Yaliyojiri katika kesi ya Mbowe na Wenzake. Tumaini Swila amaliza ushahidi. Mawikili wa Serikali wafunga Ushahidi. Jaji kutoa uamuzi 18/02/2022

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,758
4,305
Habari Wakuu,

Leo 15/ 02/ 2022 shahidi wa 13 anatarajiwa kuendelea kutoa ushahidi wake kwenye kesi inayomkabili Mbowe na wenzake 3 baada ya Ushahidi wake kutokamilika jana

Kujua Kesi ilipoishia fungua kiungo hiki: Yaliyojiri Mahakamani kesi ya Mbowe na wenzake 3. Shahidi wa 13, Tumaini Swila kuendelea kutoa ushahidi Februari 15, 2022

UPDATES


- Jaji ameingia

Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa Mahakamani Muda huu.

Wakili wa Serikali Robert Kidando Mheshimiwa Jaji Ikupendeze naitwa Robert Kidando nipo pamoja na wakili
  • Pius Hilla
  • Abdallah Chavula
  • Jenitreza Kitali
  • Nassoro Katuga
  • Esther Martin
  • Ignasi Mwinuka
  • Tulimanywa Majige

Wakili Peter Kibatala Mheshimiwa Jaji Ikikupendeza naitwa wakili Peter Kibatala nipo Pamoja na;
  • Livino Haule
  • Emmanuel Cheng
  • Heche Edward
  • John Mallya
  • Frederick Wakili
  • Nashon Nkungu
- Jaji anaita Washtakiwa Wote wanne na wote wanaitika wapo Mahakamani Siku ya Leo

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya Kusikilizwa, Tupo tayari Kuendelea

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji nasi pia tupo tayari Kuendelea

Jaji: Shahidi nakukumbusha Ulikuwa chini ya Kiapo na Utaendelea Kuwa Chini ya Kiapo

Shahidi: Sawa Mheshimiwa Jaji

Jaji: Wakili Endelea

Kibatala: Shahidi Unakumbuka Maswala ya Sampuli ambazo Ulichukua kutoka kwa Mshitakiwa Wa kwanza, Wapili na watatu

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Unakumbuka Katika Ushahidi Wako ulitoa Tarehe 7 February 2022 Ulisema Kwamba Tarehe 30 March 2021 Nilipokea Riport ya Uchunguzi Kutoka Maabara Ya Uchunguzi Wa Maandishi Kutoka kwa koplo Khamis

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Kwa hiyo Suala la Report Mlileta wenyewe Mahakamani, na Mpaka Ukasema Mwandiko Wa Bwire unafana na Kwenye Kidaftari

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Na kumwambia Sasa Katika Report Hiyo Mwandishi anasema Kwamba Ulipeleka Sampuli 15

Shahidi: Siyo Kweli

Kibatala: Lakini Ulisoma hiyo Report

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Ikija ikaonekana Kweli Ulipeleka Karatasi 15

Shahidi: Nishasema si kweli

Kibatala: Je Ulimwambiwa Kwamba Kidaftari cha 5 star siyo Kielelezo hapa Mahakamani

Shahidi: Sikuambiwa

Kibatala: Na kuhusu hiyo Report Ulimwambiwa kuwa haiko hapa Mahakamani

Shahidi: Sikuambiwa

Kibatala: Unafahamu Kwamba Majengo Yana anuani iwe Kwa reference ya Namba au Makutano Ya Barabara Mbili au tatu

Shahidi: Nafahamu

Kibatala: Infact hata Makao Makuu Makubwa au Madogo ya Jeshi la Polisi Dodoma Yana anuani

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: na Katika Context hiyo Ndiyo Maana hata wanapiga Hatua ndiyo Maana hata Makazi Binafsi Wanaanza Kutoa anuani

Shahidi: Ndiyo nafahamu

Kibatala: Nilikusikia Ukisema Kwamba Ulitembelea Vituo Kadhaa wa Kadhaa Vya Mafuta

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Ambavyo katika Ushahidi Wako Ulisema Kwamba Vituo vililengwa Kufanyiwa Matendo Fulani katika Vituo hivyo Vya Mafuta

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Ulitaja Vituo Vipi Vya mafuta Mbali na Morocco

Shahidi: Ni GBP Kilwa road Puma KILWA ROAD, BIG BON Kariakoo

Kibatala: Kingine

Shahidi: Puma Sinza

Kibatala: Je Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Kipo katika plot namba Ngapi hicho cha Morocco

Shahidi: Nilieleza Kipo katika Barabara, Kuhusu Plot Sikueleza

Kibatala: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Mmiliki wa hichi Kituo ni nani

Shahidi: Sikumwambia

Kibatala: Twende Kilwa Mivinjeni, Je Ulisema Kipo Makutano yapi

Shahidi: Nilisema Kipo Barabara ya Kilwa

Kibatala: Kipo plot namba ngapi

Shahidi: Sikueleza

Kibatala: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba hicho Kituo kinamilikiwa na nani

Shahidi: Sikumwambia

Kibatala: Big BON Kariakoo Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kipo katika Barabara ipi

Shahidi: Sikumwambia

Kibatala: Ulimwambia Kipo katika Plot namba ngapi

Shahidi: Sikumueleza

Kibatala: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Mmiliki Wake na nani

Shahidi: Sikumueleza

Kibatala: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Vituo hivyo Ulitembelea Tarehe ipi na Saa ipi.?

Shahidi: Nilimwambia, Kwa Kutaja Tarehe

Kibatala: Kwa hiyo Kwa Ushahidi Vituo Vyote Ulitembelea Siku Moja

Shahidi: Sahihi ni Tarehe 14 August 2020

Kibatala: Muda ulitaja

Shahidi: Sikutaja

Kibatala: Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Ulienda na nani

Shahidi: Sikueleza

Kibatala: Hizo Details Kama Ulivyo Zitoa, Katika Maelezo Yako Ya Tarehe 09 August 2021 Hakuna

Shahidi: Zipo

Kibatala: Ungependa niombe Nakala halisi ya Kwako uweze Kuithibitishia Mahakama

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Mheshimiwa Jaji naomba Nipewe Nakala halisi ya Maelezo Ya Inspector Tumaini Swila, Nimejenga Msingi Wa Kutosha na Shahidi

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Hatuna Pingamizi

Kibatala: Naomba ungalie na Usome Kwa Sauti, Kisha Ukimaliza nieleze Mahala ambapo Ume Vi Discribe hivyo Vituo kama ambayo umesema

- Shahidi ANASOMA Maelezo Yake aliyo andika 06 August 2021

- Shahidi AMEMALIZA KUSOMA


Kibatala: Unafahamu Maana ya Details.?

Shahidi: Fafanua

Kibatala: Mwanzo Nilikuuliza Kwamba Vituo Vya Mafuta Ulivyo taja ulivitaja katika Details Kwamba Vina milikiwa na Mtu X

Shahidi: Ndiyo, ila siyo lazima iwe hivyo

Kibatala: Katika Maelezo Yako Unasema Mivinjeni Dar es Salaam Ulikuta Kituo cha Kuuzia Mafuta Puma. Je Kuna Mahala Umetaja Kituo cha Puma Kipo Kilwa Road

Shahidi: Kilwa Road Haipo, ila ndiyo Maana nimekuja Kutoa Ushahidi, Kwenye Maelezo siwezi Kusema Kila kitu

Kibatala: Haya pia umesema Kwamba Ulifika Bigbon Kariakoo,, Mwambie Mheshimiwa Jaji Kuwa Umetaja Makutano Ya Barabara ipi

Shahidi: Sijataja

Kibatala: Twende Pale Unaposema Kwamba Morocco Kuna Kituo cha Kuuzia Mafuta cha TOTAL, Je Kuna Mahala Popote umesema Kituo cha Morocco Kipo katika Makutano gani

Shahidi: Katika Maelezo Hakuna

Kibatala: Ulitaja Kituo Cha Morocco Kipo karibu na Mwenendo kasi, Umetaja Kituo cha Mwendo kasi hapa

Shahidi: Sijataja

Kibatala: Twende Sinza Kituo cha Puma, Je umefafanua Kuwa Kituo cha Puma Sinza lipo Barabara gani

Shahidi: sijafafanua

Kibatala: Si Umekuja Kutoa Ushahidi Wa kweli, Je Kuna tatizo Mheshimiwa Jaji akiyaona Maelezo Yako kama Ushahidi Wako

Shahidi: Hakuna.

Kibatala: Mheshimiwa Jaji Kama Shahidi alivyoomba naomba Maelezo yake yapokelewa Kama Kielelezo...

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji sisi tulichosikia, Kuna tatizo lolote Jaji akiyaona Maelezo Yako, Shahidi akasema Hakuna tatizo.

Wakili wa Serikali: Hakuna Mahala Popote ambapo amesema yapokelewe kama Kielelezo, Hapo naona Kama Kuna tatizo

Kibatala: Mheshimiwa Jaji Nakumbuka nimesema akiyaona Kama Kielelezo.? Unless kama Kuna Maelezo

Jaji: Rudia Swali lako

Kibatala: Je Shahidi Una tatizo lolote Kama Maelezo Yako Yakipokelewa Kama Kielelezo Mahakamani

Shahidi: Hakuna tatizo

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji hatuna Pingamizi

Jaji: Mahakama Inapokea Maelezo Ya Inspector Tumaini Sostenes Swila Kama Kielelezo namba D5

- Mawakili wa pande zote mbili wanakubaliana na Uamuzi Jaji kwa Kusimama na Kumuinamia Kidogo

Kibatala: Kuna sehemu Katika Maelezo Yako Unasema Kuwa lakini tangu akamatwe Mtuhumiwa Khalfani Bwire tangu akamatwe, Mheshimiwa Mbowe haijawahi Kufika Kituo chochote cha Polisi, Kumuulizia Kitu ambacho Kinafanya tuone nia yake Ovu.

