Yaliyojiri katika Clubhouse Session: Miaka 60 ya Uhuru mchango wa Kidijitali

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
625
938
1639064075388.png

Katika siku za karibuni mitandao ya kijamii na Mifumo ya Kidijitali imekuwa maeneo muhimu kwa Jamii ya Tanzania kutumia Uhuru wa Kujieleza na kupigania haki zao nyingine

Tukifurahia Miaka 60 ya Uhuru wa Tanganyika ni kwa kiwango gani tumeweza kuitumia mifumo ya Digitali katika kusimamia Haki za Binadamu, Demokrasia na Utawala Bora?

Ungana nasi katika Mjadala huu utakaofanyika kupitia Clubhouse Desemba 9, 2021.

Kujiunga na Mjadala huu bonyeza link hii hapa chini:



BAADHI YA MAWAZO NA MAONI YALIYOTOLEWA NA WADAU MBALIMBALI
Dkt. Aikande: Nimeshangaa kusoma kwenye Kitabu cha Rais Mstaafu Mwinyi kwamba kwenye Miaka ya 80 Serikali ilikuwa hairuhusu Matumizi ya Kompyuta.

Nadhani walikuwa na hofu kwamba zinaweza kuwanyima Watu kazi japokuwa kwenye Nchi za wenzetu tayari Kompyuta ilikuwa kitu cha kawaida.

Dkt. Aikande: Kwasasa tunaona Watanzania wengi wanajihusisha na Mitandao ya Kijamii. Hata ukiangalia Data za TCRA zinaonesha Watu wengi wanajiunga kutumia Intaneti

Pia, tuna mifumo mingi ya Kidijitali ambayo inatuwezesha kupata huduma pamoja na kufanya malipo ikiwemo LUKU.

Maxence Melo: Wahabarishaji wa Jamii wamebadilika kutokana na Dijitali. Wananchi Kwasasa wanaweza kuamua mambo wenyewe kwa msaada wa Dijitali

Dunia ya leo, Dijitali imezalisha Matajiri wengi sana. Kuna hata Wanasiasa ambao walikuwa juu lakini Dijitali imewapoteza.

Maxence Melo: Digitali inaweza kuja na fursa mbalimbali lakini inaweza kuja na hatari kadhaa. Unaweza kufurahia umeenda Hospitali ukapata huduma haraka, lakini kumbe taarifa zako hazipo salama.

Digitali hii hii ina watu wanaweza kuifanyia 'Manipulation'.

Zitto Kabwe: Ni muhimu kukumbuka Dijitali ni sehemu ya Sekta ndogo ya Uchumi ya Teknolojia ya Habari. Dunia nzima Teknolojia hii imekua sana

Ilikuwa ni vigumu kudhani kwamba Mtu anaweza kuwa na Simu ya Mkononi halafu akaongea na Dunia nzima. Kila Siku kuna Uvumbuzi mpya.

Zitto Kabwe: Dijitali imeshusha sana gharama za Maisha na Kibiashara ikiwemo 'Mobile Money transfer'

Hatuwezi kusema Dijitali imesaidia nini kwenye Uchumi lakini Sekta ya Habari na Teknolojia tunaona inazidi kuimarisha Uchumi wa Nchi yetu.

Zitto Kabwe: Sasa hivi unaweza kuhutubia Mkutano wa Chama Lindi lakini uko Dar es Salaam. Uhuru wa Watu pia umeongezeka sana

Kila Mtu anaweza kufungua Akaunti ya Habari, kujirekodi na akaandika habari yake vile ambavyo yeye anataka bila kuwepo lawama kwamba nimenukuliwa vibaya.

Zitto Kabwe: Zamani 'Narrative' ya Taifa ilikuwa inaongozwa na Watawala vile wanavyotaka wao. Lakini sasa hivi Jamii inaweza ikawa na mawazo tofauti na mawazo hayo yakasambaa. Mfano, Wachache ndio wanajua Desemba 10 ndio Uhuru wa Zanzibar.

Zitto Kabwe: Naona mchango mkubwa wa Dijitali katika Uhuru ndio huo Uhuru wenyewe. Uhuru wa kutoa mawazo na kupashana habari

Ukuaji wa hizi Teknolojia unafanya baadhi ya kufaidika zaidi na kuwa na nguvu. Kuna Nchi ambazo ziko nyuma na hazifahamu 'Digital Power' katika Taifa.

Zitto Kabwe: Katika kusherehekea tusisahau changamoto. Bado tupo nyuma ikilinganishwa na wenzetu. Tunapotafakari, ni muhimu kutazama tunakosea wapi

Wapi ambapo tukipiga hatua tutawafikia wenzetu wa Asia (mfano Vietman na China).

