Yaliyojiri katika kesi ya Ugaidi inayomkabili Mbowe na Wenzake tarehe21/01/2021. Kesi imeahirishwa hadi 24/ 01/ 2022

Salaam Wakuu,

Leo tarehe 21/01/2022 kesi ya Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe inaendelea.

Ungana nami katika uzi huu ili kujua kila kinachojiri Mahakamani.

Kujua kesi ilipoishia soma: Yaliyojiri katika kesi ya Mbowe na Wenzake leo 20/01/2022. Shahidi 10 amaliza, shahidi wa 11 mwingine kuanza ushahidi kesho 21/01/2022

UPDATES


Jaji ameingia Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa Mahakamani

Wakili wa Serikali Robert Kidando Ikupendeze Mheshimiwa Jaji naitwa Robert Kidando nipo pamoja na

Pius Hilla
Abdallah Chavula
Jenitreza Kitali
Nassoro Katuga
Esther Martin
Ignasi Mwinuka
Mawakili wa Serikali Waandamizi Na
Tulimanywa Majige Wakili wa Serikali

Wakili Peter Kibatala Ikupendeze Mheshimiwa Jaji naitwa Peter Kibatala nipo Pamoja na

wakili Nashon Nkungu
John Mallya
Fredrick Kihwelo
Michael Mwangasa
Michael Lugina
Khadija Aron
Maria Mushi

- Jaji anaita washitakiwa Wote Wanne na wote wanaitika wapo Mahakamani

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya Kusikilizwa na Leo tuna shahidi Mmoja, Tupo tayari Kuendelea

Peter Kibatala: Mheshimiwa Na sisi Pia Mheshimiwa Jaji tupo tayari Kuendelea

- Jaji anaandika

- Shahidi anaingia, ni kijana mrefu mweusi


Jaji: Jina Lako

Shahidi: Naitwa H4347 Goodluck

Jaji: Umri

Shahidi: Miaka 32

Jaji: Dini yako

Shahidi: Mkristo

Jaji: kazi yako

Shahidi: Askari Polisi

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Ataongozwa na Wakili wa Serikali Pius Hilla

Wakili wa Serikali Pius Hilla: Shahidi Unaitwa Nani

Shahidi: Naitwa namba H 4347 Detective Afande Goodluck

Wakili wa Serikali: Wewe ni Polisi tangu lini

Shahidi: 2013

Wakili wa Serikali: Kituo cha Kazi ni wapi

Shahidi: Nipo Central Arusha

Wakili wa Serikali: Una Cheo gani

Shahidi: Nina Cheo Cha sergeant

Wakili wa Serikali: Ulikipata lini

Shahidi: Mwaka 2021 Mwezi wa Nane

Wakili wa Serikali: Eleza Mahakama Central Police Arusha una nafasi gani

Shahidi: Ni Mpelelezi Wa Makosa ya Jinai

Wakili wa Serikali: Ukiwa Kama Askari Polisi una Majukumu gani

Shahidi: Kukamata Wahalifu Kuhoji, Kupekua, Kukamata Vielelezo Husika, Kutekeleza Majukumu Mbalimbali ninayopewa na Wakubwa Zangu

Wakili wa Serikali: Unasema Unapeleleza Kitu gani Shahidi

Shahidi: Napeleleza Makosa Ya Jinai

Wakili wa Serikali: Eleza Mahakama Tarehe 04 August 2020 ulikuwa wapi

Shahidi: Nakumbuka Nilikuwa Kazini Kituoni Central Arusha Nikiendelea na Majukumu Yangu ya Kazi

Wakili wa Serikali: Eleza Majira Ya Jioni Kitu gani Kilitokea

Shahidi: Majira ya Jioni nilipata Maelekezo Kutoka Kwa Afande Mahita Nilikuwa nahitajika Kwa Afande RCO

Wakili wa Serikali: Ulikuwa unahitajika wewe na nani

Shahidi: Mimi na koplo Francis

Wakili wa Serikali: Afande Mahita ni nani hapo Kituoni

Shahidi: Ni Msaidizi Wa OC CID

Wakili wa Serikali: Maelekezo hayo uliyatekeleza Kwa Namna gani

Shahidi: Tuliondoka Mimi na Afande Mahita Tukaenda Kwa Afande RCO

Wakili wa Serikali: Mlienda Wapi

Shahidi: Mkoani, Makao Makuu ya Polisi

Wakili wa Serikali: Wakati huo RCO Mkoa wa Arusha alikuwa ni nani

Shahidi: Alikuwa Afande Ramadhan Kingai

Wakili wa Serikali: Malipo wasili Kwa RCO Kitu gani Kilitokea

Shahidi: Tulipo fika Kwa Afande RCO Afande alisema Kuna kazi inatakiwa Kufanywa Kwa hiyo tujiandae

Wakili wa Serikali: Maelezo Ya Kujiandaa na Kitu gani

Shahidi: Mimi na Afande Francis Tulienda Kituoni Tukachukua Silaha

Wakili wa Serikali: Wewe Ulichukua Silaha gani

Shahidi: Mimi nili chukua Silaha aina ya AK 47

Wakili wa Serikali: Na Mwenzio naye alichukua Silaha gani

Shahidi: Na Yeye alichukua AK47

Wakili wa Serikali: Baada ya Kuchukua Silaha wewe Na Mwenzio Mlielekea Wapi

Shahidi: Tulielekea Kwa Afande RCO Mkoani

Shahidi: alituelekeza Tuelekee Kituo cha Polisi USA RIVER Wilaya Ya Arumeru

Wakili wa Serikali: Unakumbuka Ilikuwa Mida ya Saa ngapi?

Shahidi: Majira ya Saa 12 Jioni

Wakili wa Serikali: Safari ya Kuelekea USA RIVER ilihusisha Watu gani?

Shahidi: Afande RCO mwenyewe, Mahita, Mimi Mwenyewe pamoja na Afande Francis

Wakili wa Serikali: Baada ya Kufika USA RIVER Kilikuwaje

Shahidi: Tulielekea Kituoni Tukamkuta OC CID pale Kituoni

Wakili wa Serikali: ambaye alikuwa ni nani

Shahidi: alikuwa Afande JUMANNE

Wakili wa Serikali: Mlimkuta Eneo gani

Shahidi: Nje ya Kituo

Wakili wa Serikali: Baada ya Hapo

Shahidi: Afande alitukaribisha Ofisini Kwake, Tukaingia Wote

Wakili wa Serikali: Mkiwa Ofisini Kitu gani Kilifanyika

Shahidi: afande RCO alituambia amepewa Jukumu la Kuandaa timu kwa ajili ya Kufanya kazi, ambayo alisema ni Kazi Maalum

Wakili wa Serikali: alisema amepewa Maelekezo na nani

Shahidi: Hakusema ameelekezwa na nani

Wakili wa Serikali: Ukiacha Jukumu la Kuandaa Kikosi Kitu gani Kingine aliwaeleza

Shahidi: Afande RCO alisema amepata Taarifa Kuwepo Kwa Kikundi Cha Ugaidi ambacho Kimejiandaa Kufanya Matukio Sehemu mbalimbali Kikundi hicho Kina Watu ambao wapo Kilimanjaro Moshi. Akatuambia Kikundi hicho Kimepanga Kudhuru Viongozi akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Hai, Ole Sabaya Kikundi hicho kupanga Kufanya Maandamano yasiyokuwa na Kikomo Pia alituelekeza kuwa Kikundi hicho kinaratibiwa na Mkuu, Mwenyekiti Wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, Freeman Mbowe

Afande Kingai alitueleza Pia Kikundi hicho pia Kilipanga Kuchoma Vituo Vya Mafuta na Kukata Miti na Magogo Kuweka Barabarani ili Kuleta Taharuki Kwa Wananchi, Nchi Kuonekana Haitawaliki

Wakili wa Serikali: Jambo Jingine

Shahidi: Afande Kingai alituambia Kwa Taarifa alizo nazo Kuna Wahalifu Wapo Moshi, Kwa hiyo tunatakiwa Kwenda Moshi Kwenda Kuzuia, Uhalifu huo Usifanyike

Wakili wa Serikali: Kuzuia Uhalifu Wa Namna gani Shahidi

Shahidi: Afande Kingai aliniambia tunatakiwa tukawakamate

Wakili wa Serikali: Kuna Kitu Kingine shahidi.?

Shahidi: Baada ya Taarifa hiyo na Kupata Malekezo Tuliondoka Pale Kituoni na Kuelekea Moshi

Wakili wa Serikali: Safari ya Kuelekea Moshi ilihusisha Wakina nani

Shahidi: Ilihusisha Afande KINGAI, Inspector Mahita, Afande Francis, Mimi na DC Azizi ambaye ni Dereva, na Jumanne

Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Baada ya akiwa Mmefika Moshi, Mambo gani Yalifanywa

Shahidi: Tulifika Moshi Tukaenda Maeneo ya Central Polisi Moshi

Wakili wa Serikali: Mambo gani Mlifanya Siku hiyo

Shahidi: Baada ya Kufika Central Moshi, Afande a Kingai alikuwa amesha fanya Mawasiliano, Tukazunguka Maeneo Mbalimbali pale Mjini kuweza Kuwakamata Wahalifu hao

Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama, Kwakuwa Lengo ni Kukamata Wahalifu, Je Kazi yenu Kwa Siku hiyo Ilikuwaje

Shahidi: Kazi yetu kwa Siku hiyo ilikuwa ni Kuwatafuta Wahalifu, Lakini hatukuwa kamata

Wakili wa Serikali: Unasema Mlizunguka Moshi Maeneo Mbalimbali, aje ieleze Mahakama mlifanya hivyo hadi Saa ngapi

Shahidi: Baada ya Kuzunguka Maeneo Mbalimbali bila ya Kuwa kamata, ilipo fika Majira ya Saa Tano Kuelekea Saa Sita Afande alisema tukapumzike tutaendelea Kesho yake

Wakili wa Serikali: Kesho yake ilikuwaje

Shahidi: Nakumbuka Afande Kingai alikuwa anaendelea Kupokea Taarifa, ilipo fika Saa 6 Kuelekea Saa 7, Afande Kingai alipokea Taarifa kuwa a watu hao wameonekana Rau Madukani

Wakili wa Serikali: Baada ya Kupokea Taarifa hiyo ilikuwaje

Shahidi: Alituambia amepewa Taarifa Wapo Rau Madukani, Na Watuhumiwa hao Mmoja amevaa Tshirt ya Taifa Stars, Mwingine Shati lenye maua ya Rangi Nyekundu, Mwingine amevaa Shati lenye Maua na Koti la Kijani.