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Katika Kifungu 154 kinakataza Anachokifanya Wakili Peter Kibatala. Ingekuwa ameomba Kwa Matumizi haya anayofanya basi Ilitakiwa ajenge Msingi. Kwa Mujibu wa Kifungu Hiki, alimuelekeza Katika Maeneo ambayo alitembelea Vituo Vya Mafuta kwa Dhumuni Ya Kum Contradict, Sasa anachokifanya Kipo Nje zaidi ya kile alichoombea Kielelezo. Procedure hiyo tunai Support Kwa Uamuzi Wa Mahakama Ya Rufaa ya Lilian Jesus Vs Republic ambayo ni Criminal appeal namba 151 ya Mwaka 2018 - Unreported lakini inapatikana katika Mtandao Wa TANZII).

Kibatala: Mh Jaji hiyo Kesi anayotaja tunayo, lakini nakuwa Mwangalifu na anachokisema wacha ni reorganize, anasema Mimi najua, Kwanza Mimi Siyajui hayo, Hayo ni Maoni yao, hapa Mahakamani Kuna Uamuzi Wako wa kwamba Nyaraka Ilishaingia Mahakamani Kama Kielelezo Inaweza Kutumika. Kwanza Kifungu Cha 154 na 161 ni Vifungu Vinavyo tumika Kuingiza Nyaraka Mahakamani

Jaji: Soma Kifungu Cha 154

- Kibatala anasoma

Kibatala: Hiyo Portion ni Permissive naweza Muuliza Kwa Kumuonyesha Nyaraka au Bila Nyaraka, nahitaji Kum Contradict, Lazima ni Muonyeshe the Particular Portion ambayo nataka Kum Contradict. Hakuna Mahala inasema siwezi Kutumia Kielelezo hapa Mahakamani Kikishapokelewa. Kwanza wameweka Toroli Mbele Ya Farasi.

Jaji: Nakubalina Na wewe na Ninakubaliana naye kuwa katika Kifungu 154, inaposema Kwamba Pale ambapo Unataka Draw attention Yake Kabla ya Nyaraka inataka Kuingia Mahakamani. Suala lako wewe Unasema Wameanza Kuweka OBJECTION Kabla hawajajua kuwa Unataka Kuweka Contradict au lah. Kwa Maana hiyo na Kuacha Uendelee tuone Unachotaka Kufanya Kama utafika hapo tutajadili

Kibatala: Shahidi Tuendelee, Umepaona sehemu Unayosema Kwamba Freeman Mbowe alikuwa na Nia ovu

Shahidi: Ndiyo Kama alikuwa na Cunduct yake, angefika kituo cha Polisi.

Kibatala: Ni Sheria gani inayo mlazimisha Mbowe Kufika Kituoni Personally yeye Mwenyewe Kumtafuta Bwire Kituoni

Shahidi: Hakuna Sheria.

Kibatala: Ili Freeman Mbowe aweze Kufika Kituo Cha Polisi, Mbowe lazima awe na Information, Je Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Mlimpa Simu Khalfani Bwire Kuongea na Mke, ndugu na Jamaa

Shahidi: Sikueleza, Ila Ilikuwa inafahamika.

Kibatala: Hiyo Inafahamika na nani

Shahidi: Inafahamika Kwa Mke wake Siku tunaenda Nyumbani Kwake Kumpekua

Kibatala: Kwa hiyo Mke wake Khalfani Bwire akifahamu ndiyo Freeman Mbowe anafahamu, Je ulichunguza Ukakuta wanafahamiana

Shahidi: Sikuchunguza hilo

Kibatala: Je unafahamu Kwamba kabla ya Commital, Khalfani Bwire alikuwa na Uwakilishi Wa Mawakili Kwa Maelekezo Ya Freeman Mbowe

Shahidi: Sifahamu hilo.

Kibatala: Je Freeman Mbowe akitoa Maelekezo ya Wakili Waende Kuwakilisha Khalfani Bwire Mahakamani, Je atakuwa hajashiriki?

Shahidi: Siwezi Kujibu swali hilo

Kibatala: huwezi sababu hutaki au hujui

Shahidi: Rudia Swali

Kibatala: Kwanza Wewe umeandika Maelezo umeandika Tarehe 06 August 2021, na hapa Kwenye Commital pana onyesha Mawakili Walikwepo kwa Maelekezo Ya Mbowe

Shahidi: Sifahamu hilo.

Kibatala: Unafahamu Kwamba Siku Watuhumiwa Wanafikishwa Mahakamani, Mlikuwa Mnasema Upelelezi haujakamilika

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Ni wewe Katika Ushahidi Wako Ulisema Uliwapeleka Watuhumiwa Kisutu

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Je Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba ulipoteza Interest kiasi Kwamba huwezi Kujua Mawakili Waliokuwa Wana wawakilisha Washtakiwa

Shahidi: Kwa akili yako naweza Kusema Neno Kama hilo kweli, Kwamba Nimepoteza interest?

Mahakama: Hhahhhaa

Kibatala: Wewe ndiye Uliye Sema Kwamba wewe ndiyo Ulishiriki Kuwaachia akina Gabriel Muhina na Khalid

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Nitaishia hapo, Naiachia Mahakama

Kibatala: Je Shahidi Freeman Mbowe inamaana alikuwa Chini ya Uangalizi Kabla ya Kukamatwa

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Je Wakati Mnamfuatilia Freeman Mbowe Ulikuwa Unafahamu anaambatana na akina nani

Shahidi: Sifahamu Nilicho ambiwa, na Ramadhan Kingai, Kwamba Mtuhumiwa namba 4 anafuatiliwa Kwa Karibu

Kibatala: Katika Ushahidi Wako Ulisema Kwamba Mlimtafuta Khalfani Bwire Sinza na Coco beach

Shahidi: Sahihi

Kibatala: Sasa Je Uliwahi Kugundua kuwa huyu Mliyekuwa Mnamtafuta Sinza na Coco beach alikuwa na kazi ya Kumlinda Mbowe, na alikuwa katika Jukumu la Kumpokea Tundu Lissu.

Shahidi: Ilikuwa haifahamiki

Kibatala: Na katika Maelezo yako Umesema Kwamba Siku Mnamkamata Khalfani Bwire alikuwa anatokea Kazini kwake, Kwa Mbowe

Shahidi: Ndiyo nimeandika

Kibatala: Kwamba Siku anakamatwa alikuwa anatokea Wapi

Shahidi: Kazini Kwake.

Kibatala: kazini Kwake Kwa nani?

Shahidi: kazini Kwake Kwa Freeman Aikael Mbowe

Kibatala: Luteni Denis Urio Mtoa Taarifa wenu anasema Kwamba alimpatia Ramadhan Kingai Nambari za Simu Mshtakiwa Wa Kwanza, Wa pili na watatu, Je Uliwahi Kufahamu Uwepo wa namba za Simu

Shahidi: Katika Maelezo Yake Denis Urio alitaja Namba za Simu za Watuhumiwa Wawili ndizo alizo Mpatia Afande Ramadhan Kingai

Kibatala: Na Kwamba Katika Simu Zao na Maelezo Yao ya Onyo Hakuna Mahala ambapo Walikuwa wametaja Namba za Khalfani Bwire (Mshitakiwa Wa kwanza).

Shahidi: Sikumbuki Kama wametaja

Kibatala: Unafahamu Kufanya Triangulation ya Namba za Simu Ili Kujua Mtuhumiwa Yupo sehemu gani

Shahidi: Fafanua

Kibatala: Ni neno la Kiupelelezi ni fafanue Nini, Kufanya Triangulation Ni Kutumia Nambari ya Simu Kutaka Kujua Mtuhumiwa Yupo Eneo gani

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Katika kumfuatilia Freeman Mbowe kama Suspect Wa Ufadhili Wa Ugaidi, Je Mlikuwa Mnamfuatilia Freeman Mbowe Movement Zake za Ndani na Nje ya Nchi

Shahidi: Nilikuwa sifuatilii, Ramadhan Kingai alisema Yeye anafanya hivyo.

Kibatala: Je unafahamu Kwamba Baada ya Uchaguzi, Mtuhumiwa Freeman Mbowe alikamatwa yeye, Godbless Lema nEx Mayor Boniface Jacob, Walipewa Kufichwa Sehemu Mbali Mbali Ikiwemo Bagamoyo, na Pale Oysterbay Walipewa Dhamana

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Pia ufahamu Kwamba Baada ya Kupewa Dhamana alikuwa ana Riport Ofisi Ya RCO Oysterbay Mara kwa mara

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Pi ufahamu Kwa Utaratibu huo Huo Jeshi La Polisi Lilimruhusu kusafiri Kwenda Nje ya Nchi

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Na Pia ufahamu Kwamba alirejea Tanzania kama Mwanachi anaye tii Sheria

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Je Ulifahamu Logic ya Swali la Wakili John Malya alipokuuliza Kuhusu Rais Samia Suluhu Hassan Kwamba Mbowe alikimbia Nje ya Nchi baada ya Kutafuta Siku Nyingi kuja Kujibu tuhuma zake

Shahidi: Nilikuwa Sifahamu

Kibatala: lakini wewe Kama Mpelelezi uliye tunukiwa na DCI, lakini hujawahi Kutoa Taarifa kwa Wakubwa zako Kwamba Mtuhumiwa ambaye nilikuwa nampeleleza amekimbia Nchini

Shahidi: Sijawahi Kutoa Taarifa hizo.

Kibatala: Katika Jalada CD /IR/ 2097 /2020 Uliwahi Kuona Taarifa Kuwa Mtuhumiwa Freeman Mbowe ametoroka Nchini Katika Jalada hilo

Shahidi: Sikuwahi Kuona.

