Yaliyojiri katika kesi ya Freeman Mbowe - Novemba 18, 2021. Kesi imeahirishwa hadi Novemba 22, 2021

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
617
1,799
Salaam Wakuu,

Leo tarehe 18/11/2021 kesi ya Mwenyekiti wa CHEDEMA Freeman Mbowe inaendelea baada ya kuahirishwa siku ya jana.

Kujua jana kesi ilipoishia, soma: Yaliyojiri katika kesi ya Freeman Mbowe - Novemba 17, 2021: Kesi yaahirishwa mpaka tarehe 18/11/2021 saa tatu asubuhi

Ungana nami katika uzi huu ili kujua kila kinachojiri Mahakamani.

UPDATES

Jaji ameingia mahakamani

Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa

Wakili wa Serikali Robert Kidando anatambulisha Jopo la Mawakili wa Serikali

Pius Hilla
Abdallah Chavula
Jenitreza Kitali
Nassoro Katuga
Esther Martin
Ignasi Mwinuka
Tulimanywa Majige

Wakili Peter Kibatala anatambulisha Jopo la Mawakili wa Utetezi

Jeremiah Mtobesya
John Mallya
Dickson Matata
Idd Msawanga
Khadija Aaron
Evaresta Kisanga

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya Kusikilizwa na Jana tulikuwa tunajibu Hoja za Pingamizi na Tupo Tayari Kuendelea na Majibu ya Hoja..

Kibatala: Tupo tayari Kwa Ruhusa Yako Mheshimiwa Jaji

Jaji: Hilla Karibu

Wakili wa Serikali, Pius Hilla: Asante Mheshimiwa Jaji

Naomba Kujua niliishia Wapi

Jaji: ukiishi pale kwenye Maamuzi Kuhusiana na Hoja zilizokuwa zinaendelea

Wakili wa Serikali Pius Hilla: Nizungumzie Kidogo Kuhusiana na hiyo Disposal Order, Kwamba Hakuna ant Other getaway ambapo Kielelezo kinaweza Kutoka. Submission Yetu ni kwamba kwa kuwa Proceedings zilikuwa bado ni zile ile Kwa Maana Economic Case Namba 16 ya 2021.

Na Kwa kuwa Kielelezo hakikuwa intendend Kuwa Disposed kwa Maana ya Disposal. Kwa namna ambayo Upande wa Mashtaka Walikitumia, namaanisha Administrative tuliyotumia kuomba kwa Barua

Mwenzangu alivyowasilisha Kwako Kwamba Proceedings Za Trial Within a Trial ni Bado ndani ya Shauri hilohilo. Na Kwakuwa bado ipo Ndani ya Proceedings hizo Mheshimiwa Jaji na Kwakuwa Hapakuwa na Maombi au Sababu Kwa ajili ya Ku Dispose basi Kwa namna Ilivyokuwa ilikuwa Sahihi

Wakili wa Serikali: Naomba Kurejea Kesi ya... Dhidi ya Jamhuri, ya Mwaka 1996 Issue arising in a Trial Within a Trial inaweza Kutumika in Main Trial, ku' Cement Hoja Kwamba bado tupo Kwenye kesi ileile Moja, Kinachotakiwa ni kuonyesha Kwa Mahakama ni Kwa Namna gani Kielelezo Kimemfikia Shahidi

Na zile Sheria au Kanuni Zimefuatwa, Mheshimiwa Jaji Chain Of Custody imeelezwa Vizuri Kwenye Ushahidi, Foundation ya namna Kielelezo hiki Kimemfikia Shahidi Kimelezwa Vizuri Mheshimiwa Jaji, Mheshimiwa Jaji niongelee Kidogo Kuhusiana na Power za Deputy Registrar

Yupo sahihi Kutoa Kielelezo, Kwa sababu Mahakama ilishafanya Uamuzi Juu ya hatua za Kufuata, Kwa Maamuzi yale tayari ilikuwa ni Maelekezo Kwamba anaweza ku Perform Majukumu yale, Hata Kama Siyo Uamuzi Wa Mahakama, Ushughulikiaji wa Kielelezo ni Majukumu ya Deputy Registrar..

Wakili wa Serikali: Mazingira ya kesi yetu yalivyo ni sahihi Msajili Wa Mahakama Kushughulika Movement ya Kielelezo, Deputy Registrar ndiye Mtekelezaji wa Amri za Mahakama. Kwa hivyo ni Mamlaka Yake na Jukumu Lake Kushughulika Kielelezo Kama alivyo fanya..

Ni Wasilisho letu Kwamba Kama Wenzetu wanakubaliana Document ni authentic basi suala lingine halina nafasi, Shahidi akishaonesha Competence na akaonyesha Imemfikiaje basi Mengine hayana nafasi.

Mh Jaji nimalizie Kwa Kusema Kwamba Kwa kutambua Mazingira yote haya, Kuhusu Mapingamizi ya Wenzetu, Hakuna Hoja Nzito ya Kuzuia Detention Register Kuingia Hapa Mahakamani.. Tunaomba Mapingamizi Yatupiliwe mbali, Kielelezo Kiendelee na Tuendelee na Usikilizwaji wa Shauri hili

Wakili wa Serikali: Asante Mheshimiwa Jaji..

Jaji: Mmemaliza?

Wakili wa Serikali, Robert Kidando: Tumemaliza Mheshimiwa Jaji

Mtobesya: Tumesikia Hoja za Wenzetu, nitajibu In-chief na baada ya hapo nitaongezea Vitu Vichache..Kisha atakuja Kaka Yangu Kibatala Kujibu Inchief

Nimesikia Wameongea kuhusu Disposal Order, Lakini Sijui kwa Makusudi au Kwa Bahati Mbaya, Kwamba Wanavyosema Kwamba Proceedings Za Trial Within a Trial ni Sawa na Main Case, Naomba Kuwasilisha Mambo Manne ambayo yatakuwa ndiyo Mtazamo wangu kwenye hilo suala..

Kwanza Mheshimiwa Jaji ilikufanya Trial Within Trial, ni lazima Mahakama husika Kwa Muda Isitishe Proceedings Za main Trial iingie Kwenye zoezi la Kufanya Kesi Ndogo, halafu baadae regardless ya Matokeo ya Kesi hiyo Ndogo Mahakama husika itarejea Kuendelea na Kesi ya msingi

Mtobesya: Kwa hiyo huo ni Msingi wa Kwanza. Msingi wa Pili Mheshimiwa Jaji, Trial Within Trial, Proceedings Za Trial Within Trial, It's a factual Exercise ambayo inalenga Ku Archive Kitu Kimoja tu. Ku' prove Hoja ya Mshtakiwa ambaye anakuwa Under trial kwa kipindi hicho..

3 kama Ilivyo Kwenye Main Trial, Mwenye Jukumu la Kutaka Kuthibitisha Kama yule aliteswa au Lah ni Prosecutions, Kama ndiyo hivyo Mheshimiwa Jaji watatakiwa ku' lead Evidence Kuprove na Equally kwa mshtakiwa nae atatakiwa kulead Evidence kama alitoa Maelekezo Kwa hiari ama lah

Kwa hiyo ni Proceedings zinazojitegemea Mheshimiwa Jaji. Jambo la 4 Mheshimiwa Jaji, Katika Economic Case ya 16 ya Mwaka 2021. Mahakama hii ilishaingia ku' prove Voluntary ya Mshtakiwa Wa Pili ADAM KASEKWA. Na Mahakama ikaja na Maamuzi ya Kinachotakiwa Kufanywa kwenye Statement ya Mshitakiwa namba 2. Submission Ya kuwajibu Kaka zangu Wasomi, Ni kwanini Sisi tulidhani Kwamba Kwenye kesi hii Kielelezo hiki ambacho Mshtakiwa anaomba Kukitoa. Kiliingia Kwenye Kesi Ya Trial Within Trial na Kwamba Kielelezo hiki kiliiingia na Mahakama Ikafanya Uamuzi wake

Mtobesya: Kwanini Sisi tuli rejea Kwenye Kifungu namba 353(3) of CPA cap 20, Tofauti na Kaka yangu Chavula alivyokuwa anatafsiri, Kinasema Kwamba Mahakama ikisharidhika, Ni Vyema Ikatoa Amri Kwa Kielelezo hicho Kutoka, Itafanya hivyo baada au Wakati Mahakama ikiendelea. Labda nisome

Mtobesya ANASOMA SASA.

Mtobesya: Kwa hiyo sisi tulienda kwenye Kifungu hichi tulijua kwamba Kwakuwa Kielelezo hiki kilishatumika Kwa Kesi ya Adam Kasekwa. Kwa kuwa kilishatumika kwenye Different court Proceedings.

