Yaliyojiri katika Uchaguzi wa Udiwani kata 27 na Matokeo - Feb 9, 2014

CHOPA TATU KURA KATA TATU,

Hivi mmetumia chopa kuzunguka Je mngekuwa Kama CCM kampeni wanapiga watu wa Eneo husika ingekuwaj? Pole sana ndugu zangu CDM ndio sihasa
 
Wana jamvi ushindi wa chadema jana kata ya njombe mjini ni ishara kua speaker wa bunge la jamhuri wa muungano wa tz hayuko salama ktk uchaguzi ujao,kikubwa apishe damu changa lkn pia yeyote wa ccm njombe amekwisha hatoboi

amekwisha kwa Kata moja tu?
 
Asiyekubali kama CHADEMA imefanya vibaya uchaguzi huu ana matatizo ya kufikiri;Kama walipaswa kutetea kata 3 na MMEPATA kata 3 hii ni ishara kuwa chama kimedumaa!Maneno kama CCM imefubaa haijaonyeshwa kwa vitendo kwenye sanduku la kura

CHADEMA hawajachelewa bado warudi kwa wananchi na wasidanganywe na uwingi wa watu kwenye mikutano yao!
(1)Wasiwafuate wananchi kwa msimu,wafungue ofisi kila kijiji
(2)Waachane sasa na mambo ya uchaguzi wao wa ndani wa kitaifa bali watumie resources zote kuanzisha ofisi vijijini
(3)Wafanye kampeni za kisayansi za sio kutegemea uwingi wa watu kwenye mikutano yao(wajue hapo kijijini nani ni pro-CHADEMA na nani sio)
(4)Kampeni za kila kata ziongozwe na wazawa na viongozi wa kitaifa waende kuimarisha mahusiano tu

Wananchi WAMEICHOKA CCM lkn bado chama mbadala(CHADEMA)kinasua sua kujipanga

pamoja mkuu, kama viongozi wa chadema wana akili, wafuate ushauri. huu, tatizo viongozi wa. chadema makao makuu wanawaza kuruka na chopa tu na kulipana posho
 
Sasa kama hali yenyewe ndiyo hiyo hata hilo daftari la wapiga kura ambalo mnataka liboreshwe ndiyo mtashida hauoni kama siyo mbadala.
RITZ naamini najadiliana na mtu intelligible!
Soma vizuri comment zangu mimi cjagusia daftari nieangalia kipengere kidogo cha umwagaji senti katika chaguzi.
Nimefanya vijijini muda mrefu na karibuni nimetokea south,with poverty and ignorance wenye pesa watafanya lolote watakalo katika nchi hii.CCM itatawala sana kwa sababu umaskini na ujinga bado ni mkubwa,hilo halina shaka rest assured!!
 
Kurugenzi ya Habari ilinywea ghafla, walikuwa hawaamini wanachokiona.

Uongozi wenu chadema uko pale kujishibisha wenyewe tu. Mbowe na Slaa si viongozi ni wachumia tumbo na maneno mengi tu, wako too local.

viongozi wa chadema hawana mbinu kabisa za kushinda uchaguzi,wamebaki kumuota zito tu
 
Last edited by a moderator:
pamoja mkuu, kama viongozi wa chadema wana akili, wafuate ushauri. huu, tatizo viongozi wa. chadema makao makuu wanawaza kuruka na chopa tu na kulipana posho
Watu walioko chini ndio wanatakiwa waanze wenyewe kujua nini maana ya demokrasia ya vyama vingi,waelewe kuwa hakuna uadui,watmbue kuwa lengo ni kupeleka mbele maendeleo ya nchi.
Katika hali ya sasa hili halipo pamoja na jitihada zote za kuwaamsha.Kama mtu anaweza kutoa kura kwa 1000/-tutegemee nini?
 
Chadema bana! Kama mazuzu vile! Sasa uboreshaji wa daftari la wapiga kura unaweza kuwabadili fikra hao wananchi kwenye maamuzi yao? Mbona chadema wameshindwa hata kuwabadili mtazamo hata hao waliomo kwenye daftari la sasa? Chadema haikubaliki.
Hawa jamaa watu wa ajabu sana ebu angalia haya matokeo hapa chini.
KUTOKA KONDOA MATOKEO NI
KONDOA CCM ------------1,296
CUF---------- 935.
CDM--------29
NCCR------34
Halafu bado utasema daftari litasaidia utadhani CCM hawana watu wao wapya.
 