Wakili wa Serikali: Kwa Maana Watuhumiwa Walikuwa Wangapi

Shahidi: Walikuwa watatu

Wakili wa Serikali: Baada ya Kuelezwa walivyo Vaa nini Kilifuata

Shahidi: Tulielekea Maeneo ya RAU Madukani Kwa ajili ya kuwakamata

Wakili wa Serikali: Baada ya Kufika Ikawaje

Shahidi: Tulifika Rau Madukani, Afande Kingai akatoa Maelekezo Afande Mahita ashuke Kwenye Gari aende Kuangalia Eneo ambalo Watuhumiwa Wapo

Shahidi: Afande Mahita alishuka Kwenye Gari akaenda Kufanya Surveillance

Wakili wa Serikali: Elezea Mahakama ilichujua muda gani Kufanya Jukumu hilo

Shahidi: Haikuchukua Muda Mrefu Afande Mahita alirudi na akisema ameona Watu Watatu ambao tulikuwa tunawatafuta

Wakili wa Serikali: Aliona watu watatu Wakiwa wamekaa wapi

Shahidi: Wakiwa wamekaa Kwenye Grocery

Wakili wa Serikali: Baada ya Taarifa hiyo ya Afande Mahita, Hatua gani ilichukuliwa

Shahidi: Afande Kingai alitutaka tushuke Kwenye gari, Aligawa timu Mbili, Moja aliingoza Afande Kingai Mimi na Afande Jumanne lakini Nyingine aliongoza Afande Mahita na Francis, Dereva alibaki kwenye Gari.

Wakili wa Serikali: Baada ya hapo Nini Kilifuata

Shahidi: Baada ya Afande Mahita Kurudi alisema akuna uchochoro, alipendekeza tujigawe, Mimi na Afande Kingai timu yetu ilipita Kulia, Mahita na Afande Francis wakapita Kushoto

Wakili wa Serikali: Mkaelekea Wapi Shahidi Baada ya Kugawa timu Mbili, Mlielekea Wapi

Shahidi: Kwenye Hiyo Glocery, na Kabla hatuja fika Eneo la Tukio sisi tulisikia Afande Mahita akisema "CHINI YA ULINZI"

Wakili wa Serikali: Shahidi Sasa Umesikia Sauti ya Mahita akisema Chini ya Ulinzi nini Kilifuata

Shahidi: Tulifika Eneo la Tukio, Tukamkuta Afande Mahita na Afande Francis Wameweka Watu Chini ya ulinzi, Na sisi tukajumuika

Wakili wa Serikali: Shahidi Sasa Baada ya Kufika pale kingai alichukua Jukumu gani

Shahidi: Afande Kingai alijitambulisha Kwanza, aliwauliza Watuhumiwa Majina yao,

Wakili wa Serikali: Watuhumiwa Walikutambulisha kwa Majina yapi

Shahidi: Adam Kasekwa na Mwengine kwa Mohammed Ling'wenya

Wakili wa Serikali: Baada ya Utambulisho huo, Kingai alifanya nini

Shahidi: Kingai Alimpa Maelekezo Afande Jumanne ya kuwapekua Watuhumiwa

Wakili wa Serikali: Wakati huo Wewe Ulikuwa unafanya Jukumu gani

Shahidi: La Kuimarisha Ulinzi Maana Ndiyo nilikuwa na Silaha

Wakili wa Serikali: Afande Jumanne alitekeleza Vipi Jukumu la Kuwapekua Washtakiwa

Wakili wa Serikali: wakati huo Wewe Ulikuwa unafanya Jukumu gani

Shahidi: La Kuimarisha Ulinzi Maana Ndiyo nilikuwa na Silaha

Wakili wa Serikali: Afande Jumanne alitekeleza Vipi Jukumu la Kuwapekua Washtakiwa

Shahidi: Afande Jumanne aliwaita Mashahidi

Wakili wa Serikali: aliwatoa wapi

Shahidi: Mmoja alikuwa kwenye Grocery, na Mwingine alikuwa Kwenye Banda

Wakili wa Serikali: Unakumbuka Majina yao.?

Shahidi: Mmoja anaitwa Esther na Mmoja anaitwa Anita

Wakili wa Serikali: Baada ya Mashahidi Kufika nini kilifuata

Shahidi: Afande Jumanne alijitambulisha Kwa Mtuhumiwa Wa Kwanza, baada ya Kujitambulisha alimuamuru ainuke akaanza Kumpekua

Wakili wa Serikali: Mtuhumiwa Wa Kwanza aliye Anza Kupekuliwa ni nani

Shahidi: Ni Adam Kasekwa

Wakili wa Serikali: alimpekua Kwa Namna gani

Shahidi: Alimuamuru ainuke, ageuke na akaanza Kumpapasa Kuanzia Kichwani, alipofika Kiunoni akatoa Bastola

Wakili wa Serikali: Kiunoni alitoa Bastola Upande Upi.?

Shahidi: Upande wa Kushoto

Wakili wa Serikali: Jumanne alifanya nini baada ya Kutoa Bastola

Shahidi: Baada ya Kutoa Bastola alionyesha Juu kwa Mashahidi, Akasoma Namba A5340, alisoma Jina la ile Silaha, akasema ni LUGER

Wakili wa Serikali: Kitu gani Kingine alifanya

Shahidi: Alitoa Magazine, akahesabu Risasi zilizo kuwa ndani ya magazime

Wakili wa Serikali: Alitoa Risasi ngapi

Shahidi: alizi Hesabu ni tatu

Wakili wa Serikali: Kitu gani Kingine alichofanya

Shahidi: Baada ya hapo aliendelea Kumpekua Mtuhumiwa, akatoa Karatasi ambacho Kilikuwa na Kete za Madawa Ya Kulevya 58

Wakili wa Serikali: Alitoa Wapi hicho Kikaratasi

Shahidi: Kwenye Mfuko wa Suruali

Wakili wa Serikali: Wakati unasema Kete zinazozaniwa Dawa za Kulevya

Wakili Kibatala: Shahidi kasema kete za dawa za kulevya, hajasema zinazodhaniwa

Kibatala: Shahidi kasema kete za dawa za kulevya, hajasema zinazodhaniwa

Jaji: Mie nimeandika zinazodhaniwa, labda neno kete ndiyo sijasikia

Kibatala: Kwa sababu wewe ndiyo mkuu wacha tukubali

Wakili wa Serikali: Ikawaje

Shahidi: akanipa nishike Bastola na Kete

Wakili wa Serikali: Nini Kikaendelea

Shahidi: Aliendelea Kumpekua Mtuhumiwa, akamkuta na simu

Wakili wa Serikali: Simu ilikuwa wapi

Shahidi: Kwenye Mfuko wa Suruali Wa Adam Kasekwa

Wakili wa Serikali: Unakumbuka Ilikuwa ni simu gani

Shahidi: Ilikuwa ni Simu Ndogo aina ya Itel

Wakili wa Serikali: Kafanya nini

Shahidi: Alitoa Betri akatoa Line akasoma IMEI namba ya Ile simu, pia alisoma namba za Zile line

Wakili wa Serikali: Baada ya Kusoma zile namba alifanya nini

Shahidi: Alimuamuru Mtuhumiwa akae Chini

Wakili wa Serikali: Aliweka Wapi hiyo Simu

Shahidi: alinipa Nishike

Wakili wa Serikali: Vitu Ulipokuwa navyo Wewe, Nini Kilifanyika

Shahidi: Afande Jumanne aliniambia niende Kwenye Gari Kuchukua Bahasha Ya Kuweka Vitu hivyo, Kwa sababu Gari alikuwa imeshasogea eneo la Tukio Nikaenda Kuchukua

Wakili Wa Serikali: ulienda Umbali gani Kutoka eneo la Tukio

Shahidi: Gari ilikuwa imesogea Karibu na Eneo la Tukio, Mashahidi Is alikuwa wananiona na Watuhumiwa Walikuwa wananiona, Ni kachukua Hiyo Bahasha afande Jumanne

Wakili wa Serikali: Baada ya Kumkabidhi hiyo Bahasha afande Jumanne alifanya nini

Shahidi: Baada ya kumkabidhi hiyo Bahasha afande Jumanne alitoa Karatasi akaanza Kujaza Kwenye Zile Karatasi Vile Vielelezo

Wakili wa Serikali: Karatasi zipi

Shahidi: Za Kukamatia mali

Wakili wa Serikali: Unakumbuka zilikuwa ni Hati ngapi

Shahidi: Zilikuwa Mbili

Wakili wa Serikali: Kwanini Unasema Mbili

Shahidi: Hati ya Kwanza alijaza Silaha pamoja na zile simu na Hati Nyingine alijaza Madawa yanayo zaniwa ya Kulevya

Wakili wa Serikali: Alipokamililisha Kujaza Vielelezo alifanya nini

Shahidi: Alimsimamisha Mtuhumiwa Wa Pili

Wakili wa Serikali: Na baada ya Kujaza hizo Hati alifanyeje

Shahidi: alisaini Afande Jumanne, Mashahidi pamoja na Mtuhumiwa

Wakili wa Serikali: Kilichofuata Kilikuwa ni nini

Shahidi: Alimuamuru Mtuhumiwa akae Chini, akamuamuru Mtuhumiwa Wa pili asimame

Wakili wa Serikali: Mtuhumiwa Wa Pili ni nani

Shahidi: Mtuhumiwa wapili ni Mohammed Ling'wenya

Shahidi: Alimuamuru ainuke, ageuke, akaanza Kumpapasa kuanzia Kichwani, akatoa Kete zinazozaniwa ni Madawa ya Kulevya

Wakili wa Serikali: Zilikuwa kwenye nini

Shahidi: Kwenye Mfuko wa Suruali

Wakili wa Serikali: Na Kete zilikuwa kwenye Nini

Shahidi: Kimfuko kama Vile Vya Karanga, Baada ya kuhesabu Vilikuwa 25

Wakili wa Serikali: Baada ya Kukamilisha alifanya nini

Shahidi: alivihesabu Mbele ya Mashahidi, Baada ya Hapo alinipa Nivishike

Wakili wa Serikali: aliendelea Kufanya kitu gani

Shahidi: Aliendelea Kumpekua Mtuhumiwa alimkuta na Simu Moja aina ya Tecno

Wakili wa Serikali: Ilipatikama wapi hiyo simu

Shahidi: ilikuwa Mfukoni

Wakili wa Serikali: Baada ya Kuitoa alifanya nini..?