Na Kwamba Kwa kuwa kilisha amriwa kwenye Suala la Hiari ya Maelezo ya Mshtakiwa Wa Pili. Basi wao ilipaswa Wai' Move Mahakama Iweze Kutoa Kielelezo hicho.. Sasa Wenzetu hawakufanya hivyo Mheshimiwa Jaji, Sisi tuna Submit kwamba Kuna hatua za Kisheria Wameziruka

Mtobesya: Kwenye sehemu E Sehemu CAP 20 ndiyo inahusu Disposal of Exhibit, Mheshimiwa Jaji haihitaji Kuzunguka Sana Kuhusu Hoja hiyo. Kitu Kikishaingia Mahakama Procedure yake ya Kukitoa ni Ileile Kama Ilivyo Kiingiza hiyo ni COURT ORDER.

Na Ukisoma kwa namna hii utagundua ni Njia pekee ya Court Order, Kwa hiyo tunachokiona sisi Waliruka Utaratibu wa kupata Kielelezo. Kwa Mahakama Kujiridhisha Sababu lazima Pawe na Maombi Mbele ya Mahakama. Wenzetu hawajakisoma Kifungu hiki Vizuri Wakakielewa.

Sasa wakati Wenzetu Wana Submit walitaka Kuonyesha Kwamba Proceedings hizi ni zile ile, Logic Ndogo sana Mbona, Kwamba Shahidi PW1 kwenye kesi hii Ndogo, Kule Kwenye Kesi Ya Msingi ni PW8, Na Mahakama Ikirejea anarudi Kuwa PW8 ni Kwa Sababu Shauri ni tofauti. Hatuwezi Kusema ni Kesi Moja hii

Mtobesya: Niliwasikia Wenzetu especially Kaka Yangu Chavula Kwamba PW1 alipokuwa anaomba Kielelezo, Mahakama iliwaruhusu Wapewe, Bila Kuingilia Kilicho fanyika, Basi ni Ukiukwaji Mkubwa Sana wa Taratibu za Mahakama.

Kama Walikuwa na Order Ya Kuomba Kielelezo, hawakupaswa Kuomba Kwenye Proceedings hizi, Ni Ukiukwaji Mkubwa wa Taratibu na Mahakama Isingeweza Kuombwa Kitu ambacho Kimechukuliwa Kwenye Proceedings zingine na Kama Kweli walifanya hivyo basi Taratibu zingefuatwa kwa Mujibu wa 353 na Muongozo wa Mahakama. Na Kaka zangu hawa ni Mawakili Wasomi siwezi Kuwafundisha, Lakini Hilo halikufanyika na Kama Kilifanyika Basi Kimekiuka Utaratibu ninaousema.

Mheshimiwa Jaji Kama Kweli Proceedings hizi ni sawa Kwanini wanaomba Mahakama Ipokee tena Kwa mara ya pili Kwenye Shauri hili Kama Proceedings zote ni sawa na Kesi ni ileile? Kitendo cha Kuomba Ipokelewe tena na Mahakama ni Ushahidi Tosha Kwamba hili ni Shauri tofauti

Mtobesya: Mheshimiwa Jaji kwenye hilo naomba Kuishia hapo, atakuja Kumalizia Kaka Yangu Kibatala Kama Kuna kitu sijataja. Sababu walizotoa Kupinga Mapingamizi Yetu zinakosa Mashiko, Hivyo tunaomba Isizingatie kabisa Hoja zao zisizo na Mashiko.

Naomba niende kwenye suala la Pili Kwamba Mahakama Inakuwa Funtus Officio, Wakati Wenzetu Wanawasilisha Wa naona suala la Mahakama kuwa Funtus officio kwa Njia tofauti, Kwamba Wakati Wa Uamuzi wa Mahakama unatolewa Mahakama Ilisema Kwamba Kielelezo Kipo Competence, Relevance na Material. Kwamba PWI aliomba Kuingia Kama ID na PW2 anaomba Kiingie Kama Kielelezo. Nadhani hawakuelewa suala la Pingamizi letu labda nirudie kidogo. Mahakama Ilishaitwa Kusema Jambo Au Kupokea Exhibit hii. Na katika hilo Mahakama ilisha Exercise haki yake ya Kusema

Katika suala hilo, na Uamuzi wa Mahakama Exhibit was Rejected, Ndiyo Maana tunasema Mheshimiwa Jaji Kwamba Mwaliko huu wa Mara ya pili kwamba Mahakama iseme tena lolote ni UKIUKWAJI WA UTARATIBU. Na Unakuwa Ukiukwaji kwa Falsafa (DOCTRINE) ya Funtus Officio

Mtobesya: Funtus officio Ilishafanya Maamuzi, It's Done, wanachokifanya Wenzetu ni Kwamba Mahakama ilishakataa Inaomba iangalie tena.

Kibatala ananinong'oneza inakuwa ni Review ambayo haijafuata Utaratibu. Hapo Ndipo tunasema Wenzetu hawakuelewa Maana ya Funtus Officio

Mtobesya: Chavula anasema Kwamba PW1 aliomba iingie kama ID na PW2 anaomba iingie Kama Exhibit, Mheshimiwa Jaji Mahakama Ilisha Sema Kwamba Procedure ni zile ile tunafunga tuna Jambo ambalo Mahakama ilisha Tolea Maamuzi.

Sasa Kuna Kesi walirejea hapa Kaka zangu wasomi Mawakili wa Serikali ya NIBURO COSMAS kwamba Sisi tumekosea kulinganisha Parameters. Kwamba Mahakama imepewa Mamlaka Ya Kuamua kesi ni Funtus Officio pale ambapo Mahakama Inakuwa Inasajili kesi Nyingine

Mheshimiwa Jaji Mahakama Inakuwa Funtus Officio Pale ambapo Mahakama inakuwa imemeliza Jambo fulani siyo lazima Kesi Nzima, Kwenye kesi tuliyoitumia Jana Ilikuwa Overulled Kwasababu ilikuwa Funtus officio ndiyo Maana wakaendelea Mpaka Mahakama ya Rufaa

The Court can't go back, The Court if Funtus officio, Iwe kesi imeisha au haijaisha, lakini Hapa Kuna Jambo ambalo Mahakama Imeshalitolea Uamuzi. Kwamba Kesi Mpaka ifike Mwisho siyo Hoja ya Msingi.

Mtobesya: Sasa Mheshimiwa Jaji niishie hapo kwa Kusema Kwamba Wenzetu hawakuelewa namna ambavyo Falsafa hiyo (DOCTRINE) ya Funtus Officio inavyofanya Kazi. Kwa sababu hiyo Basi tunaomba Basi Mahakama ikute kwamba Haiwezi Kuamua Jambo hilo mara ya pili, na wakati Mahakama inafanya Uamuzi zipatie Uzito Hoja zetu kwa kiwanho hicho. Mheshimiwa Jaji Samahani Kidogo (anateta na Kibatala) Mheshimiwa Jaji Kuna Kesi ya Khatibu Gandhi Aliyosoma Kaka Yangu Hilla Kwamba Unaweza kutumia hoja za Trial Within Trial Katika main Case

Sivyo alivyo taka kutuaminisha Kaka Yangu Hila, Hoja ya Kesi hii ni Kwamba Baada ya Uamuzi Wa Kesi ya Trial Within Trial Inaweza Kutumika kama Ushahidi Katika main Case. Kwa hiyo rejea hii ipo Out of Context, haina Uhusiano na Kilichopo Mahakamani.

Kwa sababu hiyo naomba Nimalizie hapo na Nimuachie Kaka Yangu Peter Kibatala.. Ahsante Mheshimiwa Jaji.

Kibatala: Mheshimiwa Jaji Kwa Ruhusa yako naomba Niendelee hapo ambapo Kaka Yangu Mtobesya amemalizia, Kwa kweli ni Mazingira tofauti kabisa na Kesi hii, Hakuna Sehemu yoyote katika Shauri lile ku TRANS - EXHIBIT, Palikuwa hakuna kama wanachotaka Kufanya wao hapa Mahakamani

Mheshimiwa Jaji nirudi Kule Kwenye Disposal Order kama nilimuelewa Mr Chavula Kama sijamuelewa atanisamehe, Anasema hatujashambulia Kielelezo, Sasa Kama hatujashambulia Kielelezo tunafanya nini hapa?

Kibatala: Hili siyo zoezi la Nomenclature, Kwamba Uamuzi ulikuwa Juu ya Shahidi Siyo Kielelezo, Kwani wao Walikuwa wa naomba Shahidi aje? Au walikuwa Wa naomba Kielelezo Kuingia? Hapa Katika Swala la Chain of Custody, Ni kwamba haikufuatwa kwa sababu Mahakama hakuna Jambo linalofanyika Kiholela.

Kibatala Anasoma mwongozo Kama tulivyowasilisha, Walikuwa na nafasi tangu mara ya kwanza, Kwamba Kama watakitumia Walipaswa Kuomba Disposal Order, Wanajiwekea Sheria zao wenyewe na Kurekebisha vifungu kama palikuwa na Maamuzi ya Mahakama, Ambapo Maamuzi

Yakapelekea Kupatikana kwa Barua, haihalalishi Kielelezo ambacho kimefika Mahakamani bila Disposal Order, Kwa bahati Mbaya Hakuna Sehemu hata Moja Wakili Wa Serikali ametoa Sheria Wala Sheria Kesi Kwamba Naibu Msajili anaweza kumkabidhi Mtu yoyote yule Kielelezo Cha Mahakama

Kibatala: Kwa bahati Mbaya Hakuna Sehemu hata Moja Wakili Wa Serikali ametoa Sheria Wala Sheria Kesi Kwamba Naibu Msajili anaweza kumkabidhi Mtu yoyote yule Kielelezo cha Mahakama, Iwe Kwa Bahati mbaya au Kwa Makusudi, na kupitiwa siyo Dhambi kabisa

Wenzangu Wanatumia Uamuzi Wako kwamba Uliwafanya wafanye Walichofanya, Hapana Hakuna Sehemu Umesema Naibu Msajili aandike Barua. Tunachojua Mahakama ilitupilia Mbali Kielelezo. Tunachojua Mahakama ilitupilia Mbali Kielelezo. Na sasa Wanacho bila kufuata Sheria na Chain of Custody

Kibatala: Mheshimiwa Jaji Wakati na Wasilisha Kwa kutumia MWONGOZO wa Jaji Mkuu, na Walitaka kuukosoa lakini wakawa Waangalifu..

Wakili wa Serikali, Abdallah Chavula: OBJECTION, Mheshimiwa Jaji ananichonganisha, mimi sikukosoa.

Kibatala: Sawa, siyo Big Issue

Kibatala: Na wakati Hila anaongea alitaja kesi ya Gede ambayo ni Ya Mwaka 2017 na Muongozo wa Mahakama Ulitolea Mwaka 2020, Na hakuna Sehemu waliyosema Kwamba Kuna Mgongano kati ya MWONGOZO na Sheria au Sheria kesi yoyote. Na Ndiyo Maana Jaji Mkuu wa Sasa anasema alitoa Muongozo

Kwa ajili ya Kuleta HARMONY. Kibatala ANASOMA Maneno ya Jaji Mkuu suala la DISPOSAL ORDER. Na Mwisho kabisa Jaji Mkuu amezungumzia suala la Exhibit Registrar. Na sijasikia Wakili hata Mmoja anazungumzia suala la Exhibit Registrar.

Kibatala: Na Kwamba Swali ni nani alitoa DISPOSAL ORDER. Hakuna Mahala Popote ambapo Mahakama hii ilifanya DISPOSAL ORDER na Kwamba Wao wanasema kwamba ni suala la Utawala. Ni Sheria ipi imesema kwamba Disposal Order ni suala la Kiutawala?

Mheshimiwa Jaji Pia wamezungumzia suala la GEDE KONDO kuhusiana na Competence ya Shahidi, Sasa Shahidi Mwenyewe hajafikia hata kwenye Cross Examination, Kwa hiyo Kesi ya ABASI GEDE KONDO ni Rejea tofauti na haina Uhusiano na Kesi hii.

Kibatala: Nakumbushwa kuhusu Barua ya Naibu Msajili, Sisi tunasema Alitakiwa kuandika Barua ile baada ya Kutolewa Disposal Order. Suala la Mamlaka yake yatapimwa na Utaratibu za Kisheria, Sisi tunashughulikia suala Kuingia kwa Exhibit hayo ya Mamlaka Yake siyo Ajenda yetu

Kibatala: Kuna wakili wa serikali alisema kwamba zoezi la kuingiza ID ni sawa HAKUNA, Kwamba WAO walivyokuwa wanataka PW1 aingize ID ilikuwa ni sawa na HAKUNA!!? Sijui Kama alikuwa serious au anatania. Nani alileta suala la 'HAKUNAISM' hapa Mahakamani?

Kibatala: Mheshimiwa Jaji Pia suala la Falsafa (DOCTRINE) Ya Estoppel. Kuna sehemu Wenzetu wamesema Kwamba Siyo lazima Kuitumia, Sasa kwanini palikuwa na hiyo Falsafa (DOCTRINE) of Estoppel? Na wamesema Kwamba Kwenye kesi ya ISSA TOJO Mahakama haikutumia Despite Walitaja tu.

Kibatala ANASOMA Uamuzi.

Kwa kutumia Falsafa ya Estoppel, Na Principle ya Estoppel inaweza Kutumika wakati wa Kesi au kabla ya kesi, Kesi ya JULIUS MICHAEL pia walitumia Principle ya Estoppel Ukurasa wa 07, Kwamba Kanuni ya Estoppel inatajwa, Kama Una zungumzia specific issues basi Kanuni hii lazima itumike.. Na Kwamba tunawasilisha kwamba Kesi hii ipo sahihi.. Msomi Pius Hilla alisema Kwamba Admission nickitu Kimoja na DISPOSAL ni Kitu Kingine.. Sisi tunasema Pamoja na Kanuni tatu za Relevance, Competence na Veracity lakini Hakuna Paper Trade.

Kibatala: Mheshimiwa Jaji, Tunawasilisha Kwamba Kama hawakuomba Disposal Order hawawezi Kupata Exhibit, Wakiomba Wanapata Wala hakuna Njia ya Mkato hapo.. Tunakazia Mapingamizi Yetu. Asante Mheshimiwa Jaji.

Kibatala anakaa chini

Jaji: nimesikia Hoja zenu wote, ni kwamba najaribu kutafakari kabla sijaamua kupanga maamuzi yawe lini na saa ngapi. Ningeomba dakika 10 nifanye tathimini kisha nitarejea kusema uamuzi ni lini.

Jaji anatoka!

Jaji amerejea Mahakamani

Wakili wa Serikali, Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Upande wa Utetezi tupo wote isipokuwa Mr Pius Hilla alitoka Kidogo

Kibatala: Mheshimiwa Jaji sisi quorum yetu ipo kama awali tupo tayari Kusikiliza Maamuzi.

Jaji anaandika Kidogo

Jaji: Nimefanya tathimini na uwezekano wa Kesho Asubuhi utakuwa ni mgumu, tuje Jumatatu ya tarehe 22/11/2021, Shahidi unaombwa kurudi mahakamani Washtakiwa wataendelea kuwa chini ya Magereza mpaka tarehe 22/112021 Jumatatu Saa 3 Asubuhi Nawatakia weekend njema

Jaji anatoka!
 
Mbowe na genge lake wanapaswa wawe na nidhamu ya kuheshimu Mahakama.

Kama wataendelea kuleta mchezo wa kitoto wa kuichafua mahakama kwa kuleta Sarakasi zisizo na kichwa wala miguu watajiweka pabaya sana.

Jaji wa kwanza walimchafua na kumkataa.

Jaji wa pili alijitoa kwa sababu ya majukumu lkn walimchafua na kumkejeli.

Sasa Jaji huyu watatu naye wameanza kumchafua na kumkejeli.

Wanacho kifanya mawakili na wafuasi w mboe ni kutaka kuivuruga mahakama au kuishinikiza ifanye maamuzi kama wanavyo taka wao na sio vinginevyo.

Mahakama haipaswi kuingia ktk mtego huo wanao ufanya hao watuhumiwa na wafuasi wao.
 
Mbowe na genge lake wanapaswa wawe na nidhamu ya kuheshimu Mahakama.

Kama wataendelea kuleta mchezo wa kitoto wa kuichafua mahakama kwa kuleta Sarakasi zisizo na kichwa wala miguu watajiweka pabaya sana.

Jaji wa kwanza walimchafua na kumkataa.

Jaji wa pili alijitoa kwa sababu ya majukumu lkn walimchafua na kumkejeli.

Sasa Jaji huyu watatu naye wameanza kumchafua na kumkejeli.

Wanacho kifanya mawakili na wafuasi w mboe ni kutaka kuivuruga mahakama au kuishinikiza ifanye maamuzi kama wanavyo taka wao na sio vinginevyo.

Mahakama haipaswi kuingia ktk mtego huo wanao ufanya hao watuhumiwa na wafuasi wao.
Ni mwendo wa mapingamizi, mpaka mataga mtage, mainzi wa kijani!
 
Mbowe na genge lake wanapaswa wawe na nidhamu ya kuheshimu Mahakama.

Kama wataendelea kuleta mchezo wa kitoto wa kuichafua mahakama kwa kuleta Sarakasi zisizo na kichwa wala miguu watajiweka pabaya sana.

Jaji wa kwanza walimchafua na kumkataa.

Jaji wa pili alijitoa kwa sababu ya majukumu lkn walimchafua na kumkejeli.

Sasa Jaji huyu watatu naye wameanza kumchafua na kumkejeli.

Wanacho kifanya mawakili na wafuasi w mboe ni kutaka kuivuruga mahakama au kuishinikiza ifanye maamuzi kama wanavyo taka wao na sio vinginevyo.

Mahakama haipaswi kuingia ktk mtego huo wanao ufanya hao watuhumiwa na wafuasi wao.

Jaji hana uwezo na hilo linazidi kudhibitika siku hadi siku, hata yeye hapo alipo anajua kabisa kaingia kwenye tatizo kubwa. Huyo jaji asingekuwa na hukumu toka kwa rais mkononi, angeweza kufanya kazi yake vizuri. Lakini kitendo cha kukubali kupewa hukumu na majizi ya kura ndio kajimaliza.
 
Mbowe na genge lake wanapaswa wawe na nidhamu ya kuheshimu Mahakama.

Kama wataendelea kuleta mchezo wa kitoto wa kuichafua mahakama kwa kuleta Sarakasi zisizo na kichwa wala miguu watajiweka pabaya sana.

Jaji wa kwanza walimchafua na kumkataa.

Jaji wa pili alijitoa kwa sababu ya majukumu lkn walimchafua na kumkejeli.

Sasa Jaji huyu watatu naye wameanza kumchafua na kumkejeli.

Wanacho kifanya mawakili na wafuasi w mboe ni kutaka kuivuruga mahakama au kuishinikiza ifanye maamuzi kama wanavyo taka wao na sio vinginevyo.

Mahakama haipaswi kuingia ktk mtego huo wanao ufanya hao watuhumiwa na wafuasi wao.
Mahakama inatakiwa iheshimiwe na wote kwakuwa ndio chombo pekee kinacho tafsiri sheria na kutoa HAKI.
 
mboe na genge lake wanapaswa wawe na nidhamu ya kuheshimu Mahakama.

kama wataendelea kuleta mchezo wa kitoto wa kuichafua mahakama kwa kuleta Sarakasi zisizo na kichwa wala miguu watajiweka pabaya sana.

Jaji wa kwanza walimchafua na kumkataa.
Jaji wa pili alijitoa kwa sababu ya majukumu lkn walimchafua na kumkejeli.

sasa Jaji huyu watatu naye wameanza kumchafua na kumkejeli.

wanacho kifanya mawakili na wafuasi w mboe ni kutaka kuivuruga mahakama au kuishinikiza ifanye maamuzi kama wanavyo taka wao na sio vinginevyo.

Mahakama haipaswi kuingia ktk mtego huo wanao ufanya hao watuhumiwa na wafuasi wao.
Mkuu ulitoka law school mwaka gani?
 
Mbowe na genge lake wanapaswa wawe na nidhamu ya kuheshimu Mahakama.

Kama wataendelea kuleta mchezo wa kitoto wa kuichafua mahakama kwa kuleta Sarakasi zisizo na kichwa wala miguu watajiweka pabaya sana.

Jaji wa kwanza walimchafua na kumkataa.

Jaji wa pili alijitoa kwa sababu ya majukumu lkn walimchafua na kumkejeli.

Sasa Jaji huyu watatu naye wameanza kumchafua na kumkejeli.

Wanacho kifanya mawakili na wafuasi w mboe ni kutaka kuivuruga mahakama au kuishinikiza ifanye maamuzi kama wanavyo taka wao na sio vinginevyo.

Mahakama haipaswi kuingia ktk mtego huo wanao ufanya hao watuhumiwa na wafuasi wao.
Punguwani mkubwa wewe ata akili huna walikuwepo wenzako lakini walisha kimbia najua na wewe utatoka tu ni kazi sana kutetea uongo
 
Back
Top Bottom