Kwa namna nilivyokuwa najuwa kuhusu arusha nilijuwa ssm aitapata hata kura labda ya mgombeya na familiya yake kwani niliaminishwa kuwa wote wa arusha ni cdm kumne ushindani upo tena kwa tofauti ya kura 400 makamanda kweli bunduki zao zilikiwa gobole isiokuwa na risasi nyambafu
 
RITZ naamini najadiliana na mtu intelligible!
Soma vizuri comment zangu mimi cjagusia daftari nieangalia kipengere kidogo cha umwagaji senti katika chaguzi.
Nimefanya vijijini muda mrefu na karibuni nimetokea south,with poverty and ignorance wenye pesa watafanya lolote watakalo katika nchi hii.CCM itatawala sana kwa sababu umaskini na ujinga bado ni mkubwa,hilo halina shaka rest assured!!

watu wa vijijini ndio inatakiwa chadema wawabadili fikra na kuichagua chadema,ukibaki kulialia haitasaidia, mbona vijana wengi tu ni wajinga wako mjin na wanaichagua chadema
 
Watu walioko chini ndio wanatakiwa waanze wenyewe kujua nini maana ya demokrasia ya vyama vingi,waelewe kuwa hakuna uadui,watmbue kuwa lengo ni kupeleka mbele maendeleo ya nchi.
Katika hali ya sasa hili halipo pamoja na jitihada zote za kuwaamsha.Kama mtu anaweza kutoa kura kwa 1000/-tutegemee nini?

wataielewaje hiyo demokrasia bila kueleweshwa? wanaitaji elimu ya muda mrefu na sio ka mkutano kamoja tu ka masaa mawili
 
watu wa vijijini ndio inatakiwa chadema wawabadili fikra na kuichagua chadema,ukibaki kulialia haitasaidia, mbona vijana wengi tu ni wajinga wako mjin na wanaichagua chadema
Mimi sijalialia ila ukweli ndio huo with poverty and ignorance CCM is for EVER!!
 
njombe mjini chadema wameshinda kwa ajili ya weakness ya ccm, kuwalipisha ushuru wafanyabiashara kiholela,michango ya shule, na kuliwa kwa hela iliyotengwa kwa ajili ya maji, kumeiua ccm. na wala sio sera za chadema zimewapa ushindi, ndio maana asilimia kubwa ya walioipigia kura chadema ni wanawake wafanyabiashara wa sokoni mjini na wahanga wa kero hizo
 
Kwa namna nilivyokuwa najuwa kuhusu arusha nilijuwa ssm aitapata hata kura labda ya mgombeya na familiya yake kwani niliaminishwa kuwa wote wa arusha ni cdm kumne ushindani upo tena kwa tofauti ya kura 400 makamanda kweli bunduki zao zilikiwa gobole isiokuwa na risasi nyambafu

Verry true!
 
Hii ni hadithi ya mbaazi na Jua mkuu...

Ni blah blah na porojo za mtaani tu..

Ila ukweli ni Kwamba CCM ndio iko Madarakani, JK ndio Rais na pia jana CCM imeshinda Kata 23 bila Chopa wala M4C/OPD...

Hayo mengine tumeanza kuyasikia tangu 1995...Hivyo hakuna jipya hapo..

Na ni kweli hakuna jipya kwa sababu YA ZAMANI BADO HAYAJA EXPIRE! Lakini siku litakapokuja jipya hakika huijui wewe na hao wapambe wenu mlioifanya Ikulu kuwa pango la ''wapambe nuksi''
 
Hawa jamaa watu wa ajabu sana ebu angalia haya matokeo hapa chini.

Halafu bado utasema daftari litasaidia utadhani CCM hawana watu wao wapya.

Babuu! mara hii umeshavua ule ushungi wako kwenye ID nyingine.... kweli unazeeka vibaya. Hebu njoo tena na darsa tufyoze ilmu ya historia ya ''UKWELI'' ya Tanzania sheikh!
 
sasa kuna ulazima gani kwa chadema kushiriki uchaguzi wakati wanajua watashindwa?
Tunaliangalia jambo hili kwa mitizamo tofauti na ndio raha ya mijadala.
Kuna sababu gani ya kukubali vyama vingi wakati unatumia hata state organs kukandamiza opposition?Ushahidi tele-kesi za ugaidi,kinasa sauti chini ya kitanda cha Slaa,mawasilianao ya ZZK na Nzoka na mengi tu.
 
kuna magazeti yameandika chdm imeshinda kata nane hii habari wameitoa wapi?

Kwani weye hutufahamu?
Tungelishinda hizo namba ulizozitaja tulikuwa hatukamatiki, na kwakuwa umeona tupo kimya jua kimeeleweka, na hayo matokeo ya kushinda hata hizo kata 3 twashukuru Mungu mno.

Ujinga mkubwa tumeutaka wenyewe na kujiamini kupita kiasi!

Sasa twajiandaa kwa uchaguzi mkuu tena tuone itakuwaje! Lakini tutafanyiza vikao vingi tu ili tupate kutatua hii migogoro ya ndani kwa ndani.

Kikubwa zaidi wale watendaji wakuu itabidi wayakubali mawazo hata ya wachache ndo SIASA ilivyo.

Tofauti na hapo tutapigwa mtama tena na tutakuja na ile slogan yetu NCHI haitawaliki!
 
Back
Top Bottom