Kibatala: Twende kwa Washtakiwa ambao Umewaleta wewe Mwenyewe, Je Washtakiwa Gabriel Muhina na Khalid Walifanya nini Mpaka Wawe Kwenye Kesi

Shahidi: Sikuwahi Kufahamu

Kibatala: Ulishawahi Kujulishwa Kuwa kwanini Wapo Kwenye kesi.

Shahidi: Ramadhan Kingai aliniambia Kuna Taarifa Za Ki Intelijensia zinazosema kuwa ni Wahalifu

Kibatala: Wewe Kwenye Faili uliona Jambo lolote ambalo lilikuwa linawahusu Watuhumiwa Wale

Shahidi: Sijawahi Kuona Jambo lolote Katika Jalada Kuhusu Wale Watuhumiwa.

Kibatala: Je Walikaa Muda gani Vile

Shahidi: Mwaka Mmoja

Kibatala: Freeman Mbowe amemaliza Mwaka Mmoja

Shahidi: Hapana

Kibatala: Nikisema huenda baada ya Mwaka Mmoja pia Mtaona hana Hatia nitakuwa nawaonea. Je Luteni Denis Urio alishawahi Kuwaambia Kuhusu Gabriel Muhina na Khalid

Shahidi: Hapana

Shahidi: Ya Dar es Salaam au Moshi?

Kibatala: Wewe unaona Ipiga Kengele Katika Kesi hii

Shahidi: Keys Hotel Moshi

Kibatala: bila Shaka Sababu ya Kaaya

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Je Ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kwamba Kaaya alikwambia Lolote Kuhusu Keys Hotel

Shahidi: Hapana Siku Mwambia

Kibatala: Kaaya alikwambia Kuhusu Uwanja wa Mpira Longido

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Kuna Mahala Popote Umemwambia Mheshimiwa Jaji Kuhusu Kaaya Kumukueleza Mambo ya Uwanja wa Longido

Shahidi: Sikueleza

Kibatala: Je Katika Maelezo...

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Tunapinga Swali hilo

Kibatala: Hapa Mahakamani ulitoa ushahidi Kwamba Baada ya Kupokea Simu 8 kutoka Forensic Beaural ukazikabidh kwa Askari Polisi anaitwa Charles

Shahidi: Sahihi

Kibatala: Wakati una kabidhiwa Simu hizo Nane, Uliwahi Kufafanukiwa kwanini Kuna simu Moja a ilikuwa na Chaji Baada ya Mwaka Mmoja na Nusu

Shahidi: Hapana

Kibatala: Wewe Binafsi Uliwahi Kufahamu Kwanini Simu hiyo ikiwa na Chaji kwa Zaidi ya Miaka Miwili Tangu Ichukuliwe Kutoka Kwa Luten Denis Urio

Shahidi: Nilikuwa Sifahamu Kwa sababu zilikuwa zimefungwa

Kibatala: Je Uliwahi Kumfahamisha Kwamba Simu namba P28 iliwahi kugoma Kuwaka Hapa Mahakamani, pamoja na Jitihada Kubwa za Denis Urio

Shahidi: Sikuwahi Kufahamishwa

Kibatala: Lakini Hukuwahi Kuambiwa Kuwa kuwa Kuna simu moja iligoma kuwaka

Shahidi: Sikuwahi Kuambiwa

Kibatala: Tarehe 10 August 2020 Ulimpigia Simu Luteni Denis Urio

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Jeshi la Polisi lilimuwezesha Kuja Dar es Salaam

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Tarehe 11 ulimuagiza alete tena Simu zingine, Je Umuwezesha Kwenda Morogoro Kufuata Simu

Shahidi: Sifahamu.

Kibatala: Je Polisi fomu 145 zinatakiwa zibandikwe Muda gani

Shahidi: Ni Muda wowote tuh Unapo weka labeling

Kibatala: Matumizi ya Polisi Fomu 145 unayafahamu

Shahidi: Naya fahamu

Kibatala: Yameelezwa na Sheria gani

Shahidi: Kimyaaaaaaa

Kibatala: Ni PGO

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Unakumbuka PGO ipi.?

Shahidi: Sikumbuki

Kibatala: Nilisikia Kwamba hukubandika Polisi Fomu 145 kwa sababu palikuwa na uhaba wa fomu pale Ofisini

Shahidi: Siyo uhaba, Palikuwa Hakuna fomu Ofisini

Kibatala: Je Ulifafanua kwa Jaji kwanini hukumruhusu Luteni Denis Urio aende na Simu Zake, Ukipata Polisi fomu 145 Tarehe 13 August 2020

Shahidi: Siku fafanua kwa sababu Hapakuwa na Umuhimu

Kibatala: Shahidi Unafahamu Pamoja na Sheria na Kanuni, kazi za Polisi Pamoja na Wewe Kama Polisi Mnaongozwa na Hii Criminal Procedure Act

Shahidi: Ndiyo pamoja na Miongozo Mingine

Kibatala: Je Unafahamu Kwamba Criminal Procedure Act ina Vifungu vinavyoruhusu Utendwaji wa Kosa

Shahidi: Sikumbuki

Kibatala: Kwa hiyo Ukumbuki hata sehemu inayosema Kwamba unaweza Kutoa Taarifa Kuhusu Utendaji Wa Kosa siyo tuh Kwa Afisa wa Polisi Bali Kwa Mtu yoyote Mwenye Mamlaka

Shahidi: Ni sahihi nakumbuka.

Kibatala: Kwahiyo Mwenyekiti Wa Serikali ya Mtaa ni Mtu Mwenye Mamlaka kwa Tafsiri hii

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Mkuu wa Kambi ya Jeshi ni Mtu Mwenye Mamlaka kwa Mujibu Wa Sheria hii

Shahidi: Sahihi

Kibatala: Mheshimiwa sasa naomba Nipewe P1 na P13.

Kibatala: Sasa, umezungumzia Kuhusu Mipango Ya Kulipua Vituo Vya Mafuta ambapo ilikuwa utekelezwe Watuhumiwa Wanne, Ambapo Foot soldiers ni Watuhumiwa Watatu, Sasa Kwakuwa wewe Ulikuwa ni Mpelelezi, Je Unaweza Kumwambia Mheshimiwa Jaji ni Kazi ipi Maaalum ilikuwa ifanywe na Khalfani Bwire Binafsi katika Kulipua hivyo Vituo Vya Mafuta

Shahidi: alikuwa ana Kidaftari Cha Michoro ya Vituo Vya Mafuta, Alikuwa alipue Vituo Vyote

Kibatala: Wewe Umeyatoa Wapi

Shahidi: Katika Maelezo Ya Watuhumiwa Wote

Kibatala: Nitafutie Sasa Katika Maelezo Ya Adam Kasekwa anapo Sema Kwamba Khalfani Bwire alikuwa alipue Vituo Vyote, Tafadhali

- Shahidi ANAPEKUA

Shahidi: Mnamo Tarehe 1 August 2020 Muda wa Saa 11 alituita na Kutuelekeza Kuwa tukatekeleza Maelekezo Ya Kwenda Kumdhuru Mkuu wa Wilaya Lengai Ole Sabaya, pia alituelekeza Kuwa anapenda Kutembelea Club Kubwa za Kokoriko na Mile Stone Pia Tulirudi Dar es Salaam kulipua Vituo Vya Mafuta na Mikisunyiko

Kibatala: Sasa hapo Kwa Maelezo hayo ndiyo Khalfani Bwire katajwa anaenda Kulipua Vituo Vya Mafuta

Shahidi: Ndiyo Nime Jibu

Kibatala: Nimekuuliza What is Individual Role, ya Khalfani Bwire, Kwamba Wewe Ukasema Khalfani Bwire alikuwa alipue Vituo Vyote

Shahidi: Hilo ndilo Jibu sahihi sasa, Uliza lingine

Kibatala: Unapokuwa unataka Kulipua Kila Mtu anafanya Kazi fulani, Twende Kwa Mshtakiwa Wa Pili alikuwa na Jukumu lipi

Shahidi: kazi ilikuwa haijakamilika, Ilikuwa ni Mipango

Kibatala: Ndiyo sasa wewe Kama Mpelelezi, Uligundua Mshitakiwa Wa Pili alikuwa na Jukumu gani?

Kibatala: Majambazi wakivamia Benki Kuna Mtu ataenda Kwenye Safe, Mwingine atashika Risasi na Mwingine ataweka watu Chini, Sasa Adam Kasekwa alikamatwa kuwa na Jukumu gani Katika Kulipua

Shahidi: Katika Maelezo Yao hawajaeleza hayo

Kibatala: Je Katika Maelezo hayo, Wame eleza Mohammed Ling'wenya alikuwa na Jukumu gani Katika Kulipua

Shahidi: Ni Kulipua.

Kibatala: Kibatala Ni sahihi Shahidi Kwamba Katika Maelezo Uliyo ya Shika Ya Adamoo anasema "Baada ya Kufika Dar es Salaam na Kumfikisha Mheshimiwa Mikocheni" Umeona hiyo Sehemu?

Shahidi: NIMEPAONA

Kibatala: Pasome sasa

Shahidi: Baada ya Kufika Dar es Salaam na Kumfikisha Mheshimiwa Nyumbani Mikocheni Mimi na Mohamed tulipewa TSh 200,000 kwa ajili ya Kujiandaa Kwa Mavazi, Kwani Kesho Yake Tundu Lissu ndiyo alikuwa anakuja na Kumpokea Uwanja wa Ndege, Baada ya Kumpokea Tundu Lissu tulibakia Dar es Salaam Mpaka Tarehe 31 July 2020

Kibatala: Sasa Wewe Kama Mpelelezi Ulithibitisha hayo Katika Upelelezi kuwa Wali rudi Dar es Salaam

Shahidi: Nilithibitisha Kupitia Maelezo Yao

Kibatala: Ulithibitisha baada ya Kumpokea Tundu Lissu, Waliendelea Kutoa huduma Mpaka Tarehe 31 July 2020

Shahidi: Waliendelea Kushiriki Vitendo Vya Uhalifu

Kibatala: Soma hayo Maelezo sehemu ambayo baada ya Tarehe 27 na Kabla ya 31 july 2020 Kama Walifanya Matendo ya Kigaidi.

