Uchaguzi 2020 Yaliyojiri katika Kampeni za Tundu Lissu Jijini Mwanza

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Mgombea Urais wa Chadema Tundu Lissu leo anatarajiwa kuitikisa jiji la Mwanza katika mkutano mkubwa wa Hadhara katika viwanja vya Furahisha.

Tayari maandalizi yamekamilika na maandamano makubwa ya kumlaki yanasubiriwa kuanza wakati wowote kutoka sasa

Tayari mgombea huyo ameshafanya mikutano minne ya kampeni ambapo mitatu ilikuwa jijini DSM na mmoja ulikuwa jijini Arusha hapo Jana.

Chadema katika uchaguzi mkuu huu inatumia kauli Mbiu ya Uhuru,Haki na Maendeleo ya watu.

#UhuruHakiNaMaendeleoyawatu#
#Niyeye2020#

----

Tundu Antipas Lissu Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewasili Mwanza kwa kishindo kikubwa.

Akiambatana na Mgombea Mwenza pamoja na Mwenyekiti wa chama Freeman Mbowe mgombea huyo amelakiwa na umati mkubwa wa watu ambapo maandamano yameanzia katika Uwanja wa ndege kuelekea Uwanja wa Furahisha.

Msururu mkubwa wa Bodaboda,magari na watu kujipanga kandokando ya Barabara ndivyo vilivyopamba mapokezi yake.

-------------------

Yaliyojiri mkutanoni Viwanja vya Furahisha

Akihutubia Malaki ya watu mgombea wa Urais Tundu Lissu alilaani serikali ya CCM kwa kumhujumu zao la Pamba ambalo no kitega uchumi Cha watu wa Kanda ya ziwa.

Lissu amesema serikali yake itawajali Wafanyakazi na kila mwaka wataongezewa mshahara kwa mujibu wa sheria za nchi.

Amesema serikali yake inafuata kauli Mbiu ya Uhuru Haki na Maendeleo ya watu.

Amesema serikali yake itaondoa ukandamizaji wa wafanyabiashara ambapo kwa Sasa Mamlaka ya Mapato Tanzania imekuwa sehemu ya kuhujumu na kuua biashara za Watanzania.

Awali Lissu alisema tangu arejee nchini Mapokezi ya Mwanza ndiyo yamevunja Rekodi kwa wingi wa watu
IMG-20200901-WA0076.jpg
 
Anaenda tu kukamikilisha ratiba Mwanza kule huwaambii kitu kuhusu Magufuli. Na kwa kuwa Lisu amekuwa akiponda ujenzi wa reli ya mwendokasi kwenda Mwanza atapata jibu Leo wengi hawataenda mkutanoni

Tena Mwanza mjini linashushwa daraja la nguvu Busisi
 
Amekuwa akiponda ununuzi wa Ndege jibu atalipata mwanza Ndege ukiuliza wauza samaki mitaani watakuambia jinsi abiria wa Ndege wanavyobeba samaki kwa wingi.

Hapo akienda na porojo zake za kupinga ununuzi wa Ndege aone wavuvi na wauza samaki watakavyoguna hata Kama Ni Chadema.

Ndege nyingi hufurika Mwanza kubeba samaki kupeleka nje ya Nchi kibao akiponda ununuzi wa Ndege Mwanza hata mtu wa mtaani atamzomea sababu wanajua umuhimu wa Ndege kwenye biashara yao ya samaki
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom