Yaliyojiri katika kesi ya Freeman Mbowe: Jaji aahirisha kutoa uamuzi mpaka tarehe 17/11/2021 saa tatu asubuhi

Nikiangalia rufaa zinazokatwa, na waliohukumiwa kushinda rufaa zao, MAANA YAKE MAJAJI NA MAHAKIMU KUNA NAMNA WANALINDWA PINDI WANAPOTOA HUKUMU ZISIZO NA HAKI
Kwa hapa tulipofikia kuna haja ya kuhoji uadilifu wa mahakama na kujua hatua stahiki za kuchukua.
 
Naomba kuuliza, hivi ikifahamika kuwa hakimu au jaji ametoa hukumu kwa kupindisha sheria ni hatua gani za kisheria anachukuliwa? Isije ikawa nao wana kinga ya hukumu za kupindisha sheria, hivyo kutoa mwanya wa kufanya wapendavyo kinyume na sheria.
Yule Jaji wa Kwanza alipolalamikiwa kabla hajajitoa akaibuka Jaji Mkuu na kusema kuna utaratibu wa kuwawajibisha Majaji wanapopindisha Sheria. Akatoa mlolongo mrefu kama treni ya Kigoma.
 
Yule Jaji wa Kwanza alipolalamikiwa kabla hajajitoa akaibuka Jaji Mkuu na kusema kuna utaratibu wa kuwawajibisha Majaji wanapopindisha Sheria. Akatoa mlolongo mrefu kama treni ya Kigoma.

Hiyo ndio sababu majaji wanaweza kufanya watakalo. Usishangae ukasikia hata rais yuko kwenye katiba ya kumuwajibisha jaji. Huku nyuma ya pazia rais ndio kabambikia kesi!
 
Ila kusema ule ukweli Mnowe si gaidi jamaani.

Atakufa mtu kwa uonevu huu wa kuwatesa kukaa ndani
 
Hii kesi inaendeshwa kimagumashi sana, jaji kila wakati wa kutoa maamuzi anaahirisha halafu kesho yake anajisahaulisha walipoishia.
Eti km jana alijifanya kusahau, ila sio kusahau anafanya kusudi hata kama kaairisha leo, kesho atatupilia mbali pingamizi
 
Eti km jana alijifanya kusahau, ila sio kusahau anafanya kusudi hata kama kaairisha leo, kesho atatupilia mbali pingamizi
pingamizi atalitupilia ,amesema kesho ni maamuzi lakini shahidi awepo kuendelea na ushahidi Sasa hapo si maamuzi tayari
 
Salaam Wakuu,

Leo tarehe 16/11/2021 kesi ya Mwenyekiti wa CHEDEMA Freeman Mbowe inaendelea.

Kujua jana kesi ilipoishia, soma: Yaliyojiri kesi ya Freeman Mbowe na wenzake Nov 15,2021

Ungana nami katika uzi huu ili kujua kila kinachojiri Mahakamani.

UPDATES;
- Jaji ameingia Mahakamani..

- Kesi inatajwa..

Wakili wa Serikali: Robert Kidando anatambulisha Jopo la Mawakili wa Serikali..
1. Jenitreza Kitali
2. Abdallah Chavula
3. Pius Hilla
4. Nassoro Katuga
5. Esther Martin
6. Tulimanywa Majige
7. Ignasi Mwinuka

Wakili Peter Kibatala anatambulisha Jopo la Mawakili wa Utetezi..
1. Jeremiah Mtobesya
2. John Mallya
3. Seleman Matauka

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya Uamuzi Mdogo

Peter Kibatala Mheshimiwa Jaji na sisi tupo tayari Kupokea Malekezo

Jaji: Jana nilihairisha shauri Jana Jioni, nikasema Nitasoma uamuzi leo... Lakini kutokana na wingi wa hoja naomba muda zaidi mpaka kesho.. Nikakamilishe kuandika uamuzi... Naomba radhi kwa hairisho hili ambalo hatukulitarajia wote..

- Mawakili wa pande zote wanasimama kukubaliana

Jaji: kama nilivyosema kwamba nahairisha shauri mpaka Kesho, UPANDE WA MASHTAKA MTAMLETA SHAHIDI ATAKAA KIZIMBANI NA ATAENDELEA KUTOA USHAHIDI Nahairisha mpaka kesho saa 3 asubuhi.

- Jaji anatoka!

Kooooooooooortiiiiiiiiii..

===
Kesi ya ugaidi inayomkabili mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu imeahirishwa hadi kesho kutokana na kutokukamilika kuandikwa uamuzi kuhusu uhalali wa shahidi wa Jamhuri anayedaiwa kupanda kizimbana akiwa na diary, simu na kalamu

Akitoa uamuzi huo leo Jumanne Novemba 16, 2021 Jaji Joachim Tiganga amesema ameshindwa kukamilisha kuandika uamuzi huo kutokana na wingi wa hoja zilizotolewa na mawakili wa pande zote.