Shahidi: Alianza Kusoma IMEI namba na Baada ya hapo alijaza Hati ya Ukamataji

Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama, Unasema alijaza Je alijaza Kitu Gani

Shahidi: Alijaza Hati ya +Kukamatia Mali, Certificate of Seizure

Wakili wa Serikali: Alijaza Hati ngapi

Shahidi: Alijaza Hati Mbili, Ya Kwanza Ya Madawa ya kulevya na Hati Ya Pili alijaza Simu

Wakili wa Serikali: Baada ya Kukamilisha Vielelezo, Jumanne alifanya nini

Shahidi: Jumanne alisaini, Mashahidi walisaini Pamoja na Mtuhumiwa alisaini

Wakili wa Serikali: Nani alikabidhiwa Vielelezo Vilivyokamatwa

Shahidi: Afande Jumanne Baada ya Kukamilisha Kujaza Vielelezo, aliweka Kwenye Bahasha akanikabidhi Mimi

Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama sasa Kwamba Upekuzi na Ujazaji wa Zile Hati zimekamilika nini Kilifuata

Shahidi: Afande Kingai alitoa Maelekezo Twende kwenye Gari Pamoja na Watuhumiwa

Wakili wa Serikali: Wakati huo Gari Ilikuwa wapi

Shahidi: Gari ilikuwa aimepaki Pembeni ya Barabara ambapo ni Karibu na Eneo la Tukio

Wakili wa Serikali: Baada ya Kufika Kwenye Gari Kitu gani Kilifanyika

Shahidi: Baada ya Kufika kwenye Gari Afande Jumanne alini kabidhi Hati ya Makabidhiano ambayo aliandaa Yeye Afande Jumanne

Wakili wa Serikali: Hati ya Makabidhiano ilikuwa inahusiana na Vielelezo Vipi

Shahidi: alinikabidhi Hati ya Silaha Pamoja na Simu, Hati za Madawa alibaki nazo

Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Kwamba Hati Mliyokabidhiana Silaha na Jumanne Utaitambuaje

Shahidi: Ina Jina Langu, Ina Namba yangu H4347 ina Jina la Afande Jumanne, Ina Vielelezo ambavyo Nimekabidhiwa

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Shahidi anaonyesha Uwezo Wa Kutambua, Naomba Kielelezo namba P12

Wakili wa Serikali: Angalia Nyaraka hiyo, Ni nini

Shahidi: Hati ya Makabidhiano ambayo Afande Jumanne alinikabidhi

Wakili wa Serikali: kuna Vitu Gani

Shahidi: Kuna Majina yangu, namba yangu, Tarehe Niliyokabidhiwa na Vielelezo Nilivyo kabidhiwa

Wakili wa Serikali: Hati hiyo ni ya Tarehe ngapi

Shahidi: 05 August 2020

Wakili wa Serikali: anaye kabidhi ni nani na anayekabidhiwa ni nani

Shahidi: anaye kabidhi ni Afande Jumanne na ninaye Kabidhiwa ni Mimi Goodluck

Wakili wa Serikali: Unamkabidhiwa Vitu gani

Shahidi: Pistol namba A5340 aina ya Luger, pamoja na Risasi 3 ndani ya Magazine

Wakili wa Serikali: Makabidhiano hayo Yalifanyika Wapi

Shahidi: Tulifanya Ndani ya Gari Baada Ya Kuni kabidhi Zile Documents

Wakili wa Serikali: Kwa Mujibu wa Hati hivi Vitu Vimekamatiwa Wapi

Shahidi: Kwa Mujibu wa Hati Vitu Vimekamatiwa RAU Madukani Moshi

Wakili wa Serikali: kutoka Kwa nani

Shahidi: Kwa Adam Kasekwa

Wakili wa Serikali: kuna Kumbukumbu namba hapo, inasomekaje

Shahidi: CD/IR /2097 /2020

Wakili wa Serikali: Naomba Kurudisha Kielelezo Mheshimiwa Jaji

Wakili wa Serikali: Baada ya Zoezi la Makabidhiano, ni Kitu gani Kilichofuatia

Shahidi: Tulielekea +Kituo Cha Polisi Moshi

Wakili wa Serikali: Wakina nani Mliolekea Kituo cha Polisi Moshi

Shahidi: Afande Kingai, Jumanne, Mahita, Francis, Dereva na Mimi pamoja Watuhumiwa Wawili

Wakili wa Serikali: Watuhumiwa Wawili akina nani

Shahidi: Adam Kasekwa na Mohamed Ling'wenya

Wakili wa Serikali: Kwenye Gari Mnasema alikuwa Wewe Kingai, Mahita na Jumanne Mlikuwa Kwenye gari ipi

Shahidi: Gari ya RCO

Wakili wa Serikali: Coplo Francis alipanda Gari ipi Shahidi Kwenye Gari Nyingine ambayo alipanda yeye na Mashahidi,

Wakili wa Serikali: Mashahidi Gani

Shahidi: Ni Anita Pamoja na Esther

Wakili wa Serikali: Ifahamishe Mahakama Mlivyofika Kituo cha Polisi Central Moshi, Mambo gani Yalifanyika

Shahidi: Tulipofika Kituoni Afande Kingai aliwauliza Kwa Taarifa Tulizo nazo Mlikuwa Watatu, Mmoja Yupo wapi Kwa hiyo Tulipofika Kituoni Afande Jumanne na Mahita Walishuka kwenye Gari Mimi, Afande Kingai, na Dereva Hatukushuka Kwenye Gari Pamoja na Watuhumiwa

Wakili wa Serikali: Ni kwanini Hamkushuka Kwenye Gari?

Shahidi: Ni Kwa sababu Afande Kingai alisema tunatakiwa turudi Kumtafuta yule Mtuhumiwa Mmoja, ambaye ni Mtuhumiwa Wa tatu

Wakili wa Serikali: Ilichukua muda gani

Shahidi: Baada ya Muda Afande Mahita na Jumanne Walirejea Kwenye Gari, Waliporejea ndiyo tuliondoka Kituoni

Wakili wa Serikali: Mliondoka Kuelekea Wapi

Shahidi: Kuekea Sehemu tuliyokamata Watuhumiwa, Ambapo Watuhumiwa Walisema Kuwa Yule Mwenzao alibaki pale

Wakili wa Serikali: Kwa hiyo Dhumuni la Kurudi kule lilikuwa ni nini

Shahidi: Ni Kumkamata Mtuhumiwa Wa tatu ambaye alikuwa pamoja na Watuhumiwa

Wakili wa Serikali: Nini Matokeo ya kazi yenu

Shahidi: Baada ya Kufika Eneo la tukio hatukumpata, Afande Kingai akawauliza tutampataje, Wakatuonyesha Maeneo ambayo tungempata Mtuhumiwa wa tatu ambaye Walikuwa naye

Wakili wa Serikali: Baada ya Kuelezwa hivyo Mlichukua Hatua gani

Shahidi: Tulikuwa tunazunguka Maeneo ambayo Watuhumiwa walikuwa wanatupitisha ili Kumkamata Mtuhumiwa Wa tatu

Wakili wa Serikali: Ufutailiaji Wa Mtuhumiwa Wa Tatu, Umesema Walimtaja Kwa Jina gani

Shahidi: Walimtaja Kwa Jina la Kakobe

Wakili wa Serikali: Ilikuwaje Ufutailiaji wake

Shahidi: Ufutiliaji Wa Siku hiyo hatukumkamata Mtuhumiwa

Wakili wa Serikali: Baada ya KumKosa Mtuhumiwa, Ilikuwaje

Shahidi: Afande Kingai alielekeza Tuwarudishe Watuhumiwa Kituoni

Wakili wa Serikali: Utejelezaji huo huo huo Ulifanyikaje

Shahidi: Tulienda Kituoni Watuhumiwa Walifikishwa Charge Room ambapo Mahita na Afande Jumanne ndiyo Walishuka

Wakili wa Serikali: Baada ya Kuwa weka Mahabusu Ilikuwaje

Shahidi: Tulirudi na Kuendelea na ufutiliaji

Wakili wa Serikali: Ikawaje

Shahidi: Tulifika Hotelini ambapo Mimi na Afande Kingai Tulishuka na Mahita na Jumanne Walibaki Kwenye Gari

Wakili wa Serikali: Sasa Siku iliyofuata Tarehe 06 August 2020 Nini Kilifuata

Shahidi: Ilikuwa Majira ya Saa 11 Asubuhi, Tulifika Kituoni Central Pale Moshi, Tuliwa chukua Watuhumiwa

Wakili wa Serikali: Kwa Madhumuni gani

Shahidi: Kwa Madhumuni Ya Kwenda Kumtafuta Mtuhumiwa Wa tatu

Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Matokeo Ya Utafutajinwa Mtuhumiwa Wa tatu Ilikuwaje pale moshi

Shahidi: Matokeo Ya Kumtafuta Mtuhumiwa Wa tatu, Hatukufanikiwa Kumpata

Wakili wa Serikali: Mlifanya Utafutaji Maeneo Gani

Shahidi: Tulienda Moshi Mjini, Aishi, Boma. Ng'ombe, na Baadae Sakina Arusha

Wakili wa Serikali: Ufutailiaji Wenu wa Tarehe Sita Mlifanya hivyo Hadi Saa ngapi

Shahidi: Tulifanya Ufutailiaji Mpaka Saa 12 Jioni, Baada ya Kutoka Arusha Tulirudi Moshi Mjini

Wakili wa Serikali: Ni Kitu gani Kilitokea Hiyo Majira ya Saa 12 Jioni

Shahidi: Tulirudi Moshi Pale Polisi Central, Afande Kingai alikuwa anafanya Mawasiliano, Baada ya Hapo Afande Kingai alirudi Kwenye Gari akasema Watuhumiwa Wanatakiwa Kupelekwa Dar es Salaam

Wakili wa Serikali: Baada ya Maelekezo hayo Ikawaje

Shahidi: Mimi, Afande Kingai, Mahita na Afande Jumanne tulianza Safari ya Kuelekea Dar es Salaam

Wakili wa Serikali: Ifahamishe Mahakama Mlifika lini

Shahidi: Baada ya Kufika Central Moshi, Tulifika pale Njia panda Himo, Gari iliharibika, na Afande a Kingai akafanya Mawasiliano ilikupata Gari Nyingine Kuelekea Dar es Salaam

Wakili wa Serikali: Hapo Njia panda Himo Kitu gani Kingine Mlifanya

Shahidi: Tukiwa tunasubiria Gari Nyingine Kutoka Moshi, Afande Kingai alikuja na Chakula Ndizo Nyama ambapo tulikula Pamoja na Watuhumiwa

Wakili wa Serikali: Gari ilitoka wapi

Shahidi: Ilitoka Moshi, Gari ya Afande RPC

Wakili wa Serikali: ieleze Mahakama Kwamba Mlifika lini Dar es Salaam

Shahidi: Baada ya Gari ya RPC Kufika tulianza Safari ambapo tulifika Tarehe 07 August 2020

Wakili wa Serikali: Ilikuwa Majira ya Saa ngapi

Shahidi: Ilikuwa Majira ya Alfajiri ya Saa 11

Wakili wa Serikali: Mlifika Wapi

Shahidi: Tulifika Dar es Salaam Central police, Baada ya Kufika Walikabidhiwa Charge Room

Wakili wa Serikali: Washtakiwa Walikabidhiwa Wapi

Shahidi: Charge Room ya Central Dar es Salaam

Wakili wa Serikali: Shahidi Sasa Mmewakabidhi Watuhumiwa Charge Room, Je Ni Shughuli zipi zingine Mlifanya Siku hiyo

Shahidi: Afande Kingai alitoa Break, Kwenda Akunawa Uso, Tulienda Kunawa Uso Baadae Saa 1 Asubuhi Tulirudi Kituoni

Wakili wa Serikali: Baada ya Saa 1 Kurudi Mlipewa Maelezo gani

Shahidi: Afande Kingai aliniambia Nikabidhi Vielelezo Kwa Afisa Vielelezo Pale Central

Wakili wa Serikali: Ukitekeleza Vipi

Shahidi: Nilienda Kwa Mtunza Vielelezo, Nikamkabidhi Silaha

Wakili wa Serikali: Ulimkabidhi Silaha ipi

Shahidi: Nilimkabidhi Silaha iliyokamatwa kwa Mtuhumiwa Adam Kasekwa Bastola A5340 aina ya Luger Pamoja na Risasi 3