Shahidi: Walikuwa Wameshakula Njama na Kushiriki Vitendo Vya Kigaidi

Jaji: Elewa Swali, Swali ni Kilichofanyika Kati ya Tarehe 27 na 31 July 2020

- Shahidi ANAPEKUA, ANASOMA SEHEMU TOFAUTI

Kibatala: Nataka wakiwa hapa Dar es Salaam kati ya Tarehe 27 na Tarehe 31 July 2020

Shahidi: ukitaka nijibu hivyo huwezi Kupata, Kwa Maana ambayo unataka Hakuna Maneno Hayo, Kwa Maana ya Maneno yote Ukisoma utaona tu..

Mahakama yote: Hhahhaha

Kibatala: Twende Kwenye Maelezo ya Mohammed Ling'wenya, Pale inaposema "Baada ya Mazungumzo Yetu Mheshimiwa Mbowe... "
Shuka Mpaka Sehemu Mh Mbowe alikuwa ana Kunywa Bia aina ya Kilimanjaro, Je umepaona hiyo Sehemu

Shahidi: NIMEPAONA

Kibatala: Anza pale katika Maongezi yetu

Shahidi: Katika Maongezi yetu Mheshimiwa Mbowe Alianza Kwa Kuuliza Kama Siasa tunaijua, tuka Mwambia sisi siasa hatujui, akatueleza Kwamba Katika Jimbo lake la Hai, Vijana Wale wanapigwa na wengine Wanatukanwa, Mheshimiwa Mbowe Alisema Kwamba alishawahi Kufikisha Malalamiko Mpaka kesho Rais, pia IGP Alishampatia Taarifa, akasema Kwamba atalifuatilia hilo"

Kibatala: Je wewe Kama Mpelelezi Ulithibitisha hilo Kwamba sehemu ya Mazungumzo Yao palikuwa na Mazungmzo ya siasa

Shahidi: Katika Maelezo Yao Nilithibitisha

Kibatala: Na anasema Kwamba Mheshimiwa Mbowe ansema Kwamba Watu wake Wanapigwa na Yeye Mbowe anatukanwa Je wewe Kama Mpelelezi Ulithibitisha walichosema

Shahidi: Nilitumia Maelezo

Kibatala: Maelezo yanasema Kwamba Mbowe alimwambia Mohammed Ling'wenya Kwamba Mbowe alifikishwa Malalamiko Polisi Kwa IGP ambaye ni Boss Wako, Je Uliwahi Kuthibitisha Kwa IGP Kama aliwahi Kupokea Malalamiko Yake Dhidi Ya Sabaya

Shahidi: Hapana

Kibatala: Nenda tena Katika Sehemu Imeandikwa Kesho yake

Shahidi: Kesho yake baada ya Kuamka , Muda wa Saa 2 Asubuhi, Dar es Salaam tulifika Saa 4 Usiku, Mheshimiwa Mbowe alituita Ndani Kwake, Mheshimiwa Mbowe akaanza Kutuambia Kuhusu Malipo yetu kwa Mwezi Kwamba tutalipwa.

Shahidi: TSh 300,000, na Mheshimiwa Mbowe alitupatia TSh 200,000 kila Mmoja Kwa ajili ya a kwenda Kununua Mavazi, Kesho yake tulikuwa tunaenda Kumpokea Tundu Lissu, Kesho yake Tarehe 27 Tulielekea airport Kumpokea Mheshimiwa Tundu Lissu.

Shahidi: Ambapo Mheshimiwa Mbowe na Khalfani Bwire Binafsi walikuwa katika Gari yake Nyeusi....

Kibatala: Inatosha hapo, Nina Maswali Kadhaaa

Shahidi: MHESHIMIWA JAJI NAOMBA NIENDE WASHROOM (CHOONI)

Kibatala: Ni sahihi Sasa Kwa Mujibu Wa Maelezo Hayo, Kwenye Tarehe Ambayo Mohammed Ling'wenya anasema Walikutana Kwa Mbowe Dar es Salaam na content ilikuwa ni Kuhusu Malipo kwa Mwezi na Malipo ni TSh 300,000, Je ni kweli Ulithibitisha Kwamba Majadiliano hayo Yalifanyika.

Shahidi: Kwa Mujibu Wa Maelezo ndiyo Ilivyo, Ni sahihi

Kibatala: Ni sahihi pia Shahidi Kwa Mujibu wa Maelezo hayo Mbowe akimuachia Maswala ya Kuhusu Mishahara Kwa Katibu wake na Mbowe ambaye Ling'wenya anasema hamjui Kwa Jina, Je ni sahihi

Shahidi: Rudia hapo

Kibatala: Ngoja nisome, Tulikubaliana Malipo ya Mshahara itakuwa TSh 300,000, Ambapo Mbowe alimkabidhi Majukumu hayo Katibu wake.

Kibatala: Ni sahihi Kwamba Kasekwa na Mohamed Ling'wenya walienda Airport Walitokea Ofisi za Chadema

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Ni sahihi Kwamba Baada ya Kutoka Airport walirejea Ofisi CA Chadema ambapo Palikuwa na Kikao Mpaka Saa 2 Usiku

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Je Ulithibitisha Kwamba Kakobe na a Katibu walienda Kutafuta Suruali za Kaki kama kombati, Mabuti, Suti

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Je ni sahihi Kwamba Suruali za Kaki kama kombati ni Vazi Rasmi la Chadema

Shahidi: Kimyaaaaaaaaaa

Kibatala: Je ni sahihi Kwamba Mohammed Ling'wenya anasema kama alivyosema Adam Kasekwa Walifika Dar es Salaam kuanzia Tarehe 27 Mpaka Tarehe 31 July 2020

Shahidi: Ni sahihi.

Kibatala: Swali la mwisho kwako. Je, wewe kama Mpelelezi tangu kesi hii ifunguliwe imeshawahi kuwa na washtakiwa saba?

Shahidi: Sahihi

Kibatala: Je, kuna mshtakiwa yeyote ambaye ameshawahi kuhukumiwa kifungo katika kesi hii?

Shahidi: Hakuna mshtakiwa ambaye amehukumiwa kifungo.

Kibatala: Mheshimiwa Jaji Sina Swali lingine kwa shahidi huyu. Naomba Kurudisha Vielelezo Vyote

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji nitaanza Mimi na Baadae atakuja wakili Mwenzangu. Mheshimiwa Jaji naomba Kupatiwa Kielelezo P1 na P 13.

Wakili wa Serikali: Shahidi Uliulizwa Maswali Kadhaa Kuhusiana na Maelezo Ya Onyo ya Adam Kasekwa na Mohamed Ling'wenya. Kielelezo namba 13 katika Maelezo Ya Mohammed Ling'wenya Kuna eneo Mahususi Kuhusiana na Swala la Ulipuaji wa Visima Vya Mafuta kama. Kielelezo namba P1 Samahani siyo 13 hasa katika Maelezo yanayo anzia Muda wa Saa 10

Shahidi: Nimepata

Wakili wa Serikali: Katika Eneo hilo alikuuliza Majukumu Yapo Mahususi ambayo Mshitakiwa Wa kwanza ameyafanya katika Kulipua Vituo Vya Mafuta, wewe Ukasema Mpaka Usome yote ndiyo utajua Majukumu, Sasa pitia Kwanza Maelezo.

Shahidi: Nimeona

Wakili wa Serikali: Kwanini Ulisema Kwa Mujibu wa Eneo alikuwa halipui Visima Vyote

Shahidi: Kwenye Maelezo hapa Imeandikwa ikishakamilika, alituelekeza Kurudi Dar es Salaam Kwa ajili ya Kufanya Kazi Nyingine. Nyeti ya Kulipua Vituo Vyote Vya Mafuta, Na Kwamba na Yeye alikuwa katika Njama ya Kulipua Vituo Vya Mafuta, Nilikuwa namaanisha hivyo kutokana hilo Eneo

Wakili wa Serikali: Katika Maelezo hayo Uliulizwa Majukumu Mahususi ambayo Adam Kasekwa Aliya fanya, Ukasema hayajaelezwa
Ni kwanini Ulisema hivyo?

Shahidi: Kwa sababu Vituo Vya Mafuta ni Vya Dar es Salaam, na Ukisoma Utaona Kuwa Ni Kulipua Vituo Vya Mafuta Dar es Salaam

Wakili wa Serikali: Pia alikurejea Katika Kielelezo namba 13 ambayo ni Maelezo Ya Mohammed Ling'wenya. Umeulizwa Maswali hapo ili husiana na Maongezi Ya Mshahara, na Kwamba Maelekezo sasa ya Kukamilisha, Majukumu aliachiwa Katibu wake ambaye alisema hamjui Kwa Jina, Je eneo hilo umeliona

Shahidi: Ndiyo nimeona

Wakili wa Serikali: Ukasema Jambo hilo halikutekelezwa, Kwanini Ulisema hivyo?

Shahidi: Ukija Kusoma Mbele Utaona Tulikuwa tunasubiria Mahitaji yetu, Kwahiyo Hilo Swala haikuwepo, na wao Walikuwa wanatumia kama Wahalifu Baada ya Kushawishiwa.

