Yaliyojiri katika vikao vya CCM Dodoma - Julai 10-12, 2015. Magufuli achaguliwa kuwa mgombea Urais | Page 316 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yaliyojiri katika vikao vya CCM Dodoma - Julai 10-12, 2015. Magufuli achaguliwa kuwa mgombea Urais

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by JamiiForums, Jul 10, 2015.

 1. JamiiForums

  JamiiForums Official Robot

  #1
  Jul 10, 2015
  Joined: Nov 9, 2006
  Messages: 5,104
  Likes Received: 2,303
  Trophy Points: 280
  Wakuu habari,

  Tunawaletea kinachojiri kwenye Vikao vya CCM vinavyoendelea Dodoma.

  Fuatana nasi... Karibuni sana.

  ==================

  Updates:

  1.
  Sasa mchakato unaanza rasmi, Wajumbe kamati ya Maadili wanaingia Ukumbini, CC itafuata, haijajulikana kama na NEC itafanyika leo, itategemea na muda utakao tumika na vikao viwili hivyo.

  2.
  Rais Kikwete ameingia Ukumbini muda huu

  3.
  Kikao cha Usalama na maadili kinaendelea. Hiki hata kikiisha hakina briefing. kama kawaida, Ulinzi umeimarishwa na state

  4.
  Kuweka Updates si rahisi kama mnavyodhani sababu ulinzi ni mkali na hakuna aliyeruhusiwa kuingia na simu. Kumbuka hii ni kamati ya maadili, hivyo kuweni wavumilivu. Kikao kinaendelea.

  5. 14:46
  Kamati ya maadili imemaliza kazi yake, sasa ni zamu ya CC kuingia, lakini Rais Kikwete katoka, Kikao kitaanza akirudi.


  6. Update 16:00
  Wajumbe wa CC ndo wameingia sasa hivi, watapewa majina matano na kamati ya maadili ya Wagombea urais.

  7.Update 16:55
  Team inayomuunga mkono Edward Lowassa zaidi ya watu 200, wamekutana mchana huu Katika Ukumbi wa St. Gasper, kuweka msimamo iwapo huyo wanayemtaka hatakuwemo kwenye Top 5 ya Wagombea waliopitishwa na kamati ya maadili.

  8.Update 18:50
  CC imemaliza Kikao chake, Nape amesema majina matano yaliyopendekezwa yatatolewa baada ya Kufuturu.

  9. Update 22:55
  CC bado inaendelea, sasa hivi watu wa catering wanawapelekea vyakula na vinywaji (Pengine ni daku ya leo kwa waliofunga?)

  Julai 11, 2015:

  1. Update 01:00
  CC imemaliza kikao chake; Nape kakutana na waandishi na kuna tetesi kuwa kuna kundi lilikuwa linajipanga kufanya mapinduzi ya Mwenyekiti wa CCM. Aidha, Nchimbi na wenzake wawili wameondoka wakiwa wamejaa jazba na wameonekana kutokubaliana na maamuzi ya CC. Updates zaidi zinafuata...

  2. UPDATE 01:20

  Hatimaye 5 Bora imejulikana, ni:

  1) Bernard Membe

  2) John Magufuli

  3) Asha Rose Migiro

  4) January Makamba

  5) Amina S. Ali
  .
  [​IMG]
  3: Update 12:00
  Nchimbi, Mkono na Kibajaji wamezuiwa getini wasiingie mkutanoni kisa hawana vitambulisho. Baada ya tafrani ya takribani robo saa wajumbe hao wameruhusiwa kuingia.


  4: Update 12:15
  Mwenyekiti wa CCM Taifa, mh. Kikwete amefungua kikao cha Halmashauri Kuu Taifa (NEC) cha kuchuja majina matano nafasi ya kugombea Urais.

  5: Update 12:51
  NEC imemaliza kikao cha kupiga kura, Tatu bora inatangazwa hivi punde (Kama itatokea)

  6: Update 13:05
  Kikao cha Halmashauri Kuu kimepitisha jina la Dr. Shein kuwa mgombea wa Urais Zanzibar.

  7.Update 13:25
  Wanec wametoka nje, hawana imani na CC, wanahoji kwanini Membe apite 5 bora, Lowassa aachwe?. Wametishia kuifuta CC. Ngoma imeachwa wazee kina Mwinyi na Mkapa wamebaki wakishauriana na viongozi nini cha kufanya.

  8. Update 13:33
  Hali ni tete Dodoma, Wapambe wa Lowassa, Wametishia Amani, Wamejikusanya kwenye bustani ya Nyerere Squre Wanaimba. Tunamtaka Lowassa tunamtaka Lowassa...!!

  9:Update 14:00
  Mkutano umefunguliwa na Mwenyekiti wa chama Rais Kikwete na kuahirishwa baada ya Dakika saba kwa kile wanachodai ni kuruhusu watu wakapate Chakula cha mchana. Wakati Mwenyekiti wa Chama anaingia, Wajumbe wa NEC walimpokea kwa wimbo wa "Tuna imani na Lowassa" hadi rais anakaa wameendelea kuimba
  .


  10: Update 17:30
  Mkutano wa NEC, wajumbe wanapiga kura hivi sasa kupata wagombea tatu (3) BORA. Mkutano mkuu wa Taifa Utaanza saa TATU usiku.

  12 Julai 2015

  01: Update 00:45
  Wagombea tatu bora wamejinadi mbele ya Mkutano Mkuu. Wajumbe wamepiga kura.

  Matokeo yatatolewa tarehe 12 Julai, 2015 siku ya Jumapili saa 4 Asubuhi.

  Mwenyekiti wa CCM Taifa ameahirisha kikao.

  2.Update: 13:50

  Spika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Anna Makinda ambaye ni Mwenyekiti wa uhesabuji kura akisaidiana na Spika wa Zanzibar wanamkabidhi Rais Kikwete Kazi walioifanya jana, Kisha Rais Kikwete anamruhusu Anna Makinda Kutangaza matokeo.

  Update 12:55
  Ana Makinda Anasema;

  Kura zilizopigwa zilikua 2422

  Kura zilizo haribika zilikua 6

  Kura halali 2416.

  Mawakala walikua;

  Makilagi

  Hassan Juma

  Rodrique Mpogoro

  Baada ya kuhesabu Kura Matokeo yalikua hivi;

  Asha Migiro kura 56 sawa na asilimia 2.4%

  Amina Ali kura 253 sawa na asilimia 10.5%

  John Magufuli alipata 2,104 sawa na asilimia 87.1%

  Mshindi atakaye gombea Urais kwa tiketi ya CCM, ni John Pombe Magufuli

  3. Update 14:00
  John Magufuli amteua Samia. S. Hassan kuwa Mgombea mwenza.
  jf2.png

  Mwisho
   
 2. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #6301
  Jul 12, 2015
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,893
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  Hiyo post niliileta Mimi , na alieongezewa ulinzi alikuwa Makongoro Nyerere , kwa busara za baraza la ushauri, na ushauri wao ulikubaliwa na JK , na jk alikubali lakini top 5 ya wazee wa ushauri ilipoenda kanati kuu kikwete akaikataa na kuchukua yake na kuipitisha kimabavu na maghufuli hakuwemo ndipo wazee wakashaur tena awekwe maghufuli baada ya mapendekezo ya awali kukataliwa ambao walikuwa
  1 Pinda
  2 Bilal
  3 Asha rose
  4 Makongoro
  5 Jaji ramadhani
  Kikwete akawatosa wazee na kuja na list yake na walipomuuliza chaguo lake akasema Membe , ndipo mkapa akachukia wakachenjiana kwenye kikao ila kikwete akalazimisha ila akakubali maghufuli kwani alijua ni msindikizaji , baada ya kukubali marais wastaafu wa Tanzania na Zanzibar wakaomba maghufuli apigwe tafu na mchezo ndipo ulipoanzia , nazani wote mashahidi kilichotokea NEC kwa chaguo la kikwete na familia yake , ambapo ndani ya NEC ridhiwan alipiga kampeni za wazi kwa Membe na Asha rose

  Baada ya kupigwa NEC JK aliishiwa pozi ikabidi nguvu iende kwa asha rose migiro akimtumia riz one na membe wampigie kampeni akiwemo nape na makonda, dili likashtukiwa maana iliundwa propaganda ya ni zamu ya mwanamke , wajumbe MM walipozipata wakasema OK tutapiga kura za kukuonesha sisi ndio CCM na sio wewe

  Upepo ukaanza someka baada ya maghufuli kuingia ukumbini yaani ni kelele na vifijo hali ambayo nape hakuipenda pia kikwete mwenyewe hadi kuwaambia kwa sauti watu wa geita tulieni hii ilikuwa ni kutengrneza UFA wa kikabila lakini ilishindikana , na MM imemuonesha adabu kikwete na familia yake , pia MZEE Warioba,Dr salim , kinana, MZEE mkapa, MZEE mwinyi na Karume wamefurahi sana kwani jamaa aliwadharau sana wakati yeye ndiye aliwaomba ushauri na akasema watakachokubaliana yeye atanaliki ,


  Pia amesahau akistaafu na yeye ataenda baraza la ushauri , hivyo watamcheka sana kwani hatakuwa na nguvu tena ,

  Magufuli haziivi na kikwete mtu asiwadanganye, kumbukeni kikwete alikuwa anamchukia sana magufuli 2005 hadi akataka ampoteze kisiasa kwa kumpa wizara ya samaki,

  Magufuli ni zao la rais mkapa, na MZEE mkapa sasa atakuwa huru sana na kufurahi chaguo lake kushinda


  Ngoja nifatilie mkutano, now pinda anaongea

  Itaendeleea kujua , zaidi wakati wa uteuz na vikao vya maridhiano​


   
 3. c

  chuwaalbert JF-Expert Member

  #6302
  Jul 12, 2015
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 3,513
  Likes Received: 1,800
  Trophy Points: 280
  ......at the end Laigwanan ndani.... Pole Comrade. Kepteni wa watu wenye safwari yenye matumaini NJE. Safari ya MATANIO kwa kuliweka Taifa katika vurugu HAIWEZEKANI. Ni kweli kumkata Lowassa yabidi ujipange. hapa uko sawa. Na watu walojipanga kweli kweli.
  1. Ilitakiwa Bunge limalize shughuli kwanza.
  2. Ilibidi ratiba itibuliwe.
  3. Ilibidi Waliolipwa kufanya fujo kwa kukatwa kwa Laigwanan wadhibitiwe na vyombo vya dola.
  4. ..........nk.....nk.....
  Upo? Asubiri kugombea 2020, kama afya itaruhusu. Kwa Sasa atakayeshindana na Daktari Silaha ni Daktari wa Ualimu na Kemia, ambaye wengi wanafikiri ni Mhandisi wa Ujenzi......
  Bye bye Lower Sir.
   
 4. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #6303
  Jul 12, 2015
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,348
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 0
  UKAWA hajatangaza mgombea. PERIOD
   
 5. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #6304
  Jul 12, 2015
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 15,404
  Likes Received: 2,055
  Trophy Points: 280
  mkuu ocampo four labda amtafute hemedy ally msaidizi wa bashe pale 4u.. hadi huruma au aje kwangu Nkuhungu nimpe nauli.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #6305
  Jul 13, 2015
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,493
  Likes Received: 1,002
  Trophy Points: 280
  Ina maana humjui mgombea wa Urais kupitia Demokrasia ya UKAWA kuwa ni Dr Slaa?
  subiri vurugu yake PERIOD
   
 7. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #6306
  Jul 13, 2015
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,493
  Likes Received: 1,002
  Trophy Points: 280
  Mkuu sipati picha,
  siku hiyo nilikuwepo jirani katika hizo nyumba karibu na uwanja wa ndege lakini sikuambulia wahusika wote wa NMC leo ndio umenifungua
  funika kombe ...
   
 8. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #6307
  Jul 13, 2015
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,493
  Likes Received: 1,002
  Trophy Points: 280
  Mkuu upo sahihi kabisa, kuna kipindi Mkuu aliomba pooo watu wakale kwanza
  NEC walifyatuka hawakuficha jamaa kuipanga familia nzima madarakani, licha ya kukamata 5m kila mtu wakaona isiwe shida wakahama kwa EL na kumbeba Maguufull
  alichotuudhi Makongo ni mtindo wake usiobadilika wa kubeba mabag (malooser) tena wahudumu Doible H
   
 9. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #6308
  Jul 13, 2015
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,196
  Likes Received: 256
  Trophy Points: 180
  the second wife is always a mistress...!! ndiyo sababu mke wa kwanza lazima akubali kwanza kabla second hajaingizwa ndani....mke ni mmoja tu.

  Hata huko ukawa the best is Dr Slaa.....sexual relationship yake iko safi? Alifunga ndoa na Rose Kamili? how about the current one...Ms Mushumbuzi kama sijakosea jina?.....masuala ya ngono ni magumu mno? ndiyo maana viongozi wengine huamua kukaa kiseja tu kama Putin.
   
 10. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #6309
  Jul 13, 2015
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,169
  Likes Received: 528
  Trophy Points: 280
  Lowassa alikuwa anajua kashfa zake hataweza kupita lakini wametumia kampeni kulimbikizia pesa za wafanyabiashara waliodanganywa. Hizi ni mbinu za kifisadi na kitapeli Lowassa kapata pesa nyingi wakati huu wa kampeni kuliko wakati mwingine wowote kwa wafanyabiashara hasa wa kihindi kutoa pesa nyingi ya shughuli mbalimbali. Sasa ni wakati wa kutafuta project nyingine ya kuingiza pesa!
   
 11. kivava

  kivava JF-Expert Member

  #6310
  Jul 13, 2015
  Joined: Apr 2, 2013
  Messages: 5,519
  Likes Received: 4,201
  Trophy Points: 280
  Punguza umbea kijana,hizo habari zako za kijinga source yake ni ipi?
   
 12. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #6311
  Jul 13, 2015
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,832
  Likes Received: 2,109
  Trophy Points: 280
  Mkuu hata usingeandika haya yote tayari AVATAR yako imeshamjibu
   
 13. baro

  baro JF-Expert Member

  #6312
  Jul 13, 2015
  Joined: May 12, 2014
  Messages: 2,209
  Likes Received: 1,462
  Trophy Points: 280
  Mkuu mbona umecopy post yangu niliyoiandika page ya 610 , na kujimilikisha bila kuni ackonoledge
   
 14. F

  FUSO JF-Expert Member

  #6313
  Jul 14, 2015
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 13,181
  Likes Received: 3,446
  Trophy Points: 280
  kweli nimeamini URAIS hauna ubia - WAMEKATA.
   
 15. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #6314
  Jul 14, 2015
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,051
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
  Bado nasimama na msimamo huu kuwa Makongoro ndiye alikuwa mgombea sahihi kwa ccm kuikabili UKAWA iliyojipanga vilivyo.

  Tusubiri mgombea wa UKAWA tuone nini kitakachojiri.
   
 16. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #6315
  Jul 14, 2015
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,051
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
  Bado nasimama na msimamo huu kuwa Makongoro ndiye alikuwa mgombea sahihi kwa ccm kuikabili UKAWA iliyojipanga vilivyo.

  Tusubiri mgombea wa UKAWA tuone nini kitakachojiri.
   
 17. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #6316
  Jul 14, 2015
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,051
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
  CCM inepuuza nguvu ya jina la Nyerere!
   
 18. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #6317
  Jul 15, 2015
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,612
  Likes Received: 2,380
  Trophy Points: 280
  Juzi tumeona kitimutimu cha kumtafuta mgombea Urais kwa tiketi ya CCM ulivyo acha nyasi zimelala pale Dodoma ilikuwa ni mshikemshike pale ukumbini na haswa wajumbe wa NEC.

  Katika watia nia walikuwa ni wanasiasa Nguri naweeza kusema nikianza na hawapa chini ambao hawakupenya Tano bora!


  1. Dr Ghalib Bilal-Makamu wa Rais
  2. Mizengo Peter Kayanza-Waziri Mkuu
  3. Wasira-Waziri wa Kilimo
  4. Jaji Ramadhan-Jaji Mkuu mstaafu
  5. Mark Mwandosya-Waziri asiyekuwa na Wizara maalumu.

  Katika hao nilio wataja wote ni watu wapo katika ngazi za juu serikalini kasoro Jaji Mstaafu.

  Cha kushanga nikuwa wote hao hakuna hata mmoja aliyeweza kupita katika tano bora!

  Je, nikwa sababu ya kuwa hawana vigezo vya kuwa rais je walipata vipi hayo madaraka hadi Mkuu wa nchi kushindwa kuwapitisha katika 5 bora?

  Bado napatwa na wasiwasi iweje Naibu waziri wa Mawasiliano apite 5bora Makamu wa rais na Waziri mkuu wa serikali iliyopo madarakani hata asipitishwe 5 bora?

  Swali; Je, ile kamati ya Usalama na Maadili ya CCM inaongozwa na nani??Je ina mamlaka ya kukata jina la mgombea??au yenyewe kazi yake nini?

  Kama ni kuweka kasoro za mgombea na CC kuzichambua iweje majina haya hayakufika CC?

  Je, waliopenya watapata ushirikiano wa hawa ambao hawakufika 5 bora?

  Je, huyo alipenya atakibeba chama??
   
 19. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #6318
  Jul 15, 2015
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 25,403
  Likes Received: 26,227
  Trophy Points: 280
  Sio CCM iliyopuuza,Mako kasema kamati ya maadili iliweka jina lake la kwanza tano bora ila kwenye KK kuna mtu mmoja kwa madaraka take akakata jina lake na alipoulizwa sababu hakujibu. Jee MTU huyo ni nani na kwa mini alimtoa Mako aliyependekezwa na kumuweka Bernard?
   
 20. P

  Pohamba JF-Expert Member

  #6319
  Jul 15, 2015
  Joined: Jun 2, 2015
  Messages: 16,516
  Likes Received: 25,648
  Trophy Points: 280
  Mwaka huu Kamati kuu, Halmashauri kuu na Mkutano Mkuu vilikuwa vikao vya kupiga mihuri, Maamuzi yote yalifanywa na Jakaya kupitia kinachoitwa kamati ya Maadili, Kamati kuu ilikuwa na vikao viwili, cha kwanza kilijumuisha wote kasoro Jerry Slaa, Sofia Simba, Kimbisa, Nchimbi na Sadifa kwa kuwa wanajulikana ni Team Lowassa Nape aliviita 'vikao vya mashauriano ' baada ya kupewa taarifa na kukubali ndo kikaitishwa kikao rasmi cha kamati kuu kikapewa taarifa rasmi lakini Haikuwa ngeni kwa wote isipokuwa watu wa Lowassa, kila walipofurukuta wakabanwa mbavu kisawasawa.
   
 21. D

  Dopas JF-Expert Member

  #6320
  Jul 15, 2015
  Joined: Aug 14, 2010
  Messages: 1,151
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  1. Umri mkubwa,
  2. hawajaonesha cha pekee katika madaraka madogo waliyopewa cha kuwafanya wakabidhiwe tena madaraka makubwa zaidi
  3. Isingewezekana wote 38 wawe kwenye tano bora.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...