Yaliyojiri katika kesi ya Freeman Mbowe - Januari 10, 2022. Shahidi namba 8 aendelea kutoa ushahidi. Kesi imeahirishwa hadi kesho 11/01/2022

Uwa ni jaji mzuri sana tunafanya nae kazi anatendaga haki sana sema hii kesi ni ya kisiasa sana akitenda haki lazima aumie eg kumtoa mjini na kumpeleka mazingira magumu etc. Trust me tiganga ni jaji mzuri
Jaji anaweza kupelekwa kijijini???!!! Ni wapi kuna maeneo magumu ambayo unaweza kumpeleka Judge?
 
Unapokuwa Unaangalia Kipengele Kimoja kikiwa Kimekatika Kimoja basi Mnyororo huo Unakuwa Umekatika.. Katika Kushughulika na Vielelezo Hivyo kuwa Vipo namba ambavyo Vinakatwa Mpaka Vinafika Mahakamani. Siyo Sahihi Shahidi Mmoja tu anapotoka Ushahidi Kueleza Kwa niaba ya wengine Kuhusiana na Mnyororo Kuvunjia au kutovunjika.

Ngamia amevunjwa uti wa mgongo kwa ubua.

Uamuzi wa leo unategeneza matundu makubwa katika kesi hii namba 16 ya mwaka 2021 iliyowasilishwa na Jamhuri.
 
Exhibit ambayo inatakiwa Labeled inatakiwa Kuwa Paper Pin, PGO 229(8) Kuwa label hiyo inatakiwa Kuwa ni Minor number, na Vingine.. Kutokana na Malekezo hayo ya Kisheria yaliyoelezwa katika PGO Hiyo ni wazi Kuwa Alama iliyowekwa siyo alama ambayo PGO 229 Imeitambua na kuelekeza.

Kazi kweli kweli kufanya kazi kwa mazowea ya kukamia bila kufuata PGO
 
Wakili Nkungu: Unafahamu Kwamba PGO inasema Kinyume Kwamba Askari hategemewi Kutumia Kumbukumbu zake?

Shahidi: Mie sifahamu, ila nafahamu Sifa ya Askari ni Kumbukumbu

Wakili Nkungu: Kwa hiyo PGO inaposema Kuwa Askari asitegemee Memory yake inadanganya

PGO ! PGO !
 
Wakili Nashon Nkungu: kutokwepo kwa Nyaraka Hakuna Mtu Mwingine Kwa Hakika ataeleza Kuwa Watu hawa walifikishwa Moshi

Shahidi: Sasa Mimi si Nipo hapa Ndiyo Nina Uhakika..

Wakili Nashon Nkungu: Kwa hiyo Nyaraka hizi ni Urembo

Shahidi: Kimyaaaaaaaaaa

Wakili Nashon Nkungu: Ushahidi Wa Nyaraka Muhimu zinazoelezwa na Sheria hujatoa hapa Mahakamani

Shahidi: Mimi sijaleta Nyaraka hiyo

Wakili Nashon Nkungu: Wakati Mpo Moshi Watuhumiwa Walikuwa Wanalala wap

Mashahidi wa Jamhuri leo walipata wakati mgumu sana kutokana na umakini wa mawakili wa upande wa utetezi.
 
Shahidi: Walikuwa ni Wahalifu

Kibatala: Kama Wahalifu Kwanini Mliwaachia

Shahidi: Kwa sababu hapo kuwa na Ushahidi Wa Kutosha.

Kibatala: Sasa Watu ambao Umekosa Ushahidi unawaita Wahalifu?

Shahidi: Kimyaaaaaaaaaa

Hatari sana utendaji wa jeshi letu la Polisi kutoa hukumu bila mahakama kuwatia hatiani watuhumiwa.
 
NATAFUTA KESI ZAKE NA KUZISOMA KUONA KAMA ZINA MANTIKI YA KISHERIA MAANA HUU USHENZI ANAOUFANYA ANAKUWA MTUMISHI WA SHETANI NA LANA JUU
Wakili msomi umejua nichekesha leo. Msomi tuachane na hizi judgements, msomi natamani mbowe atoke hata leo ila na wewe unajua jaji yeyote atakaehusika kwenye kesi hii kazi anayo maana ni kesi ya kisiasa ina maelekezo kutoka juu karibu na mbinguni😂
 
Nawasalimu kwa jina la jamuhuri

Kama mnafatilia kesi ya Mbowe kwa shahidi huyu wa 8 nahisi

Utaona kuna upotoshwaji mkubwa sana Rais wa nchi anadanganywa na wasaidizi wake sana.

Alipohojiwa na BBC alisema wenzake na Mbowe wanatumikia vifungo tayari.

Shahidi wa leo anasema hajui kama kuna mtu ameshahukumiwa kwenye kesi hii.
Ukiangalia kwa haraka utaona kabisa kuna watu wanamdanganya mama mchana kweupe naye mama bila kufikiria anaenda kuuropokea huo uongo kwa ulimwengu.

Ehh bwana liponye taifa lako

Maendeleo hayana chama
 
Nawasalimu kwa jina la jamuhuri

Kama mnafatilia kesi ya Mbowe kwa shahidi huyu wa 8 nahisi...
Mama ni muongo muongo sana, ndo shida ya watu wa Pwani kuwapa madaraka makubwa ya kuongoza nchi. Nilimuona majuzi kwenye kitchen party anarembua jicho au siyo yeye?
 
Back
Top Bottom