Wakili wa Serikali: Pia katika Kielelezo hicho hicho namba 13, ila ili Nikuulize Swali Soma Kipande hiki

Shahidi: Watu wake Mheshimiwa Mbowe Wanapigwa na Yeye anatukanwa na Vijana Wa Sabaya, alishawahi Kufikisha Malalamiko Yake Mpaka Kwa Mheshimiwa Rais, pia aliwahi Kufikisha kwa IGP

Wakili wa Serikali: Ukasema Lakini Wewe hukuthibisha

Shahidi: Kwa sababu hili Tukio lilikuwa hakijaripotiwa, na Mimi nilikuwa si husiki Kupeleleza hilo

Wakili wa Serikali: Wakati Unaulizwa Kuhusu Zile PF 145 hususani zile ambazo Ukijaza Tarehe 13 ambapo Ulipokea Tarehe 12, Ukaulizwa Kwamba Kwanini Ukijaza Tarehe 13 na Hukumuita Tena Luteni Denis Urio wakati Unajaza tena, Ukasema Hapakuwa na Umuhimu

Shahidi: Ni Kwa sababu tulishajaza Hati ya Makabidhiano, na Wakati Wa Kujaza hiyo PF 145 Hawajibiki Kuwepo, inajazwa na Askari

Wakili wa Serikali: Uliulizwa Kama Ulifanya Upelelezi Wowote Kuhusu Keys Hotel Moshi, Ukasema hakuwa na Umuhimu

Shahidi: Ni Kwa sababu yeye alienda Keys Hotel Kumsubiria Freeman Mbowe, na Baada ya Pale ndiyo Walienda Aishi Hotel ambapo Kule alimkabidhi Majina ya Watu wa Sabaya.

Kibatala: Mheshimiwa Jaji tunaona angeishia Aishi Hotel, lakini naona wanaenda Overboard

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji sisi Hatuoni ni Jambo Jipya, Sisi tunaona Majibu haya ni Valid kwa Shahidi Wetu Kuzungumzia

Jaji: Mr. Kibatala nitakupa Muda wa Kufanya tena Cross examination tena

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Basi Mheshimiwa Jaji naomba tuishie pale, Mwisho Aishi Hotel, Bila Kusema kilichijiri kule Kupunguza Mlolongo.

Wakili wa Serikali: Shahidi Ulikuwa pia Unaulizwa katika Nafasi yako kama Mpelelezi, Kama Unafahamu Kwamba Mshitakiwa Namba Nne aliwahi Kutoroka Nchini, Wewe Ukasema Kuwa halikuwa Jukumu lako, Je ni Kwanini Ulisema hivyo.

Shahidi: Nilisema hivyo Kwa sababu Taarifa za Kufuatiliwa Mwenendo Wako Mtuhumiwa Namba Nne Freeman Mbowe, nilijulishwa na Afande Ramadhan Kingai, Bila Kuniambia nani anaye fuatilia. Na niliposema pia Hapakuwa na Taarifa Zozote za Mtuhumiwa Namba Nne, Ni kweli Sikujulishwa hizo Taarifa Wala sikusikia

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji naomba airisho Fupi ili tukirudi tuweze Kuendelea na Re:examination

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji hatuna Pingamizi, Mallya alikuwa anatania kuwa nisiombe Jaji amlinde Shahidi

Jaji: basi tunapata airisho Mpaka Saa 7 na Dakika 45

- Jaji anatoka

MAPUMZIKO MAFUPI MPAKA SAA 7:45
- Jaji amerejea Mahakamani

Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa tena Muda huu

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji upande wa Jamhuri Quorum yetu ipo Kama ambavyo tulikuwa kabla ya Kuhairisha

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji na sisi Pia Quorum yetu ipo Kama ambavyo ilikuwa kabla ya Break na tupo tayari Kuendelea

Jaji: Karibu tuendelee

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Shahidi Uliulizwa Maswali Kadhaa Kuhusiana na Vile Vituo Vya Mafuta Ulivyo enda Kuvitembelea Kwa Maana ya Big Bon Kariakoo, Puma Sinza na Puma Kilwa Road. Sasa Uliulizwa swali Kuhusiana na Details ambazo umezitoa Mahakamani, Ukasema Umezitoa kwa Maana Ulifahamu Maana ya Details. Ukaulizwa Details za Plot namba, Mmiliki na Makutano ya Barabara Ukasema Siyo lazima ziwepo Katika Maelezo yako.

Shahidi: Ndiyo Nilisema Kwamba Siyi lazima kwa sababu Mimi Nimekuja Mahakamani, Nimeapa na Nilieleza Maelezo Yangu

Wakili wa Serikali: Ulijibu swali Kwamba hukuweka hizo Details lakini Details hizo Umetoa hapa Mahakamani, Ni Kwanini Umetoa Details Mahakamani na Hukuweka kwenye Maelezo yako

Shahidi: Ili Mahakama iweze Kuelewa Zaidi, Ni Maeneo gani yaliyo kuwa yanepangwa Kufanyiwa Vitendo Vya Uhalifu

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba kwa Mara Nyingine tupatiwe Kielelezo namba 1 na Kielelezo namba 13 Inspector Swila Uliulizwa Maswali hukusiana na Mtu Mmoja anaitwa Justine Kaaya Kuhusu Kushiriki Vikao Vya Kigaidi, Ukasema ni kweli alishiriki Bila yeye Kufahamu Lengo la Kikao ila Mshtakiwa alifahamu lengo la Kikao, Ni Kwanini

Shahidi: Nilikuwa namaanisha Kwamba Wakati Mshtakiwa Namba 4 anaomba Majina Ya Watu Wanaofuatana na Ole Sabaya, alikuwa anajua Lengo la Kupata Vitu hivyo ni Kufanya Vitendo Vya Kigaidi, Wakati Kaaya anatoa Vitu hivyo hakujua Lengo la Mshtakiwa namba 4 ni Lipi?

Wakili wa Serikali: Pia Uliulizwa Maswali hapa na Wakili Nashon Nkungu, Kama ni Kosa Kama ilivyojitokeza kwa Luten Denis Urio Kumtafutia Mtu Watu wa Kufanya Vitendo Vya Ugaidi, Ukasema Inategemea, Eleza hapo.

Shahidi: Nilikuwa namaanisha Kwamba haitakuwa Kosa Kama Utakuwa Unamtafutia huyo Mtu Kwa Lengo Kusaidia Vyombo husika

Wakili Nashon Nkungu: Mheshimiwa Jaji nilicho Uliza ni Kama Lilikuwa ni Kosa kwa Shahidi Denis Urio Kukubali Mpango Wa Ugaidi Siyo Kwenda Kufuta.

Shahidi: Niliposema Inategemea Inaweza Kuwa Kosa au Siyo Kosa, Nilikuwa namaanisha Kuwa Kama atatafuta watu hao Kwa Lengo la Kuzia Uhalifu na na Kushirikiana na Jeshi la Polisi na Vyombo Vya Ulinzi (Jeshi la Polisi) haitakuwa Kosa, na Uhalifu huo Umezuiwa kwa walengwa Kukamatwa na Kufikishiwa Mahakamani

Wakili wa Serikali: Umeulizwa Maswali Kadhaa Kuhusiana na Taarifa Aliyotoa Luteni Denis Urio Kwa DCI Kwamba awe anatoa Taarifa Kwa Kingai na Denis Urio alitoa Taarifa Kwa Kingai Kwamba Tarehe 18 July Mpaka Tarehe 04 August 2020 Ukasema Haku kuwa na
Ufutailiaji Bado. Ulimaanisha nini

Shahidi: Nilimaanisha Kwamba Taarifa ambazo Luteni Denis Urio ambazo alipewa na Mshtakiwa Namba 4 alikuwa bado ajaanza Kufanyia Kazi, Mpaka Tarehe 4 alipoanza Kuwasiliana na Mtuhumiwa Namba 1 nilimaanisha Kwamba Taarifa ambazo Luteni Denis Urio ambazo alipewa na Mshtakiwa Namba 4 alikuwa bado ajaanza Kufanyia Kazi, Mpaka Tarehe 4 alipo Anza Kuwasiliana na Mtuhumiwa Namba 1, Na wakati Wanawasiliana nao.

Wakili wa Serikali: Bado Ujaulizwa Swali

Wakili wa Serikali: Pia Uliulizwa Swali Kuhusiana na Hati ya Makabidhiano Baina yako na Denis Urio Tarehe 11 August 2020, Je Ile fomu Jinsi Ilivyo Ulionyeshwa hapa Ukasema Fomu ile Haionyeshi Kama Denis Urio ni Shahidi

Shahidi: Nilieleza hivyo Kwa sababu fomu ile huwa tunatumia Askari Tunapokabidhiana Vielelezo. Nilitumia fomu hiyo Kwa Luten Denis Urio Kwa sababu yeye ni Shahidi, Niliweza Kusaini Katika Fomu hiyo na Yeye akasaini

Wakili wa Serikali: Shahidi Inspector Swila Uliulizwa hapa Maswali Kuhusiana na Vifaa Vya Mshitakiwa Wa Nne ambazo ni Simu na Computer Kadhaa, Ukasema Kwamba Ulipeleka Katika Maabara Ya Uchunguzi Na Siku Ile Mbayo Ulianza Kutoa Ushahidi Wako ndiyo Uchunguzi Wake Ulikuwa Umekamilika.

Shahidi: Nilikuwa Namaanisha Kwamba Upelelezi Wa Shauri hili Umekamilika tangu Tarehe 18 July 2021, Kuhusu Tarehe ya Juiz Kuhusu Uchunguzi Ilikuwa ni Kuhusu Uchunguzi Wa Ziada Wa Vielelezo Vya Mshtakiwa Namba 4 ambao Ulikuwa unafanya Na Maabara Ya Uchunguzi ya Makosa Ya Mtandao.

