Yaliyojiri katika Mkutano Mkuu wa CHADEMA Desemba 18, 2019 katika Ukumbi wa Mlimani City, Dar

Uonezi, dhuluma, chuki, wivu na umwambafai umejaa kwa MaCCM na mawakala wao!!
Tuzidi kuomba Mungu ili mkutano umalizike salama!!
Lazima tupambane kwa nyanja zote ili haki ya Watanzania ipatikane.
Katiba mpya ni muhimu saana kwa ukombozi na ustawi wa taifa letu.
VIVA CDM ALUTA COTINUA.
VIVA TANZANIA.
 
Mbowe ndio nani?

USSR

Sent using Jamii Forums mobile app
Nenda kapate habari za Mbowe kwa Magufuli maana ndiye mwenyekiti wa chama mwenzie ambaye anasumbua kichwa chake na ndiye pekee ambaye kagoma kumpa sifa za mgongo wa chupa hata wakiwa pamoja umbali wa kurusha ngumi.
Yawezekana humjui kwa vile wewe ni boya!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna mtu wa kumtoa Mbowe kwenye kiti anachokita na baada ya Uchaguzi kumalizika, Mwambe atafukuzwa ndani ya CHADEMA!

Yaliyomkuta Zitto mwaka 2014 yanaenda kumpata Cecil Mwambe!
Zitto mwenyewe aliyefukuzwa ameridhika na adhabu ile kwani anajua alivunja kifungu gani cha katiba na ndio maana hujawahi msikia akilalamikia kufukuzwa kwake.
Kama msomi, huoni aibu nawe kuingia kwenye mkumbo wa waropokaji kuhusu jambo hilo?

Hata Bungeni, Zitto kwa kutambua sheria inasemaje alijitoa mwenyewe kwani alijua anapaswa kufukuzwa kisheria amevunja katiba iliyomleta na kumdhamini Bungeni.

Kwa hiyo acha hizo! Au nawe umeivua elimu yako uwe sawa na wanaccm wengine?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aulizaye ataka kujua: Molema, mbona hamkutupa kura zilizopigwa na walivyopata washindani wa leo ie Mbowe alipata ngapi na Mwambe aliata ngapi?
Swali zuri, lakini pamoja na kuwa sio najibu swali hilo nadhani kilichokuwa kinafanywa ni kudhibitisha wagombea ili kama kuna mjumbe ana pingamizi aliweke lijadiliwe ili apitishwe au akwamishwe.

Dalili ni kuwa hapakuwa na pingamizi kwa wagombea hivyo wakapitishwa majina yao.
Ngoma ya kidemokrasia ni Leo. Ndipo kinafanyika kitu ambacho CCM wameshindwa kukifanya kwa miaka mingi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kichwa cha habari hakiakisi habari yenyewe!! Yaliyojiri au yatakayojiri? au kikao kishafanyika na sasa ni maigizo tu?
 
CHADEMA, uchaguzi huu eidha ni kaburi lenu, au mwanzo wenu wa maisha mapya.
Chagueni mtu atayeweza juzushinda fitna, hila, na mbinu chafu za CCM, vinginevyo mwaka kesho bungeni atarudi Sugu peke yake
Mkuu wagombea wawili tu yule padikikizi alikimbia, amebaki pandikizi mwingine, naye atakatwa tu. Hisia zako negative peleka kwa mkeo
 
Back
Top Bottom