Elections 2015 Yaliyojiri katika vikao vya CCM Dodoma - Julai 10-12, 2015. Magufuli achaguliwa kuwa mgombea Urais

JamiiForums

Official Robot
Nov 9, 2006
6,092
2,000
Wakuu habari,

Tunawaletea kinachojiri kwenye Vikao vya CCM vinavyoendelea Dodoma.

Fuatana nasi... Karibuni sana.

==================

Updates:

1.
Sasa mchakato unaanza rasmi, Wajumbe kamati ya Maadili wanaingia Ukumbini, CC itafuata, haijajulikana kama na NEC itafanyika leo, itategemea na muda utakao tumika na vikao viwili hivyo.

2.
Rais Kikwete ameingia Ukumbini muda huu

3.
Kikao cha Usalama na maadili kinaendelea. Hiki hata kikiisha hakina briefing. kama kawaida, Ulinzi umeimarishwa na state

4.
Kuweka Updates si rahisi kama mnavyodhani sababu ulinzi ni mkali na hakuna aliyeruhusiwa kuingia na simu. Kumbuka hii ni kamati ya maadili, hivyo kuweni wavumilivu. Kikao kinaendelea.

5. 14:46
Kamati ya maadili imemaliza kazi yake, sasa ni zamu ya CC kuingia, lakini Rais Kikwete katoka, Kikao kitaanza akirudi.


6. Update 16:00
Wajumbe wa CC ndo wameingia sasa hivi, watapewa majina matano na kamati ya maadili ya Wagombea urais.

7.Update 16:55
Team inayomuunga mkono Edward Lowassa zaidi ya watu 200, wamekutana mchana huu Katika Ukumbi wa St. Gasper, kuweka msimamo iwapo huyo wanayemtaka hatakuwemo kwenye Top 5 ya Wagombea waliopitishwa na kamati ya maadili.

8.Update 18:50
CC imemaliza Kikao chake, Nape amesema majina matano yaliyopendekezwa yatatolewa baada ya Kufuturu.

9. Update 22:55
CC bado inaendelea, sasa hivi watu wa catering wanawapelekea vyakula na vinywaji (Pengine ni daku ya leo kwa waliofunga?)

Julai 11, 2015:

1. Update 01:00
CC imemaliza kikao chake; Nape kakutana na waandishi na kuna tetesi kuwa kuna kundi lilikuwa linajipanga kufanya mapinduzi ya Mwenyekiti wa CCM. Aidha, Nchimbi na wenzake wawili wameondoka wakiwa wamejaa jazba na wameonekana kutokubaliana na maamuzi ya CC. Updates zaidi zinafuata...

2. UPDATE 01:20

Hatimaye 5 Bora imejulikana, ni:

1) Bernard Membe

2) John Magufuli

3) Asha Rose Migiro

4) January Makamba

5) Amina S. Ali
.

3: Update 12:00
Nchimbi, Mkono na Kibajaji wamezuiwa getini wasiingie mkutanoni kisa hawana vitambulisho. Baada ya tafrani ya takribani robo saa wajumbe hao wameruhusiwa kuingia.


4: Update 12:15
Mwenyekiti wa CCM Taifa, mh. Kikwete amefungua kikao cha Halmashauri Kuu Taifa (NEC) cha kuchuja majina matano nafasi ya kugombea Urais.

5: Update 12:51
NEC imemaliza kikao cha kupiga kura, Tatu bora inatangazwa hivi punde (Kama itatokea)

6: Update 13:05
Kikao cha Halmashauri Kuu kimepitisha jina la Dr. Shein kuwa mgombea wa Urais Zanzibar.

7.Update 13:25
Wanec wametoka nje, hawana imani na CC, wanahoji kwanini Membe apite 5 bora, Lowassa aachwe?. Wametishia kuifuta CC. Ngoma imeachwa wazee kina Mwinyi na Mkapa wamebaki wakishauriana na viongozi nini cha kufanya.

8. Update 13:33
Hali ni tete Dodoma, Wapambe wa Lowassa, Wametishia Amani, Wamejikusanya kwenye bustani ya Nyerere Squre Wanaimba. Tunamtaka Lowassa tunamtaka Lowassa...!!

9:Update 14:00
Mkutano umefunguliwa na Mwenyekiti wa chama Rais Kikwete na kuahirishwa baada ya Dakika saba kwa kile wanachodai ni kuruhusu watu wakapate Chakula cha mchana. Wakati Mwenyekiti wa Chama anaingia, Wajumbe wa NEC walimpokea kwa wimbo wa "Tuna imani na Lowassa" hadi rais anakaa wameendelea kuimba
.