Jaji: Rudia namba ya silaha iliyokabidhi

Shahidi: Ni A5340

Wakili wa Serikali: ambayo Ulimkabidhi Nani

Shahidi: Nilimkabidhi Staff sergeant Nuru

Wakili wa Serikali: Shahidi Silaha ilikamatwa Tarehe 05 August 2020, Ukaikabidhi Tarehe 08 August 2020, amuda wote Silaha ilikuwa Kwa nani

Shahidi: Muda wote Silaha nilikuwa nayo Mimi

Wakili wa Serikali: Shahidi Baada ya kuwa Umemkabidhi Silaha, Ni Jukumu lipi lingine ulitekeleza

Shahidi: Nilikabidhi Simu

Wakili wa Serikali: Simu Ulimkabidhi Nani

Shahidi: Afande Swila

Wakili wa Serikali: Huyu Swila ni nani

Shahidi: Ni Askari Wa Hapa Dar es Salaam

Wakili wa Serikali: Ulimkabidhi Simu zipi

Shahidi: Simu zilizokamatwa Kwa Watuhumiwa Kule Moshi ambazo ni Itel na Techno pamoja na Line

Wakili wa Serikali: Baada Ya Kukamilisha Jukumu la Kukabidhi Vielelezo, Nini Kilifuata

Shahidi: Afande Kingai alisema tuendelee na Ufutailiaji Wa Taarifa, akatuambia yeye Pamoja na Afande Jumanne Watabaki

Wakili wa Serikali: Kwenye Makabidhiano ya Silaha, Risasi pamoja na Magazine, Mlikabidhiana Vipi

Shahidi: Nilisaini Hati ya Makabidhiano na yeye akasaini

Wakili wa Serikali: Ilikuwa Tarehe Ngapi

Shahidi: Tarehe 07 August 2020

Wakili wa Serikali: Hati Uliyotumia Kukabidhi Silaha, Ukiona Utaitambuaje

Shahidi: Nitaitambua Sabanu Ina Jina Langu, Force Namba yangu, Vielelezo Vyenyewe, pia Ina Jina la Mtu ambaye anakabidhiwa

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Shahidi anaomyesha Uwezo Wa Kutambua, Kwa ridhaa ya Mahakama naomba Nimuonyeshe

Wakili wa Serikali: Hiyo ni nini

Shahidi: Ni Hati ya Makabidhiano

Wakili wa Serikali: Ina Vitu Gani vinavyothibitisha Uhusiano Wako na Hiyo Nyaraka

Shahidi: Ina Jina Langu, Goodluck, Force Namba Yangu H 4347, Ina Vielelezo, Jina la sergeant Nuru

Wakili wa Serikali: Nani aliye andika

Shahidi: Mimi Mwenyewe

Wakili wa Serikali: Unaiomba nini Mahakama

Shahidi: Naiomba Mahakama Ipokee Kama Ushahidi Wangu Hati inapelekwa kwa Jopo la mawakili wa utetezi na wanaipitia.

Wakili Nashon Nkungu: Mheshimiwa Jaji sisi akwa niaba Ya Mshtakiwa Wa Kwanza Hatuna OBJECTION

Wakili John Mallya: Mheshimiwa Jaji Sisi kwa niaba ya Mshtakiwa Wa Pili hatuna Pingamizi

Wakili Fredrick Kihwelo: Mheshimiwa Jaji Kwa Niaba ya Mshtakiwa wa tatu Sina Pingamizi

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Kwa niaba ya Mshitakiwa wa Nne pia Hatuna Pingamizi

- Sasa Hati inachukuliwa Kutoka Upande Wa Mawakili Wa Utetezi Kwenda Katika Meza ya Jaji Jaji anapokea kutoka Kwa Karani wa Mahakama anasoma na Kuanza Kuandika Kidogo

Jaji: tuliishia Kielelezo Namba, 35..! Basi Naipokea Na Itakuwa Kielelezo namba 36

- Mawakili wa pande zote mbili wanakubaliana na Uamuzi Jaji kwa Kusimama na Kumuinamia Kidogo

- Hati Inapelekwa kwa Shahidi Goodluck Minja, anatakiwa asome Yote Kwa Sauti kama ambavyo Sheria ya Ushahidi Inavyotaka


Wakili JOHN MALLYA: Mheshimiwa Jaji Naomba Shahidi asome Kama Ilivyo andikwa Kuna Vitu anaviruka.. Shahidi anaanza kusoma upya

Wakili John Mallya: Mheshimiwa Jaji Bado shahidi ana skip (anaruka) Baadhi ya Maeneo Shahidi anasoma upya

- Shahidi anamaliza, kusoma karatasi ya Kurasa Moja, Hati ya Makabidhiano..

Wakili wa Serikali: Shahidi Hati hiyo ni ya Tarehe Ngapi

Shahidi: Tarehe 07 August 2020

Wakili wa Serikali: anayekabidhi ni nani

Shahidi: NI Mimi H 4347 DC Goodluck anayekabidhiwa ni D 7853 staff Sarjent Nuru

Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Staff Sargent Nuru anakabidhiwa Kitu gani

Shahidi: Anakabidhiwa Silaha aina ya Pistol A5340, Magazine na Risasi Tatu

Wakili wa Serikali: Kwa Mujibu wa Hati hiyo Vitu hivyo Vimekamatiwa wapi

Shahidi: Rau Madukani, Moshi

Wakili wa Serikali: Vili kamatwa Lini

Shahidi: Tarehe 05 August 2020

Wakili wa Serikali: Kumbukumbu namba zipi Shahidi CD/IR/2097/2020

Wakili wa Serikali: Hiyo Kumbukumbu namba Uliandika Kwa Madhumuni yapi

Shahidi: Ndiyo namba ya kesi

Wakili wa Serikali: Kwa Mujibu wa fomu yako Hapa Kuna Maeneo Umeweka Deshi, Ujajaza... Kutoka Kwa Mtuhumiwa Deshi, anaye tuhumiwa kwa Makosa ya Deshi

Shahidi: Kwa sababu Kumbukumbu namba ya CD/IR /2097 /2020 ina Jina la Mtu aliyekamatwa nayo na Kosa lililo husika

Wakili wa Serikali: ieleze Mahakama Kwamba Bastola hii ambayo Ulimkabidhi Kwa Sargent Nuru Ukiiona Leo hii Unaweza Kuitambua Kwa namna ipi

Shahidi: Naweza Kuitambua Kwa Sababu ina Serial number ambayo Ipo Kwenye mwili wa Silaha na Jina

Wakili wa Serikali: Ni namba Ngapi

Shahidi: A5340

Wakili wa Serikali: Hilo Jina Lipo sehemu gani

Shahidi: Jina Lipo Upande Wa Kushoto, namba zipo Upande wa Kulia Kwenye mwili Wa Bunduki

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Shahidi anaonyesha Uwezo Wa Kutambua Kielelezo, Naomba Kielelezo namba P 3

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba Kumuonyesha Shahidi Kielelezo

Shahidi: Anakabidhiwa Mfuko wa nailoni Inayoonyesha Ndani (Transparent)

Shahidi: Hii ni Silaha aina ya Pistol, Niliyo Mkabidhi sergeant Nuru, Niliyokamata Kwa Mtuhumiwa Adam Kasekwa

Wakili wa Serikali: Ilikatwa Kwa Mtuhumiwa Wapi na Lini

Shahidi: Tarehe 05 August 2020, Rau Madukani

Wakili wa Serikali: Kitu gani Kina thibitisha Kwamba Ndiyo hiyo

Shahidi: aina Serial number A5340 ipo Upande wa Kulia na Jina la Luger

Wakili wa Serikali: Shahidi Ieleze Mahakama, Mnamo tarehe 08 August 2020 Unakumbuka nini

Shahidi: Tarehe 08 August 2020 Tulikuwa tunaendelea na Ufutailiaji Wa Watuhumiwa Wengine ambao wapo Hapa Dar es Salaam

Afande alitoa Maelekezo kuwa Watuhumiwa Wahamishwe Kutoka Central Dar es Salaam kwenda Kituo cha Polisi Mbweni

Wakili wa Serikali: Nani alitoa Maelekezo

Shahidi: aliniambia Afande Mahita kaambiwa na Afande Kingai

Wakili wa Serikali: Kituo Cha Polisi Mbweni kipo wapi

Shahidi: Kipo Dar es Salaam

Wakili wa Serikali: Ilikuwa ni Majira Ya Saa ngapi

Shahidi: Ilikuwa ni Majira Ya Sa 5 Asubuhi

Wakili wa Serikali: Mliwahamisha Watuhumiwa Wakina nani

Shahidi: Tuliotoka nao Moshi Walikuwa ni Adam Kasekwa na Mohamed Ling'wenya

Wakili wa Serikali: Mlioshiriki zoezi la Kuwatoa Central Kuwapeleka Mbweni Ni akina nani

Shahidi: Afande Jumanne, Mahita, Swila Pamoja na Mimi na Dereva

Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Baada ya Kufika Mbweni akitu gani Kilifanyika

Shahidi: Baada ya Kufika. Mbweni Waliingia Charge Room Mimi nikabaki nJe

Wakili wa Serikali: Unaposema Charge Room unamaanisha nini

Shahidi: Ni Chumba cha Mashitaka, Ambapo sehemu ya Kusikiliza Kesi na Malalamiko ya Wananchi

Wakili wa Serikali: Baada ya Kukabidhi Mlielekea Wapi

Shahidi: Baada ya Washitakiwa Kukabidhiwa Tuliondoka kituoni

Wakili wa Serikali: Mlienda Wapi

Shahidi: Kwenda Kutafuta Taarifa za Watuhumiwa mbalimbali

Wakili wa Serikali: Tarehe 09 August 2020 Siku hiyo ulikuwa wapi

Shahidi: Tulikuwa a Maeneo Mbalimbali hapa Dar es Salaam tukiwa tunafutailia wahalifu wengine

Wakili wa Serikali: Majira ya Jioni ulikuwa wapi

Shahidi: Nilikuwa Maeneo ya Temeke

Wakili wa Serikali: Ikawaje

Shahidi: Nilifanikiwa Kumkamata Mtuhumiwa Mwingine ambaye Nilikuja Kufahamu anaitwa Khalfani Bwire

Wakili wa Serikali: Bwire alikatiwa Eneo gani

Shahidi: Maeneo ya Kituo cha Polisi Chang'ombe

Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Mazingira ya Ukamataji Wa Bwire Yalikuwaje

Shahidi: Alikuwa katika Gari ya Abiria, Kwa hiyo ile Gari ya Abiria ilielekezwa Kuingia Kituoni

Wakili wa Serikali: Gari ya Abiria ya aina gani

Shahidi: Daladala,

Wakili wa Serikali: Ikawaje

Shahidi: IKaingia Kituo cha Polisi Chang'ombe

Wakili wa Serikali: Baada ya Kukamatwa?

Shahidi: Aliingizwa Mahabusu

Wakili wa Serikali: Kabla ya Kumuingiza mahabusu

Shahidi: Afande Kingai alimpekua

Wakili wa Serikali: alimpekua Sehemu gani

Wakili wa Serikali: katika Maungo yake

Wakili wa Serikali: Alikutana na Nini

Shahidi: Kwenye Upekuzi alikuwa na Simu Mbili

Wakili wa Serikali: Simu gani Kama Unakumbuka

Shahidi: Simu aina ya Bundy na Simu aina ya Techno

Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama hivi Vitu vilipayikana Sehemu gani

Shahidi: Vilipatikana Mfukoni

Wakili wa Serikali: Baada ya Upekuzi Ikawaje

Shahidi: Mtuhumiwa Aliingizwa Mahabusu Kituo cha Polisi Chang'ombe

Wakili wa Serikali: Wewe Ulieleka wapi

Shahidi: Tuliendelea na Ufutailiaji Wa Taarifa Nyingine zilizo kuwa zimetolewa

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Naona no Saa Saba Kasoro, Naomba Hairisho tupate Health Break kwa DAKIKA 45 baada ya hapo tuendelee

Kibatala: Mheshimiwa hatujui kabakisha kiasi gani, Kama ni Dakika 20 tuvumilie kama ni zaidi ya hapo tuhairishe

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji bado nina muda zaidi nitaomba hairisho tu

Wakili Peter Kibatala: Kwa kesi hiyo hatuna pingamizi

Jaji: Basi nahairisha mpaka saa 1:45


========

- Jaji ameingia Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa Mahakamani tena

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Quorum yetu ipo Vile Vile kama awali tupo tayari Kuendelea

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Nasisi pia tupo tayari Kuendelea, Quorum yetu ipo Kama Mwanzo

Jaji :Shahidi nakukumbusha Ulikuwa unaendelea Kutoa Ushahidi wako, Ulikuwa Chini ya Kiapo na Utaendelea Kuwa Chini ya Kiapo

Wakili wa Serikali: zile simu alizokuwa nazo Bwire zilienda wapi

Shahidi: Afande Kingai alinikabidhi mimi

Wakili wa Serikali: Ukazipeleka Wapi

Shahidi: Nilipewa Maelezo Ya Kumkabidhi Afande Swila

Wakili Wa Serikali: Ni Lini na Ni wapi

Shahidi: Baada ya Kurudi Polisi Central Dar es Salaam, Nilimkabidhi Afande Swila

Wakili wa Serikali: Tarehe 10 August 2020 Siku hiyo ulikuwa wapi

Shahidi: Nilikuwa bado naendelea na Zoezi la Ufutailiaji, Siku hiyo Afande Kingai alitoa Maelekezo ya Kwenda Kumpekua Bwire Nyumbani Kwake, Maeneo ya Yombo Kilakala

Wakili wa Serikali: Yombo Kila Kala Ipo wapi

Shahidi: Ipo Maeneo ya Temeke

Wakili wa Serikali: Kwenye huo Upekuzi Vilipatikana Vitu gani

Shahidi: Vitu Vingi zikiwemo Sare za Jeshi la Wananchi

Wakili wa Serikali: Mbali na Nguo za Jeshi la Wananchi la Wananchi, Nini Kingine

Shahidi: Kidaftari cha 5star na Kisu cha JWTZ

Wakili wa Serikali: Baada ya Upekuzi Mlielekea Wapi

Shahidi: Tulielekea Kituo Cha Polisi Chang'ombe

Wakili wa Serikali: Tarehe 13 August 2020 Ulikuwa wapi

Shahidi: Nilikabidhi wa Simu Kwa ajili ya Kwemda Kuzi kabidhi Makao Makuu Ndogo ya Polisi, Maabara Ya Uchunguzi

Wakili wa Serikali: Alikukabidhi nani

Shahidi: Alini kabidhi Afande Swila

Wakili wa Serikali: Ulipewa simu Ngapi

Shahidi: Nilipewa Simu nane

Wakili wa Serikali: Mbali na Simu ulipewa nini

Shahidi: Na Barua

Wakili wa Serikali: Vielelezo hivyo ulitakiwa Kupeleka Wapi

Shahidi: Makao Makuu Madogo ya Jeshi la Polisi, Kitengo Cha Cyber ambapo Afande Ndowa ndiyo alinipokea

Shahidi: Nilimkabidhi Afande Ndowo

Wakili wa Serikali: Tarehe 25 November 2020 ulikuwa wapi

Shahidi: Nilikuwa bado naendelea Kufuatilia Kuhusu Wahalifu Tuliokuwa tunawatafuta

Wakili wa Serikali: Ulikuwa wapi

Shahidi: Nilielekezwa kwenda Kuchukua Silaha

Wakili wa Serikali: Silaha Ipi.?

Shahidi: Kielelezo ambacho kilikamatwa Moshi Maeneo ya RAU, Moshi

Wakili wa Serikali: Baada ya Maelekezo hayo

Shahidi: Nilienda Kwa Sgt. Nuru, Nilichukia Silaha Nikaenda Makao Makuu Ndogo Ya Polisi Kwa Uchunguzi

Wakili wa Serikali: Silaha aina gani ulilkadhiwa

Shahidi: Silaha aina ya Pistol A5340 aina Ya Luger ambayo ilikuwa na Magazine na Risasi 3

Wakili wa Serikali: Huyu Nuru Alikukabidhi Kwa namma gani

Shahidi: Tulisainishana Hati ya Makabidhiano

Wakili wa Serikali: Hati ya Makabidhiano uliona Leo Utaweza Kuitambuaje

Shahidi: Naweza Kuitambua Kwa Kuona Jina langu, Force Namba yangu, aina ya Silaha na Jina la aliye Nikabidhi

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Shahidi ameonyesha Uwezo wa Kuitambua

Wakili wa Serikali: Shahidi Ieleze Mahakama Nyaraka Uliyo nayo ni Kitu gani

Shahidi: Ni Hati ya Makabidhiano

Wakili wa Serikali: Ina Kitu gani Kinacho weza Kuthibitisha Kuwa Unaifahamu

Shahidi: Ina namba la Silaha, Pistol namba A5340

Wakili wa Serikali: Kitu gani Kingine

Shahidi: Kuna Risasi Tatu Ndani ya Magazime

Wakili wa Serikali: Kitu gani Kingine

Shahidi: Ina Sahihi yangu, H 4347 DC Goodluck

Wakili wa Serikali: Kigezo Kingine

Shahidi: Ina Jina la aliyenikabidhi

Wakili wa Serikali: Unaiomba nini Mahakama Kuhusiana na Nyaraka hiyo

Shahidi: Naiomba Mahakama Ipokee Kama Ushahidi

-Nyaraka inaenda Kwenye Benchi la Mawakili Wa Utetezi Mawakili wa washtakiwa wote hawana Pingamizi.. Nyaraka Inapelekwa Kwenye Meza ya Jaji Kupitia Karani wa Mahakama Jaji Napokea kama Kielelezo Namba 37

Mawakili wa pande zote mbili wanakubaliana na Uamuzi Jaji kwa Kusimama na Kumuinamia Kidogo


Wakili wa Serikali: Shahidi Soma Nyaraka Kwa Sauti Shahidi SHAHIDI anasoma kielelezo namba 37 kama ambavyo Sheria ya Ushahidi inataka, pale ambapo Kielelezo Cha Nyaraka Kinapo pokelewa Kisomwe Chote na Shahidi anayekitoa..

Mallya: Mheshimiwa Jaji ameongeza Kitu ambacho hakijatajwa hapo, shahidi wa Jamhuri anasoma upya.

Wakili wa Serikali: Hati hiyo ni ya Tarehe Ngapi

Shahidi: Tarehe 25 November 2020

Wakili wa Serikali: anaye kabidhi nani na anakabidhiwa Nani

Shahidi: Anakabidhiwa DC Goodluck na anayekabidhi ni sgt. Nuru

Wakili wa Serikali: Kwa Mujibu wa Hati hiyo Silaha hiyo ilikamatwa lini na wapi

Shahidi: Ilikamatwa Tarehe 05 August 2020 Rau Madukani

Wakili wa Serikali: Kumbukumbu namba ni Ipi

Shahidi: CD/IR/2097/2020

Wakili wa Serikali: hiyo ni Kumbukumbu namba ya Kitu gani

Shahidi: Ni Kumbukumbu ya Kesi

Kibatala: Mheshimiwa Jaji Tunapinga anachofanya Wakili Pius Hilla, aliyetakiwa Kusema Ni Kumbukumbu ya Kesi ipi Ilitakiwa Kusema na Shahidi Siyo Yeye Wakili

Jaji: Rudia Swali lako

Wakili wa Serikali: Shahidi Kumbukumbu namba Inayo Tajwa hapo ni Ya Nini

Shahidi: Ni Kumbukumbu ya Kesi inayohusiana na Kesi ya Kula Njama ya Kutenda Matendo Ya Ugaidi

Wakili wa Serikali: Shahidi Sasa Umemkabidhi wa Pistol Luger na Magazine Yenye Risasi Tatu, Vitu hivyo ulivipelela Wapi

Shahidi: nilivipeleka Makao Makuu Madogo Jeshi la Polisi, Kitengo Cha Uchunguzi

Wakili wa Serikali: Ulivipeleka Wapi

Shahidi: Makao Makuu Ya Jeshi la Polisi Kwa Uchunguzi zaidi

Wakili wa Serikali: Baada ya Kufika Ulimkabidhi nini

Shahidi: Nilikabidhi Silaha ambayo Nilichukia kwa sgt. Nuru

Wakili wa Serikali: Silaha gani

Shahidi: Ni Silaha aina ya Pistol A5340, Magazine Pamoja na Risasi

Wakili wa Serikali: Pamoja. A Vielelezo Hivyo Uliwasilisha na nini

Shahidi: Nili Wasilisha na Barua ambayo Ilikuwa na Maelekezo ya Nini cha Kufanya

Wakili wa Serikali: Shahidi Sasa ieleze Mahakama, Vielelezo Hivyo Ulimkabidhi Kwa Utaratibu Upi

Shahidi: Baada ya Kufika Kituoni Makao Makuu Ya Polisi tulikabidhiana Kwa Hati Ya Makabidhiano

Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Hati ya Makabidhiano Uliyotumia Kukabidhiana Ukiona Utaitambuaje

Shahidi: Nitaitambua Ina Jina Langu, Force Namba yangu, Jina la Ninaye mkabidhi, Kumbukumbu namba

Wakili wa Serikali: Kumbukumbu namba ipi.?

