#COVID19 Yaliyojiri katika mjadala wa Wasiochanjwa katika Club House ya Jamiiforums tarehe 12/11/2021

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
625
938
1636730849974.png
Utoaji wa Chanjo ya #COVID19 umekuwa ukihamasishwa kona zote za Dunia huku baadhi ya Nchi zikichukua hatua za kuweka Vikwazo kwa Watu ambao hawajapata Chanjo kurudi Maofisini, kusafiri au kushiriki shughuli za kijamii

Wasiochanja wana sababu mbalimbali ambazo zinawapelekea kusitasita katika kufanya Maamuzi.

Ungana na Jamii Forums katika Mjadala na wasiochanja unaofanyika sasa ili kusikiliza na kutoa maoni yako.

Kujiunga na Mjadala huu bonyeza link hii hapa chini

Yanayojiri

Hoja zinazotolewa na wasiochanjwa
Mdau 1: Sababu zangu za kutokuchanja mpaka sasa ni kwasababu sijaamini katika ushughulikiaji wa Janga la #COVID19. Kuna taarifa nyingi na taarifa ambazo tumezipata ni za upande mmoja. Japokuwa nami ni mhanga wa kuugua katika wimbi la kwanza kabisa ila sijachanjwa.

Mdau 2: Changamoto kubwa kwetu ni kwamba bado tunaficha takwimu. Hatusemi kwa uwazi Chanjo zimekuja na wangapi wamechanja. Hivyo kimsingi sitachanja labda niambiwe taaluma yangu inalazimisha kuchanja

Mdau 3: Mimi sijachanja kwasababu siiamini Serikali na hata Nchi za wenzetu waliochanja ni wanaomini Serikali zao. Afrika Viongozi wetu hawaamini. Pili hizi Chanjo zimekuja kwa Msaada wakati Mimi nilitegemea kuona Serikali yangu imenunua hizo Chanjo.

Mdau 3: Mimi nipo kwenye masuala ya Afya na kitu ambacho kilinishangaza ni upungufu wa Vifaa vya kujikinga. Kama ulininyima Vifaa nitakuamini vipi ukiniletea Chanjo. Watu tunafika sehemu tunapoteza Uaminifu kwa Viongozi. Chanjo zenyewe tulizopata kuna Nchi nyingine hawazitaki.

Mdau 4: Nilisikia kwa Tanzania kwa Wanawake wenye miaka zaidi ya 40 wakichanja wanapata tatizo. Hii imeleta uoga kwa baadhi ya Watu. Pia, sisi ni Wazazi hivyo Wataalamu watusaidie tunafanyaje kuwasaidia Watoto wetu.

Mdau 5: Mimi sijachanjwa na wala sidhani kama nitachanjwa kwasababu siamini Uongozi wetu tangu Corona ipoingia. Walituaminisha tofauti na sasa hivi wanaongea tofauti. Pia siwaamini Wanasayansi kwasababu wana nia zao hivyo wakileta taarifa wanaleta kama ilivyo kwenye Sayansi.

Mdau 5: Hadi sasa hatuna tafiti za ndani zilizofanyika juu ya #COVID19 tafiti nyingi ni za nje ambazo tunazotumia. Ukosefu wa tafiti unafanya nikose imani na wanasayansi, na pia viongozi kukosa misimamo ni suala linalotia shaka.

Mdau 6: Unaambiwa huyu Kirusi anabadilika badilika. Sasa hofu yangu kwamba Chanjo ilitengenezwa kwa variant A je, akija variant B bado itafanya kazi? Pia, wanasema walitengeneza Chanjo kwa kuchukua sehemu ya kirusi. Sasa aliyepata Corona si tayari ameshatengeneza kinga?

Mdau 7: How come mgonjwa wangu alipata #COVID19 hata baada ya kuchanjwa? Hili ndilo linalonisukuma mimi kutokuchanjwa

Mdau8: Nilipokuwa Ufaransa Daktari aliniambia nyie Waafrika mna inborn immunity is it true?

Mdau8: Kuna watu ambao walikaa karibu na watu waliougua #COVID19 lakini hawakuambukizwa inakuaje hii?

Mdau9: Kinachonirudisha nyuma hakuna utofauti kati ya mtu asiyechanjwa. Mtu asiyechanjwa naye anaweza kuambukizwa #coronavirus na pia anapaswa kuchukua tahadhari kama asiyechanjwa.

Mdau9: Jambo kubwa linalonirudisha nyuma ni suala la kiimani. Mfano suala la travelling restriction watu kiimani wanalichukulia kama New World Order

Hoja na Majibu kutoka kwa wataalamu wa Afya
Dr. Osati: Nimeshangaa kuona Mtu ambaye anafanya kazi kwenye Sekta ya Afya anakuwa na mtazamo hasi kuhusu Chanjo. Ukiangalia Chanjo karibu zote (takriban 15) tunazochanja Tanzania zinatoka Nchi nyingine. Hakuna Chanjo tunayotengeneza sisi wenyewe. Zote ni Msaada.

Dr. Osati: Chanjo zote za Corona zimetengenezwa kwa ajili ya kusaidia Mwili kutengeneza Kinga. Kiujumla Chanjo hizi zimekuwa salama sana. Mpaka leo waliochanja ni zaidi ya bilioni 4 ambao ni zaidi ya nusu ya Watu Duniani. Dunia haiwezi kuacha kutoa Chanjo kwasababu Watu wanapinga. Corona inasambaa kama Moto wa pori na Nchi nyingi ziliingia kwenye Lockdown. Hapa Tanzania ndio hatukufanya hivyo.