10: Update 17:30
Mkutano wa NEC, wajumbe wanapiga kura hivi sasa kupata wagombea tatu (3) BORA. Mkutano mkuu wa Taifa Utaanza saa TATU usiku.

12 Julai 2015

01: Update 00:45
Wagombea tatu bora wamejinadi mbele ya Mkutano Mkuu. Wajumbe wamepiga kura.

Matokeo yatatolewa tarehe 12 Julai, 2015 siku ya Jumapili saa 4 Asubuhi.

Mwenyekiti wa CCM Taifa ameahirisha kikao.

2.Update: 13:50

Spika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Anna Makinda ambaye ni Mwenyekiti wa uhesabuji kura akisaidiana na Spika wa Zanzibar wanamkabidhi Rais Kikwete Kazi walioifanya jana, Kisha Rais Kikwete anamruhusu Anna Makinda Kutangaza matokeo.

Update 12:55
Ana Makinda Anasema;

Kura zilizopigwa zilikua 2422

Kura zilizo haribika zilikua 6

Kura halali 2416.

Mawakala walikua;

Makilagi

Hassan Juma

Rodrique Mpogoro

Baada ya kuhesabu Kura Matokeo yalikua hivi;

Asha Migiro kura 56 sawa na asilimia 2.4%

Amina Ali kura 253 sawa na asilimia 10.5%

John Magufuli alipata 2,104 sawa na asilimia 87.1%

Mshindi atakaye gombea Urais kwa tiketi ya CCM, ni John Pombe Magufuli

3. Update 14:00
John Magufuli amteua Samia. S. Hassan kuwa Mgombea mwenza.




jf2.png


Mwisho
 

mcubic

JF-Expert Member
Mar 3, 2011
10,267
2,000
Seriously when did UKAWA get eaten in this CCM propaganda machine?i have not heard of anything about UKAWA presidential hopefuls or procedures in any platform in the same extent CCM has theirs, yet UKAWA wants to win the election.
UKAWA needs to get it's PR team together.., amateur time is seriously over.
 

Mwasita Moja

JF-Expert Member
Dec 31, 2015
2,906
2,000
Tena mimi nadhani JK ilikuwa zaidi hata ya huyu jamaa.....

Huyu Magufuli anafaa kuwa waziri tu lakini si urais.

Kuna watu watakuja kuona aibu kwa niaba yake huyu mtu....niaminie haya nayosema.

Kama watu walikuwa wanaona Kikwete wakati mwingine anatuaibisha akienda kwa mfano huko Davos kwenye yale makongamano basi huyu ndo bomu zaidi mara 100.

Mtaja nambia tu....
Comment za kipuuzi kabisa
 

Mwasita Moja

JF-Expert Member
Dec 31, 2015
2,906
2,000
Watanzania ni wepesi sana wa kuzugika na kwa mtaji huo CCM itatawala kwa muda mrefu saaaana.

Hii inanikumbusha 2005. Watu wengi sana walifurahi lakini mwishowe ndo hao hao wakaishia kuvunjika moyo.

Na hapa natabiri tena kama nilivyotabiri miaka 10 iliyopita [natamani bcstimes.com ingekuwa bado ipo tuyarejee yote niliyoyatabiri wakati ule].

Huyu jamaa naye ni bomu kabisa na huenda ni bomu kuliko hata Kikwete.

Hana kabisa presidential cachet.

Hata uelewa tu wa kanuni za diplomasia nyepesi nyepesi unampiga chenga.

Mtaja nambia kama bado tuko hai......
Comment za kipuuzi kabisa
 

Mp Kalix2

JF-Expert Member
Oct 4, 2010
5,947
2,000
Wakuu habari,

Tunawaletea kinachojiri kwenye Vikao vya CCM vinavyoendelea Dodoma.

Fuatana nasi... Karibuni sana.

==================



Update 12:55
Ana Makinda Anasema;

Kura zilizopigwa zilikua 2422

Kura zilizo haribika zilikua 6

Kura halali 2416.

Mawakala walikua;

Makilagi

Hassan Juma

Rodrique Mpogoro

Baada ya kuhesabu Kura Matokeo yalikua hivi;

Asha Migiro kura 56 sawa na asilimia 2.4%

Amina Ali kura 253 sawa na asilimia 10.5%

John Magufuli alipata 2,104 sawa na asilimia 87.1%

Mshindi atakaye gombea Urais kwa tiketi ya CCM, ni John Pombe Magufuli

3. Update 14:00
John Magufuli amteua Samia. S. Hassan kuwa Mgombea mwenza.




View attachment 267563

Mwisho
Image sielewei
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom