Yaliyojiri jijini Arusha katika kuaga Miili ya Wanafunzi wa Lucky Vincent waliopata ajali ya gari

Neno sahihi la salamu kwa marehemu ni R.I.A ( Rest In Accordance) lakn kwa kuwa hawa wengi bado ufaham wao haukutambua sana mema na mabaya,,,,,,,,,,, mm kama Mchungaji namwachia Mungu .

Ila natoa wito kwako ww ambaye unajua mema na mabaya. Na ujiulize kama Mungu ameruhusa watoto wadogo wafe,,,,,je ww MTU mzima???????
 
afe04de03a828090a46ac4e2f3eb68a0.jpg


Je Shetani Ana nguvu zaidi ya M'Mungu. ??
 
Tumepatwa na msiba ila cha kushangaa sijaona wasanii wetu kutunga wimbo wa maombolezo ni watu wa ajabu sana nyie wasanii. mnashindwa hata kutunga nyimbo za maombolezo kumbukeni mulipo pata matatizo kama kutekwa tulikuwa pamoja
Kweliii! Ata amolapa sijamuona au ana nauri?
 
Tumeumia sana na hakuna anayeweza kuelezea maumivu yetu...

Watanzania wote tumefikwa na msiba huu mzito kabisa na unaumiza sana.Malaika hawa wamefikwa na mauti yasiyowastahili kabisa...

Mungu awapokee kwa amani....
 
AYI MAMA MWANANGU.

Kilio hiki kilio, siwezi kukizuia,
Siyo langu kusudio, kalele kuwapigia,
Sababu kuna tukio, lafanya miye kulia,
Ayi mwenzenu mwanangu, leo ametangulia.

Machozi jama machozi, sina yameniishia,
Ila mwenzenu majonzi, bado yamenizidia,
Hata kusema siwezi,nabaki nagugumia,
Ayi mwenzenu mwanangu, leo ametangulia.

Msiba huu msiba, wenzangu nawaambia,
Umekuwa kama mwiba, kooni ulonasia,
Jama wanipa adhaba, nashindwa ivumilia,
Ayi mwenzenu mwanangu, leo ametangulia.

Mkaja ule mkaja, bado naukumbukia,
Damu nyingi zilovuja, mwana nikijazalia,
Musidhani naleleja, uchungu 'menirudia,
Ayi mwenzenu mwanangu, leo ametangulia.

Ajali hizi ajali, hadi lini Tanzania?
Lawama kwa serikali, kwa macho kuwafumbia,
Madereva makatili, leseni kuwaachia,
Ayi mwenzenu mwanangu, leo ametangulia.

Mkanda jama mkanda, mwana hakuutumia,
Dereva pamwe na konda, lawama nawatupia,
Wangewafunga mikanda, kabla ya gia kutia,
Ayi mwenzenu mwanangu, leo ametangulia.

Milanga jama milanga, miongo karne pia,
Izidi mbele kusonga, mwana ulipo sikia,
Hakuna wa kunipinga, moyoni utasalia,
Ayi mwenzenu mwanangu, leo ametangulia.

Tamati sasa tamati, wino umeniishia,
Nilivyo nusu kaputi, kifo ninasubiria,
Nasema haya kwa dhati, duniya nawaachia,
Ayi mwenzenu mwanangu, leo ametangulia.

...t...a...m...a...t...i..

Share shairi hili mara nyingi uwezavyo.
Mpumzike kwa Amani watoto wetu.

07 Meyi 2017 Jumapili 12:29Pm
[HASHTAG]#JiniKinyonga[/HASHTAG]
Dotto Rangimoto Chamchua(Njano5)
Call/whatsp 0622845394 Morogoro.
 
Kweliii! Ata amolapa sijamuona au ana nauri?
acheni hzo nyimbo nying tu zimetungwa na kuimbwa na wasanii weng tu,wakiwemo bongofleva artists na gospel,sema hamjaskiza radio.au mlitaka wapige live pale uwanjani,wakat watu wakiomboleza?
 
Ni msiba mkubwa nashidwa hata neno la kuelezea. Niseme tu nimeumia, nimeumia na tumeumia kama taifa, hasa nikielewa kuwa mauti umewakuta wakati wanaenda kujipima weledi wao katika Nyanja ya elimu kwa ajili ya majaliwa ya Tanzania ya kesho. kwa kweli inauma sana. Eheeh Mola pokea watoto wako hawa na wajalie kukakaa na malaika wako watakatatifu milele na milele AMINA.
 
Kuna jamaa nadhani siku ya Leo ameonja adhabu za kijeshi.mwanajeshi alikuwa akitusisitiza tukae chini ili watu wa nyuma wapate kuona kinachoendelea mbele akawa mkaidi kwa kuogopa kuchafua suruali.msoja akainama kwenye kidimbwi akachota tope hakampaka matakoni akamwambia kaa jamaa akakaa bila kupenda
 
AYI MAMA MWANANGU.

Kilio hiki kilio, siwezi kukizuia,
Siyo langu kusudio, kalele kuwapigia,
Sababu kuna tukio, lafanya miye kulia,
Ayi mwenzenu mwanangu, leo ametangulia.

Machozi jama machozi, sina yameniishia,
Ila mwenzenu majonzi, bado yamenizidia,
Hata kusema siwezi,nabaki nagugumia,
Ayi mwenzenu mwanangu, leo ametangulia.

Msiba huu msiba, wenzangu nawaambia,
Umekuwa kama mwiba, kooni ulonasia,
Jama wanipa adhaba, nashindwa ivumilia,
Ayi mwenzenu mwanangu, leo ametangulia.

Mkaja ule mkaja, bado naukumbukia,
Damu nyingi zilovuja, mwana nikijazalia,
Musidhani naleleja, uchungu 'menirudia,
Ayi mwenzenu mwanangu, leo ametangulia.

Ajali hizi ajali, hadi lini Tanzania?
Lawama kwa serikali, kwa macho kuwafumbia,
Madereva makatili, leseni kuwaachia,
Ayi mwenzenu mwanangu, leo ametangulia.

Mkanda jama mkanda, mwana hakuutumia,
Dereva pamwe na konda, lawama nawatupia,
Wangewafunga mikanda, kabla ya gia kutia,
Ayi mwenzenu mwanangu, leo ametangulia.

Milanga jama milanga, miongo karne pia,
Izidi mbele kusonga, mwana ulipo sikia,
Hakuna wa kunipinga, moyoni utasalia,
Ayi mwenzenu mwanangu, leo ametangulia.

Tamati sasa tamati, wino umeniishia,
Nilivyo nusu kaputi, kifo ninasubiria,
Nasema haya kwa dhati, duniya nawaachia,
Ayi mwenzenu mwanangu, leo ametangulia.

...t...a...m...a...t...i..

Share shairi hili mara nyingi uwezavyo.
Mpumzike kwa Amani watoto wetu.

07 Meyi 2017 Jumapili 12:29Pm
[HASHTAG]#JiniKinyonga[/HASHTAG]
Dotto Rangimoto Chamchua(Njano5)
Call/whatsp 0622845394 Morogoro.
Mkuu una mambo ya kitoto kweli aisée!
 
Back
Top Bottom