Wakili wa Serikali: Pia Uliulizwa Maswali hapa kati ya Kipindi cha Tarehe 14 July 2020 Mpaka Mwezi 05 August 2020 Kama Uhalifu Ulikuwa Umeshatendeka, Ukasema Inategemea na Mpango wa Uhalifu Wenyewe.

Shahidi: Nilikuwa namaanisha Kuwa Kama Kikundi Mipango yake ya Kutenda Uhalifu Itakuwa Umekamilika Basi Uhalifu Utafanyika lakini Kama Kikundi haijakamilisha Mipango Yake Yenyewe Ya Kutenda Uhalifu basi Uhalifu Auwezi Kukamilika.

Wakili wa Serikali: Sasa Inspector Swila Uliulizwa Pia Maswali Kuhusiana na Yake Maoni ya Uchunguzi Wa Kisayansi Kwenda Airtel, Kuhusiana na Khalfani Bwire na Freeman Mbowe pamoja na Denis Urio, namba zote tatu ziliombewa Taarifa, Lakini Taarifa zikaja za Denis Urio na Freeman Mbowe lakini Taarifa ya Khalfani Bwire Haipo, Ukasema Ipo Katika Taarifa Ya Mbowe

Shahidi: Katika Uchunguzi Wa Miamala ya Freeman Mbowe Palikuwa pia Pana Taarifa Ya Uchunguzi Ya Miamala Khalfani Bwire Katika Miamala Ya Freeman Mbowe

Wakili wa Serikali: Pia Uliulizwa Maswali hukusiana na Taarifa Uliyopo Katika Kielelezo namba 26 na Maelezo ya Denis Urio. Mulipo Ulizwa Kuhusiana na Kilichopo Ukasema hakutakuwa na Utofauti ya Maudhui, Je Ulimaanisha nini?

Shahidi: Nilikuwa namaanisha Ni Ujumbe Wa Maneno Ulipo Katika Vielelezo hivyo, Kwani ufanyqa na Mtuamaji na Mtumwaji
Ina Onekana Mwisho Katika Taarifa Iliyo andaliwahi na Maabara Ya Uchunguzi Kitengo Cha Makosa ya Mtandao.

Wakili wa Serikali: Uliulizwa Kuhusu Upokelewaji Wa Taarifa Kutoka Kwa Denis Urio na Ukathibitisha akiyepokew Taarifa Kwenye ni DCI wakati huo palikuwa na Deputy DCI Charles Kenyela,Ukaulizwa Kaa Mazingira yake si alitakiwa amuachie Deputy DCI Kuongozwa Upelelezi, Ukasema Si Kweli.

Shahidi: Nilipo Sema Kwamba Afande DCI hakupaswa Kumuachia Deputy DCI Kuendelea na Upelelezi Wa Shauri Hilo, Kwa sababu Taarifa Za Uhalifu Zilitoka Upande Mwingine ambapo zilipokelewa na Afande DCI.

Wakili wa Serikali: Uliulizwa Kuhusu Taarifa Iliyo fika DCI Kuja Kwako Kwamba Ilikuwa ni hear say Ukasema Ndiyo, Ulikuwa na Maana gani

Shahidi: Askari anaye pokea Taarifa anakuwa anafuata Moja Kwa Moja Kutoka Kutoka Kwenye Chanzo, Hiyo haizuii Kufungua Jalada.

Wakili wa Serikali: Uliulizwa pia Kuhusiana Na lini hasa, Licha ya Kuwa Mpojeaji wa Taarifa wa Kwanza, Je ni Lini hasa Ulichukua Maelezo Yake Tarehe 04 October 2020, Ukaulizwa Kwanini Kesi hii isichukuliwe ya Kutungwa.

Shahidi: Siyo Ya Kutunga Kwa sababu Taarifa Ilitolewa, Watuhumiwa Wakakamatwa na Hatimaye Wakafikishwa Mahakamani.

Wakili wa Serikali: Kwamba Wengine Wanasema ni Kulipua Vituo Vya Mafuta na Wengine Wanasema Kuchoma Masoko Katika Maeneo ya Mkusanyiko, Ukasema Kulipua na Kuchoma ni Kitu tofauti na Baadae Ukasema Kulipua na Kuchoma ni Terminology, Je Ulikuwa Unamaanisha nini?

Shahidi: Ni Terminology Watu wanshindwa Kutofautisha lakini haiondoi Lile Kosa la Kutenda Vitendo Vya Kigaidi

Wakili wa Serikali: Uliulizwa Maswali Kadhaa Kuhusiana na Kielelezo namba 4 na namba 5 kwa Maana ya Maganda 2 ya Risasi (Kielelezo Na 4) na Kielelezo namba 5 ni Kielelezo Cha Risasi.

Wakili wa Serikali: Ukaulizwa Kuhusu Kutofautiana Moja anaitwa Luger na Nyingine Jina tofauti
Ukasema Kwa Upande wa Risasi ni tofauti, Je Ulimaanisha Nini

Shahidi: Nilikuwa namaanisha Risasi Siyo Muhimu Kuwa na Utambulisho, hazina Utambulisho ambao ni tofauti

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Napinga kabisa Majibu hayo, Kwamba Risasi hazina Utambulisho tofauti

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji sisi tulisikia hilo, Sijui Kama Upande Kinzani walisikia hilo

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji naomba Kuendelea na Swali Lingine

Wakili wa Serikali: Shahidi Uliulizwa Swali Kuhusiana Na Justin Elia Kaaya, Ukaulizwa Kama Kuna Mfanano Wowote Kati ya Maelezo akiwa Mtuhumiwa na Akiwa Shahidi, Wewe Ukasema hayawezi Kufanana, Kati ya Onyo na Ushahidi, Isipokuwa yale Maelezo ya Msingi

Shahidi: Nilikuwa namaanisha Maelezo Ya Kwanza yalikuwa yanaelezea Kosa, Wakati haya ya Pili ni Shahidi haya Elezei Kosa Lolote

Wakili wa Serikali: Pia Uliulizwa Maswali katika Kielelezo namba 13 ambayo ni Maelezo Ya Onyo Ya Mshtakiwa Mohammed Ling'wenya, Kwamba Katika Maelezo Yake hasa ile Nia ya Kumdhuru Lengai Ole Sabaya Ilikuwa siyo Kuleta Taharuki ila Kushambulia Viongozi Wa Serikali

Shahidi: Nilikuwa namaanisha Kwamba Katika Maelezo Yake Hakusema kwa nia ya Kuleta Taharuki, Lakini Kwa Malengo Yaliyokusidiwa na ambayo Shahidi alieleza Kutoka. Kwa Mshtakiwa Namba 4 Vitendo V a Kumdhuru Kiongozi not Vitendo Vya Kuondoa Amani na Kufanya Nchi Isitawalike

Wakili Peter Kibatala: OBJECTION Mheshimiwa Jaji Samahani Neno Kuondoa Amani tulishawahi Kutaja hapa Mahakamani.

Wakili wa Serikali Robert: Kidando Mheshimiwa Jaji Neno Kuna Ndoa Amani tunalitoa

Wakili wa Serikali: Inspector Swila Kuna Maswali Kadhaa hapa Uliulizwa hasa Kuhusu Mshitakiwa Wa Pili na Watatu pale Morogoro
Kuhusiana na Swala la Kwenda Kwa Freeman Mbowe, katika Maelezo Yao ya Onyo Ya P1 na P13 hawa wote Wanasema Walipoondoka Walienda Moshi Wakati Maelezo Mengine ya Denis Urio Wanasema Walipo ondoa Walienda Dar es Salaam, Uliulizwa Kama Kuna Mgongano Ukasema Hakuna

Shahidi: Ni Kwa sababu Maelezo Yote Lengo ni Kwenda Kukutana na Freeman Mbowe, Maelezo haya Mgongano Wowote Kwa sababu Mtu ambaye Walitakiwa Kukutana naye Walikutana naye Moshi Kama wanavyo eleza Katika Maelezo Yao, Ni Wazi Walikutana na Mshtakiwa Wa kwanza

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji naomba nano Wazi liondoke ni Opinion zake

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Sawa Liondoke

WS: Uliulizwa Maswali Kuhusiana na Kiwango Cha Pesa ambacho Kila Mshitakiwa Anadai Katika Maelezo Yake Ya Onyo alipewa na Luten Denis Urio, Ambapo Adam Kasekwa ansema Walipewa 87,000. Urio anasema aliwapa TSh 199,000. Wakati huo Mohammed Ling'wenya anasema ni TSh 195,000.

Wakili wa Serikali: Ukaulizwa Viwango hivyo Vina fanana Ukasema Vina fanana, Kwanini

Shahidi: Kwa sababu Wote walipokea Pesa kwa Luten Denis Urio na Kila Mtuhumiwa alitoa Maelezo Yake Kwa Hiari Yake. Kwa sababu Pesa ilitumwa na Mtu ambaye alikuwa anajua nia ya Kuwa waleta Watu hao kwake ni Kwa nia ya Kutekeleza Vitendo Vya Kigaidi

Wakili wa Serikali: Uliulizwa Maswali Kuhusiana na Maelezo yale Uliyo Kuandika Denis Urio Kama Kuna Sehemu alikwambia amemwambia Freeman Mbowe asitumie Namba yake atumie ya Wakala au Vijana Wake, Wewe Ukasema Kwamba ikiwa Kwa sababu Ya Kumuweka Karibu, Ukasema Sehemu hiyo Kwenye Maelezo Haipo. Uliulizwa swali Kuhusiana na Kielelezo namba P1 ambayo ni Maelezo Ya Adam Kasekwa ambayo ni IMEI namba Kwa Kulinganisha na Kielelezo namba 23 ambayo ni Riport Kutoka Uchunguzi Wa Kisayansi.

Lakini Ikawa na Utofauti Kwamba Katika Maelezo Ya Onyo palikuwa na Utofauti Wa Namba 3, Wewe Ulisema Katika Maelezo Ya onyo Kipo ila Kwenye Cyber Riport Haipo ila Ukasema haimaanishi Kitu tofauti.

Shahidi: Nilimaanisha SIMU hiyo IMEI ya Kwanza Ipo Katika Maelezo ila Kwenye IMEI ya Pili ndiyo Kuna Utofauti, Kwa hiyo Kukosea Kwa hiyo ya Pili haimaanishi ni Kitu cha pili

Kibatala: Mheshimiwa Jaji naomba Neno Kukosewa ni Ushahidi Mpya anataka Kuingiza Kwa Malango Wa Nyuma

Jaji: Maneno halisi ni Kukosekana

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Ndiyo Mheshimiwa Jaji

Wakili wa Serikali: Inspector Swila Jana Ulionyeshwa Maelezo Ya Onyo Ya Adam Kasekwa Ambapo yeye Anadai Kukamatwa Rau Madukani Saa 5 Asubuhi, Wakati Mtuhumiwa Mwenzake anazungumzia Kukamatwa Saa 7 Mchana, Ukaulizwa Kama huu Utofauti Ulifanyia Kazi, Ukasema Kila Mmoja alisema Kwa Ufahamu wake

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Uliulizwa pia Kiwango Cha Pesa cha TSh 195,000 ambacho Luten Denis Urio aliwapatia Pesa kwa Namna Mbili, Sasa Washitakiwa Wanaongeala Kupewa Pesa Kiwango hicho, Wewe Ukasema ni Hali ya Kawaida, Eleza Kwanini.

Shahidi: Nilikuwa namaanisha Ya Kwamba, Kila Mmoja alitoa Maelezo Kwa Kadri ya Ya Ufahamu wale na Kumbukumbu Zake

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Naomba Kukomea hapa Wenzangu Pia wataendelea

Wakili wa Serikali Pius Hilla: Mheshimiwa Jaji Nina Maswali Machache.

Wakili wa Serikali: Shahidi Kama Unakumbuka Uliulizwa Swali na Wakili Nashon Nkungu, Kuhusiana na OC Forensic Kukaa na Exhibit Na Kuviandaa Kwa ajili ya Uchunguzi, Ukajibu siyo Sahihi Kwamba OC Forensic Ndiye anakaa na Exhibit, Fafanua sasa.

Shahidi: Niliweza Mahakama Kwamba Siyo Sawa Kwamba OC Forensic anakaa na Vielelezo baada ya Kukamatwa, Badala yake Vielelezo vinakaa kwa Mpelelezi aliyekamata baada ya hapo Vitaandakiwa Barua kwenda Kwa OC Forensic

Shahidi: Niliweza Mahakama Kwamba Siyo Sawa Kwamba OC Forensic anakaa na Vielelezo baada ya Kukamatwa, Badala yake Vielelezo vinakaa kwa Mpelelezi aliyekamata baada ya hapo Vitaandakiwa Barua kwenda Kwa OC Forensic.

Wakili wa Serikali: Uliulizwa pia Kuhusiana Na Watuhumiwa Wa Kwanza Mpaka watatu, Kwamba Muda gani Walianza Kuwa na Guilty Mind, Ukasema Pale Walipo Kubali Kushawishiwa.

Shahidi: Mtuhumiwa Wa Kwanza Mpaka Watatu hawakuwa na Taarifa Kuhusu Njama Za Mtuhumiwa namba 4, Mara tuh Baada ya Kukutana Mtuhumiwa Namba 4 ndiyo Walishawishika Kuacha Kutoa Taarifa na Kuamua Kushiriki Katika Vitendo Vya Uhalifu Hali ambayo Ilipelekea Wao Kukamatwa huko Moshi Mtuhumiwa Wa Pili akiwa na Silaha, Walipo hojiwa wakakiri Kula Njama hizo na Kukubali Kufanya Vitendo Vya Uhalifu Ikiwepo Tukio la Kumdhuru Lengai Ole Sabaya ambapo Walikamatwa wakiwa katika Utejelezaji Wa Tukio la Namna hiyo.


Wakili wa Serikali: Uliulizwa Maswali Pia Kuhusiana Na Uhamishoni Wako, Ulijibu Kuwa ni Kwa Mujibu wa Kazi na Ukajibu Siyo Kweli Kwamba Timming Ya Uhamishoni Wako Ilikuwa ni Ya Kimkakati

Shahidi: Nilikuwa na maanisha Kwamba Nilihamishwa kwa Uhamisho wa Kawaida January 2020

Wakili wa Serikali: Uliulizwa Maswali Kuhusiana na Jinsi Afande DCI alivyo na Maslahi binafsi Ukasema Siyo Kweli

Shahidi: Si Kweli Kwamba ana maslahi Binafsi, Afande DCI alipokea Taarifa Kutoka Kwa Mtu Mwingine, Siyo Kweli alikuwa ana Maslahi binafsi.

Wakili wa Serikali: Uliulizwa Kuhusu Register Ya 251/ 2021 Ukasema Register hizo Muhimu Katika Utunzaji wa Vielelezo

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji ninachokumbuka Mimi, Ni Umuhimu Wa Utunzaji wa Register Vituo Vya Polisi.

Jaji: Lakini Hapakuwa na Neno Vituo Vya Polisi, hilo Neno Vituo liondoke

Wakili wa Serikali Pius Hilla: Mheshimiwa Jaji Sasa Mtu akisema Polisi anamaanisha nini, Tutakuwa hayunaisaidia Mahakama Yako na Sababu ya Re Examination Itakuwa haipo

Jaji: Sina hakika Kama Shahidi alitafsiri Vituo, Kuleta Nano Vituo ni Concept Mpya

Wakili wa Serikali Pius Hilla: Mheshimiwa Jaji tunaondoa Nano Vituo

Shahidi: Niliposema Register hizo ni Muhimu kwa Polisi Kwa sababu Inasaidia Kuonyesha Kumbukumbu za Vielelezo Hivyo, na Inaonyesha aliye kabidhi na aliyekabidhiwa, Kama Nilivyo eleza Kwamba Simu Nilikabidhi Kwa koplo Charles na Silaha Kwa Sajenti Nuru.

Wakili Pius Hilla: Uliulizwa Maswali Mengi Kuhusiana Na Ile Miamala, Moja ya eneo Uliulizwa Kila shillingi Iliyotumwa
Majibu yako Ukasema Siyo lazima Ku' trace Kila shillingi Bali ni Knowledge Ya mtumaji.

Shahidi: Nilikuwa namaanisha Kwamba Katika Shauri hili Mtumajinwa Fedha ambaye ni Freeman Mbowe alikuwa anatuma Pesa Kufadhili Vitendo Vya Ugaidi

Wakili wa Serikali Pius Hilla: Mheshimiwa Jaji ya Kwangu naomba niishie hapo niachie Wenzangu

Shahidi: MHESHIMIWA JAJI NAOMBA NIENDE WASHROOM (CHOONI)

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji hatutakuwa na Swali zaidi Kwa Shahidi namba 13, Naomba Kukomea hapo

- Jaji anaandika Kidogo hapa Mahakama Ipo Kimya

Jaji: Shahidi tunakushukuru, Asante Kwa Ushahidi Wako
Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Baada ya Shahidi huyu namba 13 Tumefanya Assessment Ya Kesi Yetu Kwa Maana ya Ushahidi Ambao Umetolewa Mpaka Sasa ni Maoni yetu Kwamba tume' Discharge Burden ambayo tunatakiwa Kisheria hivyo tunaialika Mahakama Yako tukufu Chini ya Kifungu cha 41 (1) cha Sheria Ya Uhujumu Uchumi na Makosa ya Rushwa ya 2019.

Uone Kwamba Washtakiwa Wote Wanne Wanayo kesi Ya Kujibu, Hivyo taratibu za Sheria zifuatwe ili Shauri hili liweze Kuendelea Katika Hatua zinazifuatia za Kuanza Kujitetea. Baada ya Kusema Hayo tunaomba Kufunga Kesi Yetu Kwa Upande Wa Jamhuri. Asante Mheshimiwa Jaji.

Jaji: Kabla Ya Amri ya Kufunga Upande Wa Utetezi Mna chochote Cha Kusema?

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Kuhusu Amri ya Kufunga hapa, hatuna cha Kusema, Tutasema baada ya Amri ya Kufunga

- Jaji anaendele Kuandika

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Kwa Mahakama haizungumzii haya a Maombi tunayo yaomba, Bali Baada ya Kufunga Upande Wa Mashitaka Wanapofunga, Basi Upande Wa Utetezi Wanapata nafasi ya Kufanya Submission Ya NO CASE TO ANSWER.

Kama Mahakama Itatukubalia Kufanya Submission Ya NO CASE TO ANSWER tunaomba Maombi Madogo 2

1. Mahakama tukufu ikipendezwa tunaomba tunapatiwe Mwenendo Wa Kesi Kuanzia Mwanzo Mpaka Sasa

2. Mahakama Itutuhusu tufanye Submission Ya NO CASE TO ANSWER Kwa Wasilisho la Mdomo

WS Pius Hilla: Mhe Jaji Samahani Sijajua Kwa Hatua hii Wakili Peter Kibatala anaweza Kusemea Washitakiwa Wote

Kibatala: Mhe Jaji Haina shida Nimeongea Kwa niaba ya Jopo ila kama Mtaamua Kuwa Kila Mmoja aulizwe haina shida, Utachukua Dakika 10 kufikia Malengo yale yale.

Jaji: Nita uliza Kila Mmoja

WS Pius Hilla: Mhe Jaji Samahani Sijajua Kwa Hatua hii Wakili Peter Kibatala anaweza Kusemea Washitakiwa Wote

Kibatala: Mhe Jaji Haina shida Nimeongea Kwa niaba ya Jopo ila kama Mtaamua Kuwa Kila Mmoja aulizwe haina shida, Utachukua Dakika 10 kufikia Malengo yale yale.

Jaji: Nitauliza Kila Mmoja

NASHON NKUNGU: Mhe Jaji Nimesikia Upande Wa Mashitaka Sisi hatuna Pingamizi Kwa ajili ya Kufunga Ushahidi Wao, Na Mheshimiwa Jaji Tunaomba Ikupendeze Mawasilisho ya NO CASE TO ANSWER tutafanye Kwa njia ya Mdomo, Pia tunaomba tupatiwe Mwenendo Wa Kesi na Kama itabidi na Vielelezo. Ni hayo Kwa niaba ya Mshtakiwa wa kwanza. Mheshimiwa Jaji Kwa niaba ya Mshtakiwa wa Pili Tumesikia Kufungwa kwa kesi ya Jamhuri na hatuna Pingamizi, Naunga Mkono Wakili Wa Mshtakiwa Wa Nne na Mshtakiwa Wa kwanza, Na Ombi lao la Kufanya Wasilisho La No CASE TO ANSWER tufanye Kwa Njia ya Mdomo. Ni hayo tu Kwa niaba ya Mshtakiwa wa Pili..

Wakili Fredrick Kihwelo: Mheshimiwa Jaji Kwa niaba ya Mshtakiwa wa tatu, Pia hatuna Pingamizi Kwa Upande Wa Jamhuri Kufunga Kesi yao, Niungane na Mawakili Wa Upande Wa Utetezi Kwamba tuweze Kupewa Mwenendo wa Kesi na Kufanya Wasilisho Letu Kwa Njia ya Mdomo.

Wakili Fredrick Kihwelo: ni hayo tu Kwa niaba ya Mshtakiwa wa tatu.

- Mahakama ipo Kimyaaaa, Wakati Jaji anaandika, na Kusubiri Kutolewa Uamuzi Mdogo wa iwapo Submission zifanyike kwa Njia ya Mdomo Mahakamani au Maandishi na Kuwasilishwa kwa Msajili wa Mahakama... Tunasubiri!

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Wakati tunaiomba Mahakama Kwenye Kifungu Cha 41 tuliridhia Kwa sababu Mahususi kuwa Mahakama Inaweza Kufanya Maamuzi hayo Tunaporejea Kifungu Cha 41(1) cha Sheria ya Uhujumu Uchumi na Makosa ya Rushwa, Tulikuwa aware na Kifungu cha 293(1) cha CPA kwa Mawakili Wa Utetezi kwa Mazingira ambayo Wameomba hapa Mahakamani. Hivyo Mheshimiwa Jaji, Katika Kuwasilisha Hoja yetu hapo, na Kama Utaona Inafaa Kufanya hivyo Kwa Wasilisho basi tunaomba tufanye Kwa Njia ya Maandishi na tuweze Kuzi Wasilisha hapa Mahakamani

Lakini pia Mheshimiwa Jaji tulikuwa tunaangalia katika Kifungu cha Hoja ya Kwanza cha 41 Trial hii Umechukua Muda Mrefu. Hatujajua Kuwa Nyaraka za Mwenendo wa Kesi zitchukua Muda gani Ukizingatia Umebakia Muda Machache Kuhusu Usilikizwaji Wa Shauri hili.

Jaji: Mpaka leo karani wangu amechapa kurasa 1400 za Kesi hii, sijajua Itakuwa imebakia kurasa ngapi, nafikiri Jana na leo atakuwa amefikisha kurasa kama 1500

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Tulikuwa tunawashawishi wenzetu tukaongee ofisini kwako.

Jaji: Nyie (mashtaka) Mnaonaje

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji hatuna pingamizi la kuteta faragha (Ofisini Kwako)

Jaji: Sawa

- Jaji anatoka Mahakamani, Kuelekea Ofisini Kwake, na Mawakili wa pande zote mbili...

Tunasubiri Uamuzi.

Mawakili wa pande zote mbili wamerejea Mahakamani, Jaji Pia amerejea Mahakamani..

Jaji: basi mahakama baada ya kuwa imejadiliana na mawakili wa pande zote mbili , kwa kuzingatia mazingira ya pande zote mbili kwa kutumia Kifungu cha 40, Mahakama Itapitia yenyewe Kwa ushahidi wa upande wa mashtaka

Kama washtakiwa watakuwa na kesi ya kujibu au hapana siku ya Tarehe 18 february 2022, NATOA AMRI..

- Jaji anatoka!
 
Wa kwanza.

Wananzengo, huu utaratibu wa judge kuandika mwenyewe, ina tija kweli katika kufanikisha usikivu kwa hoja, kuona katikati ya mistari kwa kusoma picha ya uso msemaji anaposema, na uhakika wa usahihi wa kinachoandikwa?

Ninadhani kuna umuhimu wa kuwa na wachapishaji wa kuandika kwa shorthands zaidi ya wawili hasa kwenye mashauri makubwa kama haya, ili kuepuka makosa ya uandishi, upotoshaji wa makusudi, na utulivu kwa judge.
Mara kadhaa nimeona Mh. Judge mjadala ukiendelea, wanapo refer kwake, anauliza. "Ulikuwa unasemaje kweli?". Kitu kinachoashiria uwezekano mkubwa wa omissions, additions au alterations ambazo zinaweza kuathiri hatima ya shauri bila kitu cha kulinganishia kwenye rufaa.

Ushauri wangu, kama hakuna wataalam wa kuandika, kuwe na tape au video recording ili ikitokea ubishi waweze ku re-play badala ya kutegemea Judge kaandika nini.
 
Samahan lkn nauliza tu, hivi Kibatala anavosimamia hii kesi malipo yake analipwa na Mbowe, au anasimamia km mwanasheria wa chamaa au kesi haihusu chama ina muhusu mbowe km Mbowe.
 
Wa kwanza.

Wananzengo, huu utaratibu wa judge kuandika mwenyewe, ina tija kweli katika kufanikisha usikivu kwa hoja, kuona katikati ya mistari kwa kusoma picha ya uso msemaji anaposema, na uhakika wa usahihi wa kinachoandikwa?

Ninadhani kuna umuhimu wa kuwa na wachapishaji wa kuandika kwa shorthands zaidi ya wawili hasa kwenye mashauri makubwa kama haya, ili kuepuka makosa ya uandishi, upotoshaji wa makusudi, na utulivu kwa judge.
Mara kadhaa nimeona Mh. Judge mjadala ukiendelea, wanapo refer kwake, anauliza. "Ulikuwa unasemaje kweli?". Kitu kinachoashiria uwezekano mkubwa wa omissions, additions au alterations ambazo zinaweza kuathiri hatima ya shauri bila kitu cha kulinganishia kwenye rufaa.

Ushauri wangu, kama hakuna wataalam wa kuandika, kuwe na tape au video recording ili ikitokea ubishi waweze ku re-play badala ya kutegemea Judge kaandika nini.
Wananzengo sisi tuta refer hapa hapa kwenye hizi updates ambazo haziachi hata nukta.

Nina Uhakika Jaji Liganga huwa anapitia hizi Updates. Hata mawakili wa serikali wanapata fursa kurejea kilichojiri.

Huu ubunifu wa kuripoti moja kwa moja umekuja na faida nyingi

Tutacompile kwenye pdf shauri zima.
 
Wa kwanza.

Wananzengo, huu utaratibu wa judge kuandika mwenyewe, ina tija kweli katika kufanikisha usikivu kwa hoja, kuona katikati ya mistari kwa kusoma picha ya uso msemaji anaposema, na uhakika wa usahihi wa kinachoandikwa?

Ninadhani kuna umuhimu wa kuwa na wachapishaji wa kuandika kwa shorthands zaidi ya wawili hasa kwenye mashauri makubwa kama haya, ili kuepuka makosa ya uandishi, upotoshaji wa makusudi, na utulivu kwa judge.
Mara kadhaa nimeona Mh. Judge mjadala ukiendelea, wanapo refer kwake, anauliza. "Ulikuwa unasemaje kweli?". Kitu kinachoashiria uwezekano mkubwa wa omissions, additions au alterations ambazo zinaweza kuathiri hatima ya shauri bila kitu cha kulinganishia kwenye rufaa.

Ushauri wangu, kama hakuna wataalam wa kuandika, kuwe na tape au video recording ili ikitokea ubishi waweze ku re-play badala ya kutegemea Judge kaandika nini.
Wacahapishaji wako na jaji anaandika pia na huyu anayetuletea hapa anaandika na mawakili nao wanaandika.Lengo ni moja kuwa nakumbukumbu sahihi zilizoandikwa na kukiwa na tofauti wanalinganisha..
 
Samahan lkn nauliza tu ,HV kibatala anavosimamia hii kesi malipo yake analipwa na mbowe,au anasimamia km mwanasheria wa chamaa au kesi haihusu chama ina muhusu mbowe km mbowe ,

Wakati mwingine basi uwe una uliza maswali ya msingi. Inawezekana umeuliza kwa nia njema. Ila sasa ndiyo hivyo tena. Swali lako halina mashiko.

Yaani ni sawa na kwenda hospitali, unamkuta mgonjwa amejeruhiwa vibaya na majambazi! Unamkuta Daktari anamhangaikia ili apone! Halafu unauliza "hivi gharama za kumponya huyu mgonjwa atatoa nani?"

Nadhani kila mtu atakushangaa. Maana siyo kipaumbele kwa wakati huo! Isipokuwa ni mgonjwa kupona kwanza.
 
41 Reactions
Reply
Back
Top Bottom