Uchaguzi 2020 Yaliyojiri katika mapokezi ya Tundu Lissu leo Oktoba 19 mikoa ya Kilimanjaro na Arusha

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Mgombea wa Urais CHADEMA Tundu Lissu leo ataendelea na Kampeni zake katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini.

Arusha na Kilimanjaro ngome Kuu za CHADEMA tangu mfumo wa vyama vingi uanze wanatarajiwa kufanya mapokezi ya kufuru kwa Mgombea huyo ambaye tathmini zote zinaonyesha atapata ushindi wa zaidi ya asilimia 60%.

Jimbo la Hai anakogombea Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe ni moja ya sehemu atakazotua Tundu Lissu kumnadi Jemadari wa Siasa za Upinzani Tanzania.Ni wiki iliyopita tu Kamanda wa Polisi Hai bila aibu alimropokea Mbowe hadharani kwamba hatashinda ubunge jimboni humo.Wananchi wa Hai walisema Mungu amemuumbua OCD huyo akaropoka hadharani kilichokuwa kimepangwa nyuma ya Pazia.

Katika mkutano wa Hai CHADEMA inatarajiwa kumkaribisha Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Maalim Seif Sharrif Hamad ambaye atapanda Jukwaani kumnadi Mwenyekiti mwemzake ambao ni marafiki wakubwa katika siasa za Tanzania

Pia baada ya kutoka Hai mgombea huyo wa Urais atatua Moshi mjini Jimbo ambalo limekuwa Upinzani kwa miaka 25 sasa
----------------
Maalim atikisa Moshi
Mwenyekiti wa ACT Maalim Seif ametinga viwanja vya mashujaa Moshi kumnadi Tundu Lissu kuwa Rais wa JMT.Katika salaam zake huku akishangiliwa kwa Malaki ya watu Maalim Seif alisema Hakuna ubishi Sasa kwamba Tundu Lissu ndiye Rais skate wa Tanzania.

Picha 2 za Mwanzo ni Lissu na Sheikh Ponda wakiwa Mto wa Mbu Monduli


Lissu.jpg
IMG-20201019-WA0067.jpg
IMG-20201019-WA0068.jpg

 
Mkuu Molemo pamoja sana kamanda. yale Mafuriko ya jana pale Karatu imewafanya watu upande wa pili wakate tamaa....Asubuhi hii saa tatu Mh. Rais anayesubiri kuapishwa atazungumza na wana-Karatu mambo makuu mawili.

1. Ilani ya uchaguzi ya CDM [Uhuru, Haki na Maendeleo ya watu]
2. Elimu kwa mpiga kura na namna ya kujihami na uharamia wowote. Mwaka huu kitaeleweka
 
Mgombea wa Urais Chadema Tundu Lissu leo ataendelea na Kampeni zake katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini.

Arusha na Kilimanjaro ngome Kuu za CHADEMA tangu mfumo wa vyama vingi uanze wanatarajiwa kufanya mapokezi ya kufuru kwa Mgombea huyo ambaye tathmini zote zinaonyesha atapata ushindi wa zaidi ya asilimia 60%.

Kazi inaendelea, Haturudi nyuma..
.....Tar 28-Oct ni siku ya kumtoa nyoka aina ya ndumilakuwili pangoni kwake na kumpeleka mbuga za Burigi kule Chattle...
 
Mkuu Molemo pamoja sana kamanda. yale Mafuriko ya jana pale Karatu imewafanya watu upande wa pili wakate tamaa....Asubuhi hii saa tatu Mh. Rais anayesubiri kuapishwa atazungumza na wana-Karatu mambo makuu mawili
1. Ilani ya uchaguzi ya CDM [Uhuru, Haki na Maendeleo ya watu]
2. Elimu kwa mpiga kura na namna ya kujihami na uharamia wowote. Mwaka huu kitaeleweka
Pamoja Sana mkuu.Chombo chetu Cha habari Kiko na msafara Kama utakuwa jirani tunaweza kuonana.
 
Back
Top Bottom