Yaliyojiri kesi ya Mbowe leo Novemba 3, 2021: Shahidi Upande wa Mashitaka ashindwa kutokea Mahakamani, kesi yaahirishwa hadi Novemba 4, 2021

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,445
7,813
Baada ya jana kuahirishwa, Kesi ya mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe inaendelea kuunguruma leo mahakamani. Jana kesi ilisikiliza shahidi ambae ni mwanasheria wa kampuni ya mawasiliano ya Tigo. Leo Jamhuri inaleta shahidi mwingine. Kuwa nami.

=========

Jaji ameingia..

Kesi inatajwa..

Robert Kidando anatambulisha Jopo la mawakili wa serikali Peter Kibatala anatambulisha Jopo la mawakili wa utetezi Jaji anawaita washtakiwa na wote wanaitika kwa kusimama

Wakili wa Serikali: Shauri lina kuja kwa ajili ya Kusikilizwa. Mpaka Jana Jioni tulipata Shahidi ambaye tulipanga Kuja naye Leo. Lakini Asubuhi amepata Tatizo la Ki Afya lililosababisha Kushindwa Kuja Mahakamani. Kwa sababu hiyo tunaomba Hairisho Mpaka Kesho

Wakili wa Serikali: Na Kwamba Kwa sababu hii ipo Nje ya Uwezo Wetu pia tunaweza Kupata Shahidi Mwingine

Jaji: Wakili wa Utetezi, Kibatala: Kwa Kufuata amri ya mahakama Iliyokuwa imetolewa Jana, sisi kwa upande wetu tulikuwa tumejiandaa vizuri, Lakini kama wenzetu wanasema hivyo ndiyo Ilivyo tunaomba wenzetu kesho wajitahidi, tuweze kuendelea ili tuweze kumalizia kwa wakati

Jaji: umezungumzia Kwa niaba ya wote au!? Kibatala: kwa niaba ya wote Mheshimiwa Jaji anainama, anaandika. Mahakama ipo kimya wakati Jaji akieendelea kuandika Sura za watu wengi zimeweka makunyanzi Washtakiwa wanacheka na kunong'onezana Jambo fulani, hatuwasikii.

Jaji: kuzingatia maombi yalitolewa na wakili mwandamizi Robert Kidando shahidi kushindwa kufika mahakamani Na kuzingatia ukweli kwamba maombi hayo hayajapingwa na utetezi Nahairisha Shauri mpaka kesho saa 3 ambapo upande wa mashtaka mnaaelekezwa kuleta mashahidi

Jaji anatoka!
 
Leo tarehe 03/11/2021 ni siku nyingine ambapo kesi hii inaendelea kusikilizwa.

Baada ya Shahidi kutoka Tigo Bwana Freddy Kapala kutoa ushahidi wake , tunatarajia leo kupata Shahidi mwingine.

Kama kawaida JF itakuwa hewani kukuletea kila kinachojiri , usikae mbali
 
Mkuu replica nikupongeze kwa kazi nzuri ya moyo wa kujitolea kutuanikia kila kinachoendelea hapo mahakamani hakika unafanya kazi kubwa na ngumu kwa watanzania ambayo inastahili mshahara mkubwa kuliko ule wanaolipwa wale mazuzu kule uzuzuni shukrani pia kwa mkuu erythrocyte,G day!!!
 
Screenshot_20211102-214026.jpg
 
Back
Top Bottom