JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 625
- 938
KUSHIRIKI MJADALA HUU TAFADHALI GUSA LINK HII HAPA CHINI
Childhood Cancer Services and Challenges in Tanzania
Wednesday, September 29 at 6:00pm EAT with Lovelet The First, Sam Gidori, Maulid Seleman. September is Childhood Cancer Awareness Month.Welcome to a community dialogue on services provided to children with cancer in Tanzania, the challenges and opportunities.Organisers: MUHAS and MNH.
www.clubhouse.com
Mjadala huu unamulika huduma ya saratani kwa watoto pamoja na changamoto mbalimbali. Baadhi ya mambo muhimu yaliyozungumziwa na wataalamu.
Dkt. Shakilu: Saratani kwa Watoto haina tofauti kama inavyowapata Wakubwa. Mwili huzalisha Seli ambazo hukua kwa haraka kuliko kawaida na kuzalisha uvimbe
Chembechembe hai za Saratani hujenga uwezo wa kuepuka Kinga ya Mwili (zinakiuka Mabadiliko ya Vinasaba) na kusambaa Mwilini
Dkt. Shakilu: Kwa Watoto wadogo Saratani nyingi hutokea kwa bahati mbaya yaani hakuna sababu ya moja kwa moja ya kueleza kwanini Mtoto amepata Saratani
Tofauti na kwa wakubwa huwa kuna sababu ikiwemo uvutaji wa Sigara na mengineyo
Dkt. Shakilu: Maambukizi ya VVU kwa Watoto pia huwaweka baadhi ya Watoto kuwa katika hatari ya kupata Saratani
Sababu nyingine ni kuwa kwenye sehemu zenye Mazingira ya mionzi au 'heavy metals'. Lakini kwa Watoto wengi ni ngumu kufahamu sababu za moja kwa moja wao kupata Saratani
Dkt. Shakilu: Pia kuna aina fulani za Saratani huwashambuliwa Watu kutokana na asili yao ya Ngozi
Kwa takwimu za Marekani Leukemia huwashambua Watoto wengi wenye Ngozi nyeupe (Wazungu) kuliko wenye Ngozi nyeusi (asili ya Kiafrika)
Dkt. Shakilu: Kwa Nchi zinazoendelea tuna changamoto ya kuwa na Watoto wengi wanaopata Saratani kuliko Nchi zilizoendelea kutokana na kuwa tuna idadi kubwa ya Watoto na Vijana
Kwa Tanzania, Watoto wengi wanapata Saratani ya Damu, Figo, Jicho na Saratani ya matezi
Dkt. Shakilu: Kuna Saratani tunashindwa kuzigundua kutokana na uhaba wa Vifaa vilivyopo
Kugundua Saratani ya Ubongo ni lazima Mgonjwa awekwe kwenye mashine Maalum ambapo hapa kwetu inapatikana kwenye hospitali chache. Hivyo wengi hufariki kabla ya kugundulika
Dkt. Shakilu: Saratani ya Damu inafanana kwa dalili na malara kwa hiyo hutibiwa Malaria kutokana na kushindwa kupima saratani zilizopo
Kwa sababu hiyo wanapofariki huandikwa kama wamekufa kwa Malaria lakini inakuwa ni saratani iliyosababisha kifo
Dkt. Shakilu: Changamoto kubwa ya Watu kutogundulika mapema kwa Watoto ni kwasababu baadhi ya Saratani dalili zake zinafanana na Magonjwa mengine ya Watoto
Kikubwa ni sisi kuboresha huduma zetu ili tuweze kuwagundua mapema Watoto wanaoumwa
Dkt. Heronima: Bugando huduma za Saratani zilianza 2007 na kipindi hicho tulikuwa tunapokea Watoto chini ya 100. Hata hivyo wengi walikuwa wakipelekwa Muhimbili wakifuata huduma bora zaidi
Kwa sasa kila wiki tunapata Watoto 5 - 7. Saratani tunazozipata zinatofautia Kijiografia
Dkt. Heronima: Kwa Watoto Uchunguzi umejitahidi kuboreshwa ambapo walichunguza kwanini Saratani ya Lymphoma inatokea sana ambapo walibaini sababu mojawapo ni uwepo wa Malaria
Dkt. Shakilu: Kwa Saratani ambazo hazileti uvimbe ni kuangalia endapo Mtoto anapata Dalili za mara kwa mara yaani zinazojirudia au aliyetibiwa lakini hapati nafuu ni muhimu awekwe kwenye kundi la kuangaliwa kwa uwezekano wa kuwa na Saratani
Dkt. Esther: Kwa kanda ya kasikazini watoto wanaongoza kupata saratani ya damu na saratani ya matezi
Saratabi ambazo zinaongoza zinategemea sana maeneo ambayo mtu anatokea. Mwaka 2017 KCMC ilipokea watoto 200 waliokuwa na saratani
Dkt. Esther: Tuligundua asilimia 70 ya Wagonjwa ambao walikuja wakiwa na Saratani tayari walikuwa wametibiwa kwa Mitishamba au kwenda kwa Waganga
Hali hii inafanya wengi wachelewe kufika kupata Matibabu kutokana na Watanzania wengi kuwa na mazoea ya kupenda Mitishamba
Dkt. Lulu: Hapa Tanzania huduma za kuhudumia Saratani ya Watoto zimeimarika sana tofauti na hapo Nyuma
Kwa Nchi nyingi Watoto wenye Saratani hipata huduma ktk Idara ya Watoto na sio kwenye Taasisi za Saratani kama Watu wazima. Saratani hutibiwa kwa Dawa, upasuaji na mionzi
Dkt. Lulu: Saratani inaweza kutibiwa kwa namna tatu ambayo ni dawa tiba, upasuaji na mionzi
Zamani huduma ya mionzi ilikuwa Ocean Road lakini kwa sasa viko vituo vingine vinavyoanza kutoa tiba ya mionzi
Dkt. Lulu: Zamani huduma ya mionzi ilikuwa Ocean Road lakini kwa sasa vipo Vituo vingine vinavyoanza kutoa tiba ya mionzi
Kugundua Saratani unahitaji vipimo na vifaa vya hali ya juu ambapo kuna vipimo vya kuchukua kinyama au uroto. Pia unaweza kuhitaji MRI au CT-Scan
Dkt. Lulu: Kuna tatizo la uelewa na imani potofu kuhusu saratani za watoto ambalo lipo kwa ngazi ya jamii na watoa huduma za afya
Wengi wanadhani saratani ni kurogwa au saratani haziponi ambapo pia wahudumu wa afya hushindwa kugundua na kuwapa watoto rufaa mapema
Dkt. Lulu: Changamoto huwa watoto hufika kwenye matibabu wakiwa wamechelewa ambapo 80% huwa 'advanced stage'
Saratani ni suala la muda, ukichelewa inasambaa na linakuwa tatizo kubwa. Tunategemea vituo vinavyosambaza mikoani vitasaidia kuwafikisha watoto mapema
Dkt. Lulu Chirande: Hakuna Serikali inaweza kugharamia tiba ya Saratani 100%. Hata Bima za Afya haziwezi kulipia tiba
Nchi zinazoendelea tuna nafasi ya kutengeneza huduma zilizo bora. 60% ya Watoto wanasumbuliwa na Saratani ambapo asilimia nyingi wapo katika nchi zinazoendelea