje kwenye kitu ili u- sign wakati una pingu miguuni, au wakati upo utupu nk

Lazima tujue mateso ni nini lakini lazima pia tujue kuwa kipigo ni sehemu ya mateso.

so wakati wa ku-sign shahidi hakuwa na mateso yoyote na ndiyo maana aka-sign.
Maelezo hutoka mdomoni mwa mtuhumiwa lakini Mwandishi ni Polisiccm wakati wa kusaini si wanamfungua kidogo kisha anafungwa tena pingu ni mateso makubwa kwa watu ambao hawana hatia yeyote, kitendo cha kupigwa kisha utoe Maelezo ni kinyume cha haki za binadamu na pia ni kinyume cha Sheria na katiba ya Tanzania
 
1. Ni kama tu Jeshi litakanusha maelezo ya washitakiwa [makomandoo] ya sababu za kuondolewa jeshini na waka - concur na sababu za upande wa mashitaka (Jamhuri)..

2. Hata hivyo, lipo moja linaweza kumfunga na kumletea utata mwajiri [JWTZ] wa kina Adamoo na wenzake iwapo atakataa sababu walizozitoa na kuja na zake wasizojua wao, ni kujibu swali hili kwa usahihi: Waliondolewaje kazini/jeshini? Taraibu za kisheria za ku - fire, hire and suspend za utumishi majeshini zilifuatwa...?

3. Hopefully, JWTZ hawataweza kushiriki ujinga na uhayawani huu Wa wanasiasa...!
Hao tayari walikuwa wapo nje ya jwtz kwa sababu mbalimbali hawakuwa watumishi wa jwtz mpaka kipindi uonevu wa kuwabambikia kesi unaanza, isipokuwa huyo mmoja LT urio yeye bado alikuwa bado ni Mtumishi huku akituhumiwa kufanya connection ya hao Asikari kupelekwa kwa mbowe, kwa kifupi hao walinzi wa mbowe siyo magaidi bali wamebambikiwa kesi kwa lengo la kumdhoofisha mbowe na chadema kwa ujumla mpigie sele 0787132277 au 0715132277 akupe full story
 
Hiki kituo ni kwa kazi maalum !! kimya kimya wanaume wanalia aisee !!
Mbinu za kumhoji mtu kwa kumpiga kumtesa ni Mbinu za kijinga sana kwani hupelekea mtu kusema uongo ili apate kuepuka mateso, huo ujinga umedhihilika mahakamani sasa
 
Kwahiyo kwa maelezo ya shahidi namba mbili na mtuhumiwa namba tatu ni kuwa polisi wamemtupa/wamemuua Mosses Lijenje au?
Hapo ndipo kuna utata mkubwa na pia yasemekana Lt Urio ameteswa kwa uonevu kisa kuwa na undugu na mbowe na kusaidia kumpatia walinzi ambao walikuwa watumishi wa jwtz awali kabla ya kuachishwa kazi
 
Alafu jamaa hawakutegemea kabisa kama shahidi wa leo anaweza kuwa alishuhudia Urio akipewa mateso.

Imagine Urio ni Luteni wa jeshi ametendwa namna hiyo.

Wapishi wa hii kesi na DPP wasipokua makini wanaweza kusababisha mgogoro mkubwa baina ya haya majeshi.
Jwtz wasikubali huu ujinga wa ziro na vijana wake we need to hear something from mabeyos boys vs polissm.
 
Kwa mjibu wa watuhumiwa ni kwamba Polisiccm wakiwabambikia kesi ya ugaidi na pia wamewabambikia dawa za kulevya ni uonevu ulioje,kitendo cha kuwapiga kuwatesa kisha kuwalazimisha wakili vya Polisiccm ni uonevu ni kinyume cha Sheria za Nchi na kinyume cha haki za binadamu,endapo haki itatendeka wakaenda kushinda kesi, ni muhimu kuwafungulia kesi wale Polisiccm wote walioshiriki vitendo vya kuwapiga kuwatesa kuwachulia pesa zao, huku jitihada zingine za kuwasomea Albadiri zikiendelea ili iwe somo kwa Polisiccm wote wanaoshiriki vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu kwa wapinzani Tanzania
 
