Elections 2015 Yaliyojiri katika vikao vya CCM Dodoma - Julai 10-12, 2015. Magufuli achaguliwa kuwa mgombea Urais

Juzi tumeona kitimutimu cha kumtafuta mgombea Urais kwa tiketi ya CCM ulivyo acha nyasi zimelala pale Dodoma ilikuwa ni mshikemshike pale ukumbini na haswa wajumbe wa NEC.

Katika watia nia walikuwa ni wanasiasa Nguri naweeza kusema nikianza na hawapa chini ambao hawakupenya Tano bora!



  1. Dr Ghalib Bilal-Makamu wa Rais
  2. Mizengo Peter Kayanza-Waziri Mkuu
  3. Wasira-Waziri wa Kilimo
  4. Jaji Ramadhan-Jaji Mkuu mstaafu
  5. Mark Mwandosya-Waziri asiyekuwa na Wizara maalumu.

Katika hao nilio wataja wote ni watu wapo katika ngazi za juu serikalini kasoro Jaji Mstaafu.

Cha kushanga nikuwa wote hao hakuna hata mmoja aliyeweza kupita katika tano bora!

Je, nikwa sababu ya kuwa hawana vigezo vya kuwa rais je walipata vipi hayo madaraka hadi Mkuu wa nchi kushindwa kuwapitisha katika 5 bora?

Bado napatwa na wasiwasi iweje Naibu waziri wa Mawasiliano apite 5bora Makamu wa rais na Waziri mkuu wa serikali iliyopo madarakani hata asipitishwe 5 bora?

Swali; Je, ile kamati ya Usalama na Maadili ya CCM inaongozwa na nani??Je ina mamlaka ya kukata jina la mgombea??au yenyewe kazi yake nini?

Kama ni kuweka kasoro za mgombea na CC kuzichambua iweje majina haya hayakufika CC?

Je, waliopenya watapata ushirikiano wa hawa ambao hawakufika 5 bora?

Je, huyo alipenya atakibeba chama??
☝️
 
Back
Top Bottom