Yaliyojiri katika mkutano wa One belt one road huko uchina.

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
20,396
24,974
Mkutano wa One Belt One Road umefunguliwa leo na Rais wa China Mhe Xi Jinping. Mkutano huo unahudhuriwa na Wakuu wa Nchi 20..na Mawaziri 100.

Tanzania inawakilishwa na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhe Prof Makame Mbarawa.

China imecommit usd 600Billion kwa ajili ya uwekezaji around Silk Road route countries.

Kutoka kwenye mkutano huu kuna habari njema mbili kwa nchi yetu.

1) Kesho kutwa Tanzania na China zitasaini Mkataba wa kufungua soko la China kwa bidhaa za muhogo kutoka Tanzania.

Hii ni fursa kubwa kwa wakulima wetu na wawekezaji wa viwanda cha kuprocess muhogo kuzalisha bidhaa mbalimbali. .

2) Habari njema ya pili.....kesho utasainiwa Mkataba wa joint venture ya two largest cement manufacturers wa China-SINOMA na Hegya kujenga Industrial Park na kiwanda kikubwa cha cement mkoani Tanga.

Kiwanda hicho kitakapokamilika kitazalisha ajira 4000 na kuzalisha tani milioni 7 za cement kwa mwaka ambazo asilimia 60 itakuwa exported nje kwenye ujenzi wa miradi mbalimbali ya ujenzi wa miundombinu under One Belt,One Road.

Kutokana na uwekezaji huo Mkubwa, Mkuu wa mkoa wa Tanga Mhe Martin Shigela amealikwa pia na Serikali ya China kushiriki kwenye mkutano huu wa OBOR.

Tumejulishwa na wawekezaji hao miongoni mwa watakaoajiriwa watatoa kipaumbele kwa Watanzania waliosomea China.

Hiyo ni fursa pia kwa wale wenye interest ya real estate hii ya kununua viwanja Tanga kwa ajili ya kudevelop nyumba za makazi na majengo ya biashara kwani uwekezaji huo mkubwa utapelekea multiplier effects kwa sekta nyingine zote.


Kwa wale wenye interest ya kilimo natoa rai kwenu changamkieni hii fursa ya kulima muhogo na kuuza kwenye soko la China.

Watakaofaidi zaidi ni wale watakaoweka viwanda vya kuprocess bidhaa za muhogo na kuzi export huku..muhimu ni kutafuta uwezekano wa kupata teknolojia rahisi kuanzisha processing plants ndogo za muhogo ili kuongeza thamani ya bidhaa hizo.

Cha muhimu zaidi kwa mwenye interest ya ku export muhogo shurti asajili kampuni yake wizara ya kilimo huko nyumbani ili iwasilishwe kwenye Mamlaka za China.

Kuna criteria za kuqualify. Mtafahamishwa na Wizara ya Kilimo.

Kila kheri katika kupambana kuondokana na umaskinikini.

KIZURI KULA NA MWENZAKO AU UMPENDAYE

As received!
 
Ok ngoja niwahi maneromango kuandaa mashamba,

by the way,apart from ugali kuna bidhaa ipi tena ya mhogo?
 
Ok ngoja niwahi maneromango kuandaa mashamba,

by the way,apart from ugali kuna bidhaa ipi tena ya mhogo?
 
Kwa silka za watanzania navyowafahamu,Umetoa taarifa nzuri na mwenye akili na uthubuti ni mwanzo wa kukaa chini na kuchora mipango kuhusu fursa kama hizo.

Lakini wataanza kutoa negative response mpaka utashangaa na kujiuliza shida Sasa ni nini kuhusu maendeleo ya kwao binafsi na nchi kwa ujumla!??!
 
Tatizo ni pale siasa zitakavyotawala ktk sekta huyo,utashangaa. Suburini mtaona tena si mbali sana
 
Shukrani wa taarifa.

Ni wakati wa serikali sasa kuona ni namna gani ya kuhusisha mikataba hii na real production. Kunahitajika mikakati. Kama uzalishaji wa mbegu bora, mafunzo ya ukulima wa kisasa, pembejeo. Kukiwa na uhakika wa soko unaweza kufanya hata contract farming-kilimo cha mkataba. Hii inaweza kupelekea mitaji ikawafikia wakulima. Shida yakishanza mambo ya urasimu- kama ukitaka kuuza China lazima upitie wizara ya kilimo. Miongozo ingetengenezwa na kuwaacha watanzania waifuate hiyo miongozo- ikiwa ni pamoja na mambo ya kusafirisha chakula nje-kama kutahitaji umuhimu wa pekee kwa soko hili.

Kwa ujumla haya mambo ndiyo tungetaka vyama vyote vionyeshe namna gani ya kusonga mbele. Tumebakiwa kusema tu RAMBIRAMBI za wafiwa zimeliwa. Wanaopiga kelele sijui wamechanga kiasi gani. Mkoa una oversee mamilioni ya hela kupitia miradi mablimbali. Wasipige huko waje wapige za rambirambi.

Nimelisema hapa, pamoja kwamba siyo mahali pake ila propaganda za wanasiasa juu ya rambirambi sinakera sana. Wafiwa wako kimya. Halafu kuna mmoja amesema Makamu wa Raisi aliyewekuwepo Arusha ni kama mtoto katumwa.....yaani haya yanatoka kwa mtu anaeheshimika.
 
Back
Top Bottom