Jana yaliibuka malumbano ya kisheria katika mahakama hiyo kuhusiana na uhalali wa shahidi kupanda kizimbani akiwa na diary, simu na kalamu.

Upande wa utetezi unadai kuwa shahidi huo alikuwa anatumia vifaa hivyo wakati akitoa ushahidi wake Ijumaa, jambo wanalosisitiza kuwa ni kinyume cha sheria na utaratibu.

Chanzo: Mwananchi
Upumbavu mtupu, CCM kuna Siku mtalipa haya
 
Eti km jana alijifanya kusahau, ila sio kusahau anafanya kusudi hata kama kaairisha leo, kesho atatupilia mbali pingamizi

Huyo jaji hana uwezo kabisa na hiyo kesi, na kadiri kesi inavyoendelea anazidi kuchanganyikiwa. Kwanza anajaribu kuibeba jamuhuri, lakini ushahidi unaotolewa na upande wa jamuhuri una walakini sana, sasa anawajibika kubalance huo ushahidi wa kubumba ili aonekane bado anaimudu hiyo kesi, lakini hadi hapo alipo ameshachanganyikiwa. Nadhani anatengeneza mazingira ili upande wa upinzani upinzani waseme hawana imani naye ili ajitoe haraka sana. Lakini kimsingi jaji ameshakata moto, na hiyo kesi inamlemea kwani ni ya kutunga.
 
Jaji hana kauli nyingine anayoweza kuitoa zaidi ya hiyo...

Na sababu ni moja tu, kuwa, bado shahidi hajavuliwa sifa za kuwa shahidi...

Lakini sheria haidanganyi, iko wazi. Na hoja za kisheria za upande wa utetezi ni nzito na zina nguvu zaidi kuliko za washtaki...

Habari njema ni hii...HUYU SHAHIDI HAENDI ZAIDI YA HAPO ALIPOFIKIA..!

Jaji hana pa kutokea. Yuko uchi mchana kweupe. Ni lazima achutame tu...
Jana Kibatala kamwambia jaji anazan mashahidi wangapi watapanda na Diary na simu kwenye kutoa ushahidi kama jaji akisema haikua makosa maana watakua Wana refer maamuzi ya jaju huyu
 
Huyo jaji hana uwezo kabisa na hiyo kesi, na kadiri kesi inavyoendelea anazidi kuchanganyikiwa. Kwanza anajaribu kuibeba jamuhuri, lakini ushahidi unaotolewa na upande wa jamuhuri una walakini sana, sasa anawajibika kubalance huo ushahidi wa kubumba ili aonekane bado anaimudu hiyo kesi, lakini hadi hapo alipo ameshachanganyikiwa. Nadhani anatengeneza mazingira ili upande wa upinzani upinzani waseme hawana imani naye ili ajitoe haraka sana. Lakini kimsingi jaji ameshakata moto, na hiyo kesi inamlemea kwani ni ya kutunga.
Cha ajabu pia Kuna maamuzi ambayo anayatoa na bado anajikanganya wakati akina kibatala wakiwa wanayatumia katika kuomba miongozo mbalimbali
 
Jana Kibatala kamwambia jaji anazan mashahidi wangapi watapanda na Diary na simu kwenye kutoa ushahidi kama jaji akisema haikua makosa maana watakua Wana refer maamuzi ya jaju huyu
Ndiyo maana nimesema, huyu Jaji this time hana upenyo wa kutokea...

Ameyakoroga na hana budi ayanywe hivyo hivyo na uchungu wake...

Huyu shahidi HAWEZI KWENDA ZAIDI YA HAPO ALIPOFIKA...

Sheria inamtazama Jaji Joachim Taganga kwa macho makali. Hawezi kukwepesha tena macho yake. In sharti tu aseme "NDIYO"...
 
pingamizi atalitupilia ,amesema kesho ni maamuzi lakini shahidi awepo kuendelea na ushahidi Sasa hapo si maamuzi tayari
Yaan wanafanya ujinga hata wasio jua sheria wanaona upumbavu wao waziwazi, lakini pia hata hawaoni aibu ugaidi uliopangwa kufanywa nchi nzima na watu watatu na pistol moja yenye risasi 3 ambazo na zenyewe sjui haziendani akyanani nawaombea mabaya yoote yawafike na hila zao
 
Huyo jaji hana uwezo kabisa na hiyo kesi, na kadiri kesi inavyoendelea anazidi kuchanganyikiwa. Kwanza anajaribu kuibeba jamuhuri, lakini ushahidi unaotolewa na upande wa jamuhuri una walakini sana...
Yaan hapo alishindwa aandike nn hapo waliairisha kesi wakakae jopo zima waandikeeeeee mwisho wa gazeti aseme anatupilia mbali pingamizi.
 
Back
Top Bottom