Dr. Osati: Mtu hupata Kinga kwa namna 2. Moja ni Kinga ya kuzaliwa ndio maana tunasisitiza Mama Mjamzito kula vizuri. Kinga ya 2 Mtu anaipata pale anapopata tatizo kama kuumwa. Mtu kupata tatizo sio lazima lihusike na Chanjo ingewezekana kupata tatizo hilo kupitia namna nyingine.

Dr. Osati: Watu wanaopata Presha ambayo haijadhibitiwa anaweza kupata tatizo la Damu kuganda. Pia Kirukari, Shinikizo la Damu au unene kupita kiasi na wanaovita Sigara wako katika hatari ya Damu kuganda. Tatizo la Damu kuganda liligundulika kwenye Chanjo ya J&J na #AstraZeneca. Utafiti ulipofanyika iligundulika Watu walipata tatizo walikuwa na sababu zingine za Kiafya zilizopelekea tatizo.
Hivyo hakuna udhibitisho wa moja kwa moja kwamba Chanjo ndio zilileta tatizo.

Dkt. Osati: Tulipokuwa wadogo tulichanja chanjo ya TB ile ya BCG lakini ukiwapima watu leo utawakuta na vimelea vya TB kwa kuwa tunachangamana. Hata kwenye chanjo ya #COVID19 ni hivyo, kwa hiyo kupata maambukizi ni kwa sababu tunachangama.

Dkt. Osati: Chanjo za Polio zilianza ikiwa moja kwa sasa hivi ziko nne. Chanjo ya 'Tetanus' ilianza moja sasa hivi ziko tano. Chanjo huongeza kinga zinapopungua, ndio maana kuna chanjo ya 'Booster' kwa #COVID19.

Dkt. Osati: Chanjo haifanyi kazi ya kuzuia usipate #CoronaVirus inasaidia kukukinga na homa kali itokanayo na Virusi vya Corona. Hivyo, unaweza kupata #COVID19 lakini haitakuwa kali kama mtu asiyechanjwa.

Dkt. Osati: Ukichanganya suala la chanjo na imani, siasa na sayansi hatutafika. Mambo ya imani yatatuchanganya. Nashauri tuiache sayansi ichukue nafasi yake.

Dkt. Mariam: COVID19 ni janga ambalo limeipiku magonjwa mengine kama malaria, TB na UKIMWI. Watu zaidi ya milioni 250 wameambukizwa, hali hii imeweka ulazima wa kupata chanjo kwa haraka.

Dkt. Mariam: Dkt. Mariam: Suala la 5G ni 'myth' si kweli kwamba chanjo imekuja kutengeneza 'Network'. Ni muhimu kupata chanjo kwa kuwa anayepata chanjo hata akipata kirusi hakiwezi kumdhuru kama asiyechanja.

Dkt. Baraka Nzobo: ARV na Condom zinatoka kwa wazungu lakini hatujawahi kuzishuku kuwa zinataka kutumaliza. Ndugu zetu wanatumia ARV na wanaishi vizuri tu. Hakuna anayetaka kutumaliza.

Dkt. Baraka Nzobo: ARV na Kondomu zinatoka kwa wazungu lakini hatujawahi kuvishuku kuwa vinataka kutumaliza. Ndugu zetu wanatumia ARV na wanaishi vizuri tu. Hakuna anayetaka kutumaliza.

Dkt. Baraka Nzobo: Virusi vya Corona vina uwezo wa kugandisha damu mwilini kwa 16.5%. Kwahiyo mtu anayeogopa kupata chanjo ya UVIKO-19 anajiweka kwenye hatari ya kuganda damu kwa asilimia 16.5 pindi apatapo Maambukizi ya Corona.

Dkt. Baraka Nzobo: Unapopona #COVID19 mwili unatengeneza kinga ndio lakini kinga hiyo huaribika baada ya miaezi mitatu
 
Mdau 3: Mimi nipo kwenye masuala ya Afya na kitu ambacho kilinishangaza ni upungufu wa Vifaa vya kujikinga. Kama ulininyima Vifaa nitakuamini vipi ukiniletea Chanjo. Watu tunafika sehemu tunapoteza Uaminifu kwa Viongozi. Chanjo zenyewe tulizopata kuna Nchi nyingine hawazitaki.
Hii pia mimi ilinifanya nisichanje, yani hospitalini vifaa vya kujikinga halafu kwa nini kuleta chanjo za mabilioni? Kwa nn hizo pesa msilete vifaa vya kinga?
 
CCM wametuchanganya sana, mwanzoni chanjo si madhubuti hazifai tumieni nyungu...ghafla bin vuu ooh chanjeni..tushike lipi.
 
Mchango wangu ni huu
 
Kwahiyo yanakusanywa Maoni ili baadaye waone wanawashawishi vipi watu wachanje!

Mimi sitachanja.
 
Mtu aliyeanza kututoa kwenye reli ni Magufuli rais wa awamu ya 5. Baada ya kutilia shaka hizi chanjo na kusema hataruhusu hii chanjo hapa nchini na wale wasaidizi wake kumuunga mkono ndio tatizo lilipo anzia.

Watu wa aina ya Gwajima ndio wamesambaza hofu na mashaka kwa watu na pia wataalamu wa afya nao wameshindwa kujenga hoja za kushawishi watu waende kuchanja.

Sijachanja, ila nitachanja, acha mgambo watangulie, mie mjeda ntakuja nyuma.
 
Back
Top Bottom