Yaliyojiri kesi ya Mbowe leo Novemba 3, 2021: Shahidi Upande wa Mashitaka ashindwa kutokea Mahakamani, kesi yaahirishwa hadi Novemba 4, 2021

Mchawi wao namba moja ni yule Askofu Mwamakula, ndio ana tunguli zote, mzuieni asiingie mahakamani.
Wanaloga balaa! hadi mashahidi wanasahau baadhi ya maneno, aisee!! pia kuna wabibi/wamama wamebeba madude ya ajabu kwenye mikoba yao, unawakuta wamejibanza katikati ya ukumbi wanafanya mambo yao! Duh! aise wamezidi.
 
Nimekuta mahali taarifa kuwa shahidi wa sita kwenye kesi fake ya Freeman Mbowe Jana aliingia mitini.

Sikusikia taarifa hizi, ila kama ni kweli basi hao mashahidi 20 wengi watapotea au watajipoteza.
 
Baada ya jana kuahirishwa, Kesi ya mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe inaendelea kuunguruma leo mahakamani. Jana kesi ilisikiliza shahidi ambae ni mwanasheria wa kampuni ya mawasiliano ya Tigo. Leo Jamhuri inaleta shahidi mwingine. Kuwa nami.

=========

Jaji ameingia..

Kesi inatajwa..

Robert Kidando anatambulisha Jopo la mawakili wa serikali Peter Kibatala anatambulisha Jopo la mawakili wa utetezi Jaji anawaita washtakiwa na wote wanaitika kwa kusimama

Wakili wa Serikali: Shauri lina kuja kwa ajili ya Kusikilizwa. Mpaka Jana Jioni tulipata Shahidi ambaye tulipanga Kuja naye Leo. Lakini Asubuhi amepata Tatizo la Ki Afya lililosababisha Kushindwa Kuja Mahakamani. Kwa sababu hiyo tunaomba Hairisho Mpaka Kesho

Wakili wa Serikali: Na Kwamba Kwa sababu hii ipo Nje ya Uwezo Wetu pia tunaweza Kupata Shahidi Mwingine

Jaji: Wakili wa Utetezi, Kibatala: Kwa Kufuata amri ya mahakama Iliyokuwa imetolewa Jana, sisi kwa upande wetu tulikuwa tumejiandaa vizuri, Lakini kama wenzetu wanasema hivyo ndiyo Ilivyo tunaomba wenzetu kesho wajitahidi, tuweze kuendelea ili tuweze kumalizia kwa wakati

Jaji: umezungumzia Kwa niaba ya wote au!? Kibatala: kwa niaba ya wote Mheshimiwa Jaji anainama, anaandika. Mahakama ipo kimya wakati Jaji akieendelea kuandika Sura za watu wengi zimeweka makunyanzi Washtakiwa wanacheka na kunong'onezana Jambo fulani, hatuwasikii.

Jaji: kuzingatia maombi yalitolewa na wakili mwandamizi Robert Kidando shahidi kushindwa kufika mahakamani Na kuzingatia ukweli kwamba maombi hayo hayajapingwa na utetezi Nahairisha Shauri mpaka kesho saa 3 ambapo upande wa mashtaka mnaaelekezwa kuleta mashahidi

Jaji anatoka!
Labda shahidi alikua hajakariri point zake za uongo za kwenda kusema mbele ya mahakama
 
Nimekuta mahali taarifa kuwa shahidi wa sita kwenye kesi fake ya Freeman Mbowe Jana aliingia mitini.

Sikusikia taarifa hizi, ila kama ni kweli basi hao mashahidi 20 wengi watapotea au watajipoteza.....
Zitakua za kweli mkuu, hata ningekua mimi ningeingia mitini maana kutetea uongo dio kazi ndogo, yale maswali ya Kibatala na Malya wewe huyaogopi?
 
Ubarikiwe na Bwana mkuu kwa kutupatia kila kinachoendelea hapo mahakamani kwa hii kesi ya kubumba ukweli na uongo utajulikana Mungu atakuwa upande wa akina mbowe.
 
acheni kuroga, mnachafua mazingira.
kwani nini hamjiamini?!
walinzi wa mahakamani fanyeni kazi yenu ipasavyo.
 
Back
Top Bottom