Jwtz wasikubali huu ujinga wa ziro na vijana wake we need to hear something from mabeyos boys vs polissm.
Hawakuwa watumishi wa jwtz kipindi wanaenda kwa mbowe tayari walikwisha acha kazi isipokuwa yule mmoja Lt urio ambaye ni ndugu yake mbowe alikuwa bado ni Mtumishi wa jwtz lakini hukuwa Moshi Eneo la tukio ametuhumiwa kufanya connection ya kazi kwa hao Asikari wengine
 
Mkuki kwa nguruwe babaako angepewa mateso kama haya akiwa uchi wa nyama na kupigwa marungu kwenye makalio nyayo na kuchomwa kwa bisi bisi makalioni usingeandika ujinga kama huu.
Sheria Duniani kote hairuhusu kumpiga mtu kumtesa mtu kisha umwandikishe Maelezo, ukifanya hivyo hayo yanakuwa ni Maelezo batili, mbinu za kuwapiga kuwatesa watu ambao siyo magaidi ni uonevu unyanyasaji wa kishetani ambao hauna Tija kwa Tanzania, ni wakati wa kuondokana na huo ujinga Taifa lijikite kuleta maendeleo umoja wa kitaifa
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
NINI KILIKUWA KINAENDELEA JESHINI?
Je ndani ya jeshi kulikuwa na fukuto kuhusu mustakabali wa nchi kuendelea kutawaliwa na CCM?

Hii kesi inaibua mengi mtambuka kuhusu wanajeshi kuwekwa mahabusu na kuteswa
ndefu na Juu alikuwa amevaa Combat lakini siyo ya kitanzania

Nikamwambia Mimi nimekamatwa na tumeletwa hapa sijui ni Wapi

Akaniambia "Hapa ni Tazara Kituo cha Polisi"

Wakati naongea na Yule mrangi kuna mwingine akajitokeza kijana Mweusi, nikawambia nimeletwa hapa lakini Mimi nilikuwa ni Askari

Yule akijana Mweusi akasema Vipi MIC? MIC ni neno la Kijeshi

Nikamwambia Mbona wewe upo hapa.?

Akaniambia Mimi ni Askari nilikuwa naswali kwa Azizi Ally kambi yangu ni Twalipo

Alipokuwa amepaki Pikipiki nje akiwa anaswali ndani, wakamsubiri atoke wakampini wakamleta Tazara na akasema yupo Tazara kwa Miezi nane.

Nikamuuliza shida nini.?

Akasema wanaoletwa hapa ni Kesi za Kigaidi.

Shahidi: Siku inayofuata nikiwa kwenye Cello siku inayofuata nikasikia Kilio, nikachungulia Kule Nyuma nikaona watu niliiokuwa nao Depo JKT , TPDF na 92KJ Komandoo (Wadepo wangu)

Nilishuhudia Chuma Chugulu na Alex akiwa na Kijitabu na wenzie wakiwa Wanadepo Wenzangu Kupitia Matundu ya Dirisha walikuwa wanamtesa Mtu. Ambapo baade nilimfahamu yule Mtu Kwa Majina anatolewa Kwenye Magari Mabovu alipokuwa anateswa kwa kushikwa na Mtu Mmoja na Mmoja yupo nyuma yake nilimfahamu aliyekuwa anateswa Kuwa ni Dennis Urio ambaye ni Luteni wa Jeshi ambaye alinitafutia hii Kazi ya VIP PROTECTION kwa Mwenyekiti wa Chadema

Mallya: Awali ulisikia Kilio baadae ukaona Mtu Mwenye kitabu na Rungu na baadae Urio anatolewa Kule kwenye Magari Mabovu, kwa aufahamu wako nani alikuwa anateswa Kule?

Shahidi: Kwa nilivyoona Mimi Leteni Dennis Urio ndiye alikuwa anateswa. Siwezi Kuwa na Ukahika nao ila Kama Dakika 15 Mpaka 20

Mallya: Kipi ulitangulia Kuona Kwanza Kati ya Wanadepo Wenzio na baade Askari Polisi na Urio?

Shahidi: Nilishuhudia Alex ndiye wa kwanza Kutoka baadae katoka Chuma Chungulu na Mapolisi wakiwa na Urio
 
Back
Top Bottom