Shahidi: Ni CD /IR /2097 /2020

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Shahidi ameonyesha Uwezo Wa Kuitambua

Wakili wa Serikali: Eleza Nyaraka hiyo ni Nini Shahidi

Shahidi: Ni Hati ya Makabidhiano ambayo Nilimkabidhi Coplo Hafidh

Wakili wa Serikali: Ina Vitu Gani ambavyo Vimekufanya Uitambue

Shahidi: Ina Jina Langu pamoja na Sahihi yangu

Wakili wa Serikali: Inasomekaje

Shahidi: H 4347 DC Goodluck

Wakili wa Serikali: Kingine

Shahidi: Ina Jina la Ninaye Mkabidhi, Eneo ambapo Vilikamatwa

Shahidi: Naiomba Mahakama Ipokee Kama Ushahidi wangu

-Nyaraka: Inapelekwa Kwenye Benchi La Mawakili Wa Utetezi Mawakili Wote wa washtakiwa hawana Pingamizi

Jaji: Naipokea Kama Kielelezo namba 38

Jaji: Shahidi Usome Kwa Haraka Haraka

Shahidi ANASOMA kama ambavyo Sheria ya Ushahidi inataka, Shahidi anapotoka Kielelezo ambacho ni Nyaraka Kusoma Mbele Ya Mahakama

Wakili wa Serikali: Ni Hati Ya Tarehe Ngapi

Shahidi: Tarehe 25 November 2020

Wakili wa Serikali: anayekabidhi nani na anayekabidhiwa nani

Shahidi: anakabidhiwa Detective Coplo Hafidh, Anayekabidhi ni mimi DC Goodluck

Wakili wa Serikali: Nyaraka Inakabidhiwa Wapi

Shahidi: Inakabidhiwa Forensic Beaural, Kwa Detective koplo Hafidh

Wakili wa Serikali: Kuna Kumbukumbu Namba hapo, Ieleze Mahakama Inasomekaje

Shahidi: CD/IR /2097/2020

Wakili wa Serikali: Ni Kumbukumbu namba ya kitu Gani

Shahidi: Ni Kumbukumbu namba ya Kesi ya Kula Njama ya Kutenda Matendo Ya Ugaidi

Wakili wa Serikali: Inahusiana na nini

Shahidi: Vielelezo Vilivyo kamatwa Siku hiyo

Wakili wa Serikali: Ieleze Mahakama Kwamba Malipo Kuwa Moshi Baada ya Kuwakamata Watuhumiwa Mpaka Kuwa leta DAR ES SALAAM nani alikuwa ana husika na Ulinzi Wao

Shahidi: alikuwa ni Afande Mahita Pamoja na Mimi

Wakili wa Serikali: Tarehe 5 August 2020 Malipo wa kamata Watuhumiwa hali zao Zilikuwaje Mpaka Mnafilisha Mahabusu

Shahidi: Hali zao zilikuwa nzuri Waka Hapakuwa na Malalamiko Yoyote

Wakili wa Serikali: Tarehe 06 August 2020 Washitakiwa Walikuwa na Hali gani

Shahidi: Pia walikuwa na Hali Nzuri

Wakili wa Serikali: Tarehe 07 August 2020 Siku mnayofika Dar es Salaam, Washtakiwa Walikuwa na Hali gani

Shahidi: Walikuwa na Hali Nzuri, Na tulikula pamoja

Wakili wa Serikali: Je Watuhumiwa Uliowakata Tarehe 05 August 2020 na Tarehe 09 August 2020 Wapo Hapa Mahakamani.?

Shahidi: Ndiyo Wapo Hapa Mahakamani

Wakili wa Serikali: Ifahamishe Mahakama Uliowakata Tarehe 05 August 2020 ni Yupi ni Yupi

Shahidi: aliye Vaa Tshirt yenye Mstari Kijani, Nyeupe na Nyeusi nilimkamata Tarehe 05 August 2020

Wakili wa Serikali: Mwingine shahidi

Shahidi: aliye Vaa Tshirt ya njano na Draft anaitwa Adam Kasekwa, Nilihusika Kumkamata Maeneo ya Rau Madukani

Wakili wa Serikali: Mwingine

Shahidi: Mwingine Ni amevaa Kanzu Nyeupe na Baraka Shia, anaitwa Khalfani Bwire, Nilihusika Kumkata Dar es Salaam, Tarehe 09 August 2020

Wakili wa Serikali: Mwingine Kama Yup

Shahidi: Hakuna Mwingine niliye husika Katika Ukamataji

Wakili wa Serikali: ambao ulihusika Katika Ukamataji Uliwa kamata kwa Tuhuma zipi

Shahidi: Kula Njama za Kutenda Matendo Ya Ugaidi

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Sitakuwa na Swali Lingine

===========

- Anasimama Wakili Nashon Nkungu kutoka Jopo la Mawakili wa Utetezi

Nashon Nkungu: Shahidi ulijitambulisha wewe ni Askari kutoka Jeshi la Polisi ni Sahihi

Shahidi: Sahihi

Nashon Nkungu: Kwa hiyo Katika Utendaji Wenu wa akila Siku, Kinachotoa Utendaji Kazi ni PGO

Shahidi: Ni sahihi Nashon

Nkungu: Kwa hiyo Utatakiwa Kuwa na Uelewa Wa PGO

Shahidi: ni sahihi

Nashon: Na Utatakiwa Kufuata Masharti ya PGO

Shahidi: Ni sahihi

Nashon: Mlifanya Safari Kadhaa na Kwa kutumia Magari ni sahihi

Shahidi: Ni sahihi

Nashon: Magari haya yalikuwa ni Magari Ya Binafsi au Ya Jeshi la Polisi

Shahidi: Magari Ya Polisi

Nashon: Na Mlifanya Safari Mkoa hadi Mkoa

Shahidi: Ni sahihi

Nashon: Ni sahihi Kwamba Gari ya Polisi Inapotokea Mkoa hadi Mkoa, unahitaji Ruhusa Ya IGP

Shahidi: Siyo Kweli

Nashon: Nisomee PGO 197 Paragraph ya 4, Shahidi...... Without a prior aprove of Inspector General

Nashon: Mueleze Mheshimiwa Jaji ina maana gani

Shahidi: Hatukubadilishana Magari, Gari zilikuwa bado za Arusha

Nashon: Kwa kuwa umeshasoma Mbele ya Mahakama, Mahakama itaona Maana Halisi

Nashon: Unafahamu STATION Diary

Shahidi: Ndiyo

Nashon: Unafahamu Kwamba Safari zote zinaanzia Polisi

Shahidi: Ndiyo

Nashon: Je Unafahamu Kwamba ni Takwa la Kisheria Kabla yakuanza Safari, CRO inatakiwa Kurekodi Muda, Takwa la Safari?

Shahidi: Mimi siyo Dereva

Nashon: Je Uliona Wakati Wote Jambo hilo Likifanywa

Shahidi: Sijaona

Nashon: Unafahamu Kwamba Gari hilo la Polisi Kinatakiwa Kuwa na MOTOR VEHICLE LOG BOOK

Shahidi: Sifahamu

Nashon: Unafahamu Kwamba Safari zote Mlizofanya Hiyo Gari Ilitakiwa Kuwa na MOTOR VEHICLE LOG BOOK

Shahidi: Sifahamu

Nashon: Unafahamu Kitu Kinaitwa Report Book

Shahidi: RB ndiyo Nafahamu

Nashon: Je Unafahamu Kwamba Baada ya Kufanya Raid Ndani ya Eneo la Kituo, Officer Incharge Wa Hiyo Raid anatakiwa Kure port Kwa Incharge Wa Hilo Eneo

Shahidi: Ndiyo nafahamu

Nashon: Na Hiyo Reporting Inatakiwa Kufanyika Kwenye Report Book

Shahidi: Siyo Lazima

Nashon: Soma PGO ya 359 paragraph ya 9(e) Shahidi ANASOMA

Wakili wa Serikali: Samahani Mheshimiwa Jaji, Wakili hajaonyesha Foundation Kuwa anataka Shahidi asome Kwa lipi

Nashon: Nimeeleza Concern Kaka Yangu Msomi Wakili Pius Hilla

Ni kwamba Mtu anapotaka OBJECTION Ya Sheria, Yeye Ndiye anatakiwa atoe kilicho sahihi Wakili hajatoa Sheria ambayo ni Proper, PGO ambayo tunatumia tangu Mwanzo wa Kesi ni hii hii ambayo na wao wanaitumia, Ukiondoa Kwamba Kuna ammendments imefanyika Mwezi July Mwaka huu

Jaji: Swali hilo unaliondoa au Lah... Concern Yake Wakati Unampa asome PGO ya Wakati gani

Wakili wa Serikali: Ni sahihi Mheshimiwa Jaji ni Vizuri Shahidi aonyeshwe ni PGO ya Toleo lipi

Nashon: Mheshimiwa Jaji Mpaka Nakuja na PGO hii tayari nimejiridhisha

Kibatala: Mheshimiwa Jaji Tunaomba Dakika 2

Nashon Nkungu: Shahidi Unafahamu Kwamba Kuna ammendments za PGO?

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Wakili hawezi Kuendelea na Mahakama Mpaka ajibu Hoja ya Mahakama

Kibatala: Mheshimiwa Jaji Mr. Hilla Hoja yake Ilikuwa ni Foundational Concern

JAJI: Hoja yangu ni kwamba anaondoa swali au anaendelea na Swali?

Nashon: Mheshimiwa Jaji Naomba kuliondoa hilo swali

Nashon: Shahidi Unafahamu Kwamba Kuna Amandments za PGO zime fanyika July Mwaka huu

Shahidi: Ndiyo nafahamu

Nashon: Unafahamu kwamba Kabla kabla ya hapo palikuwa na PGO ambayo wewe Ulikuwa Unafanyia Kazi

Shahidi: Ndiyo nafahamu

Nashon: Mheshimiwa Jaji KWA Ruhusa Yako nitaomba Unisomee 309 Paragraph 9(e)

Shahidi: ANASOMA

Nashon: Baada ya Kusoma Sheria Hii Bado Unasimamia msimamo wako Wa Awali?

Shahidi: Kwamba?

Nashon: Ulisema Siyo Lazima Kwa Nyinyi Kutoa Report Baada ya Raid Mliyo fanya Pale Rau Madukani..

Shahidi: Ndiyo Siyo Lazima

Nashon: Unafahamu SMG?

Shahidi: Ndiyo nafahamu

Nashon: SMG ni aina ya bunduki au function ya bunduki?

Shahidi: Ni function ya bunduki

Nashon: AK47 inaweza kuwa sawa na SMG?

Shahidi: Ndiyo inaweza kuwa ni SMG

Nashon: Unaweza Kueleza Wale Mashahidi Huru walipatikana Vipi?

Shahidi: Ni Afande Jumanne

Nashon: Ni Ushahidi Wako Kwamba Afande Jumanne aliwaacha Watuhumiwa akaenda Kuwaita Mashahidi?

Shahidi: Siyo Mbali sana, Bado Unaweza Kuona Watuhumiwa

Nashon: Kama Hatua ngapi?

Shahidi: Sikumbuki

Nashon: kwenye hii Bunduki Kuna label Mbili, Unaweza Kutueleza nani alizi attach?

Shahidi: Baada ya Mimi Kukabidhiwa Niliweka Kwenye Begi, Silaha Ilienda Kwa Mtunza Vielelezo Dar es Salaam, ila Mimi sifahamu

Nashon: Je ni Ushahidi Wako Silaha hii Haikuwa labelled kutoka Rau Madukani Mpaka Unafika Dar es Salaam?

Shahidi: Ndiyo Siku label

Nashon: Je Unafahamu Kwamba Kielelezo Kinatakiwa Kuwa labelled Mara Baada tu ya Kukamata Kielelezo

Shahidi: Ndiyo nafahamu

Nashon: Na Shahidi Unafahamu Kwamba Kuto label Kielelezo Ni Hatari inayo Pelekea Kuchanganyika kwa Kielelezo?

Shahidi: Ndiyo Nafahamu

Nashon: Umesema Hapa, Kwamba Muda Wote Silaha ilikuwa kwenye Begi lako, Je ulileta Hilo Begi Mahakamani Ili Mahakama Ione Uimara Wa hilo Begi?

Shahidi: Sikuleta

Nashon: Je Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Begi hilo Lina Lock au Password Ambayo wewe tu Unaweza Kufungua, au Lina zipu au Lipo wazi?

Shahidi: Sikumwambia

Nashon: Kwa kuuwa hujafanya hayo, Ni sahihi Mahakama Haiwezi Kufahamu Umadhubuti Wa Hilo Begi kwa Sababu Mahakama haijaliona?

Shahidi: Sivyo

Nashon: Je Shahidi Unafahamu Kwamba labeling ya Kielelezo inatakiwa Kuambatana na FOMU YA PF 145?

Shahidi: Ndiyo Nafahamu

Nashon: Je Unafahamu Kwamba Hiyo Polisi fomu kazi yake, ni Column 6 Kuonyesha Chain of Custody?

Shahidi: Sifahamu

Nashon: Ulisema Pia Kwenye Ushahidi wako Ulienda Pia AISHI HOTEL Saa Tano Usiku Kuendelea Kuwatafuta

Shahidi: Siyo Kweli

Nashon: Si Kweli Kwamba Mlienda Aishi Hotel katika Harakati za Kuwatafuta, Ninyi Mkabaki Nje na Jumanne na Mahita Wakaingia ndani

Shahidi: Siyo Kweli

Nashon: Hukutaja Jina la Hotel

Shahidi: Hotel ya kwenda Kupumzika siyo unayotaja

Nashon: Unauthibitisho wa risiti ya Hotel?

Shahidi: Sijaleta

Nashon: Hukuona Umuhimu Kuleta risiti

Shahidi: Nilikuwa na viongozi wangu

Nashon: jibu swali unaloulizwa

Shahidi: sikuona umuhimu

Nashon: Uliambiwa watu hawa pia wana nia kuwadhuru viongozi akiwemo Sabaya?

Shahidi: Ni kweli

Nashon: Uliwataja sasa viongozi wengine

Shahidi: Hapana

Nashon: Je ulieleza kwamba mlimwambia Sabaya kuwa kuna hatari inakaribia?

Shahidi: Sikueleza

Nashon: unaweza Kukumbuka zoezi la Ukamataji na Upekuzi, lilichukua Muda gani?

Shahidi: Siwezi Kukumbuka muda

Nashon: Je Unafahamu Kwamba PGO inataka Urekodi Kila Tukio na Muda Kwenye Diary Yako?

Shahidi: Ndiyo nafahamu

Nashon: Na wewe hukufuatisha Kama PGO Inavyotaka?

Shahidi: Walikuwa wana rekodi Viongozi Wangu

Nashon: Je Unafahamu kwamba PGO Inataka Kila Polisi Kurekodi Matukio na Muda Kwa Askari Wote+

Shahidi: Ndiyo Nafahamu

Nashon: Ni sahihi Kwamba Umesema Ulmkamata Khalfani Bwire

Shahidi: Ni sahihi

Nashon: Na Ulimpeleka Kituo gani

Shahidi: Kituo cha Polisi Chang'ombe

Nashon: Kwa Ufahamu Wako unafahamu Kwamba alipelekwa Kituo Kingine Cha Polisi

Shahidi: Sifahamu

Nashon: Na Hamkumpeleka Kituo Cha Polisi Tazara

Shahidi: Sifahamu

Nashon: Shahidi Unafahamu Kwamba Mtuhumiwa afikishwe Mahakamani Baada ya Muda gani

Shahidi: Sifahamu

Nashon: Kwa hiyo unaweza Kukaa naye Milele

Shahidi: huwezi Kukaa naye Milele, Upelelezi Ukikamilika unampeleka

Nashon: Upelelezi Unaweza Kuchukua Muda gani

Shahidi: Sifahamu

Nashon: Baada ya Kumkamata Bwire Mlimfikisha Mahakamani Tarehe ngapi

Shahidi: Hapana Sikumbuki

Nashon: Nikisema Kuwa aliandika Maelezo Chang'ombe nitakuwa sahihi

Shahidi: Sifahamu

Nashon: Nisaidie Je Mtuhumiwa anaweza kuandikwa Maelezo Kituo chochote

Shahidi: Inategemea na Mpelelezi, Kama Yupo Mpelelezi anamuandika Ndiyo

Nashon: Wakati Unamkabidhi Inspector Ndowo Simu, Je zilikuwa na Line zake

Shahidi: Zilikuwa Pamoja

Nashon: kwanu shahidi Nyie huwa Mnatumia Mali za Mtuhumiwa?

Shahidi: Kwa Matumizi Binafsi?

Nashon: Ndiyo

Shahidi: Haiwezekani

Nashon: Nikikuonyesha Chini ya Kiapo Kuwa wewe Umetumia Mali ya Mtuhumiwa utakataa?

Shahidi: Sijawahi Kutumia Mali ya Mtuhumiwa

Nashon: Je Tarehe 10 December 2020 Uliandika Maelezo Polisi Kituo Cha Polisi Kati Dar es Salaam

Shahidi: Ndiyo ni Maelezo yangu

Nashon: Mheshimiwa Jaji Sasa Kwa Kutumia Kifungu cha 164..... Anyways, Mheshimiwa Jaji naomba Kuondoa Hilo Ombi sababu ya Muda

Nashon: Je Shahidi Unafahamu kwamba unatakiwa Kumkabidhi Tu Vielelezo Mtunza Vielelezo?

Shahidi: inategemea na Mazingira

Nashon: Je Utakubaliana na Mimi Kwamba, Hukutoa Sababu Kwanini Ulimkabidhi Vielelezo Afande Swila ambaye siyo Mtunza Vielelezo?

Shahidi: Ndiyo sikutaja

Nashon: Je Unafahamu Kwamba Kuchukua Mali Bila Certificate of Seizure ni Kinyume cha Sheria

Shahidi: Nilieleza Afande Kingai alikuwa na Certificate of Seizure

Nashon: Hizo Certificate of Seizure Zilikuwa za Vifaa gani?

Shahidi: Ni simu

Nashon: Na ni Ushahidi Wako Kwamba Umetoa hapa Mahakamani hiyo Certificate of Seizure

Shahidi: Sijatoa Mahakamani

Nashon: Na Unafahamu Kwamba Ungetoa Certificate of Seizure ingeonyesha Muda?

Nashon: Je Unafahamu Detention Register

Shahidi: Ndiyo

Nashon: Ni sahihi Ujatoa Detention Register Ya Moshi

Shahidi: Ndiyo sijatoa

Nashon: alisema Siku Tarehe 7 August 2020 Mlipofika Central Mlipewa Break ya Kunawa Uso Kabla Ya Kutoa Vielelezo

Shahidi: Ni sahihi

Nashon: Kwa hiyo Ulienda Kunawa Uso Ukiwa na Vielelezo?

Shahidi: Ndiyo

Nashon: na Muda wa Kuna wa Uso Ulikuwa Lisaa Limoja

Shahidi: Ndiyo

Nashon: wewe na Sgt. Nuru Mlikabidhiana Bastola A5340

Shahidi: Ndiyo

Nashon: Na Hiyo ndiyo Ilikuwa Discription ya hicho Kielelezo

Shahidi: Ndiyo

Nashon: kama Nuru alitaja Kielelezo kwa Namba Nyingine kitaku ni tofauti na Ulicho taja wewe

Shahidi: hawezi Kutaja Kingine

Nashon: Unaweza Kurudia Kwa namna Kila Mmoja alivyokuwa amevaa

Shahidi: Mohamed Ling'wenya alikuwa amevaa Nguo Nyekundu na Adam Kasekwa Alikuwa amevaa Shati Jacket la Kijani

Nashon: Hukuona Umuhimu Wa Kuja na Hizo Nguo

Shahidi: Ni Nguo zao

Nashon: Hukuona Umuhimu wa kuja na nyaraka yoyote Ile ilikuthibitisha Kama Kweli Mlizunguka nao?

Shahidi: Hakuna

Nashon: Shahidi nashukuru Kwa Ushirikiano Wako

Wakili John Mallya anaingia

Mallya: Katika wale watuhumiwa kuna Mtuhumiwa anaitwa Deshi?

Shahidi: Hakuna

Mallya: Sasa umetuletea ushahidi Mahakamani, Mahakama ipokee ushahidi Wako, Mtuhumiwa na kosa

Shahidi: Mtuhumiwa deshi na kosa deshi

Mallya: Hiyo ilikuwa Kielelezo 37 Sasa Namuonyesha 38 Baada ya Namba 2097 Kuna Mkwaju 2020

Shahidi: Ni sahihi Kabisa

Mallya: Ni sahihi Kwamba Huu Mkwaju umetenganisha 2097 na 2020.. Je Katika Kielelezo P38 Kuan Mkwaju.?

Shahidi: Hakuna Mkwaju Kuna Nafasi

Mallya: Umesema katika kumbukumbu namba umesema kuna majina ya watuhumiwa

Shahidi: Ndiyo

Mallya: Sasa faili umekuja nalo

Shahidi: Sijaja nalo mimi siyo mpelelezi

Mallya: Tarehe 04 August 2020, Mahita alikufuata akakwambia Twende Kwa RCO, Ukaenda Kubeba Silaha?

Shahidi: Ndiyo, Niliambiwa Kuna kazi ya kufanya

Mallya: Ulikuwa unajua Unafanya kazi gani

Shahidi: Hapana

Mallya: Kwenye Sehemu ya Kutunza silaha, Kuna Virungu

Shahidi: Ndiyo havitumiki Siku hizi

Mallya: Kwenye store yenu ya Polisi Kuna Bastola

Shahidi: Ndiyo zipo, Ila Mimi siyo Polisi Mdogo

Malya: wewe Ulibeba AK 47

Shahidi: Ni sahihi

Malya: AK47 ina Kama Kilo 3.4 hivi bila Magazine

Shahidi: sawasawa

Malya: koplo Francis na Yeye alikuwa na Silaha na Yeye

Shahidi: Ndiyo, Askari Alisha Kuwa na Silaha lazima awe Makini

Malya: Wakati Jumanne anafanya Upekuzi Ulieleza Kuwa Bunduki Uliweka Wapi

Shahidi: Sikueleza

Malya: ulimuuliza za Mheshimiwa Jaji aina ya Nguo ulizovaa

Shahidi: Sikumueleza

Malya: Kwa hiyo Kama ilikuwa na Mifuko Michache au Mingi hatuwezi Kujua

Shahidi: Ndiyo

Mallya: Pale Rau Mlimkamata Simu Ngapi

Shahidi: Simu Mbili

Malya: Ulitueleza Upande wa Dereva Upo Upande gani

Shahidi: Sijasema Hapa Mahakamani

Malya: Je Umetuambia Uliupa Mgongo au Ulirudi Kinyuma Nyuma Askari mahili

Shahidi: Hapana Sijasema

Malya: Je alitueleza Kwamba Ulishika kwa namna gani Vielelezo wakati una AK 47 ya Kilo 3.4

Shahidi: Sikueleza

Malya: Je Ulitumabia Kuwa Ulipofika Kwenye Gari Ulishika Bahasha Kwa namna gani

Shahidi: Nilisema Kwamba Nilimwambia Azizi anipe Bahasha

Malya: Je Kuna sehemu ulitoa Utofauti wa Bastola zilizopo Kwenye Chumba Cha Kutunzia Silaha

Shahidi: Hapana Sikutoa

Malya: Je ulitoa Ufafanuzi Kuwa ulipo rudi nazo Wakati anajaza Ulikuwa unafanya Ulinganifu Mbele ya Mashahidi Pale Rau Madukani

Shahidi: Hapana Sikutoa

Malya: Naomba Kielelezo Namba P3, na Risasi zake

Malya: Leo hapa Mahakamani Ukiongozwa na Kaka yangu Pius Hilla Hilla, umeonyeshwa hapa Mahakamani

Shahidi: Hapana sijaonyeshwa

Malya: Uliambiwa Kwamba Risasi Moja Bwana Hafidh kaivunja vunja

Shahidi: Sijaambiwa

WS Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji tunaomba Swali liwekwe vizuri, Hakuambiwa atoe Risasi tatu

Malya: Ulituonyesha Risasi Tatu Mahakamani au Hukutuonyesha?

