Yaliyojiri jijini Arusha katika kuaga Miili ya Wanafunzi wa Lucky Vincent waliopata ajali ya gari

Deejay nasmile

JF-Expert Member
Nov 8, 2011
4,372
2,000
Watanzania wenzangu kwanza poleni na msiba uliotupata,kama wazazi,walezi,ndugu jamaa na marafiki..

Baada ya pole hii ya huzuni..naomba mwenye wimbo huu ambao unatumika katika background hapo clouds tv wakati huu wa maonesho ya live ya msiba huu wa lucky vicent school.anisaidie link au hata whatsapp..ndani yupo angel bernad na wasanii wengine..
 
Mtemikwila

JF-Expert Member
Aug 29, 2013
1,390

Duh!! Anyway ngoja watakupa ma bongo freva wenzio
 
bushland

JF-Expert Member
Mar 6, 2015
7,022
2,000
Kuna jamaa nadhani siku ya Leo ameonja adhabu za kijeshi.mwanajeshi alikuwa akitusisitiza tukae chini ili watu wa nyuma wapate kuona kinachoendelea mbele akawa mkaidi kwa kuogopa kuchafua suruali.msoja akainama kwenye kidimbwi akachota tope hakampaka matakoni akamwambia kaa jamaa akakaa bila kupenda
Kwa kweli tanashukuru jeshi kwa kazi iliofanya Leo, wanajeshi walikuwa Wa kutosha Tena walitapakaa Hadi nje kabisa, na baadhi ya Bara Bara Pia zilifungwa.
 
Clkey

JF-Expert Member
May 29, 2014
5,485
2,000
Ila mm nmekereka na vitu kama viwili hvi, watu kuvaa nguo zao za Ccm japo hawakuwa wengi lkn nkajiuliza hivi hawa watu waliwaza kitu gani?Kingine nmeshangaa na ubora wa spika zilizotumika, ni kama vile hawakujipanga kabisaaa watu tuliokuwepo upande wa Mashariki tulikuwa hatusikii kabisaa mwishowe watu wakaamua kufungua radio za cm zao at least tusikie kinachoendelea
Tukiachana na hayo Jeshi letu wanapaswa kupewa shukrani za dhati kwa kazi yao nzuri walofanya, polisi wetu walishindwa kabisaaaaa
 
MNANSO

JF-Expert Member
Jul 18, 2015
2,251
2,000
Mungu awatie nguvu wazazi na ndugu wa karibu.poleni watanzania wote.Bwana alitoa na Bwana ametwaa.
 
SAUTI YAKO

JF-Expert Member
Jan 25, 2014
2,523
2,000
Ila mm nmekereka na vitu kama viwili hvi, watu kuvaa nguo zao za Ccm japo hawakuwa wengi lkn nkajiuliza hivi hawa watu waliwaza kitu gani?Kingine nmeshangaa na ubora wa spika zilizotumika, ni kama vile hawakujipanga kabisaaa watu tuliokuwepo upande wa Mashariki tulikuwa hatusikii kabisaa mwishowe watu wakaamua kufungua radio za cm zao at least tusikie kinachoendelea
Tukiachana na hayo Jeshi letu wanapaswa kupewa shukrani za dhati kwa kazi yao nzuri walofanya, polisi wetu walishindwa kabisaaaaa
Upande wa speaker yani utafikiri mtu amechuka mziki wa kusikiliza sebuleni kwake akauleta uwanjani yani kila aliyekuwa hapa Leo amelaumu hiyo saund ilikuwa inaishia tu huko jukwaa LA viongoz.Nilidhani jukwaa LA viongozi lingewekwa pale lipowekwa jukwaa la magufuli enzi za kampeni wananchi wote tungeweza ona kinachoendelea.umoja wa watanzania unatia hamasa sana maana watu walijotokeza kweli kweli
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom