Yaliyojiri katika kuaga Mwili wa Marehemu Philemon Ndesamburo

Chibudee

JF-Expert Member
Dec 28, 2016
1,775
2,397
18768382_933679843440174_7154351871948262807_o.jpg




MOSHI: Mandalizi ya shughuli ya kuuaga mwili wa Mzee Philemon Ndesamburo yamekamilika katika Viwanja vya Majengo.

- Mzee Ndesamburo ni mmoja ya waasisi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA), pia alikuwa Mbunge wa Jimbo la Moshi Mjini kwa miaka 15 na Mwenyekiti wa CHADEMA wa Mkoa wa Kilimanjaro.
18951061_1503012466429409_1816816077337261440_n.jpg
18835775_1503012386429417_3074133628454645863_n.jpg

Mwili wa marehemu Ndesamburo upo njiani kuelekea uwanja wa Majengo Moshi kwaajili ya kuuaga muda huu.
18839158_626359237556678_3083088006828469765_n.jpg
18835746_626359290890006_803799849778912692_n.jpg
nd3.jpg
nd4.jpg
nde1.jpg
nde2.jpg

Mwili wa mmoja wa wazasisi wa CHADEMA na Siasa za mageuzi Mhe.Dr. Phillemon Ndesamburo umetolewa Mochwari ulipokua umeifadhiwa na kuelekea uwanja wa Majengo ili kwenda kutoa heshima za Mwisho, wana Moshi na Mataifa mbali mbali watapata nafasi ya kutoa heshima za mwisho.

Picha kutoka kwenye msafara wa kuelekea uwanja wa Majengo kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Mhe. Dkt. Philemom Ndesamburo leo Jumatatu 5 Mei 2017.
18835746_626359290890006_803799849778912692_n.jpg
18839158_626359237556678_3083088006828469765_n.jpg

Mwili wa Mhe. Dkt. Philemon Ndesamburo ukiwasili katika uwanja wa Majengo mjini Moshi kwa kwa ajili ya kuagwa na Viongozi mbalimbali pamoja na wananchi kutoka ndani na nje ya nchi.
nds2.jpg
nds1.jpg


Baadhi ya Updates:

=> Mbowe: Tanzania ni yetu sote, Arusha ni sehemu ya Tanzania hatupaswi kubaguliwa. Siogopi kusema mimi. Watu wa Kasikazini tunabaguliwa kama sio Watanzania.

=> Mbowe: Tumeenda kukodi brass band ya Polisi wametunyima wakati huwa wanakodisha hadi kwenye Maharusi. Na mzee Ndesamburo amesaidia sana kile chuo. Tulikuwa Tayari kutoa laki tatu. Wakasema tumuulize Sirro. Nmempigia simu Waziri Mkuu akasema ataifanyia kazi lakini hadi sasa hivi hakuna kitu.

=> Mbowe: Sasa hivi watu wanaogopa kujiita Masawe.

=> Mbowe: Tuliomba kumuaga Shujaa wetu kwenye Uwanja wa Mashujaa, Wakakataa.

=> Mbowe: Tukaomba tumpitishe baadhi ya Mitaa kwa sababu sio wote wenye uwezo wa kufika hapa wakakataa.

=> Sasa hivi kila sehemu inadhibitiwa hadi bungeni

=> Mbowe: Wanafurahi, wanafikiri kufariki kwa Ndesamburo basi ndo Mwisho wa CHADEMA, wanajidanganya.

=> Mbowe: Tunawapa Pole familia na Wanachadema kwa Ujumla. Hiki kifo kimetugusa

=> Kesho saa nne asubuhi tutafanya ibada kwenye kanisa la KKKT KIboroloni, baada ya hapo tunarudi nyumbani kuupumzisha Mwili.

"Na kila wakati tulipokuwa tunapitia mazingira haya na muangalia Ndesamburo na uwezo wake najiuliza huyu mzee amekosa nini kwenye maisha yake unaangalia struggle anayoifanya Ndesamburo unawaangalia vijana wa Kitanzania wanacheza pool table, tunajiuliza kizazi chetu cha kesho kinafanya nini kuenzi kazi walizofanya wakina Ndesamburo wakina Mtei na wazee wengine wengi?
Lakini ni dhahiri kutokana na hofu za watu kwamba leo tumejenga taifa lenye hofu, watu wamekuwa waoga kwa sababu viongozi wamependa kuingiza hofu katika jamii.

Ndugu zangu waombolezaji wazungu wanamsemo unaosema "The guilty are afraid" yani watu wenye hatia wana hofu.

Kwa hiyo kukosekana kwa uwakilishi wa serikli mahali hapa sio ajali ni hofu ya hatia, kwa heshima sana dada yangu Mbunge Mmasi pole na Ahsante kwa kufika Ahsante kwa ujasiri , Tunalia wote.

Nimeona vituko sana katika msiba wa Mzee wetu Ndesamburo alafu nikajiuliza mbona huyu Mzee ni mwema?
Labda niwaambie waombolezaji muelewe kwanza tuliamini kwa tukio hili la kihistoria ni vyema tukamsindikiza Mzee wetu kwa bendi ya polisi Brass Band ya polisi."

Sasa Mbunge wa Rombo Joseph Selasini anaelezea utaratibu wa kuaga. Viongozi wa dini wanaanza kwa Sala baada ya hapo watu wanaaga. Anasema wapo hapa hadi saa kumi na mbili jioni. Anasema haturhhusu Mwili wa Marehemu kupigwa picha. wakati wa kuaga aga na kuondoka. Tunao vijana wa kutosha wa kufanya kazi ya kupiga picha
 
Last edited:
Yaani Watanzania wa leo ni tofauti na wa enzi zile yaani kwenye misiba mnaweka masuala ya siasa hebu muogopeni Muumba, hakuna atakaebaki milele hapa duniani wote tutaenda mavumbini,hebu heshimuni mazishi siasa zipo na tutaziacha hapa hapa duniani wapo wapi kima Mwl Nyerere,John Komba na wengine wengi ambao walikuwa wanaijua siasa kuliko sisi ambao tunafuata mapokeo
 
Mojawapo ya Legacy ya Mzee Ndesamburo ni kuasisi chama cha siasa CHADEMA, hivyo mi sioni sababu ya wanachadema kutomuenzi muasisi wake. Hii sio siasa ni kumuenzi huyo mzee na wafuasi wake wanayokila sababu ya kufurahia kazi ya mzee huyo lakini pia kuhuzunika kufa kwake. RIP mzee Ndesapesa
 
Wakina mama mko sensitive sana na mambo ya urembo, yaani umeweza kuona vitu ambavyo wanaume hawavioni kabisa,
We unafaa sana kutunza nyumba

Ndiyo maana nimemwambia akasafishe
 
19 Reactions
Reply
Back
Top Bottom