Shahidi: Hapana Sikuonyesha

Malya: Wewe Ndiyo Ulimkabidhi Bwana Ndowo Simu

Shahidi: Ndiyo

Malya: Je ulitoa Mahakamani hiyo Hati ya Makabidhiano

Shahidi: Hapana

Malya: nani sasa ataleta Hati ya Makabidhiano ya hizo Simu

Shahidi: Miye nilimuachia Ndowo

Malya: Sasa tutamuuliza Maana Kuna su zime vunjwa Vunjwa

Shahidi: Sijui

Malya: wewe Ulieleza Kuwa Kuna Simu Kama hii imevunjwa

Shahidi: Hapana sijaeleza

Malya: Unafahamu Justine Kaaya

Shahidi: Ndiyo Namfahamu

Malya: Unamfahamu Gabriel Muhina

Shahidi: Ndiyo Namfahamu

Malya: Kwa hiyo Kwenye Faili namba CD/IR 2097/2020 Walikwepo Wote

Shahidi: Sifahamu

Malya: Kwani wakati Faili linafumguliwa Ulikuwepo

Shahidi: Hapana

Malya: Sasa Unaposema Jina Deshi Deshi lipo Kwenye Faili Kwani Unajua Kuna Majina Mangapi Kwenye Faili

Shahidi: Hapana Sifahamu

Malya: na Unaposema Bwana Jumanne alikukabidhi Vielelezo Pale Rau Madukani

Shahidi: Ndiyo

Malya: na Mashahidi Wote Waliona pale Rau Madukani Moshi

Shahidi: Ndiyo Waliona

Malya: Enheeeee Jumanne alikwenda Kujazia Fomu ya Makabidhiano Wapi?

Shahidi: Kwenye Gari

Malya: wewe unasema ulimkabidhi Afande Ndowo simu na line zake, yeye hapa Mahakamani kaleta simu pekee yake.. Nani kaiba line za wateja wangu?

Shahidi: nilimkabidhi simu zikiwa na line zake

Malya: Je Kuna uwezekano wewe ndiyo umepoteza?

Shahidi: Weeeee Hapana, Nilikabidhi Vyote

Mahakama: Kicheko

Malya: Sasa shahidi Kuna tuhuma hapa wewe na Afande Mahita ndiyo mlikuwa mnawapiga watuhumiwa kwa kushirikiana na kuwapiga kwenye nyayo..

Shahidi: Hapana Siyo kweli hakuna mtu aliye wapiga

Malya: Kuna Story Very interesting, mwanzo mlisema kuwa Afande Mahita alifanya doria akasema kuwa wapo watatu, Ila baada ya kuwakamata hawa na kuwa pekua ndiyo mkashtuka mmoja hayupo, kwanini hamkushtuka palepale?

Shahidi: Afande Kingai eneo la tukio aliwauliza wakakaa kimya!

Malya: Je Wakati unaongozwa na Wakili Pius Hilla Ulisema hilo?

Shahidi: Hapana

Malya: Sasa iweje ghafla kwenye Gari Waanze kutaja jina la mwenzao, si Kwa sababu mliwapiga?

Shahidi: Hapana walijitolea wao wenyewe kusema yupo wapi.

Malya: Wewe ulishuhudia anajaza fomu

Shahidi: Nilikuwa karibu

Malya: Ulishuhudia?

Shahidi: Nilisikia

Malya:Majina yameandikwaje?

Shahidi: Adam Hassan Kasekwa ADAMOO

Malya: Ulikwepo eneo la tukio kweli?

Shahidi: Ndiyo nilikuwepo ila Afande Jumanne ndiyo kasikia vizuri zaidi

Malya: Hati ya Makabidhiano Ya Simu, Hasa ya Adamoo Kutoka Kwa Afande Jumanne Kuja Kwako, Umetoa Mahakamani Leo

Shahidi: Hakuna

Malya: Umeonyeshwa Fomu ya Kabidhiano ya Simu?

Shahidi: Hapana

Malya: Kwa ufahamu Wako Mpelelezi Wa hii Kesi alikuwa ni nani?

Shahidi: Sifahamu

Malya: Kwenye Faili CD/IR /2097 /2020 Kuna tuhuma Ngapi?

Shahidi: Simfahamu, Zaidi ya Kula Njama

Malya: Kutoka USA Mlipotoka Kuelekea Kilimanjaro, Moshi Mjini si Mlipita Wilaya Ya Hai

Shahidi: Ndiyo

Malya: Mlipita Kwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Boma Ng'ombe Kumwambia BE CAREFUL?

Shahidi: Hapana

Malya: Nyumbani kwake Ulikwenda

Shahidi: Hapana

Malya: Ni sahihi Kwamba Sababu Ya Kuandika namba ya silaha kwenye Hati ya Makabidhiano, ilikuwa Kutofautisha hii Silaha na Nyingine

Shahidi: Ni sahihi

Malya: na Kwa Uzoefu wako wewe Mpaka Kushika AK47 ni sahihi Bullets zinatofautiana

Shahidi: Ndiyo

Malya: Je wewe Kwenye Hati ya Makabidhiano, Umetoa tofafuti ya Bullets hizi na Zingine

Shahidi: Hapana Sijatoa

Malya: Kwa Sababu zile namba za bullets Hukuandika nikikupa zile Bullets Utakumbuka?

Shahidi: Hapana siwezi Kukumbuka

Malya: haya turudi Arusha Ndugu yangu, ulipofika USA RIVER Nakuambiwa Kuwa kuna ugaidi wa kulipua vituo vya mafuta Je mliwakuta na kidumu cha petrol?

Shahidi: HAPANA

Malya: Mliwakuta na MABUMU YA KULIPUA?

Shahidi: HAPANA

Malya: Mliwakuta na Chain Saw ya kukatia Magogo?

Shahidi: Hapana

Malya: Je Ni sahihi Afande Kingai kwa nafasi yake anaruhusiwa Kutembea na Bastola?

Shahidi: Ndiyo

Malya: Je Jumamne Kwa nafasi yake anaruhusiwa Kutembea na Bastola?

Shahidi: Ndiyo

Malya: Je Wakati Unatoa Ushahidi Wako hapa Ulisema Kwamba Siku hiyo Walikuwa nazo au Waliacha kwenye Gari?

Shahidi: Hapana Sijatoa Maelezo

Malya: Mnasema Mlimkuta Adamoo na Itel, Je Ili mimi Nabisha Mlimsimgizia si ni lazima Twende Voda au Tigo na Ile Simu na Line, Wakaangalie Usajili

Shahidi: Ni sahihi

Malya: Hii simu ya Bw. Khalfani Bwire, Ni sahihi alikukabidhi Simu Baadae

Shahidi: Hapana alinipa palepale

Malya: Lakini Taratibu za Kipolisi Zinataka anapokukabidhi Kukabidhi na Kikaratasi

Shahidi: Hapana Siyo Lazima

Malya: Kuhusiana na Kukamatwa Kwa Bwire, Je Kuna Dereva au Abiria aliye shuhudia Wakati Bwire anakamatwa

Shahidi: Hakuna

Malya: Wewe Umemfahamu lini Bwire

Shahidi: Nilikuwa Simfahamu Mpaka baada ya Kumkamata

Malya: Mwambie Mheshimiwa Jaji Kuwa Ulikuwa Umjui

Shahidi: Mheshimiwa Jaji niilikuwa simjui

Malya: Je ulitoa Ufafanuzi Kwamba Ulijuaje Kwamba Yule Ndiyo Khalfani Bwire

Shahidi: Hapana Sikutoa, Ila aliyekuwa anajua ni Kingai

Malya: Mheshimiwa Jaji Sina Swali la Ziada kwa Shahidi huyu na Pia muda Umefika

Fredrick Kihwelo: Mheshimiwa Jaji Kwa Kuzingatia Swala la Muda na Ukizingatia Nina Maswali Mengi Sana, Nilikuwa naomba Hairisho

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Hakuna Pingamizi kuhusu hiyo hoja

Jaji: Jumatatu itakuwa Tarehe Ngapi

Mawakili: Tarehe 24

Jaji: Shauri linahairishwa mpaka Jumatatu tarehe 24.1.2022 ambapo shahidi ataendelea kuhoji wa na upande wa utetezi. Washtakiwa wataendelea kuwa rumande chini ya magereza mpaka jumatatu Saa 3 asubuhi Jaji anatoka
Shahidi: Wee! Hapana nilimkabidhi zote.

Mahakama: Hahahaaaa

Shahidi anaona kama anageuziwa kesi kutokana na ushahidi wa wenzake wa uongo wa awali.
 
Screenshot_20220123-132936.jpg
 
Mkuu tunashukuru kwa kutujuza hayo yote, ila mjitahidi kutochelewesha updates leo Ijumaa tunawahi ibaada, hata ukiweka vufupi vifupi sio mbaya kuliko kusubilia masaa ma tatu au manne.
Hii hadithi inastarehesha. Endeleeni kutujuza.
 
Hata mimi nasubiri maana bado ushahidi hakuna
Nadhani ungekuwepo kitambo Sana wangeshamfunga.
Ukiona kesi yoyote inachumkua mda kuisha jua ni ya kubambika.
Wangekuwa na ushahidi kitambo Sana wangeshamfunga hadi sasa wanaruka ruka tu.
 
Nadhani ungekuwepo kitambo Sana wangeshamfunga.
Ukiona kesi yoyote inachumkua mda kuisha jua ni ya kubambika.
Wangekuwa na ushahidi kitambo Sana wangeshamfunga hadi sasa wanaruka ruka tu.
Kama Sabaya kesi ilichukua mwezi mmoja tu.
 
Back
Top Bottom