Elections 2015 Yaliyojiri katika vikao vya CCM Dodoma - Julai 10-12, 2015. Magufuli achaguliwa kuwa mgombea Urais

Kama ni kweli Lowassa amekatwa ufalme wa shetani ccm umekwisha,hakuna mtu ndani ya ccm mwenye nguvu ya kupeperusha bendera ile na kushinda zaidi ya Lowassa,UKAWA tunachukua nchi kiulaini sana.Target yao ni membe,membe ataigawa vipande vipande Tanzania,hana akili huyu anataka taifa liingie OIC.
 
Mkutano Mkuu wa CCM.

1. BENARD MEMBE
2. JANUARY MAKAMBA
3. DK. ASHA ROSE MIGIRO,
4. AMINA SALUM,
5. JOHN POMBE MAGUFULI

NAKUWEKEA CV ZAO HAPA CHINI KWA KIFUPI:

A: BENARD MEMBE

Benard Kamillius Membe ni Mbunge wa Jimbo la Mtama mkoani Lindi na ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, alizaliwa tarehe 09 Novemba 1953, katika Kijiji cha Rondo-Chiponda, Wilaya ya Lindi Vijijini.

Membe ana shahada ya kwanza ya Sayansi ya Siasa na Utawala wa Umma na ana shahada ya umahiri ya Uhusiano wa Kimataifa.

Membe aliajiriwa kwenye Ofisi ya Rais na kufanya kazi kwa miaka 6 kabla hajaanza shahada ya kwanza na baadaye alirudi vyuoni kusoma na kuhitimu shahada ya umahiri, alirejeshwa tena ofisi ya Rais kabla ya kuhamishiwa wizara ya Mambo ya Nje kuwashauri mabalozi.

Membe alianza shughuli za ubunge mwaka 2000 pale alipogombea katika jimbo la Mtama, Lindi na kushinda. Mwaka 2005 alishinda tena ubunge na kuteuliwa na Rais Kikwete kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani na baadaye Wizara ya Nishati na Madini.

Aliteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa akichukua nafasi ya Bi. Asha Rose Migiro na aliposhinda tena uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, Rais Kikwete alimteua kushikilia wizara hiyohiyo ya mambo ya nje, mahali ambapo yupo hadi leo.

B. JANUARY MAKAMBA

January Yusuph Makamba ni mbunge wa jimbo la Bumbuli lililoko mkoani Tanga na ni Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.

Makamba ni mtoto wa Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, (Mzee) Yusuph Makamba na alizaliwa tarehe 28 January 1974 na ana shahada ya kwanza ya masuala ya amani (Peace Studies) na shahada ya umahiri ya sayansi ya Usuluhishi wa migogoro.

Amewahi kufanya kazi kwenye wizara ya mambo ya nje kama Ofisa wa daraja la pili na baadaye akajiunga na timu ya kampeni ya Rais Kikwete kama mtu muhimu kwenye mipango na mikakati. Kikwete alipoingia Ikulu alimteua January kuwa “Msaidizi Binafsi wa Rais Katika Mambo Maalum”.

January aligombea ubunge kwa mara ya kwanza mwaka 2010 kwatiketi ya CCM na kushinda. Katika bunge la 10 alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya bunge ya Nishati na Madini na mwaka 2011 CCM ilimteua kuwa katibu wa siasa na mahusiano ya kimataifa akichukua nafasi ya Benard Membe.

January alichaguliwa kuwa mjumbe wa kamati kuu ya CCM na tangu mwaka 2012 yeye ndiye Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.

C. ASHA ROSE MIGIRO

Dk. Asha Rose Migiro ni Waziri wa Sheria na Katiba wa Tanzania, alizaliwa tarehe 09 Julai 1956 katika wilaya ya Songea, Mkoa wa Ruvuma. Ana shahada tatu za chuo kikuu, shahada ya kwanza ni ya sheria (L LB), ya pili ni shahada ya umahiri ya Sheria (L LM) na ya tatu ni shahada ya uzamivu ya sheria (PhD).

Migiro amekuwa mhadhiri msaidizi wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam na baadaye amekuwa mhadhiri mwandamizi akifundisha katika kitivo cha sheria.

Amewahi kuwa Mkuu wa Idara ya Sheria za Katiba na Utawala na baadaye kuwa mkuu wa Idara ya Sheria za Makosa ya Jinai (Idara zote zipo katika Kitivo cha Sheria UDSM)

Mwaka 2000 aliteuliwa kuwa mbunge na Rais Mkapa na kisha akateuliwa kuwa waziri kwenye wizara ya Wanawake, Watoto na Maendeleo ya Jamii.

Ameendelea kuteuliwa katika nyadhifa za ubunge huku akikabidhiwa uongozi wa wizara hata kwenye uongozi wa Kikwete ambapo aliteuliwa kuwa waziri wa mambo ya nje kabla ya kuteuliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuwa Naibu Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa muda wa miaka mitano.

D. AMINA SALUM

Amina Salum Ali ni mtanzania mwenye asili ya Zanzibar na alizaliwa tarehe 24 Oktoba 1956. Amina ni mhitimu wa shahada ya Uchumi, pia ana stashahada ya Usimamizi wa Fedha, shahada ya umahiri (MBA) ya Usimamizi wa Biashara katika Masoko na ana stashahada ya Biashara na Masoko ya Nje.

