Yaliyojiri jijini Arusha katika kuaga Miili ya Wanafunzi wa Lucky Vincent waliopata ajali ya gari

KIPEKEE NIPONGEZE CLOUDS TV NA AZAM kwa kutokujali maslahi binafsi na kuamua kutangaza tukio hili LIVE. . Toeni somo kwa TV nyingine zinazofikiri kurusha live ni mpaka liwe tukio analokuwepo rais tu
 
Huwa mna mizaha mibaya sana msibani. Sio vizuri hivyo,wale waliopoteza watoto wao wa pekee hapo watajisikiaje kwa kauli yako hii.
Numbisa mimi hata suala la watoto au mtoto sikuwa naliwaza nimeuliza tu kama bashite yupo, chaajabu ukaingiza mambo ya watoto alafu unageuza kibao mimi nilaumiwe
 
it pains alot
Mungu awaangazie mwanga wa milele vipaji vingi sana tumevipoteza kama taifa kiujumla na zaidi kwa wazazi waliochipua ndoto na matumaini juu ya wapendwa wao
Watoto ni taifa la kesho tuwalinde, tuwatunze na kuwaonyesha njia ipasayo nao wakaitende
Pigo kubwa sana I feels it
 
Ndo mshahara wako wa kulazimisha kila kona makonda aongelewe nikakwambia bora yeye aliyeenda kuliko wewe kuonya masuala ya siasa msibani kisa makonda yupo uwanjani
Numbisa mimi hata suala la watoto au mtoto sikuwa naliwaza nimeuliza tu kama bashite yupo, chaajabu ukaingiza mambo ya watoto alafu unageuza kibao mimi nilaumiwe
 
Unaweza kuangalia Moja ya hizi link za Video hapa chini za Video.



UPDATE:

Watu kadhaa wamehudhuria na kutoa salam za rambirambi wakiwemo mkuu wa mkoa wa Manyara, Joel Bendera, kaimu jaji mkuu wa Tanzania, waziri wa TAMISEMI, George Simbachawene na anaeongea kwa sasa ni waziri wa Fedha, Philip Mpango.

Mpango: Watoto wetu hawa wametuachia mfano mzuri, walikuwa wanakwenda kufanya kazi.

Miili ya watu 35 inaingizwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid na gari la jeshi la Wananchi na vilio vinatawala kwa sasa na wengine wanaanguka. Miili hiyo inashushwa na kuwekwa sahemu iliyotengwa kwa ajili ya kuaga.

Serikali ya Kenya imemtuma Waziri wa Elimu wa nchi hiyo kuja kuiwakilisha katika shughuli ya kuagwa miili ya wanafunzi walimu na dereva.

Anaeongea kwa sasa ni makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu na anawashukuru wote waliohusika mpaka hatua hii.

Amewaasa madereva kuhakikisha wanabeba watu kulingana na uwezo wa gari na kuwa makini wawapo barabarani. Anasema matokeo ya ajali huleta vifo na masiba mikubwa.

Samia: Msiba huu umeleta msiba mkubwa Tanzania. nimalizie kwa kutoa pole kwa wafiwa, mkoa na watanzania wote kwa ujumla.
==========

Tayari Jeshi la Wananchi na Polisi wapo uwanjani wakifanya taratibu za hapa na pale kwa ajili kupokea miili.

Viongozi wa dini zote watakazoendesha ibada tayari wamewasili, Wazazi wa wafiwa pamoja Na idadi ya wananchi wanaingia uwanjani Ni kubwa kweli kweli.

Sahivi Ni wananchi wanaingia uwanjani pamoja Na askari WA kutuliza ghasia, tunasubiri miili Na viongozi WA kitaifa wingie ndo ratiba nyingine ziingie.

Mkuu WA Mkoa Na mkuu WA wilaya ndo wanaingia uwanjani kwa sasa, pamoja Na mkurugenzi WA jiji la Arusha



Waziri wa fedha Na mipango Philip Mpango tayari amekwishaingia

Walimu 30 toka serikali ya mapinduzi Zanzibar nao tayar wamekwishawali pia

Vikosi vyote vya usalama ikiwemo Magereza, jeshi la wananchi Na Polisi wapo wa kutosha Na sawa Ni judge mkuu anaingia uwanjani akiwa anaongozana Na msafara WA makamu WA Raisi

Uwanja umekwisha jaa Na tayari gari ya zimamoto zimeingia Na bado idadi ya wananchi wanaoingia Ni kubwa kweli kweli kweli, red cross nao wamejaa kwa ajili ya lolote litakalotokea hapa uwanjani,

Uwanjani watu wanapiga makofi Na vigelegele baada ya mh.Lowassa kuingia.Na watu kujisahau kuwa wapo msibani

Wakuu samahanini Sana najaribu kutuma Picha za hapa uwanjani lakini naona zinagoma sijajua kwanini, naomba yoyote alie uwanjani anisaidie tafadhali kuweka picha


Mkuu,tayar nimeomba aliepo uwanjani aweke picha hapa tafadhali, Makamu wa Raisi tayari amekwisha ingia pamoja na mh. Kinana Na Waziri wa elimu Mh.Ndalichako tayari wapo uwanjani

Tendo tunalosubiri sasahivi Ni miili kuingia uwanjani, uwanja wote Ni tulivu kabisa

Viongozi waliohudhura Ni pamoja Na katibu mkuu WA CCM Abdurahamani Kinana, Paul Makonda, mh. Lowassa, katibu mkuu Wizra ya Afya, balozi kutoka Kenya nchini Tanzania, Waziri wa elimu toka Kenya, Waziri wetu WA elimu Prof.Ndalichako, Waziri George Simbachawene, Na viongozi wengine wengi

Tayari mh. Kinana Na Mh. Mbowe wamekwishatoa salamu za rambi rambi..
Misaada mbali mbali tayari imefika Na gaharma zote za usafiri, majeneza 35 pamoja sanda mkoa umelipia gharama hizo,
Ngoro ngoro wametoa mil.15, Tanapa wametoa ml.20, Auwasa mi 1, AICC mil. 5 jiji la Arusha ml.5
View attachment 506175 View attachment 506176 View attachment 506178 View attachment 506179
View attachment 506177


Asanteni WaTanzania kwa kuwa pamoja katika hili.
 
Natoa pongezi kubwa kwa Jeshi letu kuwa pamoja na kufanya kazi kwa moyo mmoja
kweli Tuna jeshi pendwa kwa Raia wake
Mungu ibariki Tanzania
 
Ninashangazwa na watu wanao hangaika kupiga picha majeneza au kurekodi!
Wanasababisha msongamano wa watu na huenda wengine wakakosa nafasi ya kuaga.
Ili tu wapate kitu cha kuposti kwenye mitandao na kupata likes.
Watu tuwe na aibu kwa baadhi ya vitu si kila kitu ni cha kujinufaisha tuache ubinafsi.


Mwanga wa milele uwaangazie ee bwana.
 
Back
Top Bottom