Elections 2015 Yaliyojiri katika vikao vya CCM Dodoma - Julai 10-12, 2015. Magufuli achaguliwa kuwa mgombea Urais

Kusema ukweli nimeshtushwa na hii tano bora, kusema ukweli nimeumizwa na hii tano bora, si kwa sababu yeyote ile bali ni kwa sababu i was expecting CCM kunipa mgombea bora ili aje kulifikisha taifa hili linapotakiwa lifike. Nimekuwa nikiaminishwa CCM ni chama kizuri na makini kwa mustakabali wa Nchi yetu ila sasa kusema kweli naiondoa hii notion.

Kusema ukweli Mungu ananiona mie sikuwa mpenzi na siasa ila nilitokea kuvutiwa sana pale nilipomsikiliza mtia nia Prof Muhongo. Nilimpenda kwa jinsi alivo jielezea maono yake, kwa jinsi alivoelezea ni kwa jinsi gani ataitoa hii nchi hapa na kwa jinsi gani atakavoibadirisha hii nchi. Nilisikiliza watia nia wengine wote ila kwa kweli kama mtu una akili timamu lazima uamini kuwa this was the perfect candidate tuliyemuitaji. Nilifuatilia hata utendaji wake huko nyuma na nikaja kugundua ni mtu aliyedeliver kwa kiwango cha juu kabisa haijapata kutokeA katika hii nchi. Nilivutiwa pia na Jaji Ramadhani, nikavutiwa pia na John Pombe Magufuli ingawa kwa hawa hata kwenye kutangaza kwao nia hawakuelezea maono yao. Nilivutiwa pia na Mark Mwandosya kwa hekima zake na hata uwezo wake kichwani aliouonyesha kwenye kutangaza nia kwake.

Honestly sikuvutiwa na Lowassa kwa sababu ya kundi linalomzunguka kwa kuwa niliwaona ni watu ma opportunist tu wanaotaka kuidhulumu na kuimaliza nchi yetu.
Na honestly niliwadharau sana Membe na Makongoro kwa sababu kwenye kutangaza nia kwao walionesha kuwa ni watu wasio na fikra nzuri, maono mazuri na hata hawana mikakati dhabiti ya kuipeleka hii nchi mbele.
Kwa Membe kwanza tangu mwanzo nilishamdisqualify kwa kauli zake mbili alizowaigi kuzitoa kwa taifa, ya kwanza ni ile kuhusu Tanzania kujiunga na OIC aliposema hata kama chakula kinatoka kwa shetani si vibaya kukichukua na ya pili ni pale alipotamka wazi kuwa ana maadui 11 na akishika uraisi 2016 waame nchi.

Kwa mtu yeyote yule smart hizi si kauli za kutolewa na kiongozi makini na dhabiti. kwa Makongoro ni tabia zake binafsi za ulevi, wanawake na kuropoka na kusema ovyo ovyo na hii ilithibitika hata pale alipokuwa anatangaza nia na kuomba wadhamini.

Kwa upande wa Mwigulu na January hawa nao nilivutiwa nao kwa maono yao ila mwigulu aliniangusha pale alipokuwa akiicritisize serikali anayoitumikia wazi. ule ulikuwa ni udhaifu. Kwa january nilimuunga mkono na kuna post humu niliitoa nilisema CCM iamue kati ya Muhongo na Makamba ila nilisema makamba inabidi aprove something kwenye utendaji.
Sasa nimekuja kushtuliwa na hii tano bora kwa sasa kwa sababu zile best brains nilizozitarajia how comes wameziacha?????
Bora kwa Magufuli na Makamba kutokana na utendaji wa Magufuli na maono ya makamba ila kwa Migiro, Membe, Aminsa Salum Ally hapo kweli CCM wamefanya kitu ambacho kitawaangusha sana mwaka huu au hata wakipita kwa namna yaani fitna bas watatawala kwa shida haijapata tokea na hii ni kwa sababu hizi.

1. Mchakato wa kumpata mgombea umeonekana kutawaliwa na FITNA, CHUKI NA UPENDELEO WA HALI YA JUU KWA WATU WALIO KARIBU NA FAMILIA YA RAISI YAAANI MEMBE NA MIGIRO

2. MCHAKATO UMEONEKANA KUWAKATA WATU FULANI KWA VIGEZO FULANI NA KUWAACHA WATU WENYE VIGEZO VILEVILE VYA KUWAKATA WENGINE. HAPA NAMAANISHA KAMA MEMBE AMEBAKI NA IMEONEKANA ANATUMIA SANA PESA NYINGI, ANAFANYA KAMPENI NA HATA ANA VISASI KWA NINI WAMEMUONDOA LOWASSA MWENYE MABO HAYOHAYO?????

3. WATU WENYE AKILI NA WANAOYAJUA MATATIZO YA TANZANIA VIZURI NA WALE WALIOONEKANA KUWA NA UADILIFU, HEKIMA, BUSARA NA WEREDI WAMEACHWA KANDO NA HAWAJAINGIA HATA 5 BORA, HAPA NAWATAJA JAJI RAMADHANI, MAHIGA, MWANDOSYA NA HATA BILALI

4. WAMEMUACHA MTU ALIYEONEKANA KUWA WAZIRI ALIYE DELIVER VIZURI ZAIDI KWA KIPINDI KIFUPI ZAIDI ALICHOKAA KWENYE CABINET NA AMEONAKA ANA UWEZO MKUBWA SANA KIMAONO NA HATA KUIFIKISHA HII NCHI INAPOTAKIWA YAANI PROF MUHONGO

Napenda kumaliza kuwa kusema kuwa ili CCM ionekane kama inatenda haki na kuwa na fair playing ground ilitakiwa at leat kuwakata Lowassa na Membe na at least kwenye 5 bora yao kungekuwa na Jaji Ramadhani, Mwandosya, Muhongo, Magufuli na mwisho Augusto Mahiga au Amina Salum Ally.

Sasa kwa sababu wamefanya tofauti yaani imeonekana kuwa hawakuwa fair toka awali sitashangaa kutokea mpasuko mkubwa zaidi ambao utakiangamiza kabisa chama chao.
 
Mgombea wa CCM ni Mhe. John Pombe Magufuli. Safari ya Membe itaishia NEC ili kulipia gharama za lip services za watu wa Lowassa. Dr. Asha Rose atapewa u PM, Amina Mgombea Mwenza, January atapewa MFA!.

Pasco


Last time ulisema hata Lowassa akikatwa na CCM atakuwa Rais October
mbona unajikana tena now
 
Najiuliza, nani zaidi kati ya Magufuli na Membe? Mie nadhani Magufuli ana advantage sana maana Membe kwanza ataathirika na kundi la Lowassa, pili Membe ana makundi magufuli hana, Tatu kashfa ya membe kuwa ktk familia ya mkuu wa kaya yaweza muondolea sifa hiyo, lakini pia ukilinganisha utendaji wa membe na Magufuli una tofautiana sana.

Wana jamvi mnaonaje hili?


Magufuli ana lack dipomat skills. wote hawa ni watu smart, nadhan wakiweza kufanya colaboration mmoja akawa raisi na mwingine pm na imani nao sana nchi inakuwa ya viwanda na uchumi wa kati ila Prof Muhongo wamrudishe wizara ya nishati bado tunamtaka sisi watu wa wizara ya nishati tulimkubali
 
mwenyekiti ana uakika na watu wake makamba, kama sio membe,kama sio asha huyu magufuli yupoyupo tu hapo atatoswa vibaya .Mwenyekiti anafuata uabiri wa mwenye jina la kiislamu na kikristo au aliyeoa dini nyingine-asha-rose migiro, january makamba -mke mkristo, bakar benard

tutolee ulozi hapa wewe
 
Kutoka Safari ya matumaini hadi Safari ya Majonzi..

Pamoja na wadhamini Laki 8 lkn bado umekatwa.. Pole sana brother nenda Monduli ukacheze na wajukuu zako.
Kingunge -Lowasa akikatwa patachimbika
cc.msalani njooni Ukawa
 
Angalieni msifurahi sana mnaweza mkafa kwa furaha...

Too much of anything is harmful..

Its a scientific proof.
 
Mkuu umenena hapo kwa Membe wamefanya makosa makubwa sana ila nina uhakika kwenye 3 bora Membe havuki.
 
Back
Top Bottom