Balozi amina amekuwa mbunge katika Bunge la Tanzania kati mwaka 1985 – 1990, amekuwa mbunge na mwakilishi kwa wakati mmoja kati ya mwaka 1990 – 2000.

Kiongozi huyu pia ameshikilia nyadhifa za uwaziri katika Serikali ya Muungano na ya Zanzibar kwa miaka takribani 20 na mwaka 2006 alijivua nyadhifa za uwakilishi na uwaziri za Zainzibar ili kutumikia nafasi mpya ya uteuzi wa kuwa
 
Mgombea wa CCM ni Mhe. John Pombe Magufuli. Safari ya Membe itaishia NEC ili kulipia gharama za lip services za watu wa Lowassa. Dr. Asha Rose atapewa u PM, Amina Mgombea Mwenza, January atapewa MFA!.

Pasco

itakuwa heri kama huu utabir utakuwa wa kweli
 
Ikiw wa2 waliamn kuw lowasa atawez kuwepo kwny tano bora bac hata kwny kupeperush bendera ya ccm kwny uchaguz mkuu uyo membe hawezkuwepo,,atateuliw m2 mwngne kabsa
 
Najiuliza, nani zaidi kati ya Magufuli na Membe? Mie nadhani Magufuli ana advantage sana maana Membe kwanza ataathirika na kundi la Lowassa, pili Membe ana makundi magufuli hana, Tatu kashfa ya membe kuwa ktk familia ya mkuu wa kaya yaweza muondolea sifa hiyo, lakini pia ukilinganisha utendaji wa membe na Magufuli una tofautiana sana.

Wana jamvi mnaonaje hili?
 
Tanzania ijiandae na mitikisiko mikubwa ambayo haijawahi kutokea before.Awamu ya tano inahitaji Rais strong mwenye hekima na kipaji cha uongozi.
Kwenye majina hayo ni Magufuli tu mwenye sifa ya kuwa strong lakini hekima ni sifuri, so naye hafai kabisa.

Ngoja tuwasubiri Ukawa nao ila CCM imeishia hapa.Hata wakishinda urais hawatakuwa na utulivu serikalini wala ndani ya chama, na jina lolote katika haya halina uwezo wa kuibeba CCM kwenye kura za wabunge, hivyo suala la wapinzani kuongezeka bungeni ni constant, regardless of who is going to win Urais.This party is in a free fall.

Nasikitika CCM inakufa huku wapinzani nao wakiwa hawaeleweki au kasi yao ya kupanda ni ndogo huku kasi ya CCM kushuka ikiwa kubwa na hili ombwe litayumbisha nchi.

Upinzani uimarishwe haraka na kuchukua nchi hii kuliko kuendelea kuongozwa na CCM ya "kupaka rangi", this is the only safe alternative otherwise we have very difficult times ahead.
 
Kwenye Halmashauri Kuu na Mkutano Mkuu ni kura za wajumbe zinazoamua.

Hivyo nafasi kubwa anayo Dk Magufuli kwani anategemewa kupata kura nyingi za Team Lowassa na wengi wasiotaka mambo ya usultani.

Halafu hivi Membe hakuenguliwa kwa kuanza kampeni mapema, kuwa na makundi na matumizi ya fedha?

Yaani Mwandosya safari hii hakuchukua form au? Na tyson wamemmwaga aisee? Makongoro out?
 
Mgombea wa CCM ni Mhe. John Pombe Magufuli. Safari ya Membe itaishia NEC ili kulipia gharama za lip services za watu wa Lowassa. Dr. Asha Rose atapewa u PM, Amina Mgombea Mwenza, January atapewa MFA!.

Pasco

Hivi mkutano mkuu ndo unapanga nani awe pm ?
 
Huyo Mamvi aende zake,urais haununuliwi kwa namna alivyofanya yeye alikuwa na ajenda ya kutuibia kama Richmond
 
mamvi kachambia upuppu...

Mkuu kwa kipindi kirefu nilikua naingia humu kama guest tu bt umenisababishia kusign in kwa huu uabajaro wako. Hapo labda Magufuli bt hao wengine itaonekana ni mipango tu ya mkuu wa kaya coz ni wa kawaida mnoo.
 
Mgombea wa CCM ni Mhe. John Pombe Magufuli. Safari ya Membe itaishia NEC ili kulipia gharama za lip services za watu wa Lowassa. Dr. Asha Rose atapewa u PM, Amina Mgombea Mwenza, January atapewa MFA!.

Pasco

wenzio wamejipanga.....magufuli hachomoi tatu bora
 
Hapo ni Magufuli wakuu, tangu nisome Raia Mwema la juzi nikaona kabisa kumbe wengi wetu humu tulikuwa tunakwenda kishabiki, jamaa walizungumzia jinsi Kikwete alivyokuwa anafurahi kuongozana na Magufuli kwenye ziara za Mikoani maana hakuna kuzomewa tofauti na Mawaziri wengine, pi ni mtu aliyechukua fomi bila mbwembwe wala tambo za kusema ooh nitakomesha rushwa au kubeza hii serikali, pia suala la kuwa anatoka kanda ya ziwa ambako kuna wapigaji kura wengi nayo pia imekuwa kete muhimu.
Namtakia kila la kheri avuke hapo japo kwangu sijaonaga msafi huko CCM.
 
Back
Top Bottom