Zitto Kabwe: Sasa hivi Kenya wanaonekana kama wanafaidika sana Mrahaba wa M-Pesa na inaonekana kama 'Innovation' ya Kenya lakini kumbe ni ya Tanzania

Benki Kuu ya Tanzania ndio ilikuwa nyuma kuendeleza Mfumo huu. Hivyo hata suala la #CyptoCurrency pia tusiwe Watu wa kusema Hapana

David Shaban: Kuna Nchi ambazo Wananchi wake wana vizuizi katika kufanya vitu fulani kwenye Dijitali ikiwemo Korea Kusini

Kwa Tanzania naweza kusema tumepiga hatua kwenye Dijitali, Vijana wanapata ajira kwa kutengeneza 'Software'. Miaka ya 60 Mtu wa Teknolojia angetakataliwa.

Sultan Sultan: Kipindi cheti Kompyuta ilikuwa kama Lori. Kujibaragua kulikuwa kwingi kwamba Mishahara ya Wafanyakazi haitachelewa kwasababu kuna Kompyuta

Nilipokwenda Nje nilirudi 1995 na nilikuja na Kompyuta yangu ila niliingiza Airport pale kama Bangi.

BM-TZ: Siku hizi ukitaka kutuma text (ujumbe mfupi) unaandika tu. Tumetoka mbali!

Kwenye upande wa matumizi, tunatumiw Mitandao ya Kijamii na Apps. Bado tupo nyuma ikilinganishwa na wengine hususan kwenye upande wa Software

Kwenye upande wa Serikali, tupo nyuma sana.

BM-TZ: Digitali inachangia kupanua Demokrasia kwenye mijadala na maeneo mengine ambayo hayajafanyiwa kazi mfano kupiga kura kidigitali

Lakini digitali pia ina matatizo yake; mfano Masuala ya Fake News. Sheria zetu zibadilike kuendana na wakati.

BM-TZ: Mitandao inaweza kutupa wrong perception ya vitu. Mfano sasa hivi tuna mijadala mingi kuhusu Katiba. Ukisikiliza, utafikiri suala la Katibu lipo kwenye midomo ya watu wengi

Tuondoe wrong perception kwamba kitu kikiwa hot kwenye mitandao basi ipo hivyo kwenye jamii

Dkt. Aikande: Kupitia Digital Spaces wananchi wameweza kuhoji. Mfano jana baada ya hotuba ya Rais Samia Suluhu wananchi wengi walitoa maoni yao, tofauti na mainstream media

Wananchi wanaweza kuibua matatizo mbalimbali kwenye jamii mfano Rushwa na kuwawajibisha Viongozi.

Dkt. Aikande: Kuna changamoto moja ambayo Tafiti zote zinaonesha; kwenye digital spaces au democracy movements kuna challange moja tunaiita "Determinism".

Dkt. Aikande: Nafikiri kuna kitu ambacho sisi kama Watanzania kunatakiwa tukifikirie hasa wakati Serikali inaandaa Sheria ya Digitali

Mfano tunavyobinya innovation ya Vyombo vyetu inamaanisha vinakuja vingine vya nje mfano Facebook, Clubhouse na Twitter na vinakuwa na nguvu.

Asted William: Katika miaka 60 ya Uhuru, Nchi imejitahidi kwa kiasi chache kuhakikisha tunaenda kidigitali. Kuna mabadiliko makubwa, tunaweza kupata Intaneti ukiwa maeneo mbalimbali ya Nchi

Digitali imesaidia ktk upande wa Afya, watu wanaweza kuwasiliana na Daktari wakiwa popote.

Don Sompo: Kwenye miaka 60 ya Uhuru, nilichokiona ni kuwa Digitali ni kama opportunity (fursa) mpya imekuja kwa sisi vijana

Katika upande wa ujasiriamali na biashara tunaona watu wanaweza kujiajiri, kupata fedha na hata kuajiri watu wengine.

Don Sompo: Hapa Tanzania tumeona Tigo imeweza kupoteza kwa kiasi fulani baada ya Mwakilishi wao kusema hawalindi taarifa za mteja.

Ni vizuri kuchukua taarifa za watu, lakini iwe kwa kitu kinachojenga na sio kuzimanipulate ili kuwaibia na kuzitumia kisiasa. Sio kitu kizuri.

Vedasto Dunstan: Kuwepo kwa digitali kumepelekea watu kuwajibika. Hata viongozi wanakuwa makini wanapotoa kauli zao kwasababu wanaogopa

Pia, Maendeleo ya Digitali yaendane na mabadiliko ya Sheria.

Josec James: 'Internet Penetration' yetu inaongezeka kila siku. Digitali inakuja na hatuwezi kuikwepa, lakini security na privacy za Data zetu ni muhimu

Serikali ingeanza kutunga Sheria kuhusu #DataPrivacy na Security zetu. Kampuni zinazovuna Data pia zinaweza kuziuza.
 
Back
Top Bottom