Elections 2015 Yaliyojiri katika vikao vya CCM Dodoma - Julai 10-12, 2015. Magufuli achaguliwa kuwa mgombea Urais

JamiiForums

Official JF Response
Nov 9, 2006
6,200
4,984
Wakuu habari,

Tunawaletea kinachojiri kwenye Vikao vya CCM vinavyoendelea Dodoma.

Fuatana nasi... Karibuni sana.

==================

Updates:

1.
Sasa mchakato unaanza rasmi, Wajumbe kamati ya Maadili wanaingia Ukumbini, CC itafuata, haijajulikana kama na NEC itafanyika leo, itategemea na muda utakao tumika na vikao viwili hivyo.

2.
Rais Kikwete ameingia Ukumbini muda huu

3.
Kikao cha Usalama na maadili kinaendelea. Hiki hata kikiisha hakina briefing. kama kawaida, Ulinzi umeimarishwa na state

4.
Kuweka Updates si rahisi kama mnavyodhani sababu ulinzi ni mkali na hakuna aliyeruhusiwa kuingia na simu. Kumbuka hii ni kamati ya maadili, hivyo kuweni wavumilivu. Kikao kinaendelea.

5. 14:46
Kamati ya maadili imemaliza kazi yake, sasa ni zamu ya CC kuingia, lakini Rais Kikwete katoka, Kikao kitaanza akirudi.


6. Update 16:00
Wajumbe wa CC ndo wameingia sasa hivi, watapewa majina matano na kamati ya maadili ya Wagombea urais.

7.Update 16:55
Team inayomuunga mkono Edward Lowassa zaidi ya watu 200, wamekutana mchana huu Katika Ukumbi wa St. Gasper, kuweka msimamo iwapo huyo wanayemtaka hatakuwemo kwenye Top 5 ya Wagombea waliopitishwa na kamati ya maadili.

8.Update 18:50
CC imemaliza Kikao chake, Nape amesema majina matano yaliyopendekezwa yatatolewa baada ya Kufuturu.

9. Update 22:55
CC bado inaendelea, sasa hivi watu wa catering wanawapelekea vyakula na vinywaji (Pengine ni daku ya leo kwa waliofunga?)

Julai 11, 2015:

1. Update 01:00
CC imemaliza kikao chake; Nape kakutana na waandishi na kuna tetesi kuwa kuna kundi lilikuwa linajipanga kufanya mapinduzi ya Mwenyekiti wa CCM. Aidha, Nchimbi na wenzake wawili wameondoka wakiwa wamejaa jazba na wameonekana kutokubaliana na maamuzi ya CC. Updates zaidi zinafuata...

2. UPDATE 01:20

Hatimaye 5 Bora imejulikana, ni:

1) Bernard Membe

2) John Magufuli

3) Asha Rose Migiro

4) January Makamba

5) Amina S. Ali
.
attachment.php

3: Update 12:00
Nchimbi, Mkono na Kibajaji wamezuiwa getini wasiingie mkutanoni kisa hawana vitambulisho. Baada ya tafrani ya takribani robo saa wajumbe hao wameruhusiwa kuingia.


4: Update 12:15
Mwenyekiti wa CCM Taifa, mh. Kikwete amefungua kikao cha Halmashauri Kuu Taifa (NEC) cha kuchuja majina matano nafasi ya kugombea Urais.

5: Update 12:51
NEC imemaliza kikao cha kupiga kura, Tatu bora inatangazwa hivi punde (Kama itatokea)

6: Update 13:05
Kikao cha Halmashauri Kuu kimepitisha jina la Dr. Shein kuwa mgombea wa Urais Zanzibar.

7.Update 13:25
Wanec wametoka nje, hawana imani na CC, wanahoji kwanini Membe apite 5 bora, Lowassa aachwe?. Wametishia kuifuta CC. Ngoma imeachwa wazee kina Mwinyi na Mkapa wamebaki wakishauriana na viongozi nini cha kufanya.

8. Update 13:33
Hali ni tete Dodoma, Wapambe wa Lowassa, Wametishia Amani, Wamejikusanya kwenye bustani ya Nyerere Squre Wanaimba. Tunamtaka Lowassa tunamtaka Lowassa...!!

9:Update 14:00
Mkutano umefunguliwa na Mwenyekiti wa chama Rais Kikwete na kuahirishwa baada ya Dakika saba kwa kile wanachodai ni kuruhusu watu wakapate Chakula cha mchana. Wakati Mwenyekiti wa Chama anaingia, Wajumbe wa NEC walimpokea kwa wimbo wa "Tuna imani na Lowassa" hadi rais anakaa wameendelea kuimba
.


10: Update 17:30
Mkutano wa NEC, wajumbe wanapiga kura hivi sasa kupata wagombea tatu (3) BORA. Mkutano mkuu wa Taifa Utaanza saa TATU usiku.

12 Julai 2015

01: Update 00:45
Wagombea tatu bora wamejinadi mbele ya Mkutano Mkuu. Wajumbe wamepiga kura.

Matokeo yatatolewa tarehe 12 Julai, 2015 siku ya Jumapili saa 4 Asubuhi.

Mwenyekiti wa CCM Taifa ameahirisha kikao.

2.Update: 13:50

Spika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Anna Makinda ambaye ni Mwenyekiti wa uhesabuji kura akisaidiana na Spika wa Zanzibar wanamkabidhi Rais Kikwete Kazi walioifanya jana, Kisha Rais Kikwete anamruhusu Anna Makinda Kutangaza matokeo.

Update 12:55
Ana Makinda Anasema;

Kura zilizopigwa zilikua 2422

Kura zilizo haribika zilikua 6

Kura halali 2416.

Mawakala walikua;

Makilagi

Hassan Juma

Rodrique Mpogoro

Baada ya kuhesabu Kura Matokeo yalikua hivi;

Asha Migiro kura 56 sawa na asilimia 2.4%

Amina Ali kura 253 sawa na asilimia 10.5%

John Magufuli alipata 2,104 sawa na asilimia 87.1%

Mshindi atakaye gombea Urais kwa tiketi ya CCM, ni John Pombe Magufuli

3. Update 14:00
John Magufuli amteua Samia. S. Hassan kuwa Mgombea mwenza.




jf2.png


Mwisho
 
Hivi kikao cha maadili kinakuwa na update ndani ya mkutano acha uongo sibiri kikao kiishe majibu ya kueleweka yaje sasa naona kila anayeweza kuweka post anakuja na update subiri nape aje atangaze majina apo SAA kumi kama ratiba inavyosema
 
habari wanajanvi, mda huu dodoma hali si ya kawaida kama ilivyozoeleka , wapambe watia nia mbali mbali wameonekana kusononeka sana na wengine kutoweka kabisa karibia na eneo la tukio la mchakato mzima wa kumpata mtia nia, wameanza kuwapunguza wengi hasa ambao hawana vigezo kamili na mlolongo wa ukataji ulikuwa hivi

1. ametolewa ambaye elimu yake si sawa na anayetakiwa, yule mtia nia wa kigoma mr mahale,

2.wakatolewa wenye kashfa nzito sana na ni vigumu kuwasafisha hapa tuna, edward lowassa..richmond, . sospeter muhongo ,, tegeta escrow, sumaye.. uuzwaji wa nyumba zza serikali na uuzaji wa mashirika ya umma ovyo, membe kaponea chupuchupu kukatwa ana makundi ya kukigawa chama, wasira ana kashfa ya rushwa mwaka 1995,

3.uzoefu na umri, japo wote wametimiza umri lakini bado hawajawa na uzoefu wa kutosha, hapa ni kigwangala, na mwigulu nchemba.

waliotangulia kuingizwa kwenye list ni
1.asha rose migiro gender factor , uwajibikaji wake na usafi wake

2.augustino ramadhan zanzibar factor na kutokuwa na makundi na uwajibikaji wake,

3.makongoro nyerere, uwajibikaji na kuchukia rushwa kukemea hadharani wala rushwa na hali ya juu ya uthubutu kwenye maslahi ya wengi hana woga, pia nyerere factor usafi na kumuenzi mwalimu nyerere

4.pombe magufuri, uwajibikaji wake na hasa kutekeleza sheria bila kupindishwa, na muwajibikaji wa hali ya juu

5. mizengo pinda , ni kiongozi mkuu wa serikali imekuwa vigumu serikali yenyewe kushindwa kutompitisha mtekelezaji mkuu wa ilan ya chama hicho bungeni na pia akikatwa itaonekana serikali nzima ilikuwa haifai, pia ni mtu msafi mwenye busara

6. samwel sitta, kwakuwa anasimamia sana matakwa ya chama na ameweza kutoyumbishwa wakati wa katiba mpya, amepitisha mapendekezo asilimia kubwa yaliyokuwa yanapendelewa na chama chake,mbali ya hapo ana uthubutu na ni mwajibikaji,

7.mark mwandosya
8.bernad membe


hapo ndo itatoka tano bora ,tatu mpaka moja bora,
 
82 Reactions
Reply
Back
Top Bottom