Kifaurongo
JF-Expert Member
- Jan 18, 2010
- 4,217
- 2,354
Kuna watu wanadhani Kibatala na wenziwe wanafanya kazi bure. Ukweli ni kwamba mawakili wa utetezi wanajua kumuokoa Mbowe ktk tatizo hili ni kupambana kuwatoa hatiani washitakiwa no. 2 na 3. Hatima ya Mbowe inashikiliwa na maelezo ya watu hawa na mapingaamizi yote ni kujaribu kufanya kukiri kwao kusikubaliwe na mahakama. Hii ndio kazi ya Wakili wakati mwingine, kuhalalisha ukweli kuwa uongo kutumia vifungu hivyohivyo vya sheria. Ajabu kusikia watu wanashauri wajitoe.