Yaliyojiri Karimjee: Zoezi la kuaga mwili wa Marehemu Dkt. John Kijazi, rais Magufuli atoa neno

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,480
141,196
Mbunge wa Kawe Askofu Dkt. Gwajima ameongoza sala ya kumuombea marehemu Dr Kijazi nyumbani kwake Mbweni jijini Dar es salaam na sasa anaongoza msafara ambao umeanza kuelekea viwanja vya Karimjee ili viongozi na wananchi wapate fursa ya kutoa heshima za mwisho.

Zoezi la kutoa heshima za mwisho pale Karimjee itaongozwa na mkuu wa nchi Rais Magufuli

Up dates:

Viongozi wakuu wameshaketi sehemu zao na sasa anasubiriwa mh Rais Magufuli awasili ili shughuli rasmi ianze.

Screenshot 2021-02-19 at 10.36.27.png
Screenshot 2021-02-19 at 10.38.17.png
Screenshot 2021-02-19 at 10.39.23.png

Rais Magufuli ameshawasili na utaratibu unaanza rasmi na itaanza misa ya kumuombea marehemu.

=====

Rais Magufuli: Baada ya Uchaguzi wa Marudio wa Zanzibar, Maalim Seif aliniandikia barua, nilisita kidogo lakini akaandika barua ya pili na ya tatu...

Kili nilipotafuta ushauri toka Zanzibar, niliambiwa muache kwanza. Siku 1 nikaamua kumuona Maalim. Nilipoongea naye nilimwona mtu tofauti sana na nilivyomdhania

Maalim Seif alinambia: Sikushiriki Uchaguzi wa Marudio, lakini sitoshiriki kuanzisha vurugu zozote. Alinieleza kuwa yeye anapenda amani na aliitekeleza kauli yake kwa vitendo

Mara ya mwisho, Maalim Seif alikuja hadi Chato. Alinipa historia yake akiwa CCM tangu enzi za TANU. Siku zote hata alipokuwa Chato, alikuwa akihubiri UMOJA. Tumshukuru Mungu kuwa Maalim ameimaliza safari yake kwa amani

Ni matumaini yangu kuwa Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla tutaenzi mema yote aliyoyafanya Maalim Seif

Rais Magufuli: Nina historia ndefu na Balozi Kijazi. Wakati nimechaguliwa na Mzee Mkapa kuwa Naibu Waziri wa Ujenzi mwaka 1995, nilikutana na wahandisi wengi wa wakati huo; nilipotembelea barabara za Dodoma, nilikuta barabara zote zinapitika (Kijazi ndiye alikuwa Mhadisi)

Kijazi alinieleza alivyokuwa akisimamia makandarasi kusimamia ujenzi wa barabara na alivyosimamia matumizi ya fedha ingawa alikuwa anapelekewa fedha kidogo

Rais Magufuli: Mwaka 2000 baada ya Uchaguzi, niliteuliwa kuwa Waziri. Nilimwomba Mzee Mkapa aruhusu Kijazi awe Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi. Mwaka 2002 akateuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi

Magufuli.jpg

Rais Magufuli:
Balozi Kijazi aliteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini India. Aliteuliwa na Mzee Kikwete

Rais Magufuli: Kuna watu wapo hapa walikuwa watumbuliwe wamenusurika sababu ya Kijazi. Alikuwa ni mpatanishi. Hata ukitaka kumtumbua mtu Balozi Kijazi alikuwa ananiambia subiri kwanza siku mbili uangalie

Kweli ukisubiri unakuta mtu kabadilika. Wako wengine sikuwatumbua kwa sababu ya Kijazi

MAGUFULI:
Kwa kuomba na kufunga nina imani tutashinda. Tutahofu sana lakini Mungu ni muweza wa kila kitu

Niwaombe viongozi wa dini wahamasishe kuomba. Tumeshinda mwaka jana tutashinda mwaka huu.

Ninachotaka kusema magonjwa yapo, na yataendelea kuwepo

Magonjwa ya vifua na kupumua yapo. Na hayajaanzia hapa. Tuendelee kusimama kwa kuchukua tahadhari na kumtegemea Mungu. Tumeanza sana kutegemea nguvu za binaadamu, nawaomba ndugu zangu mjue Mungu yupo

Niwashukuru viongozi wa dini kwa kulisimamia hili. Tukisimama na Mungu tutashinda

Inawezekana kuna mahali tunapata jaribu kama waisrael walikuwa wakienda Kanani

Tusimame na Mungu, ndugu zangu watanzania. Kufa tutakufa tu. Unaweza kufa kwa maleria, kansa lakini kamwe tusimuache Mungu

Ndugu zetu waislamu walitangaza muda wao wa kuomba, niliambiwa na mufti

Niwaombe watanzania kama kuna mahali tumetetereka tuendelee kubaki na Mungu. Tuanze leo na ndugu zetu waislamu ambao wameshaanza

Tutahangaika sana, Mungu ni mwenye uwezo wa kilakitu

Niwaombe viongozi wa dini kama ambavyo mmekuwa mkifanya endeleeni kusisitiza maombi. Tulishinda mwaka jana, na mwaka huu tutashinda
 
Mbunge wa Kawe Askofu Dkt. Gwajima ameongoza sala ya kumuombea marehemu Dr Kijazi nyumbani kwake Mbweni jijini Dar es salaam na sasa anaongoza msafara ambao umeanza kuelekea viwanja vya Karimjee ili viongozi na wananchi wapate fursa ya kutoa heshima za mwisho.

Zoezi la kutoa heshima za mwisho pale Karimjee hall zitaongozwa na mkuu wa nchi, Rais Magufuli.

Up dates;
Rais atakuwa mc? Sijaelewa
 
Wewe vipi utahusika kitengo kipi hapo kwenye msiba?
 
Mbunge wa Kawe Askofu Dkt. Gwajima ameongoza sala ya kumuombea marehemu Dr Kijazi nyumbani kwake Mbweni jijini Dar es salaam na sasa anaongoza msafara ambao umeanza kuelekea viwanja vya Karimjee ili viongozi na wananchi wapate fursa ya kutoa heshima za mwisho.

Zoezi la kutoa heshima za mwisho pale Karimjee hall zitaongozwa na mkuu wa nchi, Rais Magufuli.

Up dates;
Who is next? Stay tuned
